(Thread)
Yafuatayo ni maelezo ya namna ya kuomba fursa za kimasomo nchini China
Maelezo haya yameandaliwa na Watanzania wanaosoma China-
kupitia HEOCT (Higher Education Opportunities in China for Tanzania)
{Huduma hii inaendeshwa BURE kwa kujitolea}
Huduma hii inaratibiwa na Shirikisho la Jumuiya za Watanzania wanaosoma China @TASAFIC kupitia makundi ya WhatsApp
1. Chinese Government Scholarships-
Imegawanyika sehemu kuu mbili-
•Unaweza kuomba hiyo scholarship directly vyuoni kupitia katika website za vyuo husika
(Vyuo husika hutumika kama agency-
Hii huwa nzuri maana Chuo kikisha kukubali, CSC wanapitisha moja kwa moja.
Katika kuomba hii utatumia Agency number- ya chuo husika wakati unajaza online.
List ya universities agency numbers zipo kwenye website ya CSC
au njia zozote za usafirishaji kulingana ma maelezo yanayokuwa yametolewa katika website ya chuo husika.
Tangazo hutolewa wizara ya elimu na TCU.
Tangazo hili huwa na vigezo vya ziada pia vinavyo ongezwa kwa utaratibu wa nchi yetu.
Hapa ukishajaza documents zako unazituma TCU na zitafanyiwa kazi na majibu yatatolewa na wizara ya Elimu.
Vyuo pia vina aina zao za scholarships.
Hii unaimba chuoni na taarifa zake hupatikana kadri unavyo fungua website za chuo husika
Nyingi sana sio FULL scholarships bali Partial scholarships
{ile number moja ya Serikali ni Full unapo ipata}
Hii number tatu nayo mfumo wake wa kuiomba ni kama wa number 2.
Ila tu tofauti yake ni kuwa hii hutolewa mara nyingi kwa wanao soma lugha ya KICHINA na mambo ya Utamaduni wa Kichina (Masuala ya Kiasili ya China)
Hizi ni Scholarship za Serikali za majimbo China
Anaweza kuomba mtu yeyote na utaratibu ni kuingia website za vyuo ulivochagua na kusoma details vizuri.
Nazo zinaweza kuwa PARTIAL au FULL katika ufadhili wake.
Hii ya mwisho kwa karatasi hii. Inajielezea kama jina lake hutolewa na Rais wa Jamhuri ya watu wa China (kupitia Ofisi ya Rais wa China)
Nayo huombwa na mtu yeyote unaweza pia pata ikiwa FULL au PARTIAL.
Hii ni aina ya scholarship ambayo Watanzania tunaweza kunufaika nayo.
Huombwa kupitia Ubalozi wa China, Tanzania. Huwa na vigezo vya ziada na limit ya waombaji.
Hii inafaida nyingi ila Wanufaika wake kwa asilimia Kubwa ni WATUMISHI WA UMMA
Zikiwemo;
•OIL AND GAS SCHOLARSHIP- Hii utangazwa ndani ya wizara ya nishati kwa ajili tu ya kusoma mambo ya OIL and Gas
•BELT AND ROAD SCHOLARSHIPS
Pamoja na Scholarship nyinginezo zinazotolewa makhsusi kwa fani mbalimbali
Kuna Scholarship zinatangazwa na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-
kupitia Wizara mbalimbali;
(hapa kuna umuhimu wa kufuatilia Matangazo ya Wizara za Nchi yetu)
Njia Kuu ni kupitia Tovuti za Scholarships za China 🇨🇳
cscscholarship.org/subject-wise-u…
(hizi hujazwa kwenye fomu za kuombea Scholarship nchini China)
cscscholarship.org/chinese-univer…
(Chinese Government Scholarship)
Yaani Viambatanishi na Process nzima:
mp.weixin.qq.com/s/3s3qpQ0Wvrei…
NB: Ubalozi wa Tanzania Nchini China- hutuma taarifa za Fursa Mbalimbali Nchini China zikiwemo Fursa za Kimasomo mbalimbali zinazoweza kuchangamkiwa na Watanzania @TZEmbassy
🇹🇿🇹🇿🇹🇿