BITCOIN, BLOCKCHAIN AND CRYPTOCURRENCIES

Turudi nyuma mwaka 2008, Bwana mmoja aitwaye Santoshi Nakamoto mtaalamu wa Computer na Hesabu alitengeneza Program na kuiita jina la BITCOIN

Je, Bitcoins ni nini na zinafanyaje kazi ?

Twende na uzi 👇

#ElimikaWikiendi
Bitcoin ni toleo la pesa taslimu ya ki-mtandao ( peer-to-peer version of electronic cash ) ambayo unaweza kutuma moja kwa moja kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine pasipo kupitia taasisi za fedha kama benki, Mobile money etc, unahitaji kuwa na internet tu

#ElimikaWikiendi
Kitu muhimu kwenye Bitcoin huwezi kugushi/forge, miamala fake haiwezi kufanyika, siyo lazima uwe na kitambulisho cha Taifa ( National ID) wala Bank account, Bitcoin iko decentralized ( imegawanyika ), mwamala ukifanyika hauwezi kubadilishwa na ina ulinzi sana

#ElimikaWikiendi
kuna bitcoins milioni 21 tu zinazoruhusiwa kuwa kwenye mzunguko na kwa sasa kuna Bitcoins milioni 18 katika mzunguko!, unaweza kujiuliza hizo Bitcoin milioni 3 ziko wapi? jibu ni "Bado hazijatengenezwa"

Mchakato wa kutengeneza Bitcoin huitwa MINING

#ElimikaWikiendi
Mining hufanywa na Wachimbaji/Miners, miners zinaweza kuwa ni computers zenye uwezo mkubwa zilizounganishwa kwenye mtandao na lazima ziwe na Bitcoin software, computers hizi hufanya hesabu ngumu ( complex Arthmetric) na computer ya kwanza kupata jibu

#ElimikaWikiendi
Huwasiliana na computers zote zilizo kwenye mtandao huo, na computers zingine lazima zihakikishe kama kweli ni jibu sahihi, na jibu hilo huitwa BITCOIN, mchakato huo wa kupata Bitcoin huitwa "Proof of Work"

Bitcoin ikipatikana hutumwa kwenye Anwani ya Mchimbaji

#ElimikaWikiendi
Hiyo anwani ya mchimbaji/Miner's address hutumika kama namba ya Account

ikiwa Mchimbaji/Miner anataka kutuma Bitcoin kwa mtu mwingine hutumia Bitcoin Wallet yake na Bitcoin wallet address ya mpokeaji kutuma hiyo Bitcoin, unaweza kutuma hata 0.000001 Bitcoin

#elimikawikiendi
Mwamala huu hudhibitishwa na kutunzwa kwenye hati/document inayoitwa "BLOCKCHAIN"

Blockchain hutunza kila mwamala wa Bitcoin unaofanywa, na hizi taarifa ziko wazi angalau watu wahakikishe kama miamala yao ni real au fake, lakini kwenye Bitcoin hakuna fake transaction
Mwanzo wakati Bitcoin imetengenezwa watu walitumua kununua coffee au pizza lakini thamani yake ikawa inapanda kwa kasi mno na watu kuacha matumizi ya kawaida na kuanza kuwekeza kwenye Bitcoin, ilianza na thamani ya $ 0.0008 na ilifikia mpaka $64,000

#Elimikawikiendi
Yaani kama ulinunua Bitcoin miaka sita iliyopita, sasa ungekuwa na faida ya zaidi 72,500,000 ya mtaji wako

Mwanzilishi wa Bitcoin aliweka wazi (Public) source code alizotumia kutengenezea Bitcoin ili watu wengine waweze kuzitumia, kuanzia hapo

#ElimikaWikiendi
Watu wametengeneza aina tofauti tofauti za Bitcoin kwa ajili ya kazi/project tofauti tofauti

Muunganiko wa hizo coins unaitwa "CRYPTOCURRENCIES" kila Coin ina matumizi yake na hazina uhusiano na Bitcoin, so unaweka kuwekeza kwenye coin uipendayo ukapata faida.

