My Authors
Read all threads
FAHAMU KUHUSU JAPHET KIRILO

#Uzi

✴️Mtanzania wa Kwanza kuachia Ubunge kisa mashamba ya kahawa 1990's

✴️Akiwa 31yrs alikwenda mpk UN kutetea wakulima
✴️Huyu ndiye alisomesha Wameru wengi akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Gen. SARAKIKYA pamoja na Babaake @CarolNdosi👇
Kwanz kabisa ktk HISTORIA ya Ukombozi wa Tanganyika kutoka kwa Mkoloni Haiwezi KUMTENGA Kirilo Japhet

Tukiwa tunaendelea hapo juu Pichani ni Japhet Kirilo (kulia), akizungumza na mmoja wa viongozi wa serikali ya kikoloni Ralph Bunche..

Tuendeleeee👇👇
Katika historia kuna matukio mbalimbali yaliyofanyika kwenye taifa hili. Leo tumwangalie Kirilo Japhet ambaye alitoka katika Mkoa wa Meru (Arusha ya sasa). Historia tunayoandika hapa leo ni kutokana na andiko la kitafiti la Dk. Simeon Mesaki wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
Andiko la Dk. Mesaki, ‘Recapping the Meru Land Case, Tanzania’ lilichapishwa katika Jarida la Global Journal of Human Social Science Economics, Vol. 13 la mwaka 2013.
Katika jarida hilo ndipo mwanazuoni huyo anatueleza namna gani ni muhimu kumkumbuka Kirilo Japhet.
Dk Mesaki anaeleza mgogoro wa ardhi uliowakumba wananchi dhidi ya uliokuwa utawala wa Ujerumani na baadaye Uingereza kama msimamizi wa Tanganyika kwa niaba ya Umoja wa Mataifa (UNO)
Anasema, mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Meru dhidi ya wakoloni ulisababisha zaidi ya watu 25 kutiwa mbaroni mwaka 1938.Wakati ukitafutwa utatatuzi wa suala hilo ndipo jina la Kirilo Japhet lilipoibuka.Kisha suala la utatuzi lilifikishwa kwenye Baraza Kuu ili kutoa suluhisho
Kirilo alikuwa mwakilishi wa wakulima wa Meru katika mgogoro huo wa ardhi. Kipindi hicho Tanganyika ilikuwa inasimamiwa na Uingereza. Umoja wa Mataifa uliipatia Uingereza dhamana ya kuisimamia Tanganyika mara baada ya Ujerumani kushindwa vita.
Kutokana na wananchi kuwa na mgogoro na serikali ya usimamizi (Uingereza) kama ilivyoanzia enzi za Ujerumani, basi wakulima waliamua kutuma mwakilishi wao kwenda Umoja wa Mataifa kulalamikia jambo hilo.
Kirilo alikuwa Mtanganyika wa kwanza kwenda Umoja wa Mataifa na kuwakilisha wananchi wa Meru. Historia inatueleza kuwa na Japhet Kirilo aliweza kuhutubia Umoja Mataifa na kuelezea kile kilichokuwa kikiendelea Meru na wakoloni kwa nyakati tofauti huku akisaidiwa na Wakili Seaton.
Kirilo alikwenda Umoja wa Maifa mwaka 1952 kwa niaba ya Wameru. Miongoni mwa mafanikio makubwa yaliyojitokeza kwenye safari hiyo ni kuongezeka msukumo wa madai ya uhuru kwa kuunganisha jitihada za viongozi wa kikabila na wale walioanza mchakato wa kuunda TANU.
Katika sehemu ya utetezi wake kuhusu wakulima hao pamoja na kusisitiza mapambano ya uhuru wa Tanganyika.
Japhet Kirilo alifanya jitihada kubwa kisiasa hapa nchini na tangu wakati wa mgogoro wa ardhi wakati wa uongozi wa Mangi Sante kule Meru.
Katika kipindi hicho inaelezwa kuwa kulikuwa na wasomi wengi katika utawala huo. Baada ya kutoa hotuba yake Umoja wa Mataifa, Japhet Kirilo alimpa mwaliko Anton Nelson (wa Freemen of Meru) ili aje Meru kumsaidia kuwafundisha wananchi wake katika masuala ya elimu na kadhalika.
Mwaka 1954 kabla ya Tume ya Umoja wa Mataifa kuitembelea Tanganyika, Mwalimu Nyerere na S. Kandoro walimuomba Japhet Kirilo kufanya ziara kote nchini kwa mwamvuli wa TANU ili kuwaelezea matatizo ya ardhi yaliyokuwa yakiikabili Meru kwa wakati huo.
@joblessforsure @LitoMidred @getrudadotto @SocialM14131092 @officialMjukuu Katika kipindi hicho TANU ilikuwa imefungiwa kufanya shughuli za kisiasa na Uingereza.

Japhet Kirilo alizaliwa mwaka 1921 na kufariki dunia mwaka 1997.

Jina lake kamili ni Kirilo Japhet Ayo Nkira, alizaliwa katika kijiji cha Poli, Nkoaranga ambapo sasa ni wilaya ya Arumeru.
Baba yake aliitwa Nganayo au maarufu Ngura Ayo, ambaye alikuwa kiongozi wa jadi kijijini hapo na wakulima wa zao la kahawa wa Meru.

