"ZINGATIA..☝️"
Retweet kwanza

Ni saa nne za usiku na mvua inanyesha tofauti na ilivyozoeleka ila naanza kuona mataa ya mji wa Dodoma..safari bado na njaa inauma..naona nikifika centre nisimame kidgo..stop ya kula ni Chako ni Chako kuna kuku wa kuchoma..nakula na kubeba nyingne..
Huwezi jua njian kuna mengi chakula muhimu..nakiwasha tena..napoanza kuitafuta Moro njiani malori mengi na ni usiku hvyo naenda kwa mwendo wa kawaida..nsije nkapunguza miaka ya kuishi..kamziki kwa mbali huku nasikia wiper zikifanya kazi kwa bidii ili tu nione uelekeo.
Baada ya kilomita 1..ndipo namwona
Koti kubwa likificha sehemu kubwa ya mwili wake zaid ya miguu iliyofunikwa na jeans nyeusi na raba..kanyoosha mkono kwa bidii kweli..
Nampita..ila baada ya kuona kuna basi dogo jingne pembeni na abiria ndani limesimama nikasimama
Nikarud nyuma kidgo huku nafsi inajisemea
"wema utakujaga kuniponza uniue unasimamaje usiku huu barabarani kumsikiliza mtu usiyemjua,movie zooote ulizoangalia..pumbav"
Naangalia kioo cha nyuma naona anahangaika kidgo na begi lake lililoonekana ni zito.. nkasema sishuki Apambane
Natoa lock..anafungua mlango wa nyuma..begi limelowa analirusha kwa seat haraka na kupanda mbele..tunasalimiana huku akiomba samahani kwa jinsi alivyoloa,,nywele zilizosogea hadi machoni zikimwaga vitonye..ananiuliza kama naelekea dar..nasema ndio..anashusha pumzi..
"Naomba twende wote maana nna kikao kesho asubuh ofisini na gari nililodhani litanifikisha mapema ndo lile limekwama..hapa nilikua najaribu kivyovyote niweze fika Dar kabla ya alfajiri.."
Namwambia haina shida..
"Ntakupa hela ya mafuta tukifika kwangu..ntashukuru sana"
Namchek..mtoto si haba..ana nyama sehemu muhimu maana sio kwa alivyoijaza seat vizuri..af cheupe flani.
Ila sijipi moyo..simjui..hanijui..hatujuani,ila tuna safar ndefu bado..natoa hazard lights nakiwasha..navuta mfuko nyuma nampa..haamini anapoona tujipande twa kuku.."ulijuaje?"
Nampa ka smile flani..
Alikua na njaa kweli..maana hakuongea kitu..alivyomaliza ndo akaanza maswali..

Nilijaribu kuyajibu..sema alionekana ni manzi mcheshi..mwongeaji..full of life..one thing ni kwamba katika maongezi yetu nilijua ana mchumba
Kidgo ikanifanya niwe na adabu kwa yale nnayotamka..
Akawa anahangaika na simu huku akilalamika mtu anayemtafuta amezima simu..na inabidi amwambie kwamba aje kumchukua kimara pamoja na hela aliyoniahidi..maana mi naishia hpo..ye anasogea mikocheni..
Najaribu kuikataa ila anakazia
Saa tisa na nusu tunaingia jijini..nafika kimara bado mtu hajapatikana..anaona kama vipi achukue boda..ila naona isiwe shida acha nimpeleke asije kupigwa tukio..ananielekeza hadi anapoishi..ni tuji apartment tuzuri..huyu wa kishua huyu basi tu ni wa kishua aliyechangamka
Namsaida kushusha begi huku akisisitiza nisubirie "huwezi kuondoka hvi hivi, i beg u"
Naingia kwa gari huku nasikilizia..dk 10,17,20..naona heh..vipi tena mbona anasumbuka sana sa hvi ningekua nakaribia kufika..sijui nishuke nikamcheck nimwambie aachane nazo tu atanitumia
Af kweli bhna atleast ntapata namba yake..ile nataka kushuka naona geti limefunguliwa kwa nguvu..anatokea manzi huku kama anakimbia..akili inajaribu waza ni nn kinaendelea..anafika upande wangu nafungua mlango anasimama huku analia..na hela mkononi..ananipa..namuuliza tatzo nn?
Hapo ndo machozi yanazidi kummwagika..namshika mkono huku namvuta kumbembeleza ili nijue nn tatzo..naamua tu nimvute nimweke kifuani..maana ndo naonaga kwenye mi movie ya mbele wanafanyaga hvyo..

