AN OPEN LETTER TO YOU BROTHER πŸ“œ

Habari za siku kaka , imekua muda mrefu sana bila mawasiliano nadhani ni vile changamoto za maisha zinatuweka mbali lakini kwa kuwa tupo chini ya anga moja natumai ni suala la muda mimi na wewe kukutana
#Thread
Matumaini yangu umzima sana hasa kiafya na harakati zako za kila siku ,ningeweza kukutumia ujumbe mfupi wa maandishi ( sms) au kukupigia simu lakini nikaona kama barua kidogo ingebeba ujumbe na hisia zote zaidi ingekupa muda wa kuitafakari tofauti na ilivo meseji ambapo ingefutwa
Dear brother, nia na dhumuni la barua hii ni kukuuliza kwamba " vipi bado una ari ile ile ya utafutaji? Vipi malengo yako bado yako vile vile? bado una sababu ya kutafuta maisha?
itakua vema kama bado upo yule yule wa zamani aliyekua na malengo mengi sana na molari
Kaka, kama ukihisi kukata tamaa tafadhali kumbuka zile ahadi zote ulizowapa wadogo zako, kumbuka yale maisha bora na mazuri uliyomyahidi mama yako na ukumbuke ile lifestyle nzuri uliyojiahidi utaishi huko mbele . Baada ya kukumbuka hayo nadhani utarudi kwenye mstari na utagundua
kwamba una sababu zaidi ya Million moja za kupambania maisha .
Siko hapa kukufundisha nini cha kufanya au ni vipi unatakiwa kuishi lakini kabla ya kuhonga simu nzuri na vitu vingi vya thamani kumbuka wadogo zako ambao hawana pesa ya Tuition , vitabu na madaftari pia
Mkumbuke baba yako ambaye aliingia madeni ili wewe ufanikishe kila ulilohitaji, zaidi umkumbuke mama yako ambaye yeye alipata madonda ya tumbo kwa kufunga mfululizo na maombi ili wewe mwanae mambo yako ya kunyooke .
Kwa ufupi kaka hauna haja ya kuwaangusha na kutoa tumaini lao
kwako.
Bwana Kaka , ukiwa unaendelea kutafuta umaarufu na kujulikana kwenye mitandao ya kijamii usisahau uhalisia wako . Ukiwa unaendelea kutumia nguvu kubwa kuonekana unapesa na maisha mazuri mbele ya watu wengi usiofahamiana nao mitandaoni usisahau kupambana na
kutajirika katika maisha yako halisi .
Dear brother , nilitamani pia kukukumbusha kuwa wewe ndiyo nyota njema ya kundi kubwa la watu walioko nyuma yako. Usiache kupambania maisha maana anguko lako linaweza kusababisha kundi kubwa kuanguka
Huo mradi wako mdogo ulioamua kuufungua
amini nakwambia sio kitu bure na hautokuacha hivi hivi ni suala la muda wewe kufika mbali . Kitendo cha wewe kuthubutu kujikita huko ni ujasiri mkubwa na sio kila mmoja yupo na ujasiri kama wako huo ndio maana sio kila kijana anafanya kile unachofanya wewe.
Samahani kaka , vipi bado uko na binti yule yule uliekuwa nae zamani? πŸ˜ƒ
Sawa, bado sipo hapa kukufundisha namna ya kuishi lakini ikitokea umempa mimba mtoto watu basi lichukue kama jukumu limeingia kwako wala usipate wazo la kuwakimbia mama na mtoto . Wajali kadri uwezavyo
Inawezekana usimuwaze sana mama mtoto lakini mfikirie yule mtoto katika ukubwa wake wa shule ya msingi pale ambapo walimu watamuagiza aende na baba kwenye kikao cha wazazi. Ataenda na nani? Vipi alimuuliza mama yake kuhusu mahali wewe ulipo ? mama yake atamjibu nini?
kwamba ulikufa? uliwatelekeza ? au uliwakimbia??
Itakua ngumu kiukweli kwa huyo mwanamke , kwako na zaidi kwa mtoto wenu.
Dear brother, nilitamani pia kukukumbusha huyo binti aliyeamua kukupenda bure kwa sasa maana ni sawa na kaamua kuchukua mzigo wake halafu apambane nao
kwa sababu sio kwamba wewe ni bora kuliko wanaume wote Duniani au umewashinda kwa vigezo wote ni yeye tuu kaamua kukubali vile ulivyo , basi mzawadie upendo .
Ndio sikukatazi kuwa na rafiki wengine wengi wa kike lakini tambua mipaka yako ile kuwapost kila siku huko whatsup status
kuwa nao kila mahali, kuonekana unawajali sana wao kuliko yeye kuna point unapoteza na anaweza asiseme lakini unakua unafeli kama mwanaume. Kwanini usimfanye yeye awe ndio best friend wako kuliko kugawana muda na nguvu kwa hao kina dada wengine ambao ni wake za watu wa baadae?
Baba yako anajua kama unalinda wake za watu huko duniani? Tambua nafasi ya marafiki na huyo binti mnyonge aliyekupenda.
Dear brother , nimeandika mengi kwa sababu ilikua muda mrefu hatujaongea ila kiukweli Kata vyote lakini usikate tamaa bado unategemewa, Ona vyote lakini
usione aibu kuitafuta rizki popote ilipo , nusa vyote lakini usinuse madawa ya kulevya ukidhani yatakusaidia kuondoa msongo wa mawazo . Panapo shida ongea na watu maana huko kuna watu wamepitia magumu zaidi yako watakusaidia au watakusogeza kwa watu waliowasaidia
Jipende panapobidi, tunaishi mara moja . Baada ya hustle zako za siku iwe mwisho wa wiki au siku yoyote inayofaa we oga , chana nywele , nukia vizuri , vipesa vyako kwenye wallet, jitoe sehemu nzuri kunywa kula vizuri kuupa mwili pole .
Kaka mwisho wa ubishoo ni majukumu , kuvaa nguo za gharama kuridhisha watu mwisho wake ni kuzivua na kujiuliza utakula nini na utakula wapi .
Wasalaam ndugu yako
@Vet_doctor87
nohtalk.com
#MyMindSpeak

