#IjueChanjoNaDaktariMwandishi
Bado naikumbuka siku ile ilipotangazwa chanjo ya kwanza ya COVID19, nilikuwa twitter, sikuwahi kufurahia matunda ya sayansi kama siku hiyo.
Wakati huo, tayari janga la COVID19 na upotoshwaji ulikuwa juu ...#UZI (SEHEMU YA KWANZA)
#DaktariMwandishi
kitu ambacho sikutegemea, ni upotoshwaji mkubwa zaidi uliokuja na chanjo.
Lakini, siwalaumu wenye maswali dhidi ya chanjo. Yapo maswali muhimu mno ambayo, hatuwezi kuyasukumia uvunguni kwa kigezo cha upotoshaji.
Ni lazima yajibiwe hata kidogo.
Nitajitahidi kutoa majibu machache.
Kabla sijajibu, naomba niseme kuwa ni sawa kuwa na maswali juu ya kile unachokipokea, lakini si sawa kusambaza taarifa za uongo na zisizo na ushahidi wowote.
Kufanya hivyo ni ugaidi. Ni uhalifu dhidi ya binadamu.
Kwanza niseme, mimi NAAMINI KATIKA CHANJO.
NAAMINI KATIKA SAYANSI.
1. KWANINI CHANJO ZA COVID19 ZIMEGUNDULIKA NA KUANZA KUTUMIKA KWA MUDA MFUPI UKILINGANISHA NA CHANJO NYINGINE?
Kujibu hili, unatakiwa kuelewa COVID19 husababishwa na kirusi cha SARS-COV-2 kilicho katika kundi la virusi aina ya CORONAVIRUSES. Virusi hivo vimefanyiwa utafiti kwa
takribani miaka 50 sasa.
Hivyo, wakati watafiti wanafanya ugunduzi wa chanjo yake, hawakuwa wakianza moja, tayari walikuwa na miaka 50 ya uelewa wa kundi hili la virusi.
Katika kundi hili lenye zaidi ya virusi 100, kuna aina 4 vinavyosababisha magonjwa ya mfumo wa upumuaji.
Mojawapo ni virusi vilivyosababisha mlipuko wa SARS(Severe Acute Respiratory Syndrome) 2002 na mlipuko wa MERS(Midde Eastern Respiratory Syndrome) 2012.
Hivyo watafiti walielewa mengi kuhusu SARS-Cov-2 kwani tayari kulikuwa na juhudi za chanjo dhidi ya ndugu zake(SARS na MERS)
Walitumia taarifa hizo kuandaa chanjo za COVID19, na kusababisha chanjo ya kwanza kupatikana ndani ya mwaka mmoja tu, tofauti na chanjo iliyotengenezwa kwa muda mfupi zaidi MUMPS ndani ya miaka 4.
Sababu nyingine ni USHIRIKIANO WA DUNIA kudhibiti COVID19. Kwa kawaida chanjo
huchukua miaka 10-15 kutengenezwa, lakini katikati ya mlipuko wa dunia wa COVID19, ulimwengu haukuwa na utajiri wa muda wala kutunishiana misuli ilhali watu wanaumwa, na mifumo ya afya duniani inaelemewa. Watafiti duniani kote walishirikiana na rasilimali zote zikapatikana.
Sababu nyingine ni MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA GENOMIC TYPING. Teknolojia hii iliwawezesha watafiti kugundua muundo wa kirusi hiki kipya ndani ya SIKU 10 tu baada ya kesi ya kwanza kuripotiwa huko WUHAN, pamoja na kufuatilia tafiti nyingine zilizokuwa zikienda sambamba.
Teknolojia pia imechangia kwa kiasi kikubwa kwasababu, licha ya uwepo wa data nyingi na maelfu ya tafiti kuhusu virusi hivi, matumizi ya SUPERCOMPUTERS yalisaidia kuzichambua kwa ufasaha na kwa muda mfupi kupata taarifa walizohitaji.
Pia, KUJITOKEZA KWA WATU WALIOKUWA TAYARI
kufanyiwa majaribio ya kwanza ya chanjo hizi. Nchi kadhaa zimetengeneza chanjo na kila nchi ilipata volunteers wa kutosha kufanya majaribio ya awali.
Lakini pia, ikumbukwe kuwa, licha ya yote haya bado chanjo zilipewa kibali cha kutumika kwa dharura.
Wakati watu wanafariki,
uchumi unadorora, na mifumo ya afya inazidiwa dunia nzima, hatua za dharura zote huchukuliwa kupunguza madhara wakati dunia ikijipanga kwa hatua za muda mrefu.
Ni sawa na unapofanya ngono isiyo salama, unakwenda kunywa PEP kwanza au unasubiri miezi 3 upime VVU ndio unywe au la?
2. JE, CHANJO ZINABADILI DNA ZETU?
Kiufupi, Hapana.
Kuelewa hili, kwanza elewa namna na wapi DNA hutengenezwa. Kati ya chanjo zimetengenezwa kwa kutumia mRNA ya kirusi cha SARS-CoV-2 kisababishacho COVID19, mfano wa chanjo hizi ni Pfizer na Moderna.
Seli zetu zina sehemu kuu 3
1. Cell Membrane(ni uzio wa seli, ambao ndio vitu huingia na kutoka kwenye seli)
2. Cytoplasm(hapa ndio shughuli nyingi za seli hufanyika ni kama jiko na sebule ya seli)
3. Nucleus(hapa ndipo DNA ilipo, ni sehemu muhimu zaidi, kama chumba cha kulala cha seli)

