ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
PART 2
Sasa basi,
Wale maaskari wawili ambao walifika Upanga nyumbani kwa Mohammed al-Asad sio tu kwamba walikuwa wamevalia kiraia tu, bali pia walifika wakiwa na gari yenye plate number za kiraia pia.
Kwa hiyo...
wakamwambia al-Asad kwamba wanahitaji kwenda naye kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiani mafupi.
Kama ilivyo kawaida al-Asad akawauliza mahojiano hayo yahusu nini haswa? Polisi wakamjibu kwamba atafahamu huko huko kituoni akifika
Bila hiyana al-Asad akaaga familia yake na kisha
akaingia kwenye gari ambalo wale askari waliwasili nalo na kisha wakaondoka.
Gari ilipowashwa iliendeshwa mpaka kufika uwanja wa ndege Terminal 1 kwenye hangar ya kampuni ya Tanzania Air Services (Sio Air Tanzania.. hii ni kampuni binafsi ambayo bado ingalipo hata sasa nchini...
hawa wenyewe wanafanya biashara ya kutoa huduma ya usafiri wa anga kwa charted na private planes. Kwa mfano hata sasa hivi ukienda pale uwanja wa ndege Terminal 1 wana karakana yao. Hii ndio kampuni ya kwanza nchini kupewa kibali cha kufanya service ndege za Cessna).
Kwa hiyo..
ile gari ikafika mpaka hapo kwenye hangar ya Tanzania Air Services.
Walipofika wakamkabidhi al-Asad kwa wazungu wawili ambao walikuwata hapo wanawasubiri.
Wale wazungu wakamtia pingu al-Asad na kumveka tambara jeusi usoni ili asiwe kuona na kisha kumpakia kwenye ndege ndogo aina
ya Cessna F406 Caravan II, ambayo mkiani ina namba ya usajili 5H-TZE mali ya kampuni ya Tanzania Air Services Ltd.
Ile ndege ikaruka moja kwa moja toka hapa Dar es Salaam mpaka nchini Djibouti kwenye mji unaoitwa Ambouli ambako vikosi vya Navy vya Marekani wana kambi ya kudumu..
ya kijeshi inayoitwa Camp Lemonnier (hii ndio kambi pekee ya kudumu ya Marekani hapa barani Afrika. Kambi hii pia inafanya kazi kama makao makui ya U.S. Africa Command (USAFRICOM)).
Ndani ya kambi hii pia kuna 'black site' maarufu ya shirika la Ujasusi la CIA ambayo wanaitumia..
kama jela ya siri kuwashikilia mateka wao muhimu ambao hawataki wajulikane kwamba wamewakamata.
Sasa huyu Asad ndio alipotolewa hapa Dar akapelekwa kwenye hiyo black site ya CIA ndani ya Camp Lemonnier nchini Djibouti
Kwa ufupi sana labda nimueleze huyu Asad.
Huyu somo ni raia
wa Yemen ambaye alikuwa ameishi hapa nchini kwetu kwa muda wa miaka 10.
Huyu bwana kwa muda huu ambao alikuwa ameishi hapa nchini alikuwa amefanikiwa kugushi cheti cha kuzaliwa kuonyesha kwamba ni mzaliwa wa hapa tz na hivyo alikuwa na hati ya kusafiria ya Kitanzania japo kwa..
uhalisia hakuwa raia wa Tanzania.
Sasa,
Masaa kadhaa baada ya kufikishwa hapo Camp Lemonnier, maafisa wengine wawili wa CIA walifika kwenye selo ya siri ndani ya kambi ambayo alikuwa anashikiliwa.
Kwa mujibub wa al-Asad mwenyewe kwa maelezo ambayo miaka kadhaa baadae alikuja..
kuwaambia wajumbe wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Afrika aliwaelezea watu wale wawili waliokuja kwenye selo yake kwamba mmoja alikuwa ni mwanamama halfcast wa kizungu na kiafrika akiwa ameambatana na mwanaume wa Kizungu ambao wote walivalia kiraia
Maafisa hao wawili
wa CIA wakaanza kumuhoji.
Swali pekee ambalo walimuuliza Asad ni uhusika wake kwenye shirika linaloitwa Al-Haramain Foundation.
Hapo nieleze kidogo,
Huyu Asad shughuli yake aliyokuwa anaifanya hapa Dar alikuwa ni muhasibu wa hilo shirika linaloitwa Al-Haramain Foundation ambao
walikuwa na ofisi zao mtaa wa Kisutu.
Shirika hili la Kiislamu lilikuwa limejikita kwenye kutoa misaada ya kiutu kama vile kujenga vituo vya watoto yatima, kusadia kulipia vijana gharama za masomo, kusambaza bure vitabu vya dini na pia kuwachangia gharama watu wanaokwenda kuhiji
Shirika hili makao makuu yake yalikuwa yako nchini Saudi Arabia na kwa hapa Afrika lilikuwa na ofisi kwenye nchi nne tu, Ethiopia, Somalia, Kenya na hapa kwetu Tanzania.
Na kwa hapa Tanzania huyu al-Asad ambaye muda huu ameshikiliwa kwenye black site ya CIA nchini Djibouti..
alikuwa ndiye muhasibu.
Maafisa hao wa CIA wakamtaka aeleze nukta kwa nukta kile ambacho Asad anakifanya ndani ya shirika la Al-Haramain
Leo nimechelewa kidogo kuweka hii Part 2 kutokana na majukumu
Kesho usikose Part 3, Nisaidie ku-retweet
Habib B Anga
To Infinity and Beyond
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
MTANZANIA #1: JASUSI WA KUKODI, UJASUSI WA BIASHARA
Thread..