β€’ β€’ β€’

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
γ€€

Keep Current with Noe_Wenc πŸ’Š

Noe_Wenc πŸ’Š Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Vet_doctor87

15 Oct
HAKUSTAHILI KUPITA NJIA NGUMU KIASI KILE
Wakati mwingine dunia inatuweka darasani kujifunza masomo ambayo hatukuwahi kuwaza kujifunza. Pengine hata mitihani ya hayo masomo hatujui itakuja lini
Tabasamu na uchangamfu wake vilificha mengi lakini hakustahili yale #Thread
Unaweza kuchagua marafiki lakini sio jirani maana wewe utajenga hapa ila atakaekuja kujenga pembeni yako hauwezi kumjua ,hivohivo kwenye kupanga chumba. Nilijikuta nimepanga chumba ambapo nyumba ya jirani waliishi familia nzuri na sisiti kusema nilivutiwa nayo kiukweli
Walikua na furaha muda mwingi .Wazazi walikua wa makamo ya miaka 34 na mtoto mdogo wa miaka 10, kutokana na uchangamfu wangu nikajikuta nimekua rafiki na baba wa hiyo familia ambaye alikua ameajiriwa kwenye kampuni moja hapa Mjini . Aliitwa Mr Beda , nilipenda sana kuwa nae hasa
Read 25 tweets
16 Jun
LET MY MIND SPEAK
So, hakuna kizazi bora kama kizazi chenye wingi wa maarifa na vijana wenye kuchangamkia fursa kila inapotokea.
SHORT THREADπŸ‘‡
My brother @veggiesfarmer once said " We are in knowledge economy,what you know is what will differentiate you and accelerate your growth, your growth will highlight your value and your value will elevate your worth.
Imekua muda mrefu nikitafuta platform ya kuweka kila kitu nlichokua nacho kichwani coz i've a lot man!! My head is about to burst!!
Nimekua nikiandika sana humu twitter but naona haitoshi
Read 9 tweets
8 Jun
WE CAN'T BE THE SAME!!

Yawezakua nyuma yako ikawa mbele yangu, au mbele yako ikawa nyuma yangu. Hii haipingiki na ni ngumu kuikataa.
Safari ni moja ya wote tunapotaka kufika ijapokua tunatofautiana maana ya mafanikio na njia ya kuyafikia
T H R E A D πŸ‘‡πŸΌ
Tusichukuliane poa kabla hatujaijua kesho yako na yangu pia.

