My Authors
Read all threads
#UZI
💨 Watu wengi wanaofanikiwa hufanya mambo yao nje ya mifumo rasmi.

✴ Ujinga wa mteja ni fursa kwa mfanyabiashara.

✴ Huyu mtu huakikisha mpinzani wake ni yeye.
#FLowMaTaTa tiririka nazo 👇👇
Twende chap chap
✴ Mafanikio ni matokeo ya chanya ya jambo fulani. Kila mmoja anayatamani hayo matokeo.

✴ Kila mtu hutumia njia zake binafsi, wengine hunakili, huiba mbinu za wenzao ili mraji wapate hayo matokeo.

✴ Watu wengi bado huendelea kufanya mambo yao ndani ya hiyo
Mifumo rasmi.

KWANI MIFUMO RASMI NI IPI?

✴ Hii ni mifumo ambayo watu wote duniani wanaitambua na huitumia kama njia au mazingira ya kuendesha mambo yao.

✴ Mfano; Mwalimu anatakiwa apatiwe mbinu za kufundisha kisha naye akafundishe ndani ya mfumo huo huo.

✴ Atakachokipata
Huko ndio mafanikio yake na hayawezi kuwa zaidi maana tayari amekwisha wekewa mpaka na yeye anaona ni sawa.

✴ Msanii anatakiwa afanye mziki wake katika huo mfumo, na yeye anaamini bila kufanya hivyo hata-trend.

✴ Mfanyabiashara anatakiwa aandae business proposal,
Afanye tafiti kwa wafanyabiashara waliomtangulia ushauri atakaoupata utatosha kutimiza malengo yake.

✴ Kuna watu wanaamini mafanikio n kuwa na nyumba, gari na familia nzuri yenye furaha. Hivyo tu vinatosha.

✴ Tayari hawa watu washajiwekea mpaka hawawezi endelea zaidi ya hapo.
MIFUMO ISIYO RASMI NI IPI?

✴ Hii ni mifumo iliyopo ndani ya uwezo wa mtu binafsi, inaweza ikawa ni ya halali haramu.

✴ Hii mifumo haifundishwi darasani.

✴ Hapa ndio utajua ujinga wa mteja ni fursa kwa mfanyabiashara.
Mtu anayetumia hii mifumo isiyo rasmi huwa ni mwizi mwizi sana.

Ana uwezo wa kukuibia ufahamu wako wa kuelewa kwamba kaiba.

Mambo anayoyafanya utayaona anayafanya kawaida kama wengine wanavyofanya. Ni Uongo
Sizungumzii masuala ya frimasoni maana hata wanaoitwa mafrimasoni wanapamba kusaka pesa kinoma hata kutuzidi sisi.

Unachotakiwa kuamini ni kwamba hakunaga pesa za miujiza. Pesa zipo mikononi mwetu.
TUJIFUNZE KWA HAWA WATU

Mtu mmoja alifungua kituo cha television na redio baada ya kugundua watu wanataka nini.

Hakutangaza Television na Redio yake kama wengine wanavyozitangaza, yeye alivipa brand kubwa na kuvipandisha hadhi vipindi vyake.
Mdogo mdogo, akaona kwanini nisianzishe media nyingine?

Huyu mtu akatoka tena nje ya mfumo rasmi, figisu zikafanyika nyimbo za msanii moja zikapigwa stop na kunyimwa mahojiano.

Taarifa zikatoka yule msanii kafungua media yake, ile media nayo muda
Tuh ikakaa kwenye mstari. Karata zikaonekana zimechangwa vyema.

Muda tena nyimbo za msanii mwingine zikapigwa stop na kunyimwa mahojiano.

✴ Kitambo tuh taarifa zikatoka naye kafungua media yake.

✴ Hizo media zikawa zinabadilishana watangazaji tuh, ili ziwe kwenye
✴ level moja. Huyu mtu akawa ashajihakikishia mpinzani wake kwenye biashara ya aina yake ni yeye.

✴ Na hakuna mtu mwingine atakayeweza kuanzia biashara inayofanana na yake akamzidi.

Kuna huyu msanii naye aliamua kufanya mambo yake nje ya mfumo rasmi.
Wasanii wenzake wakiwa wanasubiria wafanyiwe kila kitu maana wanaamini kazi yao ni kukesha studio tuh.

Yeye akaamua kufanya zaidi ya huo mziki akawa anazunguka na watu wake.

Wapiga picha, wachezaji, wapishi n.k mpaka wasanii wenzake wakaanza kumuona jamaa kama mshamba flani
Maana hata wakiwa kwenye gari wapiga picha wake walikua wanampiga na kuzipachika mitandaoni kwa wingi zaidi.

Mpaka ikafika level ambayo utazani yeye ndiye mwenye tamasha, kumbe kaalikwa tuh.

Anachokiamini ni kwamba yeye ni mtu wa media na anatakiwa aishi humo.
Na kila mwenye uhusiano naye hata kama sio msanii lazima aishi humo.

Matokeo yake watu wa kwao wanaishi humo kwa jina lake, mitandao ashaiteka.

Huyu mtu utamshindaje? Ukitaka kumpa changamoto unaona kabisa sio level zako.

Kama huna speed kaa pembeni.
Kila kitu unachokianzisha kwenye maisha ni utamu kunoga.

Hatujaumbiwa kushindwa, heshimu sana ulichonacho.

Maisha ya mtu hutafsiriwa na vitu vidogo vidogo

Jijue wewe ni nani na unatakiwa ufanye nini.

MWISHO
Written by @njiwaflow
Sponsored by @TOTTechs
FLow MaTaTa ForYou
💨 💨 FLow MaTaTa 💥

Twendeni Instagram Username: @njiwaflow
instagram.com/njiwaflow?r=na…
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Njiwa FLow

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!