#ElimikaWikiendi
HIZO COINS NI ZIPI NA ZINA-SOLVE MATATIZO GANI

Kuna Takribani aina 1000 za Cryptocurrencies, kila moja ni unique na ina matumizi yake, tuangalie chache kati ya hizo

DECENTRALIZED FINANCE

Hii tunaiita DeFi ni kama unavyotumia Banks, Mobile Money lakini haina Makato/zero cost
Haina vizingiti na hauhitaji kuwa na IDs na ina vitu vingi sana kulinganisha na Bank za kawaida

Decentralized Finance inakusaidia kupata mikopo binafsi, kutoa mikopo na kulipwa riba kwa kutumia njia inayoitwa STAKING pia unaweza kuwa na Saving Account ukawa unapata faida
Unaweza kufanya vingi kupitia Coins hizi, unaweza kufanya Michezo/Vicoba bila hata kuwajua Group Members wako, mnaweza kukusanya pesa na marafiki zako mkatumia kupata faida, na vingine vingi

Mfano wa DeFi Cryptocurrencies:
Etherum, BNB, Tron, Aaave, Uniswap

#ElimikaWikiendi
TOKENIZED ASSETS

Hizi ni Digital asset ambazo zinaweza kugawanyika katika vipande vidogo, mfano huwezi kununua Bitcoin 1 ambayo ni Tsh 99,475,529 kwa sasa, ila unaweza kununua 0.00001 ambayo ni sawa na Tsh 993.85

Hii inatumika hasa kwenye Shares za makampuni

#elimikawikiendi
Gold, Silver na Dollar, unaweza kuwa na Tokenized United state Dollar ambazo zinaitwa Stable Coins, na unaweza kumtumia mtu mwingine, pia unaweza kununua 5% ya shares za Kampuni ya Amazon na ukatapa faida

Mfano wa Tokenizing Cryptocurrency: FTX Token, USDT, USDC, NK
NON FUNGIBLE TOKENS (NFT)

Fikiria wewe msanii na umeachia Album CD yako na unataka watu wanunue, kinachotokea unakuta mtu mmoja kanunua na kutengeneza Copies kisha kusambaza kwa watu wengine, lakini kwa kutumia Blockchain mtu hawezi ku-copy kazi kama hajalipia

#ElimikaWikiendi
Digital content yoyote unaweza kuifanya NFT, hata kama Picha au Tweet, pia unaweza kununua Coin zinazolenga NFT Projects na ukazihold kusubiri thamani yake kupanda

NFT Cryptos: Enjin, Decentraland, Etherum

Pia kuna

ENTERTAINMENT TOKENS
IDENTITY AND PRIVACY TOKENS

Na nyingine
NAMNA YA KUNUNUA HIZI COINS

Kwanza unahitaji kuwa na Application/Software ya cryptocurrency wallet kufanya haya yote, App maarufu ni TrustWallet kutoka Binance Company pia kuna Browser Wallet kama Metamask na Exodus

Lakini zote siyo salama sana kutokana na

#ElimikaWikiendi
Simu/Computer zetu kutokuwa na ulinzi imara kutokana na mashambulizi ya Mtandao, Wallet ambayo ni Most Secure ni Hardware Wallet zipo kama Flash Drive na lazima ununue kutoka kwa watengenezaji/Manufacturer Mfano ni Legder Wallet
KUNUNUA COINS KWA KADI YA VISA/MASTERCARD

Njia hii lazima utumie masoko au Exchange ambayo umejisajili kwa kuhakikiwa vitambulisho na picha kuna Bittrex.com, Binance.com au KuCoin.com na kuna apps zake

Sajili kisha bofya Buy Crypto with Card
Chagua kisha weka namba ya kadi, kadi ambazo zinakubali kwa wingi ni ABSA, NMB, CRDB na FNB

