UZI:

RADAR NA MATUMIZI YAKE

RADAR
Radar ni kifupisho cha (Radio Detection and Ranging)
Ni mfumo ambao unatuma signal/ishara kwenye kitu (object) na kuchambuliwa kisha kurudisha majibu ya hicho kifaa kwa mfumo huo wa signal kupitia hewa 👇

#ElimikaWikiendi
Ili kugundua uwepo, mwelekeo, umbali, na kasi ya ndege, meli, na vitu vingine

Signal ni mawimbi (radio waves) ambayo hutumwa kwa kifaa kilicho kwenye coverage ya Radar/eneo Radar inapofika na kukichambua hicho kifaa na kurudisha majibu kwenye chanzo/muongozaji

#ElimikaWikiendi
Kwa hapa Tanzania radar zinatumika kwenye viwanja vya ndege, jeshini na kwenye Meli. Na radar zilizopo zimegawanyika katika makundi mawili: Primary na Secondary radar

Tunapozungumzia hizi primary radar tunamaanisha ni zile Radar ambazo

#ElimikaWikiendi
Zina uwezo wa kutambua kitu kilichoingia kwenye eneo lake (coverage area) na kutuma taarifa za umbali wa kilipo hicho kitu. Hizi zinatumika jeshi, Viwanja vya ndege na kwenye meli

#ElimikaWikiendi
Pia Secondary Radar kutokana na mabadiliko ya kasi ya teknolojia hawa jamaa waliamua kuiwekea hii radar vitu vingi sana kama (DME Transponder)

Ambapo hichi ni kifaa kinachosaidia kutuma taarifa zote za kitu kilichokuwa target kwenye eneo la hiyo Radar.

#ElimikaWikiendi
Hii kwa hapa Tanzania inatumika Airport. Ambapo hizi Radar zinaweza kubadilishana taarifa na ndege inayokaribia kutua kwenye Uwanja wa ndege au ndege iliyopita kwenye eneo la hiyo Radar (coverage area)

#ElimikaWikiendi
Ambapo ndege lazima iwe na hicho kifaa ambapo kinabeba taarifa zote muhimu za ndege iyo mfano: Idadi ya abiria, ndege ilipo toka - inapoelekea, muda wa kutua n.k

Kwaiyo watu wa kituo cha aridhi watazipata hizi taarifa baada ya ndege kuingia kwenye anga Lao.

#ElimikaWikiendi
Kama ndege haina hicho kifaa hawatoweza kupata Hizo taarifa.

Ndio maana sehemu kama KIA mwanzo walikuwa wanatumia Primary Radar miaka ya hapa nyuma walichofanya sio kuitoa na kuiweka Secondary Radar Bali wamezifunga zote kwa pamoja.

#ElimikaWikiendi
Kwasababu hii secondary haiwezi pata taarifa za Ndege ambayo haina hicho kifaa ndio maana wakaibakisha primary radar. Ambayo ina uwezo wa kupata taarifa ya kitu kilichoingia angani japo sio kwa undani kama secondary

#ElimikaWikiendi
Pia hata jeshini ndizo wanazozitumia. Radar za jeshini hazina uhusiano wowote na Radar za Viwanja vya ndege. Labda wakitaka kushirikiana kama kutakuwa na serious issues hilo linawezekana.

Mfano Radar ya sasa hivi iliyopo KIA imebeba anga lote la mkoa ya Kaskazini hadi Nairobi
Ndege inapotaka kutua KIA kama kuna mwingiliano hapo Kati mtu wa Ardhi ana uwezo wa kumuongoza rubani akaituishe ndege Uwanja wa Kisongo, Arusha.

Uzuri wa hizi Radar kama ndege ndiyo Imefika Anga la Tanga

#ElimikaWikiendi
Mtu wa Ardhi anaweza kuona itatumia dakika ngapi kutua KIA, Kilimanjaro na dakika ngapi kutua Kisongo, Arusha

Huwa wanawasiliana tu kawaida kama mtu anavyoongea na simu kwa kutumia Radio signal.

#ElimikaWikiendi
Na pia mtu wa Aridhi anaweza kumtengenezea rubani barabara huko angani kama rubani akishindwa kuona mbele kwa sababu ya mawingu.

Huwa wana kuwa na vipimo vyao kuzingatia maeneo ya milima na njia ambazo ndege nyingine zinatakiwa zipite.

