My Authors
Read all threads
MYSTERIES OF THE MISSING Bado Tuko na Tamthilia yetu ya jana (Documentary) Mysteries of the Missing na Leo nakusogezea tukio la pili kati ya matukio yaliyo gusa attention yetu jisogeze karibu, juisi, soda na popcorn ama andazi au bumunda itapendeza zaidi ukiwa navyo pembeni Apo
KUPOTEA KWA NDEGE YA UFARANSA NAMBA AF 447
Air France flight 447 (AF447/AFR447) ndege ya Abiria iliondoka Rio de Jeneiro Brazil kwenda Ufaransa tarehe 1 June 2009, ndege hii aina ya Airbus A330 ikawa stalled (kuwa stalled ni kitendo cha ndege kushindwa kuelea
angani na wakati mwingine kuanguka ikitanguliza mkia kitendo ambacho sio cha kawaida kwenye ndege, tunategemea ndege ianguke kutanguliza pua) ndege inapopaa kwenda juu na kufikia hatua ikawa wima haiwezi kuelea angani kwani ndege huelea juu kutokana na
mkandamizo wa chini wa hewa juu ya mabawa na msukumo wa hewa kwenda juu wa chini ya mabawa kitendo hicho huifanya ndege kuelea angani, ila pale ndege nyuzi ya mashambulizi (angle of attack) inapokuwa kubwa hakuna hewa za mkandamizo wala msukumo kwenye
mabawa ya ndege, hapa ndege lazima ianguke kwa kuwa haiwezi tena kuelea (float). Huku ndo kuwa Stalled.
Ndege iliyopata ajali hii ilikuwa ni Airbus aina ya A330-203 ikiwa na serial number 660 na kusajiliwa kwa namba F-GZCP, iliruka kwa mara ya kwanza tarehe 25 Februari 2005
na ilikabidhiwa miezi miwili baadae kwa shirika la ndege tarehe 18 Aprili 2005 wakati inapata Ajali ndo ilikuwa ndenge mpya kwenye shirika hilo la ndege. Ndege hii ilikuwa inaendeshwa na engine mbili za aina ya General Electric CF6-80EA3 zenye uwezo wa msukumo wa
kusafiri km 871-913km kwa saa
Hadi siku ndege hii inapata ajali tayari ishakuwa hewani kwa masaa 18,870 (flying hours) wataalamu na wale wenye elimu ya ndege nahisi hapa mtakuwa mmenipata

Mambo ya Muhimu Kuyajua:
Ndege hii ilibeba abiria wapatao 216 na wahudumu pamoja
na marubani watatu jumla walikuwa 228 na wote walikufa kwenye ajali hii, ngoja tuangazie uzoefu wa marubani kabla ya kuongelea miujiza ya ajali yenyewe
.Rubani Marc Dubois (PNF = Pilot not Flying) umri miaka 58 alikuwa na masaa 10,988 ya kuendesha ndege (flying
hours) ktk masaa hayo masaa 6,258 akiwa Rubani mkuu, na masaa 1,700 katika ndege ya A330 Airbus alikuwa ashaenda mizunguko 16 ya huko Amerika kusini.
. Rubani msaidizi upande wa kiti cha kushoto rubani David Robert(pilot not flying PNF) miaka 37, huyu alikuwa na
masaa 6,547 kati ya hayo masaa 4,479 yalikuwa ya A330 airbus. Alishafanya mizunguko 39 ya nchi za Amerika Kusini
. Ruban msaidizi kiti cha kulia Pierre (PF- pilot flying) aliyekuwa anaendesha ndege kwa wakati huo alikuwa na masaa 2,936 (Flight hours) kati ya hayo masaa 807 kwenye
Airbus Mke wake aliyeitwa Isabella mwl wa fizikia alikuwepo ndani ya ndege naye alikufa pia

