ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 3

Mara ya mwisho nikasema kwamba, maafisa wawili wa CIA walifika kwenye jela ya siri ya shirika hilo la Ujasusi iliyopo ndani ya kambi ya Kijeshi ya Camp Lemonnier nchini Djibouti ambako "Mtanzania" al-Asad.. Image
alikuwa anashikiliwa.

Maafisa hawa wa CIA swali pekee ambalo walikuwa wanamuhoji Asad ni kuhusu shughuli zake ndani ya shirika la Kiislamu la al-Haramain ambalo yeye alikuwa kama muhasibu hapa Tanzania

Kwa muda wa siku tatu nzima, Asad alikuwa akihojiwa kwa mtindo ambao wenyewe
CIA huita "mbinu zilizoboreshwa" (enhanced techiques) ambazo kimsingi ni mateso kama vile water boarding, sleep depravation, light depravation.

Niweke nyama hapo kuhusu hili shirika la al-Haramain ambalo CIA walikuwa wakimuhoji Asad kuhusu.

Shirika hili la misaada la Kiislamu.. Image
lilikuwa linapata fedha zake kwa kukusanya 'donations' toka kwa watu na makampuni mbalimbali duniani.

Hizo donations ambazo walikuwa wanakusanya kuna kipindi zilikuwa zinafika mpaka Dola Milioni 50 (bilioni 120 tsh) kwa mwaka.

Lakini kuna muda CIA wakaanza kupata wasuwasi juu..
ya shughuli za shirika hili.

Walikuja kung'amua kwamba ndani ya shirika hili kulikuwa na watu wa ngazi za juu ya Uongozi wa shirika ambao walikuwa na mafungamano na kikundi cha Al Qaida na Taliban.

Yaani kwamba, kwenye ule mchakato wa kukusanya donations, kuna kampuni nchini...
Saudi Arabia ambazo zinamilikiwa na Osama bin Laden, nazo zilikuwa zikichangia hili shirika mabilioni ya shilingi japo kwa siri kubwa.

CIA wakapata nadharia kwamba, fedha hizo zilikuwa hazitumiki kwenye shughuli za kawaida za shirika la al-Haramain bali zinagawiwa kwa... Image
viongozi wa mtandao wa al-Qaida sehemu mbalimbali duniani

CIA hawakujua ni namna gani haswa fedha hizi zinasambazwa toka shirika al-Haramain mpaka kuwafikia viongozi wa al-Qaida au ni akina nani haswa walikuwa wanapewa
Hawakujua hayo lakini walijua kwa hakika kabisa kwamba kitu
hicho kinafanyika.

Ndio sababu kwa nini muda huo walikuwa wanamihoji "Mtanzania" al-Asad kwa kumtesa pale kwenye jela ya siri ndani ya Camp Lemonnier.

Baada ya siku tatu za mateso, hatimaye al-Asad akaanza kufunguka

Asad alifunguka vitu vingi sana lakini nitaomba niangazie mtu
mmoja muhimu sana.

Asad aliwaeleza CIA kwamba kuna maelezo alikuwa anapewa toka juu (makao makuu ya shirika lao nchini Saudi Arabia) ofisi ya uhasibu.

Kwamba, Asad alikuwa akitumia kiasi kikubwa cha "petty cash" alizokuwa anazifanyia attachment kwa shughuli ambazo si za kweli..
na kisha kukusanya na kuna mtu alikuwa anamkabidhi.