"I cant take it anymore..mara ya tatu hii namfumania but why??"
Nakosa cha kujibu..ila nashangaa zaidi kutokumwona hata huyo mchzi akija labda kuomba hata msamaha..zile movment zinazotokeaga mtu akifumaniwa..itakua fumanizi za kishua hizi..inabdi niulize jamaa yuko wap..
"Wapo ndani na my best friend..i jst cnt believe it,wanaona aibu kutoka
Namuuliza.."so what are you gonna do"

"Twende wote unapokaa..najua umenisaidia mengi ila kwa leo tu"
Siamini flani kama pisi kama hii naweza kuondoka nayo ila kimoyomoyo najua hamna kitu itatokea..
SIKULA usiku huo kwahyo msiniulize😅..ila niliamka usafi umefanyika na chai tayar
Nilijua wakishua hawanaga hizo..tulispend siku nzima na nikamzngua akae inayofata..alikaa ndo NIKALA..
Siku anaondoka ndo nilimpa namba yangu akasema atanisaka..hakuwahi kunitafuta kamwe na nilishamsahau..
Nipo Bar nachek game ya Simba na El merrekh inaingia text tigopesa ya kilo 2..namba siijui..af text inatumwa..njoo Moyo mi Natasha..nafika..hapa ndo nauona ushua wake..katikati ya mazungumzo anaexplain kwann hakunitafuta
Af ananiuliza "Una mtoto?" Nasema sina "Una mchumba ambae uko serious nae kwamba waweza muoa" hapo nashndwa nijibu vipi huku nikiwaza "mchumba nnae ila sijawaza ndoa coz ye anaona bado na siku ya pili hajanijbu txt wala my calls myb yupo busy
Ananiangalia kwa muda lips zake zikivuta juice kwa mrija "NIOE"

Nashindwa kumjbu zaidi ya kumwambia anipe muda nicheck mambo yakoje.
Namsindikiza kwa gari yake anani hug akiparaza busu shavuni anaingia kwenye gari "weekend njoo kwangu nimehama tu booze kidgo ntakutumia location
Natikisa tu kichwa..mambo ni mengi muda ni mchache..anawasha gari anaondoka..
Huku naangalia gari likitokomea natoa simu kwa jeans nampigia bebe..inaita

"Namba unayopiga inatumika kwa sasa...."
hapo ndo naona
MAPENZI ni KAUSHENZI flani..

#fanani ✍️ hapa

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Urs truly✍️

Urs truly✍️ Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @crazyTanzanian

20 Nov 20
"SIRI YANGU🤫"

Napiga pafu moja kutoka kwenye glass...mkono unanipiga begani,tuji bia tunanimwagikia kidogo kwa tshirt,,naangalia nyuma kuangalia ni nani huyu fa**..
Nakutana na cheko moja la kihuni..kumbe Jose,
"Mjinga umemwaga bia yangu"
Ananicheki kwa dharau..anaita muhudumu ananiongezea mbili...
Inabidi nimuulize "hii jeuri imeanza lini kapuku wewe..😅

Anantizama af sura inabadilika.."kuna hela nilikua nadunduliza nimtoe mtoto wa mtu ila acha tuinywee tu bia..atleast siku niseme na mimi nshawahi kukutoa"
Nakaa nae kwa masaa kadhaa..kwakua mwana anafanya kazi ya boda naona kabisa narudi gheto vizuri kabisa...
Muda unayoyoma...nakuja cheki saa saba na nusu..nanyanyuka huku nikiwaambia wana wengine "kesho nayo siku"
Napigwa vijembe kadhaa pale..sijali namshtua mwana anisogeze ghetto
Read 18 tweets
23 Oct 20
"NILILAMBA JOKERI🃏.."