KWA KUTUMIA MOBILE MONEY

Kutumia njia hii unatakiwa kwenda localbitcoins.com jisajili huko utakutana na watu wanauza Coins na malipo ni kwa njia ya simu

#ElimikaWikiendi
Huku uwe makini, chagua mtu mwenye Review nzuri, Nunua Bitcoin kwa bei ya juu ya soko kuanzia 4% - 10% juu ya soko, huku kila mtu ana bei yake, ukitaka kununua andika ujumbe kuwa unatuma hela namba gani mwambie huwezi kutuma pesa kabla hajajibu kisha bonyeza Buy

#ElimikaWikiendi
Akijibu atakuelekeza sehemu ya kutuma pesa, ukituma hakikisha unabonyeza "I HAVE PAID" haraka ili Bitcoin zake zizuiwe na mfumo, Aki-accept malipo hizo Coins zitakuja kwako, ukipokea Coins zihamishie kwenye Wallet yako mfano TrustWallet

#ElimikaWikiendi
Ili kujua Coins za kununua tumia Platforms za Coingecko or Coinmarketcap

NOTE: Hii Article ni kwa ajili ya kujifunza, kabla ya kununua Bitcoin fanya utafiti/Research kwanza kuepuka Matapeli

Credit/Bitcoin Content Creators @TOTTechs na @NNgailo

#ElimikaWikiendi

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with #TOTTechs 🇹🇿

#TOTTechs 🇹🇿 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @TOTTechs

1 Aug
VITU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUNUNUA MacBook

Je! Unampango wa kununua MacBook mpya? Kabla ya kufanya ununuzi unahitaji kuielewa MacBook.

Aina nyingi za MacBook zinapatikana sokoni. Tutakusaidia kununua MacBook bora kulingana na mahitaji yako

Uzi mfupi 👇
Kabla ya kufanya ununuzi wowote angalia toleo la MacBook ambalo utaenda kununua. Kila Mwaka Apple hutoa toleo jipya la MacBook, unaweza kutembelea Apple’s official website, news, na social media kujua mda ambao Apple watatoa toleo Jipya
AINA ZA MacBook:

Kuna aina mbili za MacBook, MacBook Pro na MacBook Air: MacBook Air ni Nyembamba, nyepesi na ni rahisi kusafiri nayo wakati MacBook Pro ni nene kidogo.

Zote ni nzuri lakini zina utofauti sana kwenye Miundo ya ndani ( Internal Architecture & Specs)
Read 11 tweets
31 Jul
Tesla Motors ni moja ya kampuni zenye ubunifu zaidi katika magari. Elon Musk, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo kwa sasa ni mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni. Hivi karibuni, C.E.O wa Tesla na SpaceX alisema kwamba alijaribu kuuza kampuni yake ya gari kwa Apple 👇
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Apple, Tim Cook aliripotiwa kukataa kupanga mkutano kujadili ofa hiyo. Hiyo ilibainika baada ya Musk Ku-tweet kwenye Page yake juzi alipoulizwa na Mwandishi wa BBC Kuhusu Habari iliyovuma kuwa alitaka kuwa CEO wa Apple mwaka 2016
Kulingana na ripoti hiyo, Elon anadai kwamba hakuwahi kuzungumza na wala kumwandikia Tim Cook. Lakini bilionea huyo alisema aliwahi kuomba mkutano kati yake na Tim Cook juu ya Apple kuichukua Tesla, na hakupata majibu yoyote wala mkutano haukufanyika.
Read 5 tweets
24 Jul
NAMNA YA KUTENGENEZA PESA MTANDAONI

Kutoka michezo ya Betting mpaka uuzaji wa nguo katika mitandao. Kuna namna nyingi sana za kutengeneza pesa mtandaoni, nyingine zina ahadi ya kukupa utajiri mkubwa ndani ya muda mfupi., lakini je, ni kweli zinafanya kazi? 👇

