, 39 tweets, 6 min read Read on Twitter
KWANINI HARMONIZE ATATOKA WASAFI

THREAD:
ikumbukwe Miaka mitatu imepita toka kutambulishwa kwa msanii mpya katika lebo ya wasafi msanii Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize kitu ambacho kilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu yeye na familia yake na hata mwanamuziki yeyote anayechipukia kwani ni fursa ya kuweza kuonesha
..kipaji cha uimbaji kwenye kundi la watu wengi.

Wasanii wengi wanaochipukia wamekuwa wakiomba nafasi ya 'kupafomu' kwenye matamasha makubwa ili tu uwezo wao uweze kuonekana mbele za watu wengi wao hujitolea kufanya bure.
Ndio maana mwanamuziki Harmonize alipokuwa shimoni kabla ya kupewa fursa ya kusikilizwa na umma, alijaribu kwenda katika mashindano mbalimbali ikiwemo shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search ilionekana pia kutokubalika ktk uimbaji wake.Nakumbuka siku hiyo alikuwepo gesti
jaji Mcheza mpira kikapu maarufu nchini 'Hasheem Thabeet' alisikika akimrekebisha katika matamshi "Sio Maraika ni Malaika"
hivyo nimekumbushia hapo kwenye shindano hilo ili niweze kukukumbusha kwamba kukubaliwa sehemu na kuweza kushikwa mkono si kwamba unajua sana kuliko wenzako bali ni bahati tu imeangukia kwako ndio maana tunaona Wasanii wengi wanapewa nafasi redioni lakini uwezo wao unakuwa...
wa chini sana kiasi kwamba hata shabiki asiyefahamu uimbaji anakuwa anajua kabisa kwamba msanii huyo hajui.

