HAKUSTAHILI KUPITA NJIA NGUMU KIASI KILE
Wakati mwingine dunia inatuweka darasani kujifunza masomo ambayo hatukuwahi kuwaza kujifunza. Pengine hata mitihani ya hayo masomo hatujui itakuja lini
Tabasamu na uchangamfu wake vilificha mengi lakini hakustahili yale #Thread
Unaweza kuchagua marafiki lakini sio jirani maana wewe utajenga hapa ila atakaekuja kujenga pembeni yako hauwezi kumjua ,hivohivo kwenye kupanga chumba. Nilijikuta nimepanga chumba ambapo nyumba ya jirani waliishi familia nzuri na sisiti kusema nilivutiwa nayo kiukweli
Walikua na furaha muda mwingi .Wazazi walikua wa makamo ya miaka 34 na mtoto mdogo wa miaka 10, kutokana na uchangamfu wangu nikajikuta nimekua rafiki na baba wa hiyo familia ambaye alikua ameajiriwa kwenye kampuni moja hapa Mjini . Aliitwa Mr Beda , nilipenda sana kuwa nae hasa
muda nikiwa sina shughuli , wakati mwingine mbio za jioni tulikimbia nae , jioni siku za mwisho wa wiki tulitoka nae pia . Nimejifunza mengi kutoka kwake
Wema na ukarimu wake wote huo lakini hasira ya dunia ilimuwakia ndani na haikuwa rahisi kwa mtu kugundua maana alikua nakifua
"Noe amka" " Hey hey amka uje nje mara moja" ilikua ni sauti ya mtu ninaemfahamu ikiniita usiku kama wa saa tano na nusu . Ilikua namna flani ya kero maana nilichoka sana siku hiyo nikajikongoja mpaka mlangoni nimskilize , Alikua yeye Bwana Beda ameegesha gari yake
karibu kabisa na dirisha la chumba changu . Baada ya salamu na masikhara kadhaa akaja kwenye hoja ya msingi akasema" Mdogo wangu naomba leo nilale kwako hapa maana nimechelewa kurudi halafu naona usumbufu kuwagongea hapo nyumbani"
Japo ilikua mara ya kwanza kwa yeye kuja
nakuomba nimpe hifadhi sikuhofia chochote nikamruhusu akaingia mpaka asubuhi inafika akaondoka zake kwake.
Kulipopambazuka na akili yangu ikapambazuka nikaanza kuwaza nini kimemkuta huyu mtu aliyefanyika kama kaka yangu ? ni kweli sababu ilikua ile au kanificha? aagh mambo ya
watu hayo nkaamua kuachana nayo .Sasa kadri siku zilivozidi kwenda mimi na Mr Beda tukawa marafiki sana japo ratiba zake nikawa sizielewi maana ikifika jioni ye anaondoka halafu ikawa kama anarudi kesho . Siku moja Jumamosi tukatoka wote na huko ikabidi afungue kifua na kutoa
yanayomsibu , nadhani ilikua nguvu ya kimiminika cha kahawia kwenye chupa kubwa kubwa ilichangia. akaanza kwa kusema
" Mdogo wangu, binafsi nadhani napita njia ya peke yangu ambayo najikuta mpweke na nisiye na msaada wowote . Nashukuru nina nguo nzuri nzuri maana ningeonekana
chizi mbele za watu kwa ninayopitia jumlisha msongo wa mawazo" tukajikuta tunacheka wote na binafsi nikajua ni mambo ya kawaida ,akaendelea " Mimi na mke wangu mpaka sasa tuna miaka mingi tuu kwenye ndoa lakini tatizo limeibuka miezi sita sasa , tatizo lenyewe ni pale napoishi"
ikabidi niulize kuna shida gani, akaendelea akasema " Miezi sita iliyopita baba na mama wa mke wangu walikuja kunitembelea kutoka kijijini kwao huko Misungwi Mwanza na kiukweli tuliwapokea kwa furaha . Wakakaa mwezi mmoja, wakaongeza wa pili , ukazidi wa tatu hapo nikaanza
kumhoji mke wangu usiku kwamba mbona wazazi wanaendelea kuwepo hapa hali ya kuwa kule kijijini tayari tumeshawajengea nyumba na wanamifugo kadhaa ? Aiseee nilivouliza hivo ikawa kama nimemwagia mafuta moto maana mke aliwaka sana anasema nawachukia wazazi wake ,basi nikawa mpole"
