SEHEMU YA PILI #IjueChanjoNaDaktariMwandishi
Leo, saa 3 asubuhi, Rais SSH atazindua chanjo pale ikulu kwa kupata chanjo hiyo.
Wakati huo, tuendelee kujifunza kuhusu chanjo za COVID19 haswa aina ya Johnson&Johnson ambayo ndio imepokelewa. #UZI FUATILIA
#DaktariMwandishi
3. JE, NIKIPATA CHANJO YA COVID19 KUTANIFANYA NIWE NA SUMAKU (MAGENTIC)?

Hapana. Chanjo za COVID19 hazina uwezo wa kutengeneza "electromagnetic field" (uwezo wa wewe kuwa sumaku) na chanjo zote hazina metals.
Unaweza kuangalia nini kimo kwenye chanjo katika ukurasa wa CDC.
4. KWANINI BAADHI YA TAARIFA ZINASEMA TUMEPOKEA CHANJO YA JOHNSON&JOHNSON NA NYINGINE ZINASEMA "JANSSEN"?
Jina kamili la chanjo iliyopokelewa Tanzania kupitia mpango wa COVAX ni "Johnson&Johnson's Janssen(J&J/Janssen) COVID19 Vaccine" kwahiyo ni kitu kimoja wala si chanjo tofauti
IJUE CHANJO YA J&J/JANSSEN:
Huchomwa mara moja, begani.
Hii ni "viral vector vaccine"(kumradhi sijapata neno lake linalofaa la kiswahili lakini nitaelezea inavyofanya kazi)

Viral vector vaccines, zinatumia kirusi(ambacho sio kinachosababisha COVID19) kisicho na madhara kufikisha
taarifa kwenye seli kuhusu COVID19.
KIVIPI? Kirusi hiki kinapoingia kwenye seli, hutoa taarifa kwa seli kutengeneza protini ipatikanayo kwenye kirusi kinachosababisha COVID19 pekee.
Protini hii ikitengenezwa, seli inaitambua papo hapo kuwa ni kitu kigeni, hivyo mwili unatengeneza
kingamwili(antibodies) kupigana na kile ambacho mwili unadhani ni infection, hivyo mwisho, mwili unakuws umejifunza namna ya kujilinda na kupigana na virusi vinavyosababisha COVID19 bila ya kuhitaji kuumwa kwanza, na kinga hii hukaa muda mrefu.
Process hii ya mwili kupigana na
kile unachodhani ni infection, ndio huleta baadhi ya zile side effects zinazotokea.
Chanjo hizi haziingii katika DNA yako wala hazikubadilishi.
Pia, hazikusababishii infection ya COVID19 au ya kirusi kile kilichotumika kama vector.

Chukulia chanjo hii kama SHUSHUSHU(spy)
Shushushu(CHANJO) huyu anabeba taarifa za adui zako (COVID19), analeta kwenye ngome yako.
Wakati huo ngome yako imerelax, ina wanajeshi wachache tu mpakani kulinda ngome dhidi ya maadui waliowazoea.
Lakini adui huyu mpya, mwili haumtambui.
Hivyo, USALAMA WA TAIFA(seli zako sasa)
wanatumia taarifa zile zilizoletwa na SHUSHUSHU(chanjo) kutengeneza mfano(prototype) ya adui(COVID19), kisha wanatoa mafunzo mapya kwa wanajeshi(seli hai nyeupe) jinsi ya kupigana na adui.
Baadhi ya wanajeshi(SELI HAI NYEUPE) wanapewa kitengo maalum cha kukumbuka ADUI ANAFANANAJE
ili adui atakapokuja, wanajeshi wawe wamejiandaa.
Je, unadhani, kati ya ngome iliyopata taarifa kutoka kwa SHUSHUSHU(chanjo) na ile isiyopata taarifa, adui atafanya uharibifu mkubwa wapi?
Hapo utajijibu.
Hivyo ndivyo chanjo zinafanya kazi.