Yaani kwamba, katika petty cash za al-Haramain kwa tawi la Dar es Salaam.. kuna baadhi ya petty cash ambazo attachement za matumizi yake yalikuwa ni ya uongo.
Na Asad alikuwa anakusanya hizi petty cash kwa muda kadhaa (mfano..
mwezi mzima) alafu kuna mtu alikuwa anamkabidhi hiyo fedha

Kwa hiyo ukikagua vitabu vya fedha vya al-Haramain huwezi kuona transfer yoyote kwenda kwa watu wa kutiliwa shaka. Fedha hizo zilikuwa zinakuwa transfered kupitia petty cash na manunuzi bandia ambayo Asad alkuwa anafanya
kisha hela zinazopatikana kuna mtu alielekezwa awe anampatia

Mtu huyo jina lake anaitwa Mohammed Odeh (maafuru kama bwana somba), mwarabu koko ambaye alikuwa maarufu sana vijiwe vya kahawa magomeni na kariakoo kwenye miaka ya tisini (Kwenye kitabu cha SIRI & UJASUSI nimemuelezea
kirefu sana kwenye makala inaitwa "Ujasusi Sebuleni kwetu". Kama haukufanikiwa kupata nakala basi kaa stand-by.. siku si nyingi nitatangaza upatikanaji wa nakala mpya).

Labda niwadokeze kidogo kuhusu huyu mtu ambaye Asad alikuwa anawaambia CIA kwamba aliambiwa awe anampa hela.. Image
yaani huyu Mohammed Odeh 'bwana somba'.

Huyu somo alikuwa ni Mkenya na kuna kipindi aliajiriwa na kampuni ya usafirishaji mizigo majini iliyopo hapa Dar na mpaka alipangiwa nyumba maeneo ya Ilala.

Kufanya kwake huko kazi kwenye kampuni hiyo ya Kitanzania ndiko kulimpa fursa ya
kuifahamu vyema sana mitaa ya Dar na watu wake.

Baadae aliacha kazi na kurejea kwao Kenya. Akahama Nairobi na kuhamia kijiji kinaitwa Witu kipp huko Mombassa. Alafu akanunua boti ya kisasa na kuanza biashara ya uvuvi wa samaki ambao alikuwa anawaleta mpaka huku Dar kuja kuuza..
Kwenye hizo safari zake za kuja Dar kuuza samaki kwa jumla, akawa akiwaletea sana zawadi ya samaki rafiki zake wa vijiwe vya kahawa ndio mpaka wakambatiza jina la utani "bwana somba".
Huyu somo alikuwa ni mcheshi sana na mtu wa watu.

Lakini hakuna ambaye alikuwa anajua undani wa
huyu somo.

Huyu bwana uhalisia wake alikuwa ni mzaliwa wa Saudia na alilowea hapo nchini Kenya kwa miaka mingi kutengeneza 'cover' kwa ajili ya Oparesheni maalumu ambayo al-Qaida walikuwa wanataka kuifanya.

Huyu bwana akiwa huko Saudia, wazazi wake wakampeleka nchini Ufilipino
kusomea shahada ya Uhandisi.

Akiwa huko chuoni ndipo akajenga urafiki na wanafunzi wenzake ambao walikuwa na misimamo mikali ya kidini.
Yeye pamoja na hao wanafunzi wenzake wakafanya safari kwenda nchini Afghanistan kujiunga na Mujahedeen mwaka 1990.

Intelijensia inaonyesha...
kwamba mwaka 1992 Odeh alifanya Bayat kwa Osama bin Laden (kiapo cha utii).
Baada ya hapo Osama bin Laden akampeleka Odeh kwenye kambi inaitwa Sadeek Camp kupata advanced training jinsi ya kuunda milipuko chini ya legend wa milipuko Abdel Rahmen Yasin.

Baada ya hapo bin Laden...
akawapeleka Odeh na mtu mwingine anaitwa Saif al-Adel kwenda nchini Somalia kuwafunza kijeshi vijana wa Mohammed Farah ambao walikuwa wanapambana na vikosi vya Marekani (soma makala yangu ya Oparesheni Gothic Serpent).

Baada ya hapo Odeh akiwa pamoja na Mustafa Fadhil (Mmisri)..
pamoja na Fadhili Ally (Mkenya) wakaondoka nchini Somalia na kwenda kuweka makazi ya kudumu nchini Kenya jiji la Nairobi
Huyu Odeh akaoa kabisa binti wa Kikenya na kuanzisha familia na akaishi hapo Nairobi na Tanzania kwa miaka kibao. Kiswahili akakijua vyema kama vile Mzaramo wa
Maneromango.

