BIASHARA MTANDAONI: Kuna njia nyingi za kuanza kufanya biashara mtandaoni (Facebook, Twitter, Instagram). Watu wengi hua tunakwama ni wazo gani la biashara au bidhaa gani niuze itakua na wateja. Nimekuletea UZI huu ukusaidie njia fupi ya kupata bidhaa ya uhakika kuuza #GillMadini
Kuna njia 2 ambazo ntazielezea kwa ufupi. 1. Kama tayari ushafahamu ni bidhaa gani utaenda kuuza mtandaoni 2. Hufahamu bidhaa au huduma gani uchague na kuuza mtandaoni.
Last time niliongelea hili swala lakini leo pia ningependa kutoa msisitizo, Idea za bidhaa za kuuza zipo nyingi sana lakini kuna maeneo haya ukipata bidhaa zake unatoboa faster Afya, Urembo, Passion, Hobby, Interest, Activities, Self Improvement, Wealth and Money, fitness.
Kuna aina mbili ya bidhaa, zile za msimu tu, na zile za muda mrefu. Mfano Sanitizer na Mask. Hizi zilikua zina uzika kipindi cha Corona but kwa sasa hazina tena issue. Hakikisha Bidhaa yako isiwe ya msimu au labda hilo ndio liwe lengo lako
KAMA HUFAHAMU KITU GANI UUZE: STEP 1 Chukua kalamu na karatasi kisha piga mstari katikati kushoto andika title watu ambao nataka kusolve matatizo yao. Kulia andika title bidhaa ambazo zinaweza kutatua tatizo flani, bidhaa kwa watu wenye passion, feeling, emotion na kitu flani.
Anza kuandika Idea mbali mbali ambazo zinakujia kichwani. Kushoto mfano: Watu wenye meno ya Njano, Watu wenye uzito mkubwa, Watu wenye vitambi, Kupunguza uzito kwa wanawake waliotoka kujifungua, Watu wanaotaka kuongeza makalio, Watu wanaofuga paka, Urembo, Ma DJ, Wavuvi etc.
Kulia unaweza andika, Dawa ya kusafisha meno ya njano, Dawa za kupunguza uzito, Chai Ya kupunguza uzito, Dawa ya kupunguza kitambi, Accessories kwa ajili ya mbwa, Tshirt za maDJ, Make up za watu weusi, Nguo za watu wafupi, Accesories kwa ajili ya fans wa ManU, accesories za simu.
Kwenye hio hatua hapo juu andika idea nyingi unavyoweza. Kisha chagua top 10. Jinsi ya kuchuja top 10. Kuna vigezo vichache vya kuangalia amabavyo baadhi nimetaja hapo juu. 1. Lazima Product utakayochagua iwe na high demand (Kama hio product inasolve tatizo kubwa la watu wengi)
2. Low availability. Hakikisha product utakayo chagua haipatikani kwa urahisi rahisi, mfano unachagua product ya kuuza ambayo mteja anaweza kununua kwa mangi mtaani au nikiingia insta page kama 300 zinauza hio product. Unaweza kuiuza lakini inabidi uwe na mkakati madhubuti.
3. Wow Factor and High Pasived Value. Product iwe na mvuto hata mtu akiithaminisha or akifikiria kua nayo watu watakaomuona watamsifia nk. Kiujumla iwe unique kwa aina flani. Iweze ku grab attention
4. Ukiiuza upate faida zaidi ya x 3. Watu wengi hua tunajisahau hapa. Kuna vitu vingi vinachangia kula faida yako mfano matangazo pamoja na operations mbali mbali. Kwa hio bidhaa ambayo itakupa faida zaidi ya mara 3 ni nzuri kuuza.
5. Bidhaa unazotaka kuuza utanunua wapi. Utaagiza nje ya nchi au utanunua hapa hapa nchini. Ninashauri uagize nje hapo competition itakua ndogo na choice ya product ni kubwa sana. Japo hata hapa nchini kuna bidhaa nzuri zinauzwa kkoo na ukija mtandaoni huzikuti
Kama ni hapa nchini unaweza nunua bidhaa zako pia kwenye Instagram shops, Facebook Groups, Whatsapp Groups, nk. Cha muhimu tu ni kwamba sehemu ambazo unapata hizo bidhaa iwe ya uhakika. Na ina vigezo vilivyotajwa hapo juu.
