My Authors
Read all threads
UZI MREFU KUTOKA KWA RASTA

TAREHE ya leo, 6 Februari miaka 75 nyuma (1945), mwanamke wa Kijamaika kutoka kijiji cha Nine Miles, St. Ann's Parish, Cedilla Editha Malcolm maarufu kama Cedella Booker alimzaa mtoto wa kiume, Nesta. Jina kamili la mtoto likawa Nesta Robert Marley.
Neno 'Nesta' linamaanisha 'Mtume Mwenye Hekima.'

Alimzaa akiwa na umri wa miaka 18, na Kepteni Norval Sinclair Marley aliyekuwa afisa wa serikali, Mwingereza mwenye asili ya Uyahudi wa Kisyria. Hata hivyo, ndugu wa Kepteni Marley hawakuiafiki ndoa ya ndugu yao na mtu mweusi.
Nesta alifahamika pia kama Robbie kwa vijana wenzake wakati akisoma na kujifunza muziki mtaani.
Kepteni Marley alihamia kikazi Kingston, mji mkuu wa Jamaica. Cedella akapata tetesi mumewe kaoa mke mwingine. Alipothibitisha, akapigana naye chini. Kepteni Marley alifariki mwaka 1955, Nesta akiwa na miaka 10. Nesta aliwahi kumwona baba yake mara moja tu maishani mwake.
Cedella akaolewa Taddeus Livingstone, baba yake Bunny Wailer. Akahamia Kingston. Wakazaa mtoto mmoja wa kike Claudette. Ndoa yao haikudumu sana. Kwenye moja ya mahojiano yake, Bob Marley anasema, ingawa Taddy aliwanyanyasa, anamthamini kama mwanaume wa kwanza kumnunulia viatu
Miaka ya 1960 mwanzoni, Cedella aliolewa na Mmarekani, Edward Booker na hivyo kuhamia Marekani. Walizaa watoto wawili Anthony na Richard. Anthony aliuawa na polisi jijini Miami akiwa na miaka 12. Ndiyo sababu ya wimbo wa 'Johnny Was A Good Man' miaka ya baadaye.
Cedella akiwa Miami, alimtumia mtoto wake nauli ili amfuate.

Wakati huo, Robbie alikuwa ameanza masuala ya muziki. Lakini, muziki huo haukuwa ukimpa maslahi yoyote kumfanya amudu kuishi.
Vilevile, alikuwa amekutana na msichana Alfarita Anderson, aliyekuwa akiishi kwa shangazi yake, huku akiwa na mtoto mmoja wa kike, Sharon.
Nesta alikwenda Idara ya Uhamiaji kuomba pasipoti aende Marekani. Msichana mrembo, AfisaUhamiaji alimwambia Nesta kuwa jina lake ni la kike.

Akabadili mpangilio wa majina yake. Akamwandika kwenye pasipoti kama Robert Nesta Marley.

Ndiposa, akaanza kujiita Bob Marley.
Ili kuepuka vijana wenzake kama Bunny na Peter kumpiku kwa Alfarita yeye akiwa Marekani, akamwoa kabisa mpenzi wake, ambaye tayari alianza kumwita Rita.
Bob na Rita walizaa watoto wanne, huku Bob akiwaasili watoto wengine wa Rita. Wamo kwenye orodha ya watoto rasmi wa Bob. Bob alizaa na wanawake wengine tofautitofauti. Jumla ya watoto rasmi wa Bob ni 11 ingawa wapo wengine wawili wasio rasmi na kufanya idadi kuwa 13.
Aliporudi Jamaica, Bob na wenzake waliendeleza sana muziki mpya wa reggae. Wakauweka kwenye ramani ya dunia kiasi kwamba, sasa ukiwa na umri wa miaka 55, reggarle ungali muziki maarufu duniani.
Habari zake muziki zinafahamika kote ulimwenguni. Alizaliwa kwenye kijumba cha kimasikini kijijini Nine Miles. Alikufa mwaka 1981 akiwa mtu maarufu ulimwenguni akimiliki studio kubwa na nyumba 56 Hope Road, jirani na nyumba ya Waziri Mkuu.
Upande mwingine wa Bob ulihusu wanawake. Ingawa Rita alikuwa mwanamke wake wa kwanza maishani, mahusiano yao hayakuwa tambarare.
Rita alipoona Bob amekuwa mwingi, akanunua nyumba nje kidogo ya Kingston ili kuishi na wanae. Bob akaweka chumba cha kulala studio kwake. Rita anasema, vigoli walipishana.