#ElimikaWikiendi
Suala la Helicopter na Drone
Kisheria hivi vitu kabla hazijarushwa angani lazima zipatiwe vibali kutoka TCAA ( Tanzania Civil Aviation Authority) bila hivyo ni kuvunja sheria na kutishia Hali ya usalama.

#ElimikaWikiendi
Helicopter ikiwa angani bahati mbaya ikawa inaelekea kwenye njia ambayo ndege itapita mtu wa ardhini anaweza mwambia pilot wa helicopter arudi nyuma au asimame kwasababu helicopter ina inaweza kusimama sehemu moja angani na pia Drone

#ElimikaWikiendi
Vibali vya kurusha kifaa chochote angani hutolewa TCAA.

Tanzania yote imekuwa coverage na Radar, Kuna radar ipo Songwe inacover eneo lote la kusini, Radar ya mwanza Kanda yote ya ziwa, ya KIA hii ni kubwa inafika karibia na mwanza, shinyanga mpaka Nairobi.

#ElimikaWikiendi
Radar ya Airport Dar es salaam inaenda mpaka inaungana na Radar ya Songwe

Kuhusu bandari meli ndizo zinakuwa na Radar ambazo zinawasaidia mabaharia kuweza kudetect meli nyingine, ardhi, umbali na pia kusaidia mwongozaji wa Ardhi kuwasiliana na Nahodha

#ElimikaWikiendi
Maana ya Radar
ni mfumo wa kugundua vitu ambao hutumia mawimbi ya redio kuamua aina, angle, au kasi ya vitu. Inaweza kutumika kuchunguza ndege , meli , ndege za ndege , miamba iliyoongozwa , magari , mafunzo ya hali ya hewa , na ardhi.

AHSANTENI

#ElimikaWikiendi

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with #TOTTechs 🇹🇿

#TOTTechs 🇹🇿 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @TOTTechs

22 Jun
DARASA LA CRYPTO:
SEASON 1: UZI/THREAD

MEME COINS/SHITCONS

Meme Coins au Shitcoins unaweza kuziita coins za majitaka au futuhi coins

Ni coins ambazo zimekua zikipendwa sana na watu wa Crypto kwa kuwa zinaweza kukupa faida hata mara 1000 ya mtaji wako kwa muda mfupi. 👇
Meme coins zimeundwa bila kuwa na matumizi yoyote muhimu kasoro kiki inayotokana na Jina la hiyo coin.

Katika msimu huu wa Crypto, shitcoins zimekua zikipatikana sana katika Blockchain inayoitwa Binance Smart Chain (BSC) kupitia website inayoitwa Pancakeswap
na kununua inabidi uwe na salio la coin ya BSC inayoitwa BNB na iwe ndani App ya TrustWallet...utatumia adress ya hiyo coin yako ili kuinunua

Kwa kawaida tumezoea Coin inakua na project fulani ili watu wawekeze.
Sasa hizi MemeCoins hazina project yoyote zaidi ya kupigiwa Kiki
Read 19 tweets
1 Jan
APPLE

Mwaka 2021 unatabiriwa kuwa na mapinduzi ya Tekinolojia, Apple wao wamejipanga kufanya yafuatayo

UZI

◾️Apple silicon iMac

Apple wanakuja na iMac ambayo itakuwa na Apple silicon chip, kama walivyofanya kwenye MacBook, itakuwa na16 high-power cores& 4 efficiency cores ImageImage
◾️AirPods

2021 Apple wanategemea kutoa third-generation AirPods ambayo itakuwa na replaceable silicone air tips, pia wataboresha wireless chip na battery life Image
◾️iPad Pro

Apple wanakuja na 12.9 inch iPad Pro ambayo itakuwa na LED display, hii Min-LED Technology itakuwa na wide color gamut performance, high contrast and HDR, and local dimming, pia iPad Pro itakuwa na 5G connection ikisapotiwa na A14X chip kama ilivyo kwenye M1 Macs Image
Read 13 tweets
19 Dec 20
UZI

SOCIAL ENGINEERING
[ utumiaji wa madhaifu ya Mwanadamu kufanya wizi]

◾️Social engineering huchukua faida ya kitu dhaifu kabisa katika ulinzi wa taarifa za kila aina ya taasisi ambacho ni MTU

