, 10 tweets, 2 min read
My Authors
Read all threads
UZI WA MJADALA WA KIMOMBO NA KISWAHILI: SOMO KUTOKA CHINA

1. Imekuwa ni mazoea kuona China ikitajwa kwenye mjadala wa lugha hapa kwetu Tz. Mara nyingi China hutajwa ktk muktadha wa kuonesha kwamba si lazima sana kujua kimombo. Mbona Wachina hawakijui na wameendelea? Wanahoji.
2. Nataka nianze kwa kusisitiza, tuna ulazima wa kukijua kimombo. Tena tukijue vizuri kabisa. Tukiwa UDSM kama wanafunzi, Mwalimu Lwaitama aliwahi kutuonya kwamba tusijifiche kwenye uzalendo wa Kiswahili ikawa ndiyo kisingizio chetu cha kutojua na kuzungumza vizuri kimombo.
3. Mjadala ulioibuliwa karibuni una makundi mawili: wapo wanaotaka tukimudu kimombo, wapo wanaosema si lazima sana, mbona China hawakijui? Baadhi ya kundi la kwanza ni wale wanaotaka tutumie Kiswahili kujifunza kimombo. Hapo ndipo na nilipo mimi. Hili tutajadili siku nyingine.
4. Nataka kutoa uzoefu wangu kidogo tu kutoka China. Kinachoitwa Kichina au Mandarin ni lugha kama Kiswahili. China ina lugha nyingi kama sisi tu, kila sehemu ya China wana lugha yao - kama sisi tulivyo na lugha mbali mbali ukienda Mbeya au Mwanza, au Singida.
5. Kinachoitwa Kichina ni moja ya lugha hizo nyingi ila waliamua kuifanya iwe lugha rasmi na ya kufundishia mashuleni - msingi hadi vyuoni. Sisi hatujafanya hivyo kwa Kiswahili. Hoja kwamba Wachina hawajui kimombo lakini wameendelea haiakisi shauku ya Wachina kukijua kimombo.
6. Wachina wanajifunza kimombo 'kwa fujo' sana. Ukiwa Mchina kisha ukawa na umahiri wa kimombo unatamaniwa! Watoto wa Kichina, hasa wale wa sehemu za mjini, wanajifunza sana kimombo, tena kile cha Kimarekani. Wazazi wanahimiza watoto wao wajue kimombo. Hawaoni sbb kwanini wasijue
7. Hawajifichi kwenye uzalendo wa Kichina kukipinga kimombo. Hawajifichi kwenye kisingizio cha kwamba ni lugha ya mabeberu (China pia ni walikuwa wahanga wa ubeberu kwa miaka 100). Wanataka kujifunza. Wanaamini kuna fursa inayotokana na kujua kimombo, ikiwemo kujiongezea maarifa
8. Tukubaliane: hitaji la kujua kimombo ni kubwa mno. Tunaweza kutofautiana juu ya namna ya kukifundisha mashuleni lakini katu si juu ya umuhimu. Pia, kuendelea kujificha nyuma ya pazia la 'lugha ya kikoloni' haisaidii. Majina yetu, imani zetu, mavazi n.k ni zao la ukoloni.
9. Mwisho, tuache kudhihakiana pale tunapokosea kimombo. Wengi wanaodhihaki wala hawana umahiri wa lugha hiyo. Dhihaka imetujengea hofu kubwa ya kujua kimombo. Tunaogopa kukosea. Tutachekwa. China pia wana tatizo hili la kuchekana au kunyong'onyezwa pale mtu anapokosea. Tuache.
10. Ohoo! Mwisho kabisa, kabisa kabisa, haya niliyoandika juu ya China yanatokana na uzoefu wangu nilipokuwa kule. Mwingine anaweza kuwa na uzoefu tofauti na wangu. Naamini vyote ni sehemu ya ukweli.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with SHANGWE

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!