𝐂𝐈𝐀 ILIVYOTUMIA MWANAMUZIKI ARMSTRONG KUMUUA PATRICE LUMUMBA (Congo)

#Thread

Mnamo Sept 19, 1960, Mkuu wa CIA huko Leopoldville (sasa Kinshasa) alipokea SMS kupitia chombo cha siri kutoka wakuu wake huko Washington. Mtu aliyejiita 'Joe from Paris' ndiye aliyepiga simu na ..
kumwambia angefika Congo kwa ajili ya Operation maalum.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa. Baadae mkuu huyo alionywa kutozungumzia ujumbe huo na mtu yeyote. Wiki 01 baadae 'Joe' aliwasili nchini humo.

Leo nikiwa nasoma kitabu cha 𝐖𝐡𝐢𝐭𝐞 𝐌𝐚𝐥𝐢𝐜𝐞 (Author: SUZAN WILLIAMS)
kilichotoka Agosti 20, 2021, nimejikuta nikiumia sana nafsi baada ya kufahamu jinsi Marekani ilivyomuua Waziri Mkuu wa kwanza wa DR-Congo, mzalendo wa kweli, kijana mdogo mrefu, mwembamba miaka 36, kwasababu tu USA iliogopa Umoja wa Kisovieti (USSR) ikaamua kumuua.
Kifo cha PATRICE LUMUMBA kiliumiza mioyo ya watu wengi si barani Afrika, Umoja wa Kisovieti mpk Uchina.

Nitaanzia mbali ili tupate kisa kizima

📡 Cold War & CIA kuwepo Africa

📡 Louis Armstrong ni nani?

📡 Mipango ya Mauaji ilivyokaa

📡 Sababu za Kuuawa

📡 Maelezo ya SUZAN
A: COLD WAR & CIA

📋Ktk miaka ya sitini kipindi huku kwetu tunafurahia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioleta Tanzania ya Leo, huko barani Ulaya nchini Ujerumani kulikuwa na mgawanyiko wa pande mbili; Ujerumani Mashariki na Magharibi. Mgawanyiko huu ulisababishwa na nini?
📋Mnamo Agosti 13, 1961, serikali ya Kikomunisti (Germany Democratic Republic (GDR) ya Ujerumani Mashariki) ilianza kujenga ukuta mkubwa ulioitwa "Ukuta wa Kupambana na Mafashisti (Antifascistischer Schutzwall), uliojengwa kutoka Mashariki mpk Magharibi mwa mji wa Berlin.
Mji huu wa Berlin ulikuwa upande nchi ya East Germany. Hivyo Ukuta ulijengwa ndani ya nchi East Germany mjini Berlin, ukagawa mji huo ktk pande mbili.

Unaweza kushangaa ulikuwa mvutano wa aina gani, yaani Berlin ipo ndani ya East Germany halafu igawanywe tena😂😂 kwanini?👇
📋Lengo kuu la BERLIN WALL ilikuwa kuwazuia wanaoitwa "Mafashisti" wa Ujeramani Magharibi wasiingie Ujeruman Mashariki, kwani wangedhoofisha serikali ya kijamaa lkn ukuta ule uliishia kusababisha majanga makubwa nchini humo & duniani. Awali pande zote walishirikiana kwa kila kitu
📋BERLIN WALL ilidumu hadi mnamo Novemba 9, 1989, baada ya kiongozi mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Ujerumani Mashariki kutangaza kuwa raia wa GDR wangeweza kuvuka mpaka wakati wowote wanapopenda. Wakati anatangaza hivyo ilikuwa mida ya usiku, watu wengi walifurahi Sana.
📋Kabla ya kukucha umati mkubwa wa watu zaidi ya milioni 02 walipanda ukuta kuvuka kwenda Magharibi mwa Berlin. Walibomoa kwa nyundo na wengine waliweka ngazi kuteleza kwenda upande wa pili. Kuanzia siku hiyo mpk Leo, kuvunjika kwa Ukuta huo imekuwa moja sababu ya kudumu COLD WAR
#Kesho Lazima iishe..