Si rahisi kuwa mahususi sana ni mwaka gani, lakini tunakadiria kwamba katikati ya miaka ya tisini hivi Mtanzania ambaye kwa sasa nimtaje kwa jina lake moja tu la Matiko aliondoka jiji Dar kwenda nchini Afrika Kusini
Kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini tofauti na Watanzania wengi wanaozamia SA ambako wakifika uanza kwa kufanya shughuli za hali ya chini, ilikuwa tofauti kabisa na bwana Matiko ambaye aliingia SA akiwa na mtaji wa kuridhisha kutokana na fedha ambazo alizipata toka kwenye mauzo
ya sehemu ya shamba lake la karibia Ekari 300 zilizoko kijiji cha Ghesaria Wilayani Serengeti.
Matiko akatumia mtaji huo akiwa hapo SA kuanzisha biashara ndogo ndogo
Moja ya biashara aliyoanzisha ambayo ilipanda mbegu ya kumbadilisha Matiko na kumfanya aingie kwenye ulimwengu wa
Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.
Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi
Thread👇👇
Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
ombwe la weledi ambalo linaikumba idara hii adhimu ya ujasusi.
Mhe. Rais @SuluhuSamia ambaye watu wametokea kuwa na imani naye sana, tukio la leo kwa kiwango fulani limetia doa hadhi yake na kuzua maswali mengi sana
Kwamba, kosa la dhahiri namna ile limetokeaje?
Intelijensia ya
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
PART 5 (HITIMISHO)
Nikiwa nahitimisha ni vyema kusisitiza kwamba, kikosi hiki cha makomando wa Kenya ambacho kinaendeshwa kwa amri ya CIA na NIS (Idara ya Ujasusi Kenya) kwa sasa kimegawanywa kwenye vitengo viwili..
Kitengo cha kwanza ndio ile Rendition Operations Team; hawa wanahusika sana kama target anatakiwa kukamatwa akiwa hai
Alafu siku hizi kuna RRT (Rapid Response Team) hawa wanatumika zaidi kama target anatakiwa kuwaneutralized (kuuwawa) au kuhusika kuokoa mateka kama watekaji wana
mafungamano na vikundi vya kigaidi na si lazima kuwakamata wakiwa hai.
Sasa nieleze baadhi ya Oparesheni ambazo makomando hawa wa Kenya na CIA wamewahi kuzifanya.
1. Kuuwawa kwa Sheikh Aboud Rogo
- Sheikh Aboud Rogo ni moja ya watu maarufu sana kwenye masuala ya dini kuwahi...
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
PART 4
Ile taarifa ambayo Asad aliwapatia ilikuwa ya maana sana kwa CIA.
Mpaka muda huu ambapo Asad alikuwa anahojiwa (kumbuka hiyo ni mwaka Oct 2003) huyo "bwana somba" Odeh tayari alikuwa ameshakamatwa
na yuko gerezani Guatanamo Bay (alikamatwa tangu mwaka 1998).
Taarifa hii ya Asad iliwapa CIA kitu kimoja muhimu sana.. walithibitisha intelijensia yao kuhusu shirika la al-Haramain kutumiwa na al-Qaida kusambaza fedha ulimwenguni kwa watu wao.
Ushahidi huu ulitumiwa na Marekani
kushawishi Umoja wa Mataifa kulipiga marufuku shirika hilo na mpaka leo hii ninavyoandika shirika hilo ofisi zake zote ulimwenguni zimefungwa
Lakini hicho sicho ninachotaka kuandika
Ninachotaka kuandika ni namna ambavyo ile confirmation ya Asad iliwasaidia CIA kuanza kunusa kila
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
PART 3
Mara ya mwisho nikasema kwamba, maafisa wawili wa CIA walifika kwenye jela ya siri ya shirika hilo la Ujasusi iliyopo ndani ya kambi ya Kijeshi ya Camp Lemonnier nchini Djibouti ambako "Mtanzania" al-Asad..
alikuwa anashikiliwa.
Maafisa hawa wa CIA swali pekee ambalo walikuwa wanamuhoji Asad ni kuhusu shughuli zake ndani ya shirika la Kiislamu la al-Haramain ambalo yeye alikuwa kama muhasibu hapa Tanzania
Kwa muda wa siku tatu nzima, Asad alikuwa akihojiwa kwa mtindo ambao wenyewe
CIA huita "mbinu zilizoboreshwa" (enhanced techiques) ambazo kimsingi ni mateso kama vile water boarding, sleep depravation, light depravation.
Niweke nyama hapo kuhusu hili shirika la al-Haramain ambalo CIA walikuwa wakimuhoji Asad kuhusu.
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
Thread..
Kwa sasa, eneo letu la Afrika Mashariki limeguka kuwa moja ya eneo muhimu sana la kimkakati kiulinzi kwa nchi ya Marekani.
Leo nataka nikusimulie mkasa halisi wa namna gani shirika la Ujasusi la Marekani...
CIA linaendesha shughuli zake kuanzia hapa nchini kwetu Tanzania pamoja na nchi zote zingine za Afrika Mashariki.
Nataka nikusimulie mkasa wa kusisimua ili tuelewe vyema namna gani Afrika Mashariki kwa sasa imegeuka uwanja wa ushushushu wa Kimataifa kati ya Marekani na adui zake.
Ukimaliza kusoma uzi huu, utaelewa kwa nini sio kila "mtalii" umuonae ni mtalii tu kaja kushangaa swala pale Mikumi
Namna hii,
Siku fulani hivi ya tarehe 7 mwezi June mwaka 2011, kuna vijana watatu walikuwa wanasafiri kwa gari binafsi toka pwani ya Somalia kwenye mji unaitwa...