ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 5 (HITIMISHO)

Nikiwa nahitimisha ni vyema kusisitiza kwamba, kikosi hiki cha makomando wa Kenya ambacho kinaendeshwa kwa amri ya CIA na NIS (Idara ya Ujasusi Kenya) kwa sasa kimegawanywa kwenye vitengo viwili.. Image
Kitengo cha kwanza ndio ile Rendition Operations Team; hawa wanahusika sana kama target anatakiwa kukamatwa akiwa hai

Alafu siku hizi kuna RRT (Rapid Response Team) hawa wanatumika zaidi kama target anatakiwa kuwaneutralized (kuuwawa) au kuhusika kuokoa mateka kama watekaji wana
mafungamano na vikundi vya kigaidi na si lazima kuwakamata wakiwa hai.

Sasa nieleze baadhi ya Oparesheni ambazo makomando hawa wa Kenya na CIA wamewahi kuzifanya.

1. Kuuwawa kwa Sheikh Aboud Rogo

- Sheikh Aboud Rogo ni moja ya watu maarufu sana kwenye masuala ya dini kuwahi...
kutokea hapa Afrika Mashariki

Rogo alikuwa ni mtu wa misimamo mikali mno kuhusu dini na mara kadhaa alikuwa akitoa hotuba tata mno. Rogo alikuwa na umahiri wa kipekee wa kutoa hutba kufikia kiwango cha watu kumfananisha umahiri wake na Hassan Nasrallah, kiongozi wa Hezbollah... Image
Rogo alikuwa ni Imam wa msikiti maarufu wa Masjid Musa huko Mombasa.

Huyu bwana tangu mwaka 2002 alikuwa akisigana na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Mwaka huo 2002 yeye pamoja na wenzake wanne walikamatwa kwa kushutumiwa kuhusika na ulipuaji wa bomu kwenye hoteli ya Kikambala..
walisota gerezani kwa miaka mitatu kesi ikiendelea mpaka mwaka 2005 ambapo Jaji aliwaachia huru kutokana na kukosekana ushahidi wa kuwatia hatiani.

Misuguano yake na vyombo vya dola iliendelea mpaka mwaka 2012 ambapo alikamatwa tena akishutumiwa kumiliki silaha kinyume na sheria
na kushirikiana na kikundi cha Al-Shabaab kupanga shambulio siku ya Krismasi.
Sheikh Rogo akaachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 100 za kitanzania.

Mwezi July, Sheikh Rogo akamwandikia barua Waziri wa Mambo ya Nje ya Kenya kumweleza kwamba intelijensia yake imeng'amua kwamba Image
anawindwa na drones za Marekani, hivyo serikali ichukue hatua kumlinda kama raia au kuikemea Marekani

Lakini barua yake hiyo haikujibiwa na Waziri

Kitendo hiki kilimuudhi mno Sheikh Rogo na hivyo kwenye hutba zake akaongeza makali zaidi kitendo ambacho kiliwaudhi zaidi Marekani
na serikali ya Kenya.

Ndipo kile kikosi cha Rendition Operations na Rapid Response Team wakapewa "green light" kumshughulikia Sheikh Rogo

Siku ya 27 Aug 2012 Sheikh Rogo alikuwa akiendesha gari kumpeleka mkewe Khaniya hospitali. Ndani ya gari pia alikuwepo binti yake wa miaka 5
na baba yake Mzee Abdala Ali.

Walipofika barabara ya Malindi nje kidogo ya Mombasa eneo laitwa Bamburi, kuna gari isiyo na plate number ilitokea nyuma yao kwa kasi na kuwa-over take. Ilipowapita ubavuni, watu wawili walichomoza kutoka kwenye gari hiyo wakiwa na silaha nzito na..
kumimina risasi kama mvua.