Rita anasema, hamlaumu Bob kwa kuwa alikuwa 'too attractive' kiasi cha kuwa 'irresistible' kwa wasichana.
Bob alikuwa na mahusiano na Miss World 1976 Cindy Breakspeare (mama wa Damian Marley) na kukesha naye studio.

Akamwandikia nyimbo mbili tamu zaidi za mapenzi kutoka kwa Bob; Waiting in Vain (wakati akimfukuzia) na Turn Your Light Downlow (alipompata).
Rita aliposhitukia hizo nyimbo ni za mchepuko wa mumewe, akagoma kuziimba kama backing vocal kupitia I-Threes. Bob pamoja na vurugu zake zote, alimwogopa Rita.
Bob akaandika wimbo wa No Woman No Cry kubembeleza Rita, huku akimhakikishia kila kitu kitakuwa sawa. Vilevile, aliandika wimbo wa Jump Nyabinghi akimwambia Rita kuwa anapenda kumwona akiimba na kucheza reggae, kwa sababu inampa furaha kuuona upamoja wao mtamu.
Mwaka 1974, Rita alimzaa Stephanie na mwanaume mwingine, Ital. Bob hakuwa na nongwa. Alimkubali mtoto na kumruhusu aitwe Stephanie Marley. Ingawa Bob na Rita waliendelea kuwa pamoja hadi kifo chake 1981, mahusiano yao yalikufa mwaka 1975, Rita akimtuhumu Bob kuwa mwingi mno.
Kwenye kitabu chake, Bob Marley, My Son (2003), Cedella Booker anasema Rita hakuwa mwaminifu ndiyo maana Bob akaanza kurukaruka. Cedella anakwenda mbali kwa kusema, kutokana na kutokuwa mwaminifu, Rita alimsababishia Bob magonjwa ya zinaa.
Lakini, kwenye kitabu chake cha No Woman, No Cry: My Life with Bob Marley (2004), Rita Marley anasema, Bob aliwahi kumbaka mwaka 1975. Rita anaandika, kutokana na Bob kuwa kicheche, akaamua kutohusiana naye kindoa.
Pamoja na kumwambia kwa nini hawezi kumpa tena unyumba, Bob alimjia juu na kumwambia yeye ni mke wake hivyo hawezi kumnyima. Akafanya naye kwa nguvu.
Bob aliachana rasmi na imani ya Kirastafari na kunyoa Rasta panapo 4 Novemba 1980 alipobatizwa katika Kanisa la Orthodox, akpewa jina la Berhanie Selassie.

Alifariki kwa kansa Mei 11, 1981 mjini Miami, Marekani akiwa na miaka 36. Alizikwa kwa heshima ya kiserikali Mei 21, 1981.
Ingawa Bob Marley aliishi duniani kwa miaka 36 tu, ameacha urithi mkubwa kwenye muziki wa reggae, upendo na utetezi wa amani.
Kazi zake katika kuleta amani na utengamano zilimfanya kuwa Balozi wa Amani wa Umoja wa Mataifa, baada ya kuwapatanisha mahasimu wakubwa kisiasa nchini mwake, Michael Manley na Edward Seaga.
Jamaica ilimpa Bob nishani ya juu zaidi nchini humo, Order of Merit na kufanya jina lake kuwa rasmi kiserikali kama Hon. Robert Nesta Marley, O.M.
Bob Marley alikataa kwenda vitani Vietnam. Akiwa kwenye kilele cha mafanikio, CIA walitaka kumtumia. Alikataa. Baada ya kuwagomea CIA, Bob aliandika wimbo wa Rat Race. Ndani yake akasema, Rasta hawezi kuwafanyia kazi CIA.
Kwa kuthamini mchango wa muziki wa reggae ulioasisiwa na Bob na wenzake, UNESCO imeutangaza muziki wa reggae kama urithi wa dunia.
Nchini kwake Jamaica, hadi leo, kuna bango kubwa lenye picha ya Bob Marley na maandishi, 'JAMAICA SALUTES YOU FOR YOUR COURAGE.'

Nasi pia, let's do things that our nations will salute us for our courage.

MWISHO WA UZI.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Fadhy Mtanga

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!