Kwa hio bidhaa utakazo chagua inabidi iwe na vigezo zaidi ya viwili. Ikiwa navyote basi utakua umepiga mgodi. Baada ya kuchuja hio top 10 yako nini kitafuata..
STEP 2: Hapa tutafanya utafiti kufahamu je katika zile idea 10 kuna wateja au hakuna wateja. Kuna njia nyingi za kufanya huu utafiti. Kwa sababu tushajua ni watu gani na ni bidhaa gani tunataka kuuza hapo tutakua tunaangalia wateja na wauzaji wana intaract vipi na hizo products.
Tukianza na Instagram, facebook, whatsapp x facebook groups tutaangalia watu wangapi wanauza bidhaa hizi, wanauzaje, wateja waliopo wanasemaje? Unaweza kwenda mtandao kama AliExpress au Kikuu ukaangalia kuna bidhaa ngapi za aina hio, watu wangapi wamenunua, bei ipoje, nk.
Zoezi la kutafuta top 10 hapo juu linasaidia ukiwa unachagua product ya kuuza kwa sababu ukiingia instagram kwa mfano au AliExpress au Kikuu kuna products nyingi sana za kuuza unaweza ukachanganyikiwa. Lakini ukishajua umeenda kutafuta bidhaa za aina gani itakusaidia ku focus
Since tushajua ni product gani tunataka kuuza na ni kwa watu gani unaweza fanya utafiti kwa kuwauliza wateja wako wanataka nini. Mfano tunataka kuuza dawa za kupunguza vitambi unaweza tengeneza questionare ukawapa watu wenye vitambi ukapata kujua product gani ya kuwauzia
STEP 3: Tuseme kwenye utafiti wetu bidhaa ambayo tumeona inahitajika ni Chai inayoweza kupunguza unene, Mafuta ya kuongeza makalio, Vidonge vya kuondoa hangover, GPS collar kwa ajili ya paka, nk. Na tushajua hizi product zinapatikana wapi na zinauzwaje. (angalia kipengele 5 juu)
Kabla ya kuwekeza pesa zetu nyingi na kuagiza mzigo tutafanya kitu cha mwisho. Coz kumbuka tumeona kwa watu wengine kama zina demand inabidi na sisi tuwe ne proof kabla ya kukurupuka na kupoteza hela.
Tengeneza account ya Instagram na Facebook na Twitter maalum kwa kutestia product zako kabla ya kuziagiza. Kuna aina 3 ya hizi accounts 1. General Store with Generic Products, Generic Store With one product category, niche store with one product na kila moja ina effect mauzo yako
General Store with Generic Products. Hii ni nzuri kama huna malengo ya muda mrefu na hujajua bado ni bidhaa gani ina wateja na inatoka so tunatumia hii kutestia mpaka tupate bidhaa inayotoka. Hii inakua account moja lakini kuna product category mbali mbali
Mfano: Unaweza jina KariakooMart ndani yake hata ukiweka zile products zako 10 ulizo zichagua pale mwanzo na kutest moja moja. Humu ndio utakuta products za wanawake, watoto, wanyama, nk Ukipata bidhaa moja ambayo inauzika basi unaifungulia kurasa yake maalum.
Generic Store With one product category. Hii ni unakua na category moja tu ya product labda women fashion. Unaweza iita bongofashion. Humu tutatest kuuza product za wanawake, accessories, viatu, anything women related in fashion
Niche Store. Hii ni store ambayo unauza product aina moja tu. Mfano majani ya chai ya kupunguza unene. Ni product hio tu tutauza huku. Hii mara nyingi hua inatengenezwa ukisha kua umefahamu ni products gani inatoka kati ya zile kumi nilizotest hapo juu
Kumbuka account zote hizo juu lazima zizingatie misingi yote ya branding na online content creation kupata good results ya test zako. So kwa sababu ni test account ndio ulipue lipue tu.