alivokua anaongea Mr Beda kiukweli aliongea kwa hisia sana . Akaendelea akasema " kadri siku zilivoendelea kwenda baba wa mke wake akawa yeye ndio anaamua chakula gani kipikwe na bajeti ya nyumbani anapanga yeye , mdogo wangu huwezi amini mpaka muda wa kurudi nyumbani nikawa
napangiwa na baba mkwe " hapo nikaona Bwana Beda anavuta fundo moja la Bia aina ya Safari akaendelea akisema" nilivozidi kumuhoji wife akawa anasema kama nimewachoka wazazi wake yeye na wazazi wake waondoke waniache , sasa hapo nikaona kuepusha shari nikizidisha ule muda
niliyopangiwa wa kurudi nyumbani nisiende kugonga mlango niwe natafuta mahali nalala iwe lodge , au kwa marafiki na kama unakumbuka nilishawahi kuja kwako"
hapo nikashusha pumzi nzito nikaunganisha nukta nikaona hayo ni mazito kumbe hata sisi wanaume kuna wakati tunaumia sana.
Ikabidi nimuulize anampango gani katika hilo maana habari za ndoa mi sina idea kabisa mapenzi yenyewe patashika
Akadai anataka aondoke yeye kwenye nyumba wabaki wakwe zake mke na mtoto. Duuh nikaona nisitafute kujua sana nikamwambia amalize kinywaji twende maana muda ulishaenda
Sikuwahi kuwaza kama siku hiyo ndio siku ya mwisho kumuona Mr Beda maana baada ya hapo kila nilipiga simu yake haikupatikana na kwenye ile nyumba alipokua anakaa walihamia watu wengine . Nikamtakia maisha mema tuu rafiki yangu yule , nikaendelea na kilichonileta Morogoro mjini
Miezi mingi ilipita ,shule ikasonga na hatimae kipindi cha Field Practical Training kikafika ambapo mara nyingi kwa taaluma yangu tunafanyiaga kwenye taasis zenye mifugo mingi hasa Jeshini ,Mashamba ya Serikali na Magereza . Basi nikapangiwa kwenye moja ya Gereza hapa Moro
Kiukweli sikutaka kuamini kirahisi kilichokua mbele yangu maana ile napelekwa kitengo cha mifugo nikakutana na Nyampara aliyepewa asimamie hilo eneo ni mtu kama Mr Beda japo amekonda sana na rangi yake nyeupe imemezwa na ngozi ngumu nyeusi
Aliponiona akanikumbuka kabisa
Ikawa kama ananipa Sehemu yaapili ya maisha yake kilichotokea baada ya kupotezana .Alinisimulia mengi sana maana alisema " Baada ya kuachana na wewe siku zile ilibidi niende kwangu nichukue nguo zangu kadhaa na gari yangu niende mtaa mwingine na bahati mbaya simu ilipotea
...baada ya kupata chumba nikaanza maisha yangu , cha ajabu nashindwa kujua mke wangu chuki alitoa wapi maana hata kumuona mwanangu alikua ananikataza na mbaya zaidi nikaskia ile nyumba yangu walimokua wanaishi aliiuza kikubwa kilichoniumiza akawa ameolewa kimya kimya"
Kikuweli alifanikiwa kuniacha mdomo wazi nikabaki namuangalia mavazi yake ya rangi ya karoti na ndala zilizotoboka . Nikampa pole akaendelea akasema " Nilivopata hizo taarifa kama binadamu nilishikwa na hasira nikawatafuta wanapokaa nikaenda kuanzisha fujo japo sio kubwa
lakini yule mume wa mke wangu alipiga simu polisi wakaja wakanikamata na kunipeleka kituoni na hatimaye mahakamani. Mdogo wangu Noe huwezi amini mke wangu ndiye alisimama upande wa mashahidi na kusema mimi nimeingua ndani nakuvunja mali zao na kuiba fedha milion 5 ,
Hakimu akagonga nyundo nikaletwa huku kutumikia miaka 8" alipomaliza hayo aliishia kulia kaka Beda . Nilimpa leso akaniandikia anwani mahali wanakaa mke na familia yake mpya ili basi nikirudi mjini walau nikamsalimie mwanae. Nashukuru nilitimiza yote maagizo
Zaidi hatima zetu bado ni kitendawili
#End
#MyMindSpeak
nohtalk.com

