Meme Coins au Shitcoins unaweza kuziita coins za majitaka au futuhi coins
Ni coins ambazo zimekua zikipendwa sana na watu wa Crypto kwa kuwa zinaweza kukupa faida hata mara 1000 ya mtaji wako kwa muda mfupi. 👇
Meme coins zimeundwa bila kuwa na matumizi yoyote muhimu kasoro kiki inayotokana na Jina la hiyo coin.
Katika msimu huu wa Crypto, shitcoins zimekua zikipatikana sana katika Blockchain inayoitwa Binance Smart Chain (BSC) kupitia website inayoitwa Pancakeswap
na kununua inabidi uwe na salio la coin ya BSC inayoitwa BNB na iwe ndani App ya TrustWallet...utatumia adress ya hiyo coin yako ili kuinunua
Kwa kawaida tumezoea Coin inakua na project fulani ili watu wawekeze.
Sasa hizi MemeCoins hazina project yoyote zaidi ya kupigiwa Kiki
Namna ya kununua Coins itaelezwa zaidi kwenye threads zijazo.
Meme Coin kubwa kuliko zote ni Dogecoin na inaongozwa na kiki za tajiri Elon Musk
Dogecoin iliundwa kama utani kwa lengo la kuwatania watu kuwa sikuhizi watu wanaunda coin za kijinga kwahyo yeye ameunda yake inaitwa Dogecoin ikiwa na Picha ya mbwa wa kijapani anaeitwa Shiba Inu
Hii Dogecoin inapanda thamani tu pale inapokuwa inatangazwa na watu kwa lengo la kuwa watakuja kutajirika siku moja
Katika msimu huu wa Soko la Crypto (2021) tumeona hizi futuhi coins zikiingia sokoni kila leo zikiongozwa na Safemoon coin ambayo
walioiunda walikiri kuwa waliiunda bila kujua itatumika kufanyia nini na hawakujua itavuma kama ilivyovuma.
Hizi Meme Coins au Futuhi Coins, zinaweza kukupa faida kubwa ndani ya mda mfupi endapo ukiweza kuzifahamu siri zake na ukazinunua katika msimu wake na muhimu zaidi
ukijua ni muda gani wa kuziuza, Msimu wa Shitcoins huanza baada ya Bitcoin na coins nyingine nzuri kuingiza pesa na waliotajirika kuanza kutambia wenzio hapo ndio wale ambao hatujui kitu kuhusu crypto tunaingia tunakuta hakuna coin za kununua ili tutoboe
...sasa ndio shitcoin zinaundwa kutudanganya kuwa tutatoboa.
Futuhi Coins siku inavyoingia sokoni hua zinanunuliwa haraka na wamiliki na watu wanaitwa 'Whales' au 'Nyangumi' kwa kutumia software maalum zinaitwa 'trading bots' ambazo zinafanya manunuzi haraka kuliko binadamu
zinakuwahi kununua kabla yako
Whales au Manyangumi ni watu wenye pesa nyingi kiasi cha kufanya bei ya Coin ipande haraka kwa muda mfupi..hawa watu hua wanapanga dili na wamiliki wa coins Wakishanunua awali ndio sisi tunakuja kuskia coin fulani ina trend
imeongezeka thamani mara 5 au 10 hapo ndio muda watu wengi tunainunua Tukishainunua inapanda thamani tena kwa kua tupo wengi, ila sasa huu ndio muda wale Manyangumi na wamiliki hua wanauza hizo Coins zao.
Ukichelewa hapo utaambulia hasara kubwa kwa kuwa wakiuza wale wakubwa utapata hasara , njia pekee ya kuzuia hii hasara ni kuipigia promo hiyo coin wenzio wanunue ili bei isishuke...
Kwa kua hiyo coin haina matumizi yoyote ni ngumu mno kuhamasisha watu wainunue..
hivhyo mbinu chafu hutumika mfano kukuambia kuwa utatajirika kwa muda mfupi pale utakaponunua na usiuze(hodl) hadi bei itakapopanda kufika mwezini au "To the moon" .
Mbinu nyingine chafu ni wamiliki walivogundua kuwa wakiweka thamani ya coin iwe na bei ndogo watu ndio watanunua
....zaidi wakiwa na imani kuwa itafika dola $1 au $10 Hivyo Shitcoins hizi hua na bei kama $0.00000001 na kwa kuwa watu hawajui basi hununua wakitegemea kuwa wamewahi ipo siku itafika dola moja watatajirika
Ukweli ni kuwa ukinunua Meme Coin mfano ShibaInu, ili ifike thamani ya $10 inahitaji fedha zote duniani tena uzidishe mara sita , zitumike kuinunue hiyo coin ndo itafika $10
Wengi hawajui haya mambo wanashindwa kujua ni muda gani sahihi wa kuuza hivyo hupata hasara mno
Hizi meme coins hua zina majina yanayovutia wageni wa hili soko na pia zinakuwa na majina yanayofanana au yanayoendana na Coin maarufu.