AJALI
Ndege iliondoka toka Rio de Jeneiro Geleao International Airport tarehe 31 may 2009 saa 1: 29 kwa saa za brazil au (22: 29 UTC) Ikitegemewa kuwasili Paris-Charles de Gaulle
Airport saa 5 kwa saa za Ufaransa safari ya masaa 4:34. ndege ilipoteza mawasiliano baada ya masaa 3 na dakika 6 baada ya ndege kuondoka ujumbe wa mwisho ulionyesha ndege kupita eneo umbali wa km 365 kutoka Natal kaskazini mashariki ya Pwani ya Brazil. Kabla ya ndege
kuingia anga lisilo na mawasiliano (Communication dead zone)
Airbus 330 inatakiwa kuendeshwa na marubani wawili kwa wakati mmoja na kwa sheria ya kifaransa kila rubani alitakiwa kupumzika baada ya muda fulani. Hivyo basi Rubani mkuu muda wake wa kumpuzika ulivyofika
aliwaacha marubani wasaidizi na kuwapa onyo kuwa karibu wataingia eneo lenye mawimbi (turbulence), dakika 3 baadae baada ya Rubani mkuu kwenda kumpuzika ndipo kizaazaa kilipoanza wakati ndege ilipokabiliana na hali ya barafu na kuanza kujaa kwenye air speed tube (hizi ni tube
zilizopo nje ya ndege chini ya mabawa ambazo kazi yake ni kupima kasi ya upepo) baada ya kitendo hiki kutokea, ruban alikata kona ndogo kuelekea kushoto na akapunguza speed kama sheria inavyotaka kama utakuwa unaingia kwenye turbulence, mfumo wa kuzuia barafu kujitengeneza
ukawashwa kufikia 02:10:05 UTC mfumo wa ndege kujiendesha yenyewe ukaacha kufanya kazi hii labda ilitokana, na zile tube za kupima upepo kujaa barafu na kutoweza kupima tena kasi ya upepo na hapa ndege ilitoka kwenye sheria ya kawaida (normal law) na kuingia kwenye
sheria mbadala(Alternative law) mfumo wa uendeshaji wa ndege wa automatiki ukaacha kufanya kazi sekunde 3 baadae. Bonin akitumia mkono wa gia ya kushoto akasema " I have the controls" akiwa anamaanisha naimiliki ndege sasa akaanza kuendesha ndege. Ieleweke auto pilot
inasaidia sana kuzuia makosa ya aina yoyote ambayo Rubani angeweza kufanya kimakosa au kimakusudi lakini Autopilot ikiondoka hakuna chochote cha kumsaidia Rubani kuepusha ajali na makosa ya kibinadamu hiki ndo kiini cha ajali hii, baada ya Autopilot kuondoka ndege
ikaanza kwenda kulia Bonin akairudisha ndege kushoto, matokeo mabaya ya kuondoka kwa Autopilot ndege inakuwa haitulii mara iende kushoto mara iende kulia ktk harakati za kuiweka sawa Bonin ndege ikienda kushoto akawa inairudisha kulia, lakini cha kushangaza kwa haraka
katika harakati hizo akavuta mkono wa gia nyuma na kuifanya pua ya ndege kuangalia hewani hili tukio lilikuwa la kushangaza sana na hapo hapo king'ora cha ndege kuwa Stalled ( stall warning) kikaanza kulia mara 2 kutokana na pembe ya shambulio (angle of attack) kuwa juu sana na
isiyovumilika na hapa ndege ikaonyesha speed ya upepo kushuka kwa kasi ikiwa na maana ndege ilianza kupaa pua ikiwa juu na mkia ukiwa chini, kutokana na hali hiyo pembe ya shambulio (angle of attack ikaongezeka na ndege ikaanza kupaaa juu zaidi hadi kupitiliza kiwango
kinachoruhusiwa cha FL 350, wakati Rubani anapata umiliki wa ndege tena ndege ilikuwa inapaa kwa speed ya km 130km/h wakati ndege zinatakiwa kupaa kwa speed isiyozidi km 55km/h