Nipo kwenye gari nna hasira flani..nafungua whatsapp natafuta convo yetu mwanzoni kabsa..naandika "mnazingua"
Huyu ni rafiki angu wa kike,Ney, tumepanga kwenda premier ya movie flani ilikua inatoka af tuna ka dk 10 ianze,ameomba aje na rafiki zake wawili
Mi nipo na mchizi,ye ndo kamaindi mbaya. Kanimaindi mimi pamoja na huyo rafiki angu.."kubabeki,tunaenda kuanza movie nusu..si bora tukanywe bia tujue moja" 🤔nkawaza sio wazo baya ujue..
Mara nasikia milango inafunguliwa siangalii hata nyuma nawasha gari..
Nasikia sauti ya ney "kelvin,we are sorry" naongeza sauti ya mziki..
Mchzi anageuza shingo anawasalimu..naona kashalegea kuona vimwana,anaanza kuwapigisha stori pale
Njia nzima nipo kimya..hadi tunafika.
Wanashuka na mimi kma dereva nachek kma vitu vipo sawa kabla sijashuka
Read 17 tweets
15 Aug 20
"THUBUTUU...🤧"

Sijui ilikuwaje hadi nkasahau kuandika kuhusu hiki kisa..🤭
Nadhani kwasababu mchizi hakua mtu wangu wa karibu sana..ilikua ni kuonana kwenye vigenge vya stori na kitaa.

Ila siku tulijikuta wawili tu kwenye kota za tanesco anapokaa,chobingo moja yetu pendwa..
Mchizi aliitwa Saleh..
Tulisalimiana kiwana tukiulizana mishe zinaendaje na vijistori vya hapa na pale vya kupoteza muda.
Mchizi alitoa sigara mbili huku akiniuliza kama natumia..nilimjibu situmii hvyo aliiwasha yake akavuta pafu mbili kubwa..alitoa moshi nje af akabaki kaduwaa
Ilibidi nimuite mara mbili,aliposhtuka ilibidi ajicheke..nikamuuliza vipi asee mbona umeniacha peke yangu..
Nakumbuka alinambia
"aahh kmmk,nna kipengele kimoja hicho na sijui itakuaje" nkamwambia "nipange"
Alisita kidogo akaangalia sigara yake kidgo kisha akaanza kunipa stori
Read 26 tweets
27 Jun 20
"KARMA..🎭"

🌡Kama huna kifua basi usisome uzi huu haukufai maana mi natoa visa vya ukweli kama ifuatavyo...👇

Nipo na mwana ananionesha picha af ananiuliza "unaikumbuka hii"..naichek af nacheka ni picha ya kitambo kidgo,tukiwepo sisi na wasichana watatu..mmoja wao akiwa VERO
Vero mi nilimjua kipindi anatoka na mchizi wangu huyo..baada ya kukutana nae viwanja..tulikula sana bata za hapa na pale na huyu manzi,kipindi hicho anakaa mitaa ya sabasaba na wenzake.. walikua wamoto..kila weekend lazima niulizwe "shem leo wap!!nna rafki yangu nataka nikususie"
Kiukweli mchizi wangu alikua sio mtuliaji so wana tulikua tunajua saa yoyote kinaweza nuka..ila cha kushangaza haikua hvyo kwa muda mrefu..nadhani style za maisha ziliendana kiasi kwamba ilikua haiboi..
Basi hapo kati Vee kama nilivyokua namwita akapata mimba ya mchizi
Read 18 tweets
7 May 20
"LAANA...."🧞‍♂️

Wiki moja baada ya kuanza darasa la kwanza kutokana na umbo langu kua dogo kidgo kuliko wengne ilinipa ugumu maana nilishindiliwa uonevu wa kila namna..ila siku,mmoja wa wanafunzi alinikingia kifua..na si mwingine bali ni "MUDI" kama wengi tufupishavyo, jembe langu
Sikuwah kuonewa kuanzia siku hiyo na ndipo nilipojifunza ubabe..sikuwah kumwambiaga ila alikua kama kaka angu japo tulikua umri sawa ila kwa mwili wake na udogo wangu tofauti ilikua kubwa,alikua ndo rafiki wangu wa kwanza kishule shule. Alinifunza kujihami,kujilinda na ni yeye
alinifunza utukutu..asee shule nzma ilikua inamtambua. Kwa kila walimu walichomsema basi na mm nilihusika ila kwakua wengi hawakuamini mi kuhusika ivo mudi alichkua adhabu zote na hakuwah kunitaja. Ila nami nilihakikisha hafeli mitihani kwa njia yoyote na hakuwahi kuniangusha
Read 22 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!