Kiufupi mpaka kufikia hapa inabidi uwe unafahamu kidogo kuhusu social media marketing. Jinsi ya kutengeneza account zako, Kutengeneza matangazo ya instagram na facebook, kuandika caption zinazovutia na kutengeneza post zinazovutia. Angalia brand kubwa zinzvyofanya be inspired
Au shortcut unaweza tumia kama step 3 kwako itakua ngumu Ingia instagram au facebook au kikuu au AliExpress popote ambapo utakua unanunua zile bidhaa ulizochagua. Chagua bidhaa moja download picha zake. Angalia bei ambayo hio bidhaa inauzwa. Tengeneza bei yako
Then Sambaza hizo picha kwa wateja ambao ushafahamu wana tatizo ambalo hio product yako inatatua mfano dawa ya kuondoa vitambi. Unaweza sambaza kwa whatsapp groups zako, facebook groups, etc. Sishauri uwatumie ndugu na rafiki zako coz huwezi pata jibu sahihi la test yako.
Kumbuka ili uweze kufanikiwa katika biashara huhitaji kua na products kibaoooo. Unaweza kua na product moja tu na hio hio ikakutoa kimaisha. Mfano una product ukiuza faida ni 30,000 ukiziuza hizi products kwa mwezi 1000 tu tutakua wapi kwa mwaka?
Njia rahisi kabisa kuliko zote ni kutumia matangazo ya instagram na facebook. Ukiwa na budget ya 100,000 unaweza test produts 5 mpaka 10. Na ukafahamu kama inalipa au hailipi kabla hujaagiza. Pia unaweza tumia influencers kutest ideas zako.
Lets say ukishafungua page zako mfano General Store. Post products zako zote ambazo unataka kuzitest zikiwa na bei zake ambazo umepagna kuuza. Kisha lipia tangazo $1 kwa kila product kwa siku 2, Tangazo lako lilenge ile audience ambayo product yako ina solve.
Ukiwa unafanya test uwe tayari ushaweka KPI zako. Mfano if I test product x kwa siku 3 na sijapata call yoyote then hio product itakua haina demand. Hizi metrics zipo complicated but moja kuu ni mauzo kama umeweka tangazo lako vizuri na hakuna call ya mauzo achana na hio product.
Test yako ili ziwe successiful vitu vingi vitachangia. Baadhi nimeelezea juu. But hakikisha page zako ziwe kwenye hali nzuri. Jaribu kutengeneza brand, captions, targeting zako ziwe on point. Maana unaweza ona product haina demand kumbe mteja akija kwa page yako anakosa trust
Wakati unafanya product test zako wateja watakua wanakupigia simu wakitaka hizo products mfano kama product zipo hapa hapa Tanzania na tayari unaaminika unaweza kuchuka cash ukanunua hio product ukamtumia mteja. Kama bado trust haipo unaweza nunua kwa hela yako
Pia kama bidhaa haipo Tanzania labda mpaka uagize AliExpress unaweza mwambia mteja bidhaa hio imeisha kwa sasa ila kuna mzigo unakuja kama akilipia mapema atapata 10% discount. Kuna njia nyingi za kufanya but you got the idea
STEP 4: Now ushajua produt x inatoka na ina wateja hapo kazi kwako ku scale hio product yako. Hapa namaanisha kama kuifungulia niche store yake (Instagram Page yake) pamoja na kuongeza matangazo na branding iwe fresh.
TIP: Kwa wale ambao tayari wanafanya biashara mtandaoni. Kama tayari umweka tangazo lako na linakuletea wateja. Mfano tangazo langu lilikua $5 kwa siku. Nakushauri uianzishe tengazo lingine. Ongeza budget yako ya siku kutoka $5 to $10 to $20. etc kwenye tangazo lile lile
NJIA NYINGINE: KAMA USHAFAHAMU PRODUCT GANI INA DEMAND: Tumia muda wako tembelea Facebook, Instagram, Ali Express, KiKuu angalia product zenye orders nyingi kuliko zingine kwenye categories mbali mbali then test only those products. Tumia test process hapo juu
Gharama yake: Well kila kitu inaweza kua FREE kabisa but itachukua muda. But ukiwa na 50,000 - 500,000 utaifanya kwa raha na faster sana. Katika thread hii kuna tips nyingi unaweza zitumia katika sehemu zingine pia. LIKE, RETWEET.
