Kutoka michezo ya Betting mpaka uuzaji wa nguo katika mitandao. Kuna namna nyingi sana za kutengeneza pesa mtandaoni, nyingine zina ahadi ya kukupa utajiri mkubwa ndani ya muda mfupi., lakini je, ni kweli zinafanya kazi? 👇
Jibu: Sio siku zote.
Je, Utatengeneza pesa ukifata njia hizo?
Jibu: Labda, maana ni kitu kimekaa kimtego sana. Inawezekana kabisa kwamba ile kazi yako inayokupa mshahara kila mwisho wa mwezi ikakupa pesa zaidi ya hizi njia za mitandaoni au kinyume chake
Ukweli ni kwamba kuna njia za kweli zinazofanya kazi na zinazowapa watu pesa kupitia mitandao. Kuna Freelancer(Wafanyakazi huru), wajasiriamali wadogo wadogo, waandishi, Walimu, Wahasibu, Wanasheria, N.K hutumia mitandao kupata kipato
Njia rahisi zaidi ya kuingiza kipato mtandaoni ni kupitia freelancing, Hapa wengi hutumia hobby/fani zao au ile kazi ilikuwa inakulipa mshahara kama njia ya kupata kipato unaweza kuifanya mtandaoni
Mfano wewe ni mwandishi, graphics designer, mwalimu, developer, mkalimani N.K, unaweza kuyatangaza haya maarifa mtandaoni na yakaanza kukupa kipato bila ya wewe kuwepo ofisini.
Kuna watu mtandaoni wapo tayari kukulipa uwafanyie kazi bila ya wewe kuwa na ofisi
Kutengeneza pesa kama influencer unawezalipwa kwa post, affiliate links, kuwa wakala wa bidhaa za kampuni kubwa na wakati mwingine unaweza lipwa ili tu sura yako ionekane katika hafla fulani.
Sehemu rahisi za kufanya influencing ni Facebook, Twitter, Instagram na YouTube
3.Tengeneza pesa kwa Affiliate marketing.
Affiliate marketing ni utangazaji wa bidhaa ya brand fulani kwa kutumia link ya pekee wanayokupa. Link hii itatumika kuonesha ni watu wangapi wamenunua bidhaa ya kampuni hiyo kupitia tangazo uliloweka wewe.
Mfano, Leo Bohny Chengula akanipa link nitangaze simu zake, kwa makubaliano ya kwamba nachukua 10% ya kila mauzo ya hiyo simu, Mteja atakapo nunua hiyo simu kupitia ile link niliyopost mimi, Mimi nitachukua 10% ya alicholipia na Bohny atachukua yote inayobaki
Ukitaka kufanikiwa vizuri katika affiliate marketing, kitu inabidi ujue ni uandishi wa matangazo na kuwa muuzaji mzuri [ COPYWRITING SKILLS ] pia ni vyema ukafanya affiliate marketing kwa vile vitu unapenda itakuleta kipato zaidi,
Dropshipping & Dropservice ni uuzaji wa bidhaa au maarifa kama mtu wa kati (Dalali). Mf Leo najua kwamba @HabariTech ni mtengenezaji wa Mobile apps lakini mimi siwezi. Nitakachofanya najitangaza mimi kama mtengenezaji wa Mobile Apps
Mteja akipatikana app iliyotakiwa kutengenezwa kwa Tsh. 5 mil nitasema natengeneza kwa Tsh. 6 mil. Nachukua Tsh. 5 mil nampa @HabariTech anatengeneza hiyo app nampa mteja, mimi nina Tsh. 1 mil mfukoni. Hapo ni kila mtu ashinde mechi zake ( Huo ni mfano 😄 )
Dropshipping inahusika na uuzaji wa bidhaa wakati Dropservice ni uuzaji wa maarifa. Katika Dropshipping iskutishe kwamba bidhaa utazitoa wapi, Kumbuka wewe humiliki hizo bidhaa. Wewe umewapa wateja sehemu ya kununulia bidhaa
anayehangaika na kufanya packaging na usafirishaji ni yule muuzaji/mmiliki wa hizo bidhaa
Kwenye Dropservice hakikisha unajikita na vitu ambavyo unavielewa au una-idea navyo ili kuepuka hasara, unaweza kumwambia mtaje bei flani na ikawa ndogo kuliko bei halisi
Kuuza elimu uliyonayo ni njia moja wapo ya kukuingizia kipato mtandaoni. Wewe una elimu ya kutosha kuhusu somo fulani. Tengeneza kozi ya hicho unachokijua vizuri kisha uza kozi hiyo sehemu kama Udemy.com
au kama una website yako mwenyewe basi uza katika website yako, Ili uweze tengeneza kozi nzuri yafaa ukaangalia wengine wamefanya nini katika kozi zinazohusu hicho unataka kufanya itakusaidia kutengeneza kilichobora zaidi
Ebooks ni vitabu vya kielektroniki ambavyo unaweza kuvisoma kupitia simu au Computer yako, Unachohitaji kufanya ni kuandika kitabu na kukiweka katika muundo mzuri kabisa wa kuwa kitabu.
