#FAHAMU: ATHARI ZA UTOFAUTI WA KUNDI LA DAMU KATI YA MUME NA MKE.
Kuna baadhi ya wanawake wanapoteza mimba zao na wengine kupoteza watoto wao baada ya kujifungua sababu ikiwa ni utofauti wa kundi la damu kati ya mume na mke. Katika makundi ya damu kuna kitu kinaitwa RHESUS FACTOR
Kulingana na rhesus factors kuna makundi yafuatayo ya damu A+, A-, B+, B-, AB+, AB-, O+, O-.
Katika makundi ya damu mara nyingi mtoto hufuata damu ya baba. Hivyo, ikiwa kundi la baba lina antigen ya rhesus factor (A+, B+, AB+, O+) na mama akiwa hana hiyo antigen(A-,A-,AB-,A-)
Mtoto katika ujauzito wa kwanza atakuwa kama kundi la baba (rhesus positive) na hivyo mwili wa mwanamke utatengeza kinga (antibodies) dhidi kundi la baba. Hivyo katika mimba zinazofanya kiumbe kitakuwa kinashambuliwa na kinga ya mama (Rhesus incompatibility) #ElimikaWikiendi
Hii haitegemei na matokeo ya mimba ya kwanza;kama kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza salama, mimba kuharibika kutokana na sababu zingine/ mwanamke kuamua kutoa mimba.
Mimba zitakazofuatia zitakuwa katika hatari kubwa kuharibika au mtoto kufariki baada ya kujifungua. #ElimikaWikiendi
Damu ya mtoto itakuwa inavunjwa vunjwa (hemolysis) na kupelekea damu kupungua na kutengenezwa chembechembe (bilirubin) zinatakazomfanya apate manjano, kuvimba mwili kwa kujaa maji (edema). Kitalaamu hufahamika kama ERYTHROBLASTOSIS FETALIS #ElimikaWikiendi#ElimikaWikiendi
JINSI YA KUEPUKA TATIZO HILI
- Wezi wapime makundi yao ya damu kabla ya kuamua kuoana au kupata watoto,
- Ikigundulika wana utofauti wa makundi ya damu hatarishi mwanamke atashauriwa kuchomwa sindano (Anti-D) wiki ya 28-34 na masaa 72 baada ya kujifungua ili kulinda ujauzito ujao
Zaidi kwa mwanamke mwenye kundi (group O) anapopata mume mwenye kundi jingine la damu inaweza kuleta shida (ABO incompatibility) kwa mtoto kwa kupelekea ugonjwa wa manjano (Neonatal jaundice) na hata degedege ikiwa bilirubin ikikaa kwenye sehemu ya ubongo wake (Kernicterus).
TATIZO LA MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI VIZURI (HEART FAILURE).
Moyo ni kiungo muhimu ktk mwili kinachotumika kusambaza/kupokea damu sehemu mbalimbali mwilini (mapafu, ubongo, figo, matumbo n.k). Hivyo, moyo kushindwa kufanya kazi hupelekea mwili kukosa hewa na chakula. #Thread
SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA MOYO KUSHINDWA KAZI. 1. Shinikizo la damu lisilothibitiwa barabara 2. Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital) 3. Magonjwa ya mishipa ya moyo (coronary artery d'se/ischemic heart d'se) 4. Magonjwa ya tezi shingo (thyroid dysfunction) n.k
WATU WALIO KTK HATARI YA KUPATA TATIZO HILO NI; 1. Wenye shinikizo la damu 2. Kisukari 3. Wenye uzito mkubwa (obesity) 4. Watumiaji wa pombe na sigara 5. Wenye historia ya matatizo ya moyo kwenye familia yao n.k
TATIZO LA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI (KIDNEY FAILURE).
Figo ni kiungo muhimu sana kwenye mwili wa binadamu kwani hutumika kutoa takamwili kama; urea, maji ya ziada, chumvi n.k. Kushindwa kwa figo hupelekea takamwili kubakia mwilini hivyo kumletea shida mgonjwa. #Thread
SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI. 1. Kisukari 2. Shinikizo la damu 3. UKIMWI 4. Matumizi ya muda mrefu ya dawa zinazoweza kuathiri figo mfano; dawa za maumizi (diclofenac, ibiprofen n.k) 5. Matumizi ya miti-shamba 6. Pombe yaliyozidi
7. Ugonjwa wa figo kuwa na vifuko vyenye maji (polycystic kidney disease) 8. Matatizo yanayoweza kupoteza maji mwilini. Mfano; kutapika sana, kuharisha sana n.k 9. Maambukizi kwenye damu (sepsis).
FAIDA ZA KUNYONYESHA KWA MAMA NA MTOTO KIAFYA
Kutokana na utandawazi na harakati za maisha wanawake waliojifungua wamelazimika kutokunyonyesha watoto wao sawa sawa. Kitaalamu mtoto anatakiwa kunyonya miezi sita bila kupewa chakula isipokuwa dawa na chanjo tu #UZI
FAIDA KWA MAMA 1. Kumpunguzia hatari ya kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua 2. Ni njia moja wapo ya kupanga uzazi 3. Kumlinda dhidi ya kansa ya matiti na kansa ya kizazi 4. Kumjengea uhusiano mzuri na mtoto
FAIDA KWA MTOTO 1. Kuimarisha kinga ya mwili na kumlinda magonjwa mfano; magonjwaya upumuaji na magonjwa ya mfumo wa chakula kama vile KUHARISHA 2. Kumjengea uhusiano mzuri na mama yake. Hivyo kumfanya mtoto awe ni mwenye furaha na kuchangamka