Hizi ni njia zangu tu maoni binafsi yanakaribishwa pia. Kama una swali you can ask nitakua najibu navyoweza. Hii Thread sija proff read mnisamehe kwa typing erors zozote. THE END

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Gillsant 6.0

Gillsant 6.0 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @GillsaInt

May 1, 2021
𝙉𝙅𝙄𝘼 9 𝘽𝙊𝙍𝘼 𝙕𝙄𝙏𝘼𝙆𝘼𝙕𝙊𝙆𝙐𝙁𝘼𝙉𝙔𝘼 𝙐𝘼𝙉𝙕𝙀 𝙅𝘼𝙈𝘽𝙊 𝙉𝘼 𝙐𝙁𝘼𝙉𝙄𝙆𝙄𝙒𝙀 𝙆𝘼𝙏𝙄𝙆𝘼 𝙈𝘼𝙄𝙎𝙃𝘼 𝙔𝘼𝙆𝙊. #𝙀𝙡𝙞𝙢𝙞𝙠𝙖𝙒𝙞𝙠𝙞𝙚𝙣𝙙𝙞 - 𝙏𝙝𝙧𝙚𝙖𝙙 (𝙐𝙕𝙄)
Kila siku tunajishughulisha ili tutimize malengo yetu. Katika maisha kuna watu ambao wanafanikiwa katika mambo yao na kuna watu ambao hawafanikiwi. Tunajishughulisha kila siku kuyatimiza malengo hayo. Malengo yanaweza yakawa ni maswala ya Elimu, Kazi, Biashara, Uongozi nk.
Tafiti zinaonyesha ni watu wachache sana wanaotimiza malengo yao duniani kote, inawezekana ukawa miongoni mwa watu ambao hawajafanikiwa kutimiza malengo yao. Zifuatazo ni njia 9 bora zitakazokufanya ufanikiwe katika maisha yako.
Read 17 tweets
Sep 26, 2020
𝑰𝑳𝑰 𝑾𝑨𝒁𝑶 𝑳𝑨𝑲𝑶 𝑳𝑨 𝑩𝑰𝑨𝑺𝑯𝑨𝑹𝑨 𝑳𝑰𝑭𝑨𝑵𝑰𝑲𝑰𝑾𝑬 𝑽𝑰𝑻𝑼 𝑽𝒀𝑨 𝑲𝑼𝒁𝑰𝑵𝑮𝑨𝑻𝑰𝑨: 𝑼𝒁𝑰 𝑷𝑨𝑹𝑻 2
Vitu vingine vya kuzingatia wakati unakuja na wazo lako la biashara.
Yes unaweza fungua biashara kutokana na kitu unachokijua mfano Kinyozi ukafungua saluni yako au mpishi ukafungua restaurant yako. Kumbuka kwakua wewe ni mpishi mzuri sio kwamba utafahamu jinisi ya kuendesha restaurant yako vizuri. Kuna mambo mengi ya kuzingatia
Kama unataka biashara endelevu make sure huduma au bidhaa unayouza wateja wako watarudi kwako tena. Inabidi uwe na bidhaa au huduma ambayo wateja wataendelea kununua kwa muda mrefu. Mfano ni bora uwe na kampuni ya kusafisha swimming pool kuliko kua na kampuni ya ujenzi wa pool.
Read 19 tweets
Sep 26, 2020
𝑱𝑰𝑵𝑺𝑰 𝒀𝑨 𝑲𝑼𝑱𝑨 𝑵𝑨 𝑾𝑨𝒁𝑶 𝒁𝑼𝑹𝑰 𝑳𝑨 𝑩𝑰𝑨𝑺𝑯𝑨𝑹𝑨. Ili kuweza kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kuwa na wazo zuri la biashara. Je unajua jinsi ya kupata wazo hilo zuri la biashara? 𝑼𝒁𝑰, 𝑷𝑨𝑹𝑻 1
Watu wengi wamekuwa wakiniomba ushauri ni wazo gani zuri la biashara ambalo linaweza kuwapatia faida na mafanikio. Ukweli ni kwamba wazo ambalo ni bora kwa mtu fulani linaweza lisiwe bora kwako.