Social engineering ni "PEOPLE HACKING" na inahusisha 👇

#ElimikaWikiendi Image
Madhaifu ambayo binadamu tunayajenga sisi kwa sisi na kuweza kuyatumia hayo madhaifu kupata taarifa ambazo hutumika kwa faida binafsi

◾️Social engineering ni moja ya wizi mgumu kufanyika, kwa Dunia ya sasa imekuwa ni vigumu sana mtu kumwamini mtu mgeni kwake

#ElimikaWikiendi Image
Kutokana na hali halisi ilivyo hata hivyo hii imekuwa hacking ngumu sana kuizuia kutokana na uaminifu tunaoujenga baina yetu

◾️Social engineering, typically yule malicious attacker/mwizi hujiweka kama mtu mwema sana ili kupata taarifa anazotaka

#ElimikaWikiendi Image
Read 25 tweets
27 Oct 20
TWITTER FOR VPN

◾️kumekuwa na sintofahamu baina yetu na kulazimika kutumia VPN ili kuweza kupata access ya twitter

◾️Hii inasababishwa na kitu kinaitwa OUTAGE kwa jina jingine ni DOWNTIME

◾️Twende na uzi uelewe inatokeaje na kwa nini unatumia VPN/TOR/PROXIES

Uzi mfupi
◾️Outage kwa jina jingine ni Downtime ambapo ni ukosefu wa huduma flani au network, Hii inakuwa imegawanyika kwa namna mbili

👉 Unplanned outage
👉 Planned outage

◾️Unplanned outage ni ukosefu wa huduma flani au network nzima kutokana na mambo kadhaa kama vile
✴️Kuingiliwa/kuzimwa kwa network/mawasiliano na attackers (wadukuzi) hii inaitwa DOS/DDOS [ Denial of services ] attack

✴️ Kufeli kwa Hardware au Software

✴️ Kuharibika kwa vifaa flani vinavyotoa huduma ya internet

◾️Planned outage ni ukosefu wa huduma au network
Read 7 tweets
24 Oct 20
iPhone 12 Pro Max VS Samsung Note 20 Ultra

◾️Hizi ni simu zinazotamba kwa sasa Duniani ikiwa ni matoleo mapya kwa Samsung na Apple

◾️Nakuletea ulinganifi wa hizi simu, hii ni kulingana na majarida mengi kama AndroidAuthority, CNet, GSMArena, Gadget360 n.k

Twende na uzi👇 Image
◾️Samsung Galaxy Note 20 Ultra ilitoka Aug 5 na iPhone 12 Pro Max ilitoka Oct 13 lakini hii bado ni Pre-order

◾️Kila kampuni inasifia simu yake kuwa ni bora zaidi Duniani kwa sasa kutokana na teknologia ya hali ya juu iliyotumika kwenye hizo simu

◾️Tuzichambue taratibu ImageImage
◾️DESIGN

👉 Simu zote zinamwonekano mzuri lakini kuna utofauti

◾️Samsung Galaxy Note 20 ultra ni simu yenye kuonekana vizuri sana, wamechukua designing ya matoleo yote ya Note series wakaleta hii Note 20 ultra, dimensions 168.4mm/urefu 77.2/upana 8.1/angle na uzito ni 208g Image
Read 18 tweets
19 Sep 20
ENCRYPTION

Najua unasikia sana neno "Encryption" lakini kuna mengi ya kujifunza ili uelewe zaidi kuhusu encryption

◾️Encryption ni nini na aina zake ni zipi ?

◾️Encryption salama na zisizo salama

◾️Matumizi ya Encryption

◾️Faida za kufanya Encryption

Cc: @Kimkayndo
◾️ Encryption ni kitendo cha kubadili maneno au jumbe za kawaida kutoka kwenye mfumo unaosomeka kwenda kwenye mfumo ambao hausomeki, ambapo huzalisha kitu kinaitwa "cipher text"

Mfano kipindi cha utoto, watoto huongea kwa kuchanganya maneno ili watu wazima wasielewe wanaongea
nini, huu ni mfano wa encryption lakini endapo hiyo njia itatambulika kwa wengine basi hakuna tena usiri, wanaita "security through obscurity" yaani security huvunjika mara baada ya attacker kujua njia yako ya kujilinda

Katika encryption ili kuiondoa security through obscurity
Read 25 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(