Unaweza tangaza kazi yako kupitia mitandao kama FB, instagram au twitter na watu wakapenda kazi zako wakakuomba uwafanyie kazi kwa malipo, kuna platforms unaweza weka picha zako na zikauzwa mfano wa platform ni foap.com au 99designs.com
Kama wengine wanaweza pata kipato kupitia Youtube kwanini wewe ushindwe? Mtu anayelipwa zaidi na YouTube ni kijana mdogo anaitwa Ryan, anafanya reviews za toys za watoto. Kufikia 2018 channel yake ilimuingizia kiasi cha $22 mil
RADAR
Radar ni kifupisho cha (Radio Detection and Ranging)
Ni mfumo ambao unatuma signal/ishara kwenye kitu (object) na kuchambuliwa kisha kurudisha majibu ya hicho kifaa kwa mfumo huo wa signal kupitia hewa 👇
Ili kugundua uwepo, mwelekeo, umbali, na kasi ya ndege, meli, na vitu vingine
Signal ni mawimbi (radio waves) ambayo hutumwa kwa kifaa kilicho kwenye coverage ya Radar/eneo Radar inapofika na kukichambua hicho kifaa na kurudisha majibu kwenye chanzo/muongozaji
Kwa hapa Tanzania radar zinatumika kwenye viwanja vya ndege, jeshini na kwenye Meli. Na radar zilizopo zimegawanyika katika makundi mawili: Primary na Secondary radar
Tunapozungumzia hizi primary radar tunamaanisha ni zile Radar ambazo
Meme Coins au Shitcoins unaweza kuziita coins za majitaka au futuhi coins
Ni coins ambazo zimekua zikipendwa sana na watu wa Crypto kwa kuwa zinaweza kukupa faida hata mara 1000 ya mtaji wako kwa muda mfupi. 👇
Meme coins zimeundwa bila kuwa na matumizi yoyote muhimu kasoro kiki inayotokana na Jina la hiyo coin.
Katika msimu huu wa Crypto, shitcoins zimekua zikipatikana sana katika Blockchain inayoitwa Binance Smart Chain (BSC) kupitia website inayoitwa Pancakeswap
na kununua inabidi uwe na salio la coin ya BSC inayoitwa BNB na iwe ndani App ya TrustWallet...utatumia adress ya hiyo coin yako ili kuinunua
Kwa kawaida tumezoea Coin inakua na project fulani ili watu wawekeze.
Sasa hizi MemeCoins hazina project yoyote zaidi ya kupigiwa Kiki
Mwaka 2021 unatabiriwa kuwa na mapinduzi ya Tekinolojia, Apple wao wamejipanga kufanya yafuatayo
UZI
◾️Apple silicon iMac
Apple wanakuja na iMac ambayo itakuwa na Apple silicon chip, kama walivyofanya kwenye MacBook, itakuwa na16 high-power cores& 4 efficiency cores
◾️AirPods
2021 Apple wanategemea kutoa third-generation AirPods ambayo itakuwa na replaceable silicone air tips, pia wataboresha wireless chip na battery life
◾️iPad Pro
Apple wanakuja na 12.9 inch iPad Pro ambayo itakuwa na LED display, hii Min-LED Technology itakuwa na wide color gamut performance, high contrast and HDR, and local dimming, pia iPad Pro itakuwa na 5G connection ikisapotiwa na A14X chip kama ilivyo kwenye M1 Macs
◾️Hizi ni simu zinazotamba kwa sasa Duniani ikiwa ni matoleo mapya kwa Samsung na Apple
◾️Nakuletea ulinganifi wa hizi simu, hii ni kulingana na majarida mengi kama AndroidAuthority, CNet, GSMArena, Gadget360 n.k
Twende na uzi👇
◾️Samsung Galaxy Note 20 Ultra ilitoka Aug 5 na iPhone 12 Pro Max ilitoka Oct 13 lakini hii bado ni Pre-order
◾️Kila kampuni inasifia simu yake kuwa ni bora zaidi Duniani kwa sasa kutokana na teknologia ya hali ya juu iliyotumika kwenye hizo simu
◾️Tuzichambue taratibu
◾️DESIGN
👉 Simu zote zinamwonekano mzuri lakini kuna utofauti
◾️Samsung Galaxy Note 20 ultra ni simu yenye kuonekana vizuri sana, wamechukua designing ya matoleo yote ya Note series wakaleta hii Note 20 ultra, dimensions 168.4mm/urefu 77.2/upana 8.1/angle na uzito ni 208g