Kufikia 02:11:10 UTC ndege ilikuwa imepaa pua jua hadi kufikia mita 12,000 kutoka usawa wa bahari
wakati huo pembe ya shambulio ikiwa 16 (kumbuka 0° ni kwenye mstari mnyoofu, nikimaanisha ndege iko level hapo ndipo sifuri inapoanzia kwa maana hiyo ndege ilikuwa imepaa nyuzi 16 kutoka level iliyotakiwa iwe na kuongeza angle of attack kwa nyuzi 16 ilikuwa kama vile ndege
ilikuwa ndo inapaa kutoka uwanjani (take off) wakati ndege inazidi kupanda nyuzi zikawa zinazidi kuongezeka hadi kufikia 40° na hapa ndege ikawa pua juu na mkia chini kama kitendo kile kinachoonekana wakati ndege ikiwa inapaa (takeoff) tatizo kubwa wakati Autopilot inapojizima
ndege haiwezi kuzuia stall kwani Computer ndani ya ndege kama ingekuwa inafanya kazi ingezuia kitendo hicho kutokea, Madhara ya kitendo hicho hufanya ndege kapoteza uwezo wa kuelea na ndege inakuwa Stalled, baada ya hili kutokea Bonin akapiga kelele akisema (Expletive) 'siwezi
kuimiliki ndege tena" na baada ya sekunde 2 akasema siwezi kuicontrol ndege kabisa Rubani wa pili akasema "Control to the left" akimaanisha yeye ataiendesha kwa maana alikuwa amekaa kushoto (kumbuka muda wote hii kasheshe inaendelea rubani alikuwa bado kalala), basi ruban Robert
akaanza kuindesha kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuishusha pua na kupunguza angle of attack, wakati akipeleka mkono wa gia mbele ili ishushe pua chini bwana Bonin alikuwa bado kashikilia mkono wa gia chini (hapa ilikuwa kama mmoja anaweka drive kwenye gari mwengine
anaweka rivasi kwa maelezo rahisi) the inputs Cancelled each other ilikuwa kama kujumlisha moja na kutoa moja kwa wakati mmoja hali inabaki kama ilivyokuwa. King'ora cha kueleza maingizo ya maagizo mawili kwa wakati mmoja (dual inputs) kikatoa sauti ya kuwaonya. Na wakati
huo Rubani Mkuu akaingia kuona hali ilivyo akawauliza ni nini kinatokea?? Nini mnafanya? Angle of attack ilikuwa kali sana na injini za ndege zilikuwa zinafanya kazi kwa 100% kwa kipindi hiki kingora cha stall kikanyamaza, na vitu vingi vikaacha kufanya kazi kwa sababu angle of
angle of attack ilikuwa kali sana pua juu mkia chini ikaanza kushuka, baadae kidogo kama sekunde 20 Rubani alifanikiwa kuishusha angle of attack na air speed ikaanza kufanya kazi na kingora cha stall kikaanza tena kulia na kunyamaza baadae pua iliposhuka kidogo chini lakini
haikupungua chini ya nyuzi 35 (35° angle of attack) mpaka ilipoanguka baharini mkia chini pua juu (nose up) maswali yanakuja kwa nini hii hali ilitokea kwa nini Bonin alikuwa akiipandisha ndege pua juu ikiwa wazi anajua madhara yake? Alipatwa na nini? Hadi afanye hivyo? Kosa
liloua abiria wote na mke wake akiwemo??