mRNA & viral vector
chanjo inapoingia kwenye seli, inaishia kwenye Cytoplasm, haiwezi kuingia kwenye Nucleus.
Zenyewe zinabeba MAELEKEZO ya kijenetiki kutaarifu seli zetu zitengeneze kinga dhidi ya kirusi hiki.
Ni kundi moja tu la virusi liitwalo RETROVIRUSES mf. VVU lenye enzyme inayowezesha RNA
ya virusi hivyo kuingizwa kwenye DNA ya binadamu na kusaidia kutengenezwa zaidi kwa virusi hivyo, ndio maana virusi hivyo ni vigumu kupata chanjo yake na kudhibitiwa.

Kwa kawaida, mwili wa binadamu unapoingiliwa na kimelea, seli nyeupe za damu hujiandaa kupambana, katika seli
hizo, kuna ambazo zitaua vimelea hivyo na nyingine zitaweka kumbukumbu ya kimelea kile na kutengeneza antibodies(kingamwili) ambazo zitakuwa tayari kupambana iwapo kimelea hicho kitakuja tena.
Vivyo hivyo unapopata COVID19 na unapopata chanjo. LAKINI tofauti ni kwamba, antibodies
unazotengeneza baada ya kuumwa COVID19, zinakaa kwa muda mfupi ukilinganisha na zile zinazotengenezwa ukipata chanjo ya COVID19.
Na uwepo wa antibodies(kingamwili) hizo ndio zinakulinda wewe usipate ugonjwa mkali zaidi.
KUMBUKA, chanjo ya COVID19, haikukingi wewe USIPATE COVID19
bali inakukinga wewe usipate madhara makali iwapo utaumwa COVID19.
Na hii ni saabbu kubwa ya kuidhinishwa matumizi ya chanjo hizi kwa dharura, kwani:
1. Itapunguza idadi ya wanaolazwa na kuhitaji huduma za ICU, mitungi ya gesi n.k
2. Itapunguza vifo na usambaaji wa COVID19
na hivyo itapunguza mifumo ya afya kuelemewa na kuwapa nafasi wagonjwa wengine kupata matibabu vizuri na maisha yaendelee.

KWANINI BADO HALI NI MBAYA KWENYE NCHI AMBAZO WATU WAMEPATA CHANJO?
Hapa tuongelee kitu kinaitwa HERD IMMUNITY (kingajamii) hii hupatikana pale tu ambapo
asilimia kubwa ya watu katika jamii wamepata chanjo/kinga dhidi ya ugonjwa fulani.
Mfano mzuri, ni ugonjwa wa POLIO, Tanzania ilitangazwa kuwa polio-free mwaka jana baada ya chanjo za polio kutolewa kwa miaka mingi. Hii inamaanisha zaidi ya 80% ya watanzania wamepata chanjo hii
hivyo wamelinda wale wachache ambao kwa sababu moja au nyingine hawakupata chanjo hii.
Kwa chanjo ya COVID19 kwa sasa, inapunguza makali binafsi, ndio maana wizara imeorodhesha makundi rasmi yaliyopo kwenye hatari zaidi ambayo yatapewa kipaumbele kupata chanjo hii.
Israeli ni kati ya nchi zilizoonyesha matunda ya kuchanja watu wengi, asilimia kubwa ya wanaisraeli (Taifa La Mungu kama wengi wanavyoamini) wamepata chanjo, na matunda yanaonekana.

Maswali mengine yatajibiwa kwenye SEHEMU ZINAZOFUATA ZA #UZI HUU, fuatilia.
#DaktariMwandishi
@threadreaderapp please unroll

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Kuduishe Kisowile

Kuduishe Kisowile Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Kudu_ze_Kudu

28 Jul
SEHEMU YA PILI #IjueChanjoNaDaktariMwandishi
Leo, saa 3 asubuhi, Rais SSH atazindua chanjo pale ikulu kwa kupata chanjo hiyo.
Wakati huo, tuendelee kujifunza kuhusu chanjo za COVID19 haswa aina ya Johnson&Johnson ambayo ndio imepokelewa. #UZI FUATILIA
#DaktariMwandishi
3. JE, NIKIPATA CHANJO YA COVID19 KUTANIFANYA NIWE NA SUMAKU (MAGENTIC)?

