, 10 tweets, 2 min read
My Authors
Read all threads
[HADITHI FUPI] Tizama vizuri viti walivyokalia waheshimiwa kwenye picha. Hivi sio viti mahsusi ambavyo Rais na viongozi wageni wake hukalia wanapomtembelea Ikulu. Kuna hadithi fupi ya hii picha 1/
Novemba 2007, nikiwa Msaidizi wa Rais Kikwete, tulipokea ugeni kutoka Ikulu ya Marekani ukitueleza kwamba Rais Bush anafikiria kutembelea Tanzania Februari 2008 – yaani miezi minne ijayo. Tulielezwa wachache sana. Nikapewa kazi ya uratibu wa ziara hiyo kwa shughuli za Ikulu 2/
Moja ya shughuli zilizopangwa ni kusaini Makubaliano ya MCC na press conference. Timu niliyofanya nayo kazi kutoka Ikulu ya Marekani ilikuwa thorough sana sana. Awali shughuli hizi zilikuwa zifanyike ndani kwenye kumbi za Ikulu kama ilivyo ada 3/
Baadaye kukatokea mapendekezo kwamba jengo letu la Ikulu lina historia na limejengwa kipekee. Kwahiyo tukakubaliana kujenga jukwaa mbele ya jengo, ili jengo liwe backdrop/background. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza hii kufanyika. Nikatafuta wadau sekta binafsi kutusaidia 4/
Awali press conference ilikuwa ifanyike 11am, lakini wakapima jua na kuona Rais Bush atatokwa sana jasho. Tukajadili kuweka mashine za viyoyozi mbali na kuweka “air ducts” chini ya podium ili AC iwapulize kimya kimya, lakini ikaonekana kwamba microphones zitasikia upepo 5/
Kwahiyo tukaamua kubadilisha ratiba ili press conference ifanyike mapema zaidi kuepuka jua kali la Februari. Tukaingia kwenye kujadili viti watakavyokalia viongozi wakati wa kusaini. Nikawaonyesha viti spesheli vya Rais 6/
Wamarekani wakaviangalia. Baadaye wakaomba kwa heshima tubadilishe. Tukakataa. Kiongozi wao akanichukua pembeni na kuniomba kwamba Rais Bush personally, viti vinavyozidi bega anaviona vya kifalme, na hapendi. Wenzangu wakaniambia nikaongee na Rais kumuuliza. I didn’t need to 7/
Nikaamua kwamba tutamsikiliza mgeni wetu. Kazi ikawa kutafuta viti mbadala. Mwishowe tukaingia kwenye chumba kidogo cha mikutano ya staff. Tukakuta viti zaidi ya 18 vya kawaida. Tukachukua viwili. Ndio hivyo unavyoona wamekalia viongozi hapo 8/
Kwenye maisha kuna mambo muhimu na ya msingi, ambayo hupaswi kuwa “flexible” na kuna mambo muhimu lakini si ya msingi sana ambayo unaweza kuwa flexible – na maisha yakaendelea kama vile hakijatokea kitu 9/9
[END] Baada ya ratiba za mchana, jioni ikawa dinner. Kwenye hizi dhifa, menu na ratiba huandikwa kwenye kijitabu mahsusi ambacho kila mgeni hupewa (kama souvenir). Nakaa mezani na kuangalia kijitabu, naona “George Walter Bush” badala ya “George Walker Bush”. Appetite ikapotea.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with January Makamba

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!