Lakini nimesema hii yote ilikuwa ni 'cover'. Alikuwa hapa Afrika Mashariki kwa sababu maalumu. Kuna vitu alikuwa anavichunguza.

Mwaka 1995 kipindi ambacho inaaminika bin Laden alikuwa akiishi nchini Sudan, alimwita Odeh na kumtaka ampe tathimini yake kuhusu Afrika
Mashariki na namna gani wanaweza kufanya oparesheni.

(Inaaminika kwamba tathimini hii ya Odeh ndio ambayo ilifanya bin Laden kuchagua kuzilipua Balozi za Marekani Nairobi na Dar)

Baada ya kuonana na Osama, Odeh akarejea tena Nairobi.

Mwaka mmoja baadae akatembelewa nyumbani... Image
kwake na mlinzi binafsi wa bin Laden ambaye alimpa maagizo ya kujiandaa na Oparesheni Kaaba (ambayo itafanyika Nairobi) na 'Oparesheni Al-Aqsa' (ambayo itafanyika Dar)

Kwa hiyo zile safari za Bwana somba Odeh kuja Dar kuleta samaki mara kwa mara, kimsingi alikuwa anasuka mtandao
wa watu

Kwenye safari za kuja Dar kuuza samaki, Odeh aliwarecrut vijana wa Kitanzania Hamis toka Mdimuni Zanzibar na Ahmed Ghailani kushiriki kulipua Ubalozi mwaka 1998

Huyu Odeh ndiye ambaye Asad muda huu alikuwa anawaambia CIA aligizwa awe anampa hela Cash toka kwenye shirika
Poleni sana nimechelewa kwa siku mbili kuwawekea hii PART 3.

Nitafidia kwa kuweka PART 4 leo leo baadae jioni.

Be here..

Habib B. Anga
To infitnity and Beyond

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Habibu B. Anga

Habibu B. Anga Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @habibu_anga

11 Apr
MTANZANIA #1: JASUSI WA KUKODI, UJASUSI WA BIASHARA

Thread..

Si rahisi kuwa mahususi sana ni mwaka gani, lakini tunakadiria kwamba katikati ya miaka ya tisini hivi Mtanzania ambaye kwa sasa nimtaje kwa jina lake moja tu la Matiko aliondoka jiji Dar kwenda nchini Afrika Kusini Image
Kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini tofauti na Watanzania wengi wanaozamia SA ambako wakifika uanza kwa kufanya shughuli za hali ya chini, ilikuwa tofauti kabisa na bwana Matiko ambaye aliingia SA akiwa na mtaji wa kuridhisha kutokana na fedha ambazo alizipata toka kwenye mauzo
ya sehemu ya shamba lake la karibia Ekari 300 zilizoko kijiji cha Ghesaria Wilayani Serengeti.

Matiko akatumia mtaji huo akiwa hapo SA kuanzisha biashara ndogo ndogo
Moja ya biashara aliyoanzisha ambayo ilipanda mbegu ya kumbadilisha Matiko na kumfanya aingie kwenye ulimwengu wa
Read 25 tweets
5 Apr
Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.

Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi

Thread👇👇 Image
Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
ombwe la weledi ambalo linaikumba idara hii adhimu ya ujasusi.

Mhe. Rais @SuluhuSamia ambaye watu wametokea kuwa na imani naye sana, tukio la leo kwa kiwango fulani limetia doa hadhi yake na kuzua maswali mengi sana

Kwamba, kosa la dhahiri namna ile limetokeaje?
Intelijensia ya
Read 18 tweets
2 Apr
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 5 (HITIMISHO)

Nikiwa nahitimisha ni vyema kusisitiza kwamba, kikosi hiki cha makomando wa Kenya ambacho kinaendeshwa kwa amri ya CIA na NIS (Idara ya Ujasusi Kenya) kwa sasa kimegawanywa kwenye vitengo viwili.. Image
Kitengo cha kwanza ndio ile Rendition Operations Team; hawa wanahusika sana kama target anatakiwa kukamatwa akiwa hai

Alafu siku hizi kuna RRT (Rapid Response Team) hawa wanatumika zaidi kama target anatakiwa kuwaneutralized (kuuwawa) au kuhusika kuokoa mateka kama watekaji wana
mafungamano na vikundi vya kigaidi na si lazima kuwakamata wakiwa hai.

