◾️Hizi ni simu zinazotamba kwa sasa Duniani ikiwa ni matoleo mapya kwa Samsung na Apple
◾️Nakuletea ulinganifi wa hizi simu, hii ni kulingana na majarida mengi kama AndroidAuthority, CNet, GSMArena, Gadget360 n.k
Twende na uzi👇
◾️Samsung Galaxy Note 20 Ultra ilitoka Aug 5 na iPhone 12 Pro Max ilitoka Oct 13 lakini hii bado ni Pre-order
◾️Kila kampuni inasifia simu yake kuwa ni bora zaidi Duniani kwa sasa kutokana na teknologia ya hali ya juu iliyotumika kwenye hizo simu
◾️Tuzichambue taratibu
◾️DESIGN
👉 Simu zote zinamwonekano mzuri lakini kuna utofauti
◾️Samsung Galaxy Note 20 ultra ni simu yenye kuonekana vizuri sana, wamechukua designing ya matoleo yote ya Note series wakaleta hii Note 20 ultra, dimensions 168.4mm/urefu 77.2/upana 8.1/angle na uzito ni 208g
Kuna Gorilla Glass kwa mbele na kwa nyuma ili kuzuia scratch, rangi zake ni Bronze (kama ile ya @GillsaInt), White na Black
Ikiwa na Display ya 6.9 inches Dynamic AMOLED, 1440 x 3088 pixels resolution, ikiwa na refresh rate 120Hz Full HD mpaka Quad HD [QHD]
◾️iPhone 12 Pro Max kwa upande wake imechukua designing ya matoleo yote ya nyuma na kuya-modify, wamekuja na Face ID, Display yake ni 6.7 inches Super Retina XDR OLED ikiwa na 1284 x 2778 px Resolution huku refresh rate yake ni ndogo kuliko ya Samsung Note 20 ultra na resolution
yake haifiki QHD, hapo iPhone Pro Max kazidiwa point moja na Samsung
Umbo lake ni 160.8mm/urefu, 78.1/upana na 7.4/angle na uzito ni 228g ikiwa imezungukwa na Gorilla glass kuzuia scratch huku ikiwa na Ceramic shield kulinda Dispalay
◾️FEATURES
PROCESSORS and RAM
◾️Samsung Galaxy Note 20ultra imekuja na Processor yenye speed kubwa kwa sasa katika simu zote za Android, Qualcomm snapdragon 865+ Octa-core CPU ikiwa na Chipset ya Exynos 900 lakini kwa US na Europe wana Advantage ya Optimized gaming
Processor kulinganisha na kwingine
12GB RAM na storage ni 128, 256, 512GB na kuna slot ya MicroSD
◾️iPhone 12 Pro Max wamekuja na latest processor ya Apple ambayo ni A14 Bionic ikiwa na Hexa-core Processors
6GB RAM na Storage ni 128, 256 na 512 GB haina sehemu ya MicroSD
◾️CONNECTIVITY
Note 20 ultra na iPhone 12 Pro Max zote zinasupport 5G [sub-6Ghz and mmWave 5G Network ]
Note 20ultra ina snapdragon 865+ ambayo inaweza ku-connect na global 5G network popote pale inapatikana lakini iPhone 12 Pro Max inaconnect na 5G palipo na
Minara ya 5G mmWave pekee, hivyo itaadhiri baadhi ya maeneo yasiyo na mmWave towers
Hapo Samsung kamzidi point nyingine Apple
◾️BATTERY
Samsung Galaxy Note 20 ultra inakuja na 4,500 mAh batter ambayo inaweza kukaa na charge kwa siku nzima, inakuja na 25W charger kwenye Box
Note 20 ultra inasupport 15W wireless charging na 4.5W reverse charging kwa ajili ya kucharge vifaa Kama earbuds na unaweza kucharge simu nyingine
iPhone 12 Pro Max inakuja na Li-Ion 3687 mAh battery, Fast Charging 20W [ 50% in 30 minutes ] 15W wireless charging
ikiwa na Apple charger
Lakini hizo chargers haziwekwi ndani ya Box la simu, kama hauna inabidi utumie $20 kununua hivyo vitu
Apple amezidiwa point nyingine na Samsung
◾️STANDARD FEATURES
Note 20 Ultra ana S-pen, toleo hili Samsung wamesema S pen imekuwa improved
ina detect gestures na una-feel kama unaandika kwenye karatasi halisi
iPhone 12 MagSafe feature, hii inatumia Magnet/sumaku ku-attach variety of accessories kama wireless charger, phone case nyuma ya simu, iPhone amechua Point kwa Samsung
Hii imeonekana mpya kwa iPhone users
◾️CAMERA
Simu nyingi za kisasa zinashindana kutengeneza camera nzuri kuvutia watumiaji
iPhone 12 Pro Max imekuja na 12MP wide sensor, 12MP ultra-wide camera na 12MP Telephoto shooter ikiwa na 2.5x optical zoom, kuna LiDAR scanner kwa kurecord taarifa za ndani na
Pia kuna Sensor shift stabilization
Note 20 ultra inakuja na 108MP Primary camera, 12MP ultra wide sensor, 12MP telescope lens yenye 5x optical zoom na 50x hybrid zoom
Kwenye camera Samsung amewin kwenye Pixels, Samsung wana camera nzuri lakini iPhone wana camera nzuri 😂
◾️GHARAMA
◾️Samsung Galaxy Note 20 Ultra
128GB: $1,299/£1,179/€1,309
512GB: $1,449/£1,279/€1,409
◾️iPhone 12 Pro Max
128GB: $1,099/£1,099/€1,259