Hapana. Chanjo za COVID19 hazina uwezo wa kutengeneza "electromagnetic field" (uwezo wa wewe kuwa sumaku) na chanjo zote hazina metals.
Unaweza kuangalia nini kimo kwenye chanjo katika ukurasa wa CDC.
4. KWANINI BAADHI YA TAARIFA ZINASEMA TUMEPOKEA CHANJO YA JOHNSON&JOHNSON NA NYINGINE ZINASEMA "JANSSEN"?
Jina kamili la chanjo iliyopokelewa Tanzania kupitia mpango wa COVAX ni "Johnson&Johnson's Janssen(J&J/Janssen) COVID19 Vaccine" kwahiyo ni kitu kimoja wala si chanjo tofauti
Read 18 tweets
1 Apr
Just laying on bed, my body aching and my head is literally on fire.
Scrolling through same 3 apps, seeing excitements of a "long weekend" ahead.
Ooh! It dawns on me. It's Easter weekend.
My bad. I haven't been oriented to days of the week, only dates for some time because, you
know..work!
My work wants me to know date and time, I can barely differentiate a weekday and a weekend/holiday until I get on the road and wonder why the jam ain't like usual.
But, I love it here. I love this work. Maybe a lil' too much. Idk.
It's the one thing I've dreamt of all
my life, and worked for it all my life and it turned out not-so-perfect but absolutely how I wanted it to be. Idk if that makes sense lol.
But I love it here.

So, anyways. It's a bit rainy here. (well, it was). And that moment really brought a flash of memories in my head.
Read 18 tweets
1 Apr
I have to disagree with him.
These changes are NOT going to happen over a year, or decade maybe not even century.
Suffragettes fought for votes over 100yrs ago.
Yet even today, studies have shown that in some areas, women don't really have the freedom to vote for who they want.
I mean, there were cases the other year of divorces and DV because the wives voted for someone that their husbands didn't like. Actually, statistics show that DOMSTIC VIOLENCE cases go up during elections because of these incidents.
There are countries that allowed their women to
vote just few years ago.
But should we say the suffragettes of all countries work was just superficial because we still have issues in women voting? It is very ridiculous to do that.
The suffragettes and all other women movements are under the umbrella of feminism and have done
Read 21 tweets
15 Feb
BARUA KWA BINTI WA 🇹🇿 #UZI
#PARTONE
Binti,
Salaam zikufikie pale ulipo kama upepo uvumavyo kutoka baharini kwenda nchi kavu. Natumaini hujambo. Mimi sijambo.
Kila siku nakuwaza sana. Nafikiria nifanyeje kugusa maisha yako.
Kabla ya yote nijitambulishe, mimi ni #DaktariMwandishi Image
Dhumuni la barua hii, ni kusema na wewe Binti. Natamani barua hii ningeiremba kwa maua, lakini naamini maneno nitakayoandika ni mbegu tosha.
Jana ilikuwa siku ya wapendanao, haijalishi ulipokea salamu au la, naomba pokea zangu; NAKUPENDA.
Enzi hizo nikiwa sekondari, ilikuwa siku
nzuri sana. Wale ma-admire/dada wa shule/vindende tuliandikiana kadi na kupeana zawadi. Ilipoangukia wikiendi kama hii, mambo yalikuwa moto zaidi, tulipokea kadi na barua kutoka kwa marafiki mbalimbali. Tukisubiria jumatatu tuibie kuingia facebook kuchungulia salam tulizotumiwa.
Read 16 tweets
22 Sep 20
There is no need of that because girls are being taught that even before they attain menarche.
The question is, when are boys going to be taught how to actually be good husbands and their roles in marriage?
If you were a woman, you'd know that "ndoa" has been the backbone of
everything women are taught to do.
Literally, a girlchild is being groomed to be a wife from a young age, being shown their place and "responsibilities" as mothers and wives.
But I don't see that happening to a boychild. They are just let "to be boys" and suddenly they marry and
expected to transition to be men, fathers and husbands.
Nobody prepares them for that.
Nobody teaches them anything during puberty.
They are left to figure out everything themselves because "they are boys"
And then we wonder how comes the marriage institution is failing miserably
Read 16 tweets
20 Sep 20
Oooh Mama Afrika! Tunakusifu kwa kuijaza Afrika. Kwa kutupa matunda bora ya mbegu zilizopandwa kwako.
Tumeona kilio chako kutoka nyikani. Kilio chako kwa matunda yako yaliyopotea kabla hayajaiva.
Mama Afrika, kilio chako tumekisikia. Futa machozi.
Kwani #MaamuziYakoKeshoYako #UZI
Ni siku nyingine tulivu, baada ya purukushani za daladala kuwahi hospitali, nilimsalimu nesi wa zamu huku nikivaa koti langu tayari kuandaa meza kwa ajili ya kliniki ya kina mama wajawazito.
Mlipuko wa homa ya virusi vya Korona ulikuwa umeanza, na siku ile #MaamuziYakoKeshoYako
Tulikuwa na mengi ya kuongea na kina mama wajawazito.
Nesi alitupa kila mmoja jukumu la kuelezea kitu kimoja.
Kabla ya kliniki, kabla ya kugawa namba kwa ajili ya kumuona daktari, ni lazima tutoe MASOMO mbalimbali kwa faida ya kina mama wajawazito.
#MaamuziYakoKeshoYako
Read 20 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(