Hayati Japhet Kirilo alifariki dunia Mei 30, 1997, na kumwacha mkewe, Ndeleto Kirilo. Aliacha watoto sita, ambao kati yao wanne ni wasichana.
Katika watoto wake sita, wawili wa kiume ni Zakaria Kirilo na Jefferson Kirilo hawa wote wanaishi Marekani. Mwingine ninayemfaham ni Anna Kirilo ni mtoto wake wa kike ambaye anafanya kazi katika Hospitali ya Mount Meru Arusha.
Katika maisha yake Kirilo alifanikiwa kupata Elimu yake kwa miaka nane na alisomea Taalum ya Ualimu katika Chuo cha Ualimu cha Marangu mkoani Kilimanjaro. Baadaye alifanya kazi serikalini akianzia Mpwapwa, mkoani Dodoma na kisha Arusha.
Wakati alipoteuliwa kuwa mwakilishi wa wakulima waliokuwa kwenye mgogoro mjini Meru, Kirilo alikuwa na miaka 31. Pia alikuwa mashuhuri wakati akiongoza Tawi la chama cha TAA akiwa Katibu Mkuu kutoka Kanda ya Kaskazini.
Kirilo alikuwa shupavu katika ujenzi wa hoja katika vikao mbalimbali vya Baraza vya wilaya kuanzia mwaka 1950 na kuwa alama bora kwa wananchi wa Meru.
Katika kipindi hicho TANU ilikuwa imefungiwa kufanya shughuli za kisiasa na utawala wa mkoloni wa Kiingereza.
Babaake Ngura Ayo licha ya kuwa kiongozi wa kijadi, pia alikuwa Mweka Hazina wa kanisa huko Meru.
Mzee Ngura alikuwa mkulima wa kwanza kununua #Trekta mwaka 1935 na kuwa mkulima wa kisasa.
Dk. Mesaki anamwelezea Kirilo km miongoni mwa wapigania uhuru wasiokuwa na woga kpnd hicho
Alifanya kila njia kuhakikisha waafrika wenzake wanapata haki zao za msingi.

Hata hivyo, kama walivyo viongozi wowote, Kirilo Japhet hakukosa tuhuma kutoka kwa wakulima wenzake na wananchi wa Meru.
Mara baada ya kuwasili Meru akitokea Marekani, Kirilo Japhet alituhumiwa kutafuna fedha za misaada za ushirika. Jambo jingine baya lililowahi kumtokea ni kitendo cha kumiliki eneo la ukubwa wa Ekari 60 za ardhi na kumfanya Kirilo kuwa mkulima wa kiwango bora wakati huo.
Ardhi hiyo ilimsababishia matatizo makubwa na kugharimu nafasi yake ya uongozi ndani ya chama na ubunge kwa madai alikuwa Bepari (mnyonyaji).

“Nilikuwa mbunge kati ya mwaka 1971 na 1974. Nilituhumiwa kuwa na fedha nyingi, na nililazimishwa kuuza mashamba yangu,
"Ikiwa ni sharti la kuendelea na ubunge. Lakini nilikataa sharti hilo kutokana na kiasi na faida za kulima kahawa kwa wakulima wa Meru kilikuwa kikubwa. Hivyo nilichagua kuwa mwakilishi wa wakulima wa kahawa katika maeneo mbalimbali Afrika,”
Kirilo alikuwa mstari wa mbele kuendesha harambee ili kupata fedha za kuwasomesha nje ya nchi vijana wa Meru. Miongoni mwa walionufaika na harambee hizo ni Peter Pallangyo, Eliawira Ndossi, Babaake @CarolNdosi
Meja Moses Jonas Ndosi, Mathias Kaaya, Mike Urio, Ndewira Kitomari.
Meja Ndosi aliwahi kuwa Mkuu wa Kikosi cha Vifaru Jeshini (1970's) alifariki 2005 na mwingine ni Jenerali SARAKIKYA naye alisomeshwa na Kirilo ktk Chuo cha Kijeshi Sundurst Uingereza na baada ya mapinduzi ya kijeshi ya April 20, 1964 Mwl.Nyerere alimteua kuwa Mkuu wa Majeshi
Katika Lile sakata la Ardhi, Japhet Kirilo alichagua kuishi na wakulima wenzake kuliko sharti la kuuza mashamba yake (AMHT3, 1988). Kwa utawala wa kikoloni alikuwa Raia mkorofi na Mwanasiasa hatari.
Katika ujenzi wa TANU.

Japhet Kirilo alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa TANU katika Jimbo la Kaskazini alifanya kazi kubwa ya mapambano ya Uhuru na wakati wa shughuli zake aliwahi kutembelea maeneo mbalimbali hapa nchini chini ya mwamvuli wa TANU.
Baada ya kutoa hotuba yake Umoja wa Mataifa alibaki nchini Marekani kwa mwaka nzima akijifunza mambo mbalimbali, na alifanikiwa kukusanya michango ya kifedha kutoka nje ya nchi na kujenga shule za msingi, sekondari na vyuo vya ufundi kwa wakazi wa Meru.
Kirilo pia alishiriki kupanda mlima Kilimanjaro akiwa na Jenerali Mirisho Sarakikya, mtu ambaye amevunja rekodi ya kupanda Mlima huo kuliko Mtanzania yeyote.

Huyu ni miongoni mwa viongozi wa Taifa hili ambao wanataka kusahaulika na ktk mitaala ya Elimu hawajatajwa.

#END...!!🙏
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with JAPHET MATARRA

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!