Risasi 17 zilimpata Sheikh Rogo kichwani na kifuani na kufariķi papo hapo.
Hakuna mtu mwingine yeyote kwenye gari ambaye alidhuriwa isipokuwa Rogo pekee (mkewe risasi moja tu ilimpata mguuni).
Hii inaonyesha kwamba watu wale walioshambulia walimlenga.. Image
Rogo mahususi na walikuwa, watu mahiri haswa kumimina risasi zote hizo wakiwa kwenye gari inayotembea na wasikosee wakamuuwa Rogo peke yake.

Kuuwawa kwa huyu somo ambaye alikuwa ana ushawishi mkubwa Mombasa na Afrika Mashariki, kulizua maandamano makubwa ambayo watu walipoteza..
maisha. Na mpaka leo watu wangali na vinyongo.

Serikali ya Kenya mpaka leo hawajawahi kufanya upelelezi wowote au kutoa maelezo yoyote juu ya tukio hili.
Na tunafaahamu kwamba kikosi kazi cha Rapid Response Team chini ya uongozi wa CIA walitekelesa mauaji haya.
2. Kuuwawa kwa Sheikh Ibrahim Omar

- Huyu alikuwa ni mrithi wa Sheikh Rogo kwenye msikiti wa Masjid Musa hapo Mombasa. Omar aliuwawa mwaka mmoja tu baada ya kuuwawa kwa Sheikh Rogo.
Ajabu kabisa na yeye aliuwawa eneo lile lile ambalo Rogo aliuwawa na kwa staili ile ile.

Yeye na
maswahiba zake walikuwa wamesimama pembezoni mwa barabara, gari ikapita alafu mtu mwenye silaha akachomoza na kummiminia risasi Sheikh Omar.
Sheikh Omar aliuwawa ikiwa imepita wiki moja tu baada ya kutokea shambulio ya Westgate Shopping Mall. Inaonekana kama kuuwawa kwake ilikuwa Image
ni kama kisasi au kumuhusisha na shambulio lile.

Na tunafahamu pia kwamba, makomando wa Rapid Response Team walitekeleza mauaji haya ya Sheikh Omar kwa maagizo ya CIA.

3. Kuuwawa kwa Sheikh "Makaburi"
Huyu naye alikuwa mrithi wa Sheikh Rogo na Sheikh Omar kwenye msikiti ule ule
wa Masjid Musa hapo Mombasa.

Huyu somo aliuwawa mwaka 2014.

Namna alivyopigwa risasi kulikuwa kwa weledi wa ajabu na wa hali ya juu mno

Sheikh Makaburi (Abubakar Shariff) alikuwa ameshtakiwa kwa kosa la kuwa na mafungamano na Al-Shabaab.
Siku hiyo alikuwa amepelekwa mahakamani Image
Akiwa anatoka ofisini kwa hakimu kurejea 'tunduni' ambako wafungwa wanashikiliwa wakisubiri kesi zao kuitwa, gari isiyo na namba ikatokea ghafla tu na kummiminia risasi na kufariki papo hapo.

Yaani huyu alikuwa ni sheikh wa tatu kuuwawa ndani ya miaka mitatu toka msikiti mmoja..
Rapid Response Team chini ya CIA walikuwa wanatekeleza jukumu la kusambaratisha mtandao ambao waliianza tangu mwaka 2004.

Unakumbuka tukio la kwanaza ambalo tulianza nalo kwenye hii makala?
Wale, vijana watatu ambao waliuwawa na wanajeshi wa Somalia na mzungu mmoja?
Naam, ile...
ilikuwa sehemu ya hii Oparesheni ya kufyeka mtandao ambao CIA wamekuwa wakiufuatilia tangu 2004.

Niongeze jambo la mwisho.. huyu Special Operator wa CIA Bw. Michael Goodboe, mwaka jana tu hapa juzi mwezi November 2020 alikuwa nchini Somalia kwenye hizi Oparesheni.