Imagine unafanya kazi kujinufaisha wewe peke ako lakini mimi napambana natafuta maisha kwa ajili yangu ya familia yangu pia kwahiyo ukiona sipigi hatua ya maendeleo usishangae HATUWEZI KUWA SAWA.
Wote tunaishi dunia moja chini ya anga moja.
Japo wewe unavaa kupendeza na kuwa mtu anaekwenda na wakati lakini mimi mwenzako navaa kujistiri tuu..Sikulaumu wala sikuonei wivu lakini priorities zetu zinatofautiana sana kuna vingi vya msingi kwangu kuliko kuvaa.Hatuwezi kuwa sawa
Read 12 tweets
28 May
AN OPEN LETTER TO MY CRUSH πŸ’Œ

Dear crush,
Nimetuma meseji lakini nachoambulia ni Bluetick lakini najipa moyo pengine unakuaga bize, nikipiga simu mara kadhaa nikikuta inatumika basi najipa moyo utakua unaongea na ndugu yako
Nimeona ni bora leo nikuandikie barua
T H R E A D πŸ‘‡ Image
I hope uko salama
Umekua furaha yangu kila nikikuona ukipita mwenyewe au na wenzio, umekua my mood changer maana nawezakua naskiliza reggae lakini ukipita tuu nahisi nachosikiliza ni blues.
Unaniweza sana dear crush maana simu yangu imejaa screenshots nyingi za picha zako
Wananicheka marafiki jinsi navyokosa kujiamini pale napokuona,
Huwezi amini umetawala kichwa changu nakumbuka ile siku tumekutana ulivonambia nimependeza ilibidi nipite dukani kwa Mangi ninywe soda kwa kujipongeza 😁
My dear, msonyo wako kwangu naona kama busu
Read 14 tweets
18 May
I ONCE EXPERIENCED THE POWER OF LOVE ❀

Nilidhani nguvu ya treni kuvuta behewa ndio nguvu kubwa kuwahi kutokea nikapingana na fikra hizo pale nilipowaza nguvu ya maji kunyanyua meli
Nlipingana na hayo pale nilipokumbana na nguvu iliyopo katika fikra za walopendana
T H R E A DπŸ‘‡
Binafsi sijizuii kupenda inapobidi japo haimaanishi siwezi kuishi bila mpenzi, naamanisha kisu changu kina kata vyoote lakini hakikati tamaa tuu
Nikimuhitaji mtu akaona siendani nae, naachana nae najiandaa kwa "come back " kubwa πŸ˜„
Ndio kilichotokea bana enzi hizo nasoma
High school nliwahi kumpenda mtu akahitaji mpaka niwe na funguo tatu " three keys" ya gari, ya nyumba na ya ofisi nkaona nisonge mbele kama injili maana local man ntavitoa wapi vitu ambavyo wengine wanapata wakistaafu πŸ˜‚

So baada ya mission hiyo kufeli nkapenda tena.Story began
Read 30 tweets
10 May
AN OPEN LETTER TO MY FUTURE DAUGHTER πŸ’Œ

Dear daughter,
Angekuepo bibi yako ambae pia ni mama yangu leo hii siku ya MAMA duniani basi ingemuhusu yeye zaidi, lakini binafsi nimeona niitumie siku hii kukuandikia barua ili siku ukizaliwa uikute
T H R E A D πŸ‘‡
Nuru ya asubuhi haitofaa kitu bila kuona uso wako. Kifungua kinywa hakitakua na maana bila kupata kumbatio lako pindi unapoamka.

Lile tabasamu lako ukinikaribia ni ishara halisi ya binti shupavu aliyebeba urithi wa asili ya mtu mkarimu wa Afrika.
My daughter wewe ni MAMA AFRICA
Dear daughter, sidhani kama ntachelewa sana au labda ntawahi sana kukuleta duniani, lakini naamini wakati ukifika basi utakuja kuungana nasi.
Sina haraka sana ya kukupata maana nakutafutia mama ambae kwa urembo wake atakutoa binti mzuri ili usije ukamaliza pesa zako kwa make upπŸ˜„
Read 14 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!