Moja ya sababu zinazofanya biashara nyingi kufa au kutokuendelea ni kuiga, yaani mtu akianza biashara leo baada ya muda unakuta watu wengine wameiga biashara ile ile, wanaifanya eneo lile lile na kwa mbinu zile zile. Hii ni njia rahisi sana ya kushindwa kwenye biashara.
Read 22 tweets
Aug 29, 2020
JINSI YA KUANZISHA BIASHARA UKIWA UMEAJIRIWA: Biashara yoyote iwe mpya au ya zamani ina changamoto zake especially kwenye mazingira yetu. 50% Ya biashara zote ndogo zinakufa katika mwaka wake wa kwanza kuanzishwa. UZI #ElimikaWikiendi
Mtandao wa Investopedia ulitoa sababu ya biashara ndogo kufa, 1. Mtaji Mdogo, 2. Uendeshaji Mbovu, 3. Mpangilio Mbovu wa Biashara na Bidhaa yako au huduma yako haihitajiki sokoni (Hakuna wateja wanahitaji bidhaa zako). Pamoja na sababu zingine nyingi.
Sasa kama tulivyoona hapo juu changamoto ni nyingi. Kabla ya kufikiria kuanzisha biashara ukiwa umeajiriwa inabidi ujipange. Kitu kimoja kikubwa ambacho Ajira itakusaidia kipindi unataka kuanzisha biashara ni MTAJI pamoja na muda wa kujipanga kabla ya kuanza biashara full time.
Read 16 tweets
Aug 8, 2020
NJIA (Business Models) 10 ZA KUPATA PESA ONLINE. UZI Nimeshindwa kupata kiswahili cha Business Model (Mtanisaidia) Kwa uzoefu wangu watu wengi wanapotaka kuanza kufanya biashara Online or Offline. Hua wanafikiria njia moja au Mbili. #GillMadini
Kununua Bidhaa kutoka sehemu fulani au Kutengeneza hio bidhaa na kuiuza dukani or ikizidi sana mtandaoni kupitia Instagram au Facebook wachache kwenye website. Leo nimewaletea Business Models zingine 10. Ambazo unaweza kutumia kupiga hela.
Tukirejea kwenye UZI nilioandika mara ya mwisho. Kama bado haujausoma tafadhali usome Halafu rudi kumalizia Uzi huu. Leo nitatoa mfano wa wazo moja la biashara mbalo unaweza tumia njia zaidi ya 10 (10 Business Models) tofauti kuweza kufanikisha kujipatia pesa.
Read 24 tweets
Jul 11, 2020
"Namna Sahihi ya kuanzisha na kuendeleza biashara kwa mtaji mdogo mtandaoni." Nimejaribu kila naloweza kuandika points kwa kifupi ili hii topic iweze kueleweka lakini imeshindikana. Hivyo basi.. UZI (THREAD) #ElimikaWikiendi
Kutokana na uzoefu wangu biashara nyingi za mtandaoni hazifaikiwi kwa sababu zinaendeshwa kwa mazoea au kwa kubahatisha. Ukifuata mfumo wa jinsi ya kuanzisha biashara kwa usahihi huwezi kulalamika hakuna wateja au bidhaa hainunuliwi.
Hizi ni baadhi ya steps unatakiwa kuzifuta CUSTOMER RESEARCH, PRODUCT RESEARCH, MARKET RESEARCH, FINANCIALS, OPERATIONS, BRANDING, CONTENT CREATION (MARKETING), COPYWRITING, ONLINE ADVERTS, ONLINE SALES, ACCOUNT GROWTH, ALGORITHM, CUSTOMER CARE, BUSINESS FORMALIZATION
Read 21 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(