ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
PART 4
Ile taarifa ambayo Asad aliwapatia ilikuwa ya maana sana kwa CIA.
Mpaka muda huu ambapo Asad alikuwa anahojiwa (kumbuka hiyo ni mwaka Oct 2003) huyo "bwana somba" Odeh tayari alikuwa ameshakamatwa
na yuko gerezani Guatanamo Bay (alikamatwa tangu mwaka 1998).
Taarifa hii ya Asad iliwapa CIA kitu kimoja muhimu sana.. walithibitisha intelijensia yao kuhusu shirika la al-Haramain kutumiwa na al-Qaida kusambaza fedha ulimwenguni kwa watu wao.
Ushahidi huu ulitumiwa na Marekani
kushawishi Umoja wa Mataifa kulipiga marufuku shirika hilo na mpaka leo hii ninavyoandika shirika hilo ofisi zake zote ulimwenguni zimefungwa
Lakini hicho sicho ninachotaka kuandika
Ninachotaka kuandika ni namna ambavyo ile confirmation ya Asad iliwasaidia CIA kuanza kunusa kila
mtu binafsi ambaye aliwahi kupokea fedha toka al-Haramain.
Yaani kwamba, kama Odeh moja ya mastermind wa tukio la kulipua balozi mwa 1998 alikuwa anapokea fedha toka al-Haramain, maana yake ni kwamba wako pia watu wengine ambao nao wanapokea fedha toka shirika hilo.
Kwa hiyo...
walikuwa wanatakiwa kunusa na kufuatilia kila hatua mahala ambako misaada ya kifedha ya al-Haramain ilikuwa inakwenda hapa Afrika Mashariki.
Na walifanikiwa haswa kwenye ufuatiliaji huu. Wakang'amua watu wengi sana ambao walikuwa wanapokea hizo fedha.
Shida ikaja kwamba, sio tu
kwa sababu mtu alikuwa anapokea fedha toka al-Haramain basi alikuwa ni gaidi. Kuna wengine walikuwa wanapokea kama msaada tu.
Kwa hivyo walipaswa kuchambua kwa kina kujua nani alipokea fedha kwa nia ovu, na nani alipokea kama msaada
Kazi hiyo ilikuwa ni kubwa sana na walikuwa...
wanahitaji kufanya oparesheni mahususi na ya muda mrefu
Na sehemu ya kwanza ambako CIA walidhamiria kuanza nako kufanya oparesheni ilikuwa ni Kenya, kutokana na idadi kubwa zaidi ya watu wa kutiliwa mashaka waliopokea fedha za al-Haramain kuwa huko
Kwa hiyo serikali ya Marekani
wakakaa na serikali ya Kenya kuwapa pendekezo lao kwamba wanahitaji kufanya oparesheni kabambe kuusambaratisha huu mtandao. Kenya wakakataa katakata, sio kukataa mtandao huo kusambaratishwa, bali walikataa kuingiza Oparatives wa CIA nchini mwao.
Kwa muda wa karibia miezi sita..
Marekani na Kenya walikuwa wanavutana kuhusu namna gani ambavyo watatekeleza hilo suala la kusambaratisha huo mtandao.
Mwishowe wakafikia uamuzi. Kwamba, kiundwe kikosi maalumu toka vikosi vya ulinzi na Usalama wa Kenya, alafu kikosi kiwe chini ya mwambata wa CIA kwenye Ubalozi
wa Marekani jijini Nairobi.
Yaani kwamba, kikosi hiki kitakuwa na makomando wa Kenya lakini kitakuwa chini ya uongozi wa mwambata wa Kijeshi wa Marekani Ubalozi wa Kenya (afisa wa CIA).
Hiyo ilikuwa ni mwanzoni kabisa mwa mwaka 2004.
Kikosi kazi hicho kikaundwa na kupewa jina..
la "Rendition Operations Team".