Msako wa ndege na Abiria
Ndege hii ilipasa kupita katika anga la Brazil na Senegal 02:20 UTC June 1 halafu iingie kwenye anga la Cape Verde saa 03;45 UTC lakini muda mfupi saa 4:00 UTC ndege haikupatikana tena kwenye mawasiliano,
kila jaribio la kuwasiliana na hii ndege lilishindikana. Msako wa kuitafuta AF 447 ukaanza kutokea pande zote za bahari ya Atlantic jeshi la Brazil kwa kutumia ndege wakaanzia Archipelago ya Fernando de Noronha wakati Ufaransa wenyewe wakitumia ndege za utafutaji wakaanzia Dakar
Senegal wakisaidiwa na ndege maalumu ya utafutaji Casa 235, kutoka spain. Pia jeshi la majini la Amerika likatoa ndege aina ya Lockheed Martin P-3 Orion ndege yenye uwezo kupambana na mabomu ya nyambizi(anti-submarine Warfare na ndege maalumu kwa utafutaji (patrol aircraft)
Kufikia jioni siku ya tarehe 1 june baada ya kuendesha msako mkubwa viongozi wa shirika la ndege na serikali wakahisi ndege itakuwa imepotea na hakuna aliyepona
June 2 jeshi la Brazil saa 15:20 UTC liliona kipande cha mabaki ya ndege kikielea baharini
Kikiwa na dalili ya mafuta ya ndege umbali wa km 5 kaskazini mashariki mwa Fernando de Noronha mabaki hayo pia yalioneka na kiti cha ndege kilichokuwa kinaelea ambapo baadae walibahini kuwa yalikuwa ni mabaki ya ndege ya AF 447 .June 3 meli tano za utafutaji kutoka
Brazil ziliwasili sehemu ambapo mabaki ya ndege yalioneka na kuanza msako wa nguvu wakitoka eneo hilo na kwenda nje ya eneo hilo
June 6, 2009 siku tano baada ya ndege kupotea miili ya wanaume wawili ikapatikana, na kuletwa kwenye ufukwe
wa Caboclo, pia kiti cha ndege, na mfuko wa kubeba mgongoni uliokuwa na kadi ya chanjo na Computer pia sanduku ambalo lilikuwa na kadi ya inayoruhusu kupanda ndege(Boarding pass) ya AF 447 vilipatikana
Kwa ushahidi huu uliopatikana wachunguzi walifikia
maamuzi ya kusema AF 447 ilianguka na kuua watu wote
Baada ya hapo msako ukawa mkubwa uliohusisha vyombo vingi vyenye takenolojia kubwa katika kujua ndege ilipo na kupata miili yawaliokufa kwenye ajali hiyo

Kufikia tarehe 16 (siku 16 baada ya ajali) miili(maiti) 50 tu
zilipatikana zikiwa zinaelea majini ndege haikuonekana, mwili mmoja kati yao ulikuwa wa rubani mkuu, kufikia Tarehe 26 june utafutaji ulisimama na ndege haikuonekana ingawa walikuwa wamepata vipande vipatavyo 640 lakini hawakuipata ndege yenyewa na hasa Black Box ambayo
ingeweza kueleza chanzo cha ajali

Tarehe 5 Nyambizi (submarine ya Ufaransa iliondoka kwenda kusaidia msako wa kuitafuta AF 447 na hasa kukitafuta kile kibox cha taharifa (Black box) Nyambizi iliwasili eneo la ajali tarehe 10 june, ikiwa na jukumu hilo
moja la kutafuta kibox hicho kwa kutumia tekinolojia ya SONAR( Sonar ni tekinolojia ya nyambizi na meli nyingi kuweza kusikiliza milio chini ya maji au hata siginal za vitu au viumbe chini ya maji kuelewa zaidi hii technology kaangalie movie inaitwa wolf's Call)
Nyambizi hii ilikuwa na uwezo wa kwenda chini ya bahari katika kina chochote pia walikuwa wanasaidiwa na vinasa sauti chini ya maji (underwater audio device) vya Amerika vyenye uwezo kunasa sauti futi 12,000
Hapa ndo the MYSTRIES of MISSING inapoingia kwani hadi
kufikia katikati ya mwezi july 2009 black box haikupatikana Msako wa 3 ulianza Aprili 2 na kumalizika May 26 2010 karibia mwaka mzima baada ya ajali na kibox cha taarifa hakikupatikana
Hii inashangaza sana kwa kutumia utaalamu wote huo bado kwa mwaka mzima black box haikupatikana
Mwaka 2011 ulikuwa mwaka ulioleta matumaini makubwa ambapo utafutaji mwingine ulianza kwa kutumia tekinolojia kali sana mambo mengi ya kushangaza yalioneka katika msako huu wa mwisho. Mimi sitaki kukuharibia Tamthilia hii ebu itafute uone kwa nn hiki kifaa kilikuwa hakipatikani?
Na kama kilipatika? Wapi kilikojificha kwa zaidi ya miaka 3 na walitumia njia gani kukipata?? Na kilisema nini chanzo cha ajali? Utashangaa na kubaki mdomo wazi hutaamini utakachokisikia pia kuna
Kushtakiwa kwa shirika la ndege na watengenezaji wa
Airbus hapa utajiuliza kwa nini walishtakiwa? Hakika utajifunza mengi sio ya kuikosa

Kwa nyuzi(Threads) kama hizi tufuate kwenye page zetu za @cipherdotsv @cipherdotm
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!