Tarehe 6 ya Mwezi Novemba mwaka 2015 kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiongozwa na Msanii Diamond Platnumz ambapo alikuwa akisisitiza kwa wingi kwamba...
atatambulisha msanii kutoka katika LEBO yake WASAFI ambaye atakuwa msanii wa kwanza.
Mashabiki wengi waliomuamini msanii Diamond Platnumz na mimi mmoja wao tulikuwa na shauku kubwa kuskia kipaji hicho kipya chini yake, maswali nilijiuliza ni nani huyo ambaye kaaminiwa kiasi hicho nikawa sina wasiwasi na uwezo wake na kujipa asilimia mia kwamba ni lazima awe...
anafanya vizuri sana.Bwana Bwanaaa siku ya siku anatambulishwa msanii Harmonize kweli kama mashabiki wa Diamond Tuliomuamini hakutuangusha kabisa, Kibao cha kwanza tu Aiyola kilifanya vizuri kwenye chati nchini na nje pia kiukweli ilinipa furaha sana kuona muziki unakuwa kwa kasi
Ikumbukwe pia ushindani wa wanamuziki wawili Diamond na Alikiba ulikuwa uko moto sana kitu ambacho mashabiki tuliokuwepo nje ya muziki hatukuelewa tukahisi kwamba huenda mmoja kaachwa tayari ama yeye pia atakuja na Rekodi lebo ili kujibu mapigo.
Kumbe Hatukujua, nilifuatilia mahojiano ya msanii wangu pendwa Alikiba akiulizwa kuhusu wasanii hao katika LEBO ya WASAFI alivyoelezea alionesha kupendezwa na uimbaji wao na akadai kuwa huwa anawasikiliza na akasema anafanya vizuri. Basi bwana nilipendezwa na kitu hicho.
Tuachane kidogo na story za Alikiba ambaye alikuwa analeta chachu ya ushindani yeye na Boss wa Harmonize, nilichotaka kusema tu nguvu iliongezeka sana. japo kuna wengine walisema pia Sauti ya Harmonize inataka kufanana na ya Boss wake!...
mimi hilo sikulijali nilichokuwa nasikiliza ni mashairi, na kazi nzuri kutoka kwake
Walifuatana sana palipo Diamond panae Harmonize lakini walivyozidi kutambulisha wasanii wapya katika LEBO hiyo ukaribu ulipungua sana naona sasa mtoto alikuwa ameanza kujitegemea kutembea taratibu Mpaka Kenya kufanya colabo mpaka Nigeria kufanya collabo ambazo zimefanya vizuri
Inafika muda mtoto ameanza kujitegemea sasa na kuwakilisha WASAFI Vyema hata asipokuwepo Diamond palipo Harmonize wasafi inasimama vyema,Lakini hawa vijana kusimama pekee yao pia inakuwa ngumu nadhani ndio maana kuna kuwa na mameneja, washauri na Walezi Pia.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ni mmoja ya watu waliojitokeza na kuwa walezi wa WCB Wasafi nilipoziskia habari hizo nilifurahi sana kuona viongozi wanasapoti vijana kuhakikisha muziki unaendelea kuwa AJIRA na unaenda vizuri.
Na Juzi niliposikia Katika kikao fulani Mhe. Paul Makonda alisimama vyema kama mlezi na kumkana mwanae Harmonize na kutojihusisha na matumizi ya bangi na kama itagundulika ni kweli anatumia kuna adhabu yake kama mlezi ataitoa, nilipenda kuona hivyo nampongeza MLEZI.
Lakini pia Mlezi mara anapoona tatizo kwa mwanae mara ya kwanza huwa anazungumza naye pili anaposhindikana ndio anachukua maamuzi ya kumuadhibu au kuutangazia Umma kwamba Mwanangu kashindikana. Hata katika familia tabia huwa zinaanzia kukanywa ndani ya nyumba zinaposhindikana....
ndio hutoka mpaka kwa jirani. Mlezi Pia huwa ana mambo mengi mazuri aliyoyapanga kwa mwanae, Sasa pengine kuna jambo zuri linakuja mimi na wewe hatujui. Hata Alikiba Pia Hafahamu pia.
Sio Alikiba Pekee, hata Kings Music Records pia hawafahamu hayo mambo mazuri mlezi aliyopanga kwa mwanae, Nilisema hapo Awali kwamba muziki una ushindani kuna washauri pia ndani ya muziki huo, Tukizungumzia Kings Music, Kuwa na LEBO ni ndoto ya wasanii wengi.
Japo Kings Music ilipokelewa kama ni jibu la mapigo Kwa WASAFI. lakini naamini kila msanii anayo LEBO yake moyoni kuitangaza ni mipango tu haijalishi nani katangulia.
Ujio wa king Music umekuwa na mshituko mkubwa pia kwa WASAFI Kiushindani sasa naona majeshi yamekwiva pande zote mbili Vikosi viko sawa kupigana na KAZI na sio vita vingine, Kabla mshindi hajaonekana ni nani, HARMONIZE ATATOKA WASAFI
Ile kuambatana kwa Harmonize na Boss wake kupungua na kujitafutia chakula mwenyewe ni mbinu tu ambayo inamkomaza Kimuziki na Kutengeneza mashabiki wake pekee bila mgongo wa Boss. Naona hilo swala ameliweza kwa kiasi chake.
Lengo la kutoka linakuja kuhusishwa na tabia za kinidhamu, nidhamu ipi wakati Harmonize amekuwa akishukuru kila siku kufikia hatua ya kujichora tattoo ya boss wake kuonesha tu shukrani, Alipotoka nadhani anapaelewa vizuri Harmonize hawezi kubadilika kinidhamu kwa chochote kile.
Picha kadhaa hata video zimeonesha wasanii wakivuta Moshi na kutoa nje, wengine wanatumia Bhangi wengine sigara na wengine hakijafahamika ni nini, siri ya director wa video hiyo, lakini hao wamekuwa wasanii wakubwa kuliko hata harmonize, pengine labda hawana walezi kisanaa ndio..
maana wamekuwa wakiachwa kuonywa au kutumiwa Gavana kuthibitisha.
Nimesema Harmonize atatoka wasafi, lakini atatoka juu juu ya nje tu kuaminisha watu wa nje ambao hawazioni sahihi zake za mikaba,yaani kwa lugha nyingine ATATOKA KIUONGO.
Rajab Abdul Kahali Atakapotoka Wasafi atahama na mashabiki kadhaa ambao walimkubali yeye, waliikubali couple yake waliikubali kwangwaruu na Collabo zingine kali za nje alizofanya. Lengo kubwa ni Kushindana Wa nyumbani.
Ninaposema kushindana wa Nyumbani, hakika tuliokuwa na ndugu zetu tumewaacha madarasa tunalielewa hili, mfano mimi nilikuwa nashindana na Ndugu zangu kwenye matokeo kushika nafasi ya karibu darasani japokuwa walikuwa wamenizidi madarasa, lengo tu ni kurudisha Maslahi kwa wazazi.
Sasa Ule ushindani unarudi nyumbani sasa, baina ya Diamond Platnumz na Harmonize sivyo Diamond na Alikiba kama tulivyokuwa tumezoea au WCB WASAFI vs King MUSIC Kama tulivyokuwa Tumejiandaa. Hapa Suala la Rich Mavoko Tuliweke pembeni kidogo. Tutalirudia baadae.
Kwa Kudhani hivyo watu wasioelewa Wataamini nidhamu ndio imemtoa harmonize wasafi, Bhangi ndio imemtoa Rajab Wasafi, hapana Kama ni moshi mbona boss wake amekuwa akiweka picha katika mitandao akitoa moshi na hakuwahi kutumiwa Gavana kuchunguza?
Tamko hilo limetolewa na mtu muhimu kwenye uongozi ili kwamba angelitoa Diamond lingepokelewa kama kiki ya wazi wazi
HIVYO TUJIANDAE KUSKIA AMETOKA KWA NIDHAMU MBAYA, HIYO INAITWA BIASHARA
Hii inanikumbusha na habari fulani zinazosemwa juu ya wasafi na cloudsfm kwamba ni ndugu, basi bwaaana Mimi na wewe hatujui ngoja Tuendelee kuliangalia hii movie yenye masteringi kibao...
Je, Lengo ni Kumshusha Kiba? Au kiba na team yake(Kings) Au aliyemletea Kiba ndio Kamleta Diamond na ndio Kamleta Harmonize? Je, Kiba na Diamond ni watoto wa baba mmoja kisanaa? Je Mavoko naye bado yupo WASAFI?
Asante Sana, Nikutakie Wakati mwema!
Unaweza Ukashea Hii popote pale na wengine wafahamu...!! Wachangie Tuskie mawazo mbalimbali.
-Edwin Masobeji
HII SIJAKOPI POPOTE 😂😂🤣
Missing some Tweet in this thread?
You can try to force a refresh.

Like this thread? Get email updates or save it to PDF!

Subscribe to Edwin ℳasobeji
Profile picture

Get real-time email alerts when new unrolls are available from this author!

This content may be removed anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!