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Noe_Wenc 💊

Noe_Wenc 💊 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Vet_doctor87

16 Jun
LET MY MIND SPEAK
So, hakuna kizazi bora kama kizazi chenye wingi wa maarifa na vijana wenye kuchangamkia fursa kila inapotokea.
SHORT THREAD👇
My brother @veggiesfarmer once said " We are in knowledge economy,what you know is what will differentiate you and accelerate your growth, your growth will highlight your value and your value will elevate your worth.
Imekua muda mrefu nikitafuta platform ya kuweka kila kitu nlichokua nacho kichwani coz i've a lot man!! My head is about to burst!!
Nimekua nikiandika sana humu twitter but naona haitoshi
Read 9 tweets
8 Jun
WE CAN'T BE THE SAME!!

Yawezakua nyuma yako ikawa mbele yangu, au mbele yako ikawa nyuma yangu. Hii haipingiki na ni ngumu kuikataa.
Safari ni moja ya wote tunapotaka kufika ijapokua tunatofautiana maana ya mafanikio na njia ya kuyafikia
T H R E A D 👇🏼
Tusichukuliane poa kabla hatujaijua kesho yako na yangu pia.

Imagine unafanya kazi kujinufaisha wewe peke ako lakini mimi napambana natafuta maisha kwa ajili yangu ya familia yangu pia kwahiyo ukiona sipigi hatua ya maendeleo usishangae HATUWEZI KUWA SAWA.
Wote tunaishi dunia moja chini ya anga moja.
Japo wewe unavaa kupendeza na kuwa mtu anaekwenda na wakati lakini mimi mwenzako navaa kujistiri tuu..Sikulaumu wala sikuonei wivu lakini priorities zetu zinatofautiana sana kuna vingi vya msingi kwangu kuliko kuvaa.Hatuwezi kuwa sawa
Read 12 tweets
28 May
AN OPEN LETTER TO MY CRUSH 💌

Dear crush,
Nimetuma meseji lakini nachoambulia ni Bluetick lakini najipa moyo pengine unakuaga bize, nikipiga simu mara kadhaa nikikuta inatumika basi najipa moyo utakua unaongea na ndugu yako
Nimeona ni bora leo nikuandikie barua
T H R E A D 👇 Image
I hope uko salama
Umekua furaha yangu kila nikikuona ukipita mwenyewe au na wenzio, umekua my mood changer maana nawezakua naskiliza reggae lakini ukipita tuu nahisi nachosikiliza ni blues.
Unaniweza sana dear crush maana simu yangu imejaa screenshots nyingi za picha zako
Wananicheka marafiki jinsi navyokosa kujiamini pale napokuona,
Huwezi amini umetawala kichwa changu nakumbuka ile siku tumekutana ulivonambia nimependeza ilibidi nipite dukani kwa Mangi ninywe soda kwa kujipongeza 😁
My dear, msonyo wako kwangu naona kama busu
Read 14 tweets
18 May
I ONCE EXPERIENCED THE POWER OF LOVE ❤

Nilidhani nguvu ya treni kuvuta behewa ndio nguvu kubwa kuwahi kutokea nikapingana na fikra hizo pale nilipowaza nguvu ya maji kunyanyua meli
Nlipingana na hayo pale nilipokumbana na nguvu iliyopo katika fikra za walopendana
T H R E A D👇
Binafsi sijizuii kupenda inapobidi japo haimaanishi siwezi kuishi bila mpenzi, naamanisha kisu changu kina kata vyoote lakini hakikati tamaa tuu
Nikimuhitaji mtu akaona siendani nae, naachana nae najiandaa kwa "come back " kubwa 😄
Ndio kilichotokea bana enzi hizo nasoma
High school nliwahi kumpenda mtu akahitaji mpaka niwe na funguo tatu " three keys" ya gari, ya nyumba na ya ofisi nkaona nisonge mbele kama injili maana local man ntavitoa wapi vitu ambavyo wengine wanapata wakistaafu 😂

So baada ya mission hiyo kufeli nkapenda tena.Story began
Read 30 tweets
10 May
AN OPEN LETTER TO MY FUTURE DAUGHTER 💌

Dear daughter,
Angekuepo bibi yako ambae pia ni mama yangu leo hii siku ya MAMA duniani basi ingemuhusu yeye zaidi, lakini binafsi nimeona niitumie siku hii kukuandikia barua ili siku ukizaliwa uikute
T H R E A D 👇
Nuru ya asubuhi haitofaa kitu bila kuona uso wako. Kifungua kinywa hakitakua na maana bila kupata kumbatio lako pindi unapoamka.

Lile tabasamu lako ukinikaribia ni ishara halisi ya binti shupavu aliyebeba urithi wa asili ya mtu mkarimu wa Afrika.
My daughter wewe ni MAMA AFRICA
Dear daughter, sidhani kama ntachelewa sana au labda ntawahi sana kukuleta duniani, lakini naamini wakati ukifika basi utakuja kuungana nasi.
Sina haraka sana ya kukupata maana nakutafutia mama ambae kwa urembo wake atakutoa binti mzuri ili usije ukamaliza pesa zako kwa make up😄
Read 14 tweets
30 Apr
AN OPEN LETTER 💌 TO MY LOVE

Sweetheart ,
Natumai uko salama, kuandika barua ni utaratibu wa zamani maana ningeweza kukupigia simu au kutuma meseji lakini nimeona vyote hivo visingebeba hisia zangu zote kama ambavyo barua imeweza

T H R E A D 👇
Dear love, we ni binadamu wa maana sana kwangu maana umefanyika nuru katika ulimwengu wangu wangu wa huba.
Nilifikiri mwangaza wa jua la asubuhi unaumiza sana macho mpaka nilivokutana na tabasamu lako kutoka kwenye kinywa chenye meno yalopangika vizuri naam ulinivutia❤
Nilidhani apple 🍏 ndio tunda lenye thamani sana mpaka nilivokutana na rangi yako ya chungwa kwenye ngozi inayong'aa
Wanavosema Monalisa ndio mchoro wa thanani sana nadhani hawajaona ile picha yako japo umegeuka mgongo tuu lakini thamani yake ni zaidi ya Pyramids za Misri
Read 17 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!