Sasa nieleze baadhi ya Oparesheni ambazo makomando hawa wa Kenya na CIA wamewahi kuzifanya.

1. Kuuwawa kwa Sheikh Aboud Rogo

- Sheikh Aboud Rogo ni moja ya watu maarufu sana kwenye masuala ya dini kuwahi...
Read 25 tweets
1 Apr
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 4

Ile taarifa ambayo Asad aliwapatia ilikuwa ya maana sana kwa CIA.

Mpaka muda huu ambapo Asad alikuwa anahojiwa (kumbuka hiyo ni mwaka Oct 2003) huyo "bwana somba" Odeh tayari alikuwa ameshakamatwa Image
na yuko gerezani Guatanamo Bay (alikamatwa tangu mwaka 1998).

Taarifa hii ya Asad iliwapa CIA kitu kimoja muhimu sana.. walithibitisha intelijensia yao kuhusu shirika la al-Haramain kutumiwa na al-Qaida kusambaza fedha ulimwenguni kwa watu wao.
Ushahidi huu ulitumiwa na Marekani
kushawishi Umoja wa Mataifa kulipiga marufuku shirika hilo na mpaka leo hii ninavyoandika shirika hilo ofisi zake zote ulimwenguni zimefungwa

Lakini hicho sicho ninachotaka kuandika
Ninachotaka kuandika ni namna ambavyo ile confirmation ya Asad iliwasaidia CIA kuanza kunusa kila
Read 16 tweets
29 Mar
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 2

Sasa basi,

Wale maaskari wawili ambao walifika Upanga nyumbani kwa Mohammed al-Asad sio tu kwamba walikuwa wamevalia kiraia tu, bali pia walifika wakiwa na gari yenye plate number za kiraia pia.

Kwa hiyo... Image
wakamwambia al-Asad kwamba wanahitaji kwenda naye kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiani mafupi.

Kama ilivyo kawaida al-Asad akawauliza mahojiano hayo yahusu nini haswa? Polisi wakamjibu kwamba atafahamu huko huko kituoni akifika
Bila hiyana al-Asad akaaga familia yake na kisha
akaingia kwenye gari ambalo wale askari waliwasili nalo na kisha wakaondoka.
Gari ilipowashwa iliendeshwa mpaka kufika uwanja wa ndege Terminal 1 kwenye hangar ya kampuni ya Tanzania Air Services (Sio Air Tanzania.. hii ni kampuni binafsi ambayo bado ingalipo hata sasa nchini...
Read 15 tweets
28 Mar
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

Thread..

Kwa sasa, eneo letu la Afrika Mashariki limeguka kuwa moja ya eneo muhimu sana la kimkakati kiulinzi kwa nchi ya Marekani.

Leo nataka nikusimulie mkasa halisi wa namna gani shirika la Ujasusi la Marekani...
CIA linaendesha shughuli zake kuanzia hapa nchini kwetu Tanzania pamoja na nchi zote zingine za Afrika Mashariki.
Nataka nikusimulie mkasa wa kusisimua ili tuelewe vyema namna gani Afrika Mashariki kwa sasa imegeuka uwanja wa ushushushu wa Kimataifa kati ya Marekani na adui zake.
Ukimaliza kusoma uzi huu, utaelewa kwa nini sio kila "mtalii" umuonae ni mtalii tu kaja kushangaa swala pale Mikumi

Namna hii,

Siku fulani hivi ya tarehe 7 mwezi June mwaka 2011, kuna vijana watatu walikuwa wanasafiri kwa gari binafsi toka pwani ya Somalia kwenye mji unaitwa...
Read 25 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!