Pale Kenya kwenye jeshi la Polisi kuna tawi la Kijeshi ndani yake laitwa General Service Unit. Ndani ya hili tawi kuna idara ya kumlinda Rais (inaitwa G Company), Recce Company na HQ Company
Sasa, CIA kwa kushirikiana na idara ya Ujasusi ya Kenya
NIS wakachagua makomando 18 toka kitengo cha Recce ndani ya GSU.
Makomando hawa 18 wakapelekwa nchini Marekani kwenye chuo cha kijeshi cha Annapolis Naval Academy jijini Maryland.
Mafunzo haya yalikuwa adavanced training juu ya rendition na disruption operations, surveillance..
buildings storming na weapons handling.
Vijana hao 18 wa Kenya walikaa nchini Marekani wakipatiwa haya mafunzo kwa muda wa miezi sita na kisha baadae kurejea nchini Kenya.
(Hii timu ya watu 18 toka 2004 mpaka sasa imekua toka maafisa 18 mpaka kufikia maafisa 60 leo hii).
Toka mwaka huo 2004 mpaka sasa timu hii imekuwa inafanya oparesheni za kukamata na mara nyingi kuua watu ambao wanashukiwa kujihusisha na ugaidi.
Kikosi hiki kwa muda wote huu kimekuwa chini ya Special Operator wa CIA anayeitwa Michael Goodboe (pichani).
Huyu jamaa kabla ya...
Kupewa jukumu hili alikuwa ni komando kwenye kikosi adhimu na weledi wa hali ya juu cha jeshi la Marekani cha Navy Seal Team 6.
Amepigana vita nyingi na oparesheni nyingi za siri kwa weledi wa hali ya juu ya kutunukiwa nishani lukuki.
Ndipo CIA wakamchukua kuwa kama Special...
Operator kwenye oparesheni zao za siri. Na huyu ndiye akakabishiwa kile kikosi cha makomando wa Kenya wa Renditions Operations Team
Ngoja nikupe mifano ya oparesheni kadhaa ambazo kikosi hiki chini ya Special Operator wa CIA wamezifanya hapa EA
Usiku huu twaendelea mpaka mwisho
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
MTANZANIA #1: JASUSI WA KUKODI, UJASUSI WA BIASHARA
Thread..
Si rahisi kuwa mahususi sana ni mwaka gani, lakini tunakadiria kwamba katikati ya miaka ya tisini hivi Mtanzania ambaye kwa sasa nimtaje kwa jina lake moja tu la Matiko aliondoka jiji Dar kwenda nchini Afrika Kusini
Kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini tofauti na Watanzania wengi wanaozamia SA ambako wakifika uanza kwa kufanya shughuli za hali ya chini, ilikuwa tofauti kabisa na bwana Matiko ambaye aliingia SA akiwa na mtaji wa kuridhisha kutokana na fedha ambazo alizipata toka kwenye mauzo
ya sehemu ya shamba lake la karibia Ekari 300 zilizoko kijiji cha Ghesaria Wilayani Serengeti.
Matiko akatumia mtaji huo akiwa hapo SA kuanzisha biashara ndogo ndogo
Moja ya biashara aliyoanzisha ambayo ilipanda mbegu ya kumbadilisha Matiko na kumfanya aingie kwenye ulimwengu wa
Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.
Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi
Thread👇👇
Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
ombwe la weledi ambalo linaikumba idara hii adhimu ya ujasusi.
Mhe. Rais @SuluhuSamia ambaye watu wametokea kuwa na imani naye sana, tukio la leo kwa kiwango fulani limetia doa hadhi yake na kuzua maswali mengi sana
Kwamba, kosa la dhahiri namna ile limetokeaje?
Intelijensia ya
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
PART 5 (HITIMISHO)
Nikiwa nahitimisha ni vyema kusisitiza kwamba, kikosi hiki cha makomando wa Kenya ambacho kinaendeshwa kwa amri ya CIA na NIS (Idara ya Ujasusi Kenya) kwa sasa kimegawanywa kwenye vitengo viwili..