Kutokana na..
huyu bwana kuongoza oparesheni nyingi hapa Afrika Mashariki za kuuwa viongozi mbalimbali wa dini waliokuwa wanawashuku kujihusisha na ugaidi, hivyo bwana huyu kwa miaka mingi sana amekuwa anasakwa na al-Shabaab.

Hivyo hiyo mwaka jana, bado hatujui na namna gani au nani ambaye... Image
aliwapa intelijensia al-Shabaab kuhusu uwepo wa Michael Goodboe nchini Somalia, lakini Michael alipoingia tu Mogadishu msafara wake ulishambulia kwa mabomu na risasi. Michael akajeruhiwa vibaya sana na akasafirishwa na ndege ya Kijeshi kwenda nchini Ujerumani kwenye hospitali ya
jeshi ambako alifia huko.

Bado taarifa nyingi kuhusu shambulio lililomuua Michael Goodboe ziko classified hivyo itachukua muda kufahamu kinaga ubaga, lakini serikali ya Marekani imethibitisha kuhusu kifo chake.

Tunasubiri sasa kujua, ni mwambata yupi mpya wa kijeshi toka... Image
Ubalozi wa Marekani ambaye atachukua nafasi ya komando Michael Goodboe, na kama naye ataendesha oparesheni za kikatili kama mwenzake.

Na niseme oparesheni hizi sio zafanyika Kenya tu. Hapana.. hata Uganda na hapa Tanzania zafanyika.

Siku moja nitawasimulia kuhusu mwanamuziki...
aliyepata kuwa maarufu huko Uganda namna ambavyo alikuwa anaongoza Oparesheni za Kijasusi kwa niaba ya CIA
Na siku nyingine nitawasimulia kuhusu mwanamama Ms. Renee hapa Tanzania na alichokuwa anakifanya.

Tukutane tena kwenye makala nyingine

Habib B. Anga
To Infinity and Beyond

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Habibu B. Anga

Habibu B. Anga Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @habibu_anga

11 Apr
MTANZANIA #1: JASUSI WA KUKODI, UJASUSI WA BIASHARA

Thread..

Si rahisi kuwa mahususi sana ni mwaka gani, lakini tunakadiria kwamba katikati ya miaka ya tisini hivi Mtanzania ambaye kwa sasa nimtaje kwa jina lake moja tu la Matiko aliondoka jiji Dar kwenda nchini Afrika Kusini Image
Kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini tofauti na Watanzania wengi wanaozamia SA ambako wakifika uanza kwa kufanya shughuli za hali ya chini, ilikuwa tofauti kabisa na bwana Matiko ambaye aliingia SA akiwa na mtaji wa kuridhisha kutokana na fedha ambazo alizipata toka kwenye mauzo
ya sehemu ya shamba lake la karibia Ekari 300 zilizoko kijiji cha Ghesaria Wilayani Serengeti.

Matiko akatumia mtaji huo akiwa hapo SA kuanzisha biashara ndogo ndogo
Moja ya biashara aliyoanzisha ambayo ilipanda mbegu ya kumbadilisha Matiko na kumfanya aingie kwenye ulimwengu wa
Read 25 tweets
5 Apr
Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.

Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi

Thread👇👇 Image
Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
ombwe la weledi ambalo linaikumba idara hii adhimu ya ujasusi.

Mhe. Rais @SuluhuSamia ambaye watu wametokea kuwa na imani naye sana, tukio la leo kwa kiwango fulani limetia doa hadhi yake na kuzua maswali mengi sana

Kwamba, kosa la dhahiri namna ile limetokeaje?
Intelijensia ya
Read 18 tweets
1 Apr
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 4

Ile taarifa ambayo Asad aliwapatia ilikuwa ya maana sana kwa CIA.

Mpaka muda huu ambapo Asad alikuwa anahojiwa (kumbuka hiyo ni mwaka Oct 2003) huyo "bwana somba" Odeh tayari alikuwa ameshakamatwa Image
na yuko gerezani Guatanamo Bay (alikamatwa tangu mwaka 1998).