Katika majaribio, J&J/Janssen vaccine
ilionyesha uwezo wa 66.3% wa kutimiza majukumu yake.
Na hii ni sehemu ya maswali, KWANINI NIPOKEE CHANJO AMBAYO IMEONYESHA 66.3% TU YA KUFANYA KAZI ILIYOKUSUDIWA?
Mikanda ya gari(seatbelts) zinapunguza uwezekano wa kifo kwa 45% na majeraha makubwa kwa 50% TU.
Airbags zinapunguza
uwezekano wa kifo kwa kati ya 29-40% TU.
Kofia ngumu za pikipiki(helmets) zinapunguza uwezo wa kupata majeraha ya kichwa(Traumatic brain injury) kwa 52% na uwezekano wa kifo kwa 44% TU.

TAFAKARI. Lakini, licha ya % hizo kuwa "ndogo", je, tunatoa airbags kwenye magari yetu?
tunapuuzia kuvaa seatbelts na helmets? hatupigwi faini tunapopuuzia?
Ukiambiwa u-take risk ya kutokuwa na airbags kwenye gari (si inapunguza 29-40% tu?) au kuwa nazo utachagua kipi?
Vipi kuhusu seatbelts?

Kwahiyo, NDIYO. Kinga "kidogo" ni mara 100 ya kutokuwa na kinga kabisa.
Kama chanjo hii itapunguza 66.3% ya watu wanaopata madhara makali ya COVID19, kwa kutumia mfano wa takwimu zilizotolewa tarehe 10 Julai,2021 ambapo kulikuwa na wagonjwa 408, kati yao 284 wapo kwenye Oksijeni.
Kwakuwa chanjo inapunguza makali, kinadharia iwapo walio kwenye
Oksijeni kama wote wangekuwa wamechanjwa, 66.3% yao ambayo ni takribani wagonjwa 188 at most, wasingekuwa kwenye Oksijeni.
Tungesevu mitungi mingapi?
Tungesevu vitanda vingapi kwa ajili ya wagonjwa wengine?
Je, kusevu watu 188 kati ya 284 si kitu?
Hilo nitakupa dakika utafakari.
Lengo la chanjo hapa ni kupunguza madhara makali, na kupunguza mfumo wa afya kuelemewa na wagonjwa, na kutoa nafasi kwa wagonjwa wengine kupata huduma vizuri.
Lakini pia, ni kupunguza rasilimali zinazotumika kwa suala ambalo linaweza kabisa kuzuilika kwa kupunguza maambukizi.
Na chanjo huenda SAMBAMBA na tahadhari nyingine.
Chanjo haimaanishi mtu aache kuchukua tahadhari.

Bado, maswali ni mengi, hivyo fuatilia SEHEMU INAYOFUATA YA MTIRIRIKO HUU.
Kumbuka, CHANJO NI HIARI.
Ni jukumu la kila mmoja kufahamu.
FUATILIA hapa #IjueChanjoNaDaktariMwandishi
@threadreaderapp please unroll

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Kuduishe Kisowile

Kuduishe Kisowile Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Kudu_ze_Kudu

28 Jul
#IjueChanjoNaDaktariMwandishi
Bado naikumbuka siku ile ilipotangazwa chanjo ya kwanza ya COVID19, nilikuwa twitter, sikuwahi kufurahia matunda ya sayansi kama siku hiyo.
Wakati huo, tayari janga la COVID19 na upotoshwaji ulikuwa juu ...#UZI (SEHEMU YA KWANZA)
#DaktariMwandishi
kitu ambacho sikutegemea, ni upotoshwaji mkubwa zaidi uliokuja na chanjo.
Lakini, siwalaumu wenye maswali dhidi ya chanjo. Yapo maswali muhimu mno ambayo, hatuwezi kuyasukumia uvunguni kwa kigezo cha upotoshaji.
Ni lazima yajibiwe hata kidogo.
Nitajitahidi kutoa majibu machache.
Kabla sijajibu, naomba niseme kuwa ni sawa kuwa na maswali juu ya kile unachokipokea, lakini si sawa kusambaza taarifa za uongo na zisizo na ushahidi wowote.
Kufanya hivyo ni ugaidi. Ni uhalifu dhidi ya binadamu.
Kwanza niseme, mimi NAAMINI KATIKA CHANJO.
NAAMINI KATIKA SAYANSI.
Read 24 tweets
1 Apr
Just laying on bed, my body aching and my head is literally on fire.
Scrolling through same 3 apps, seeing excitements of a "long weekend" ahead.
Ooh! It dawns on me. It's Easter weekend.
My bad. I haven't been oriented to days of the week, only dates for some time because, you
know..work!
My work wants me to know date and time, I can barely differentiate a weekday and a weekend/holiday until I get on the road and wonder why the jam ain't like usual.
But, I love it here. I love this work. Maybe a lil' too much. Idk.
It's the one thing I've dreamt of all
my life, and worked for it all my life and it turned out not-so-perfect but absolutely how I wanted it to be. Idk if that makes sense lol.
But I love it here.