Kitengo cha kwanza ndio ile Rendition Operations Team; hawa wanahusika sana kama target anatakiwa kukamatwa akiwa hai
Alafu siku hizi kuna RRT (Rapid Response Team) hawa wanatumika zaidi kama target anatakiwa kuwaneutralized (kuuwawa) au kuhusika kuokoa mateka kama watekaji wana
mafungamano na vikundi vya kigaidi na si lazima kuwakamata wakiwa hai.
Sasa nieleze baadhi ya Oparesheni ambazo makomando hawa wa Kenya na CIA wamewahi kuzifanya.
1. Kuuwawa kwa Sheikh Aboud Rogo
- Sheikh Aboud Rogo ni moja ya watu maarufu sana kwenye masuala ya dini kuwahi...
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
PART 3
Mara ya mwisho nikasema kwamba, maafisa wawili wa CIA walifika kwenye jela ya siri ya shirika hilo la Ujasusi iliyopo ndani ya kambi ya Kijeshi ya Camp Lemonnier nchini Djibouti ambako "Mtanzania" al-Asad..
alikuwa anashikiliwa.
Maafisa hawa wa CIA swali pekee ambalo walikuwa wanamuhoji Asad ni kuhusu shughuli zake ndani ya shirika la Kiislamu la al-Haramain ambalo yeye alikuwa kama muhasibu hapa Tanzania
Kwa muda wa siku tatu nzima, Asad alikuwa akihojiwa kwa mtindo ambao wenyewe
CIA huita "mbinu zilizoboreshwa" (enhanced techiques) ambazo kimsingi ni mateso kama vile water boarding, sleep depravation, light depravation.
Niweke nyama hapo kuhusu hili shirika la al-Haramain ambalo CIA walikuwa wakimuhoji Asad kuhusu.
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
PART 2
Sasa basi,
Wale maaskari wawili ambao walifika Upanga nyumbani kwa Mohammed al-Asad sio tu kwamba walikuwa wamevalia kiraia tu, bali pia walifika wakiwa na gari yenye plate number za kiraia pia.
Kwa hiyo...
wakamwambia al-Asad kwamba wanahitaji kwenda naye kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiani mafupi.
Kama ilivyo kawaida al-Asad akawauliza mahojiano hayo yahusu nini haswa? Polisi wakamjibu kwamba atafahamu huko huko kituoni akifika
Bila hiyana al-Asad akaaga familia yake na kisha
akaingia kwenye gari ambalo wale askari waliwasili nalo na kisha wakaondoka.
Gari ilipowashwa iliendeshwa mpaka kufika uwanja wa ndege Terminal 1 kwenye hangar ya kampuni ya Tanzania Air Services (Sio Air Tanzania.. hii ni kampuni binafsi ambayo bado ingalipo hata sasa nchini...
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
Thread..
Kwa sasa, eneo letu la Afrika Mashariki limeguka kuwa moja ya eneo muhimu sana la kimkakati kiulinzi kwa nchi ya Marekani.
Leo nataka nikusimulie mkasa halisi wa namna gani shirika la Ujasusi la Marekani...
CIA linaendesha shughuli zake kuanzia hapa nchini kwetu Tanzania pamoja na nchi zote zingine za Afrika Mashariki.
Nataka nikusimulie mkasa wa kusisimua ili tuelewe vyema namna gani Afrika Mashariki kwa sasa imegeuka uwanja wa ushushushu wa Kimataifa kati ya Marekani na adui zake.
Ukimaliza kusoma uzi huu, utaelewa kwa nini sio kila "mtalii" umuonae ni mtalii tu kaja kushangaa swala pale Mikumi
Namna hii,
Siku fulani hivi ya tarehe 7 mwezi June mwaka 2011, kuna vijana watatu walikuwa wanasafiri kwa gari binafsi toka pwani ya Somalia kwenye mji unaitwa...