256GB: $1,199/£1,199/€1,379
512GB: $1,399/£1,399/€1,609
Samsung Galaxy Note 20ultra ni ghali zaidi ya iPhone 12 Pro Max
◾️Summary
Debate ya Android na iPhone haiwezi kuisha lakini kuna vitu vinaiongezea point Note 20ultra
◾️Higher resolution na faster refresh rate, RAM kubwa, unaweza kuweka MicroSD card, Primary camera imawin kwenye Megapixel, S pen features ni more advanced
Kwa Upande wa iPhone kuna vitu vinaongeza ubora hasa kwenye upande iOS software security, MagSafe na Ceramic shield
◾️Comment simu yako bora kati ya iPhone 12 Pro Max na Samsung Galaxy Note 20 ultra
◾️ Encryption ni kitendo cha kubadili maneno au jumbe za kawaida kutoka kwenye mfumo unaosomeka kwenda kwenye mfumo ambao hausomeki, ambapo huzalisha kitu kinaitwa "cipher text"
Mfano kipindi cha utoto, watoto huongea kwa kuchanganya maneno ili watu wazima wasielewe wanaongea
nini, huu ni mfano wa encryption lakini endapo hiyo njia itatambulika kwa wengine basi hakuna tena usiri, wanaita "security through obscurity" yaani security huvunjika mara baada ya attacker kujua njia yako ya kujilinda
Katika encryption ili kuiondoa security through obscurity
Android 11 imetoka, ni jambo zuri kwa watumiaji wa Android, simu za mwanzo Kabisa zilizoanza kupokea Android 11 updates ni Google pixels, OnePlus, Oppo, Xiaomi na Nokia. Simu zingine zitapata Android updates week chache zijazo
Tuangalie features zilizomo [ uzi ]👇
◾️ MEDIA CONTROL
Media players zitakuwa zinaonyesha media controls zote ( prev, stop, next etc) moja kwa moja kutoka kwenye "toggle bar" ( Sehemu ya juu ya simu kwenye notification pannel ambapo itaonyesha wimbo, media husika na control zake)
◾️MEDIA OUTPUT ( Quickly select media output)
Sehemu ya notification pannel ambayo itakusaidia ku-sitch/badili ambapo unaweza kuchagua utumie speaker ya simu au Bluetooth device au device yoyote ambayo iko connected na simu yako kwa haraka zaidi.
Alizaliwa South Africa akiwa na miaka 17 alihamia Canada na baadae America, ni mfanyabiashara na mwanzilishi wa makampumi makubwa kama SpaceX, PayPal, Tesla Motors
Leo nimekuletea kila kitu kuhusu Elon Musk
✴️ Historia yake na familia yake
✴️ Biashara zake
Uzi
ELON MUSK NI NANI
Ni mzaliwa wa South Africa lakini sasa ana uraia wa Marekani na Canada, ni mfanyabiashara na mwanzilishi wa makampumi ya PayPal, SpaceX na Tesla Motors, alipata pesa akiwa na umri mdogo (20's) baada ya kuuza kampuni yake ya kwanza (Zip2) kwa Compaq computers
MAISHA YAKE YA UTOTONI
Elon Musk alizaliwa June 28, 1971 huko Pretoria-South Africa, Musk alizaliwa na tatizo la kusikia ila madaktari waliweza kumtibu akiwa mdogo.
Akiwa na miaka 10 wazazi wake walitengana na aliendelea kuishi na mama yake na ndugu zake wawili
JINSI YA KUIFANYA SIMU YAKO IWE NA NAFASI ( SPACE) YA KUTOSHA
Kwa watumiaji wa Android devices nimepata maswali mengi, simu zinajaa pasipo kuwa na vitu vingi kwenye simu
Leo tuangalie namna gani unaweza kuifanya simu yako iwe na nafasi ya kutosha
Twende na uzi
Wewe ni mtumiaji wa Android phone na umekuwa ukipata shida kwenye suala la storage, unaona kama una vitu vichache lakini storage imejaa
Basi jifunze vitu hivi ambavyo vimesaidia wengi katika kuifanya simu kuwa safi katika suala la storage
1: CLEAR CACHE
unapo-install application yoyote huwa zinatumia cache file ili kuweza kukupa urahisi wa kutumia app husika, lakini hili cache file haina umuhimu sana ukifuta vitu vilivyomo haiwezi kuleta madhara
✴️ Taarifa na vitu vyote kwenye mtandao huwa vinatunzwa wapi?
✴️ Serikali na makampuni binafsi yanatunza wapi taarifa zao?
Jibu: Taarifa na vitu vyote vya kimtandao duniani vinatunzwa sehemu inaitwa DATA CENTER
DATA CENTER NI NINI?
Uzi
DATA CENTER ni nini na inafanyaje kazi?
Data center ni sehemu maalumu ambapo vifaa vya computer na mawasiliano vimewekwa kwa ajili ya kukusanya, kutunza, kuchakata (processing) na kusambaza (distribute) taarifa zote za kimtandao Duniani
Data centers zinafanya kazi Mda wote (24/7/365) kuhakikisha haukosi taarifa au kitu chochote unachokihitaji mtandaoni.
Data Center inakuwa na SERVERS nyingi ambazo zimepangwa kwenye msitari pia computer zenye uwezo mkubwa (supercomputer)