So, anyways. It's a bit rainy here. (well, it was). And that moment really brought a flash of memories in my head.
Read 18 tweets
1 Apr
I have to disagree with him.
These changes are NOT going to happen over a year, or decade maybe not even century.
Suffragettes fought for votes over 100yrs ago.
Yet even today, studies have shown that in some areas, women don't really have the freedom to vote for who they want.
I mean, there were cases the other year of divorces and DV because the wives voted for someone that their husbands didn't like. Actually, statistics show that DOMSTIC VIOLENCE cases go up during elections because of these incidents.
There are countries that allowed their women to
vote just few years ago.
But should we say the suffragettes of all countries work was just superficial because we still have issues in women voting? It is very ridiculous to do that.
The suffragettes and all other women movements are under the umbrella of feminism and have done
Read 21 tweets
15 Feb
BARUA KWA BINTI WA 🇹🇿 #UZI
#PARTONE
Binti,
Salaam zikufikie pale ulipo kama upepo uvumavyo kutoka baharini kwenda nchi kavu. Natumaini hujambo. Mimi sijambo.
Kila siku nakuwaza sana. Nafikiria nifanyeje kugusa maisha yako.
Kabla ya yote nijitambulishe, mimi ni #DaktariMwandishi Image
Dhumuni la barua hii, ni kusema na wewe Binti. Natamani barua hii ningeiremba kwa maua, lakini naamini maneno nitakayoandika ni mbegu tosha.
Jana ilikuwa siku ya wapendanao, haijalishi ulipokea salamu au la, naomba pokea zangu; NAKUPENDA.
Enzi hizo nikiwa sekondari, ilikuwa siku
nzuri sana. Wale ma-admire/dada wa shule/vindende tuliandikiana kadi na kupeana zawadi. Ilipoangukia wikiendi kama hii, mambo yalikuwa moto zaidi, tulipokea kadi na barua kutoka kwa marafiki mbalimbali. Tukisubiria jumatatu tuibie kuingia facebook kuchungulia salam tulizotumiwa.
Read 16 tweets
22 Sep 20
There is no need of that because girls are being taught that even before they attain menarche.
The question is, when are boys going to be taught how to actually be good husbands and their roles in marriage?
If you were a woman, you'd know that "ndoa" has been the backbone of
everything women are taught to do.
Literally, a girlchild is being groomed to be a wife from a young age, being shown their place and "responsibilities" as mothers and wives.
But I don't see that happening to a boychild. They are just let "to be boys" and suddenly they marry and
expected to transition to be men, fathers and husbands.
Nobody prepares them for that.
Nobody teaches them anything during puberty.
They are left to figure out everything themselves because "they are boys"
And then we wonder how comes the marriage institution is failing miserably
Read 16 tweets
20 Sep 20
Oooh Mama Afrika! Tunakusifu kwa kuijaza Afrika. Kwa kutupa matunda bora ya mbegu zilizopandwa kwako.
Tumeona kilio chako kutoka nyikani. Kilio chako kwa matunda yako yaliyopotea kabla hayajaiva.
Mama Afrika, kilio chako tumekisikia. Futa machozi.
Kwani #MaamuziYakoKeshoYako #UZI
Ni siku nyingine tulivu, baada ya purukushani za daladala kuwahi hospitali, nilimsalimu nesi wa zamu huku nikivaa koti langu tayari kuandaa meza kwa ajili ya kliniki ya kina mama wajawazito.
Mlipuko wa homa ya virusi vya Korona ulikuwa umeanza, na siku ile #MaamuziYakoKeshoYako
Tulikuwa na mengi ya kuongea na kina mama wajawazito.
Nesi alitupa kila mmoja jukumu la kuelezea kitu kimoja.
Kabla ya kliniki, kabla ya kugawa namba kwa ajili ya kumuona daktari, ni lazima tutoe MASOMO mbalimbali kwa faida ya kina mama wajawazito.
#MaamuziYakoKeshoYako
Read 20 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(