Pia kuna muda unaweza kuuziwa shitcoin ambayo utashindwa kuiuza pale faida zinapopatikana
kwakuwa wamiliki wanakua wamesepa na pesa zote zilizopo kwenye 'Float' (Liquidity) ya kubadlishia fedha zako
Shitcoins zina faida kubwa mno ila jua muda wa kuingia na wa kutoka, Pia watu wakubwa na ma rolimodo wako wanaweza kulipwa au kukudanganya makusudi ununue hiyo Shitcoin
ili yeye atajirike kwa kua anayo tayari Mara nyingine hata hao watu maarufu hili soko hawalijui watakuhamasisha ununue tu na kwa kua unawaamini unainunua...utaumia ndugu yangu. Usiamini sana watu kwenye cryptocurrency bila kufanya tafiti zako binafsi
Mwaka 2021 unatabiriwa kuwa na mapinduzi ya Tekinolojia, Apple wao wamejipanga kufanya yafuatayo
UZI
◾️Apple silicon iMac
Apple wanakuja na iMac ambayo itakuwa na Apple silicon chip, kama walivyofanya kwenye MacBook, itakuwa na16 high-power cores& 4 efficiency cores
◾️AirPods
2021 Apple wanategemea kutoa third-generation AirPods ambayo itakuwa na replaceable silicone air tips, pia wataboresha wireless chip na battery life
◾️iPad Pro
Apple wanakuja na 12.9 inch iPad Pro ambayo itakuwa na LED display, hii Min-LED Technology itakuwa na wide color gamut performance, high contrast and HDR, and local dimming, pia iPad Pro itakuwa na 5G connection ikisapotiwa na A14X chip kama ilivyo kwenye M1 Macs
◾️Hizi ni simu zinazotamba kwa sasa Duniani ikiwa ni matoleo mapya kwa Samsung na Apple
◾️Nakuletea ulinganifi wa hizi simu, hii ni kulingana na majarida mengi kama AndroidAuthority, CNet, GSMArena, Gadget360 n.k
Twende na uzi👇
◾️Samsung Galaxy Note 20 Ultra ilitoka Aug 5 na iPhone 12 Pro Max ilitoka Oct 13 lakini hii bado ni Pre-order
◾️Kila kampuni inasifia simu yake kuwa ni bora zaidi Duniani kwa sasa kutokana na teknologia ya hali ya juu iliyotumika kwenye hizo simu
◾️Tuzichambue taratibu
◾️DESIGN
👉 Simu zote zinamwonekano mzuri lakini kuna utofauti
◾️Samsung Galaxy Note 20 ultra ni simu yenye kuonekana vizuri sana, wamechukua designing ya matoleo yote ya Note series wakaleta hii Note 20 ultra, dimensions 168.4mm/urefu 77.2/upana 8.1/angle na uzito ni 208g
◾️ Encryption ni kitendo cha kubadili maneno au jumbe za kawaida kutoka kwenye mfumo unaosomeka kwenda kwenye mfumo ambao hausomeki, ambapo huzalisha kitu kinaitwa "cipher text"
Mfano kipindi cha utoto, watoto huongea kwa kuchanganya maneno ili watu wazima wasielewe wanaongea
nini, huu ni mfano wa encryption lakini endapo hiyo njia itatambulika kwa wengine basi hakuna tena usiri, wanaita "security through obscurity" yaani security huvunjika mara baada ya attacker kujua njia yako ya kujilinda
Katika encryption ili kuiondoa security through obscurity
Android 11 imetoka, ni jambo zuri kwa watumiaji wa Android, simu za mwanzo Kabisa zilizoanza kupokea Android 11 updates ni Google pixels, OnePlus, Oppo, Xiaomi na Nokia. Simu zingine zitapata Android updates week chache zijazo
Tuangalie features zilizomo [ uzi ]👇
◾️ MEDIA CONTROL
Media players zitakuwa zinaonyesha media controls zote ( prev, stop, next etc) moja kwa moja kutoka kwenye "toggle bar" ( Sehemu ya juu ya simu kwenye notification pannel ambapo itaonyesha wimbo, media husika na control zake)
◾️MEDIA OUTPUT ( Quickly select media output)
Sehemu ya notification pannel ambayo itakusaidia ku-sitch/badili ambapo unaweza kuchagua utumie speaker ya simu au Bluetooth device au device yoyote ambayo iko connected na simu yako kwa haraka zaidi.