#ElimikaWikiendi
Jibu: Sio siku zote.
Je, Utatengeneza pesa ukifata njia hizo?
Jibu: Labda, maana ni kitu kimekaa kimtego sana. Inawezekana kabisa kwamba ile kazi yako inayokupa mshahara kila mwisho wa mwezi ikakupa pesa zaidi ya hizi njia za mitandaoni au kinyume chake

#ElimikaWikiendi
Ukweli ni kwamba kuna njia za kweli zinazofanya kazi na zinazowapa watu pesa kupitia mitandao. Kuna Freelancer(Wafanyakazi huru), wajasiriamali wadogo wadogo, waandishi, Walimu, Wahasibu, Wanasheria, N.K hutumia mitandao kupata kipato

#ElimikaWikiendi
Read 25 tweets
10 Jul
UZI:

RADAR NA MATUMIZI YAKE

RADAR
Radar ni kifupisho cha (Radio Detection and Ranging)
Ni mfumo ambao unatuma signal/ishara kwenye kitu (object) na kuchambuliwa kisha kurudisha majibu ya hicho kifaa kwa mfumo huo wa signal kupitia hewa 👇

#ElimikaWikiendi
Ili kugundua uwepo, mwelekeo, umbali, na kasi ya ndege, meli, na vitu vingine

Signal ni mawimbi (radio waves) ambayo hutumwa kwa kifaa kilicho kwenye coverage ya Radar/eneo Radar inapofika na kukichambua hicho kifaa na kurudisha majibu kwenye chanzo/muongozaji

#ElimikaWikiendi
Kwa hapa Tanzania radar zinatumika kwenye viwanja vya ndege, jeshini na kwenye Meli. Na radar zilizopo zimegawanyika katika makundi mawili: Primary na Secondary radar

Tunapozungumzia hizi primary radar tunamaanisha ni zile Radar ambazo

#ElimikaWikiendi
Read 18 tweets
22 Jun
DARASA LA CRYPTO:
SEASON 1: UZI/THREAD

MEME COINS/SHITCONS

Meme Coins au Shitcoins unaweza kuziita coins za majitaka au futuhi coins

Ni coins ambazo zimekua zikipendwa sana na watu wa Crypto kwa kuwa zinaweza kukupa faida hata mara 1000 ya mtaji wako kwa muda mfupi. 👇
Meme coins zimeundwa bila kuwa na matumizi yoyote muhimu kasoro kiki inayotokana na Jina la hiyo coin.

Katika msimu huu wa Crypto, shitcoins zimekua zikipatikana sana katika Blockchain inayoitwa Binance Smart Chain (BSC) kupitia website inayoitwa Pancakeswap
na kununua inabidi uwe na salio la coin ya BSC inayoitwa BNB na iwe ndani App ya TrustWallet...utatumia adress ya hiyo coin yako ili kuinunua

Kwa kawaida tumezoea Coin inakua na project fulani ili watu wawekeze.
Sasa hizi MemeCoins hazina project yoyote zaidi ya kupigiwa Kiki
Read 19 tweets
1 Jan
APPLE

Mwaka 2021 unatabiriwa kuwa na mapinduzi ya Tekinolojia, Apple wao wamejipanga kufanya yafuatayo

UZI

◾️Apple silicon iMac

Apple wanakuja na iMac ambayo itakuwa na Apple silicon chip, kama walivyofanya kwenye MacBook, itakuwa na16 high-power cores& 4 efficiency cores ImageImage
◾️AirPods

2021 Apple wanategemea kutoa third-generation AirPods ambayo itakuwa na replaceable silicone air tips, pia wataboresha wireless chip na battery life Image
◾️iPad Pro

Apple wanakuja na 12.9 inch iPad Pro ambayo itakuwa na LED display, hii Min-LED Technology itakuwa na wide color gamut performance, high contrast and HDR, and local dimming, pia iPad Pro itakuwa na 5G connection ikisapotiwa na A14X chip kama ilivyo kwenye M1 Macs Image
Read 13 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(