Taarifa hii ya Asad iliwapa CIA kitu kimoja muhimu sana.. walithibitisha intelijensia yao kuhusu shirika la al-Haramain kutumiwa na al-Qaida kusambaza fedha ulimwenguni kwa watu wao.
Ushahidi huu ulitumiwa na Marekani
kushawishi Umoja wa Mataifa kulipiga marufuku shirika hilo na mpaka leo hii ninavyoandika shirika hilo ofisi zake zote ulimwenguni zimefungwa

Lakini hicho sicho ninachotaka kuandika
Ninachotaka kuandika ni namna ambavyo ile confirmation ya Asad iliwasaidia CIA kuanza kunusa kila
Read 16 tweets
1 Apr
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 3

Mara ya mwisho nikasema kwamba, maafisa wawili wa CIA walifika kwenye jela ya siri ya shirika hilo la Ujasusi iliyopo ndani ya kambi ya Kijeshi ya Camp Lemonnier nchini Djibouti ambako "Mtanzania" al-Asad.. Image
alikuwa anashikiliwa.

Maafisa hawa wa CIA swali pekee ambalo walikuwa wanamuhoji Asad ni kuhusu shughuli zake ndani ya shirika la Kiislamu la al-Haramain ambalo yeye alikuwa kama muhasibu hapa Tanzania

Kwa muda wa siku tatu nzima, Asad alikuwa akihojiwa kwa mtindo ambao wenyewe
CIA huita "mbinu zilizoboreshwa" (enhanced techiques) ambazo kimsingi ni mateso kama vile water boarding, sleep depravation, light depravation.

Niweke nyama hapo kuhusu hili shirika la al-Haramain ambalo CIA walikuwa wakimuhoji Asad kuhusu.

Shirika hili la misaada la Kiislamu.. Image
Read 26 tweets
29 Mar
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 2

Sasa basi,

Wale maaskari wawili ambao walifika Upanga nyumbani kwa Mohammed al-Asad sio tu kwamba walikuwa wamevalia kiraia tu, bali pia walifika wakiwa na gari yenye plate number za kiraia pia.

Kwa hiyo... Image
wakamwambia al-Asad kwamba wanahitaji kwenda naye kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiani mafupi.

Kama ilivyo kawaida al-Asad akawauliza mahojiano hayo yahusu nini haswa? Polisi wakamjibu kwamba atafahamu huko huko kituoni akifika
Bila hiyana al-Asad akaaga familia yake na kisha
akaingia kwenye gari ambalo wale askari waliwasili nalo na kisha wakaondoka.
Gari ilipowashwa iliendeshwa mpaka kufika uwanja wa ndege Terminal 1 kwenye hangar ya kampuni ya Tanzania Air Services (Sio Air Tanzania.. hii ni kampuni binafsi ambayo bado ingalipo hata sasa nchini...
Read 15 tweets
28 Mar
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

Thread..

Kwa sasa, eneo letu la Afrika Mashariki limeguka kuwa moja ya eneo muhimu sana la kimkakati kiulinzi kwa nchi ya Marekani.

Leo nataka nikusimulie mkasa halisi wa namna gani shirika la Ujasusi la Marekani...
CIA linaendesha shughuli zake kuanzia hapa nchini kwetu Tanzania pamoja na nchi zote zingine za Afrika Mashariki.
Nataka nikusimulie mkasa wa kusisimua ili tuelewe vyema namna gani Afrika Mashariki kwa sasa imegeuka uwanja wa ushushushu wa Kimataifa kati ya Marekani na adui zake.
Ukimaliza kusoma uzi huu, utaelewa kwa nini sio kila "mtalii" umuonae ni mtalii tu kaja kushangaa swala pale Mikumi

Namna hii,

Siku fulani hivi ya tarehe 7 mwezi June mwaka 2011, kuna vijana watatu walikuwa wanasafiri kwa gari binafsi toka pwani ya Somalia kwenye mji unaitwa...
Read 25 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!