Cha kufanya RT🔄 tweet ya kwanza, Follow @Eng_Matarra Uzi wote utaupata nitakapoanza kupost.

📡Rais wa Marekani alivyopitisha warrant ya kuuawa Lumumba😢

📡 Mauaji ya Katibu Mkuu @UN kwa7bu alimsaidia Lumumba

📡 Ubeligiji na Uingereza zilivyoshiriki🍷🍾
#Kumbuka:Baada ya HITLER kujiua April 30, 1945 (WWII), Germany iliona imeshindwa vita ikajisalimisha. Mwezi June kukafanyika mikutano miwili (Allied Peace Conferences). Mmoja ulifanyika JALTA (Southern Ukraine) na mwingine POTSDAM (Germany), ikiongozwa na USA, France, UK na USSR.
Moja ya maazimio ktk mikutano ilikuwa kugawanywa kwa BERLIN sababu kushindwa vita (WWII). Hivyo wababe hao waligawa mji huo hilo ktk pande 04;

📋Sehemu za mashariki ya nchi ilienda Umoja wa Kisovieti (USSR)

📋Sehemu ya magharibi ilienda ktk nchi za USA, Uingereza na Ufaransa.
Makao makuu ya Ujerumani, Mji wa BERLIN ulikuwa sehemu ya USSR umbali wa Km160 kutoka ulipokuwa mpaka kati ya East Germany na West Germany.

#WWII imeisha dunia imegawanyika makundi matatu:
📡Nchi za Magharibi
📡Nchi za kikomunisti
📡Nchi zinazoendelea (maskini)
Baada ya WWII ikaanza Vita Baridi (Cold War) Yaani vita vya uchumi, biashara, propaganda na chokochoko za kisiasa kati ya nchi za Magharibi na nchi za Kikomunisti. Kila upande ukitaka kuitawala dunia.

📋Nchi za Magharibi ni US, Western Europe na baadhi ya nchi zilizoendelea
📋Nchi za Kikomunisti ni zile zilizokataa kupelekeshwa na orders za kimataifa. Nchi hizi zilitaka zijiongoze zenyewe kwa matakwa ya wananchi na viongozi wa kikomunisti mfano Soviet Union (USSR) China n.k.

📋Nchi zinazoendelea ndio sisi watu wa Dunia ya TATU.
Hata hivyo, miaka 10 iliyopita hakuna mtu ulimwenguni angeweza kujua uwepo wa vita baridi BILA ripoti za kila siku za vyombo vya habari juu ya ushindani mkubwa uliopo kati ya pande 02:

📋Free World- ikiongozwa na Marekani na

📋Communist World- ikiongozwa na nchi za Kisovyeti.
Hivyo USA na USSR zikaanza kupambana kitikadi, kisiasa na kiuchumi kila mmoja akitaka atawale dunia

Na COLD WAR haiwezi kuisha kwa usiku mmoja tu, ni mchakato ambao kukamilika sio leo.

Neno "Vita Baridi" ni jina la kupigia stori mtaani, uhusika mzima ni Vita kuu ya 03 duniani.
Hivyo, ukiachana na Vita vya Korean War (1950/53), Vietnam War (1955/75), Angola (1975), Congo (1978) Afghanistan (1979/89), Nicaragua (1961/90) na nchi kadhaa, mwishoni mwa karne ya 20, COLD WAR ndio imekuwepo baina ya nchi zinazounga MFUMO wa KIBEPARI dhidi ya nchi za KIJAMAA.
Kwa kipindi hicho hakukuwa na vita kati ya wakoloni na makoloni yao, vita iliyokuwepo ni nani wa kupewa madaraka na makubaliano baada ya madaraka.

Hapa ndio Afrika tuliachiwa Civil wars na muda huu USA & RUSSIA (Super Powers) zilitumia Waafrika kuendelea kujiimarisha kiuchumi.
Ni nani aliyeanzisha VITA BARIDI? Huo ni Uzi mwingine.

Hivyo kuanguka kwa #Ukuta wa Berlin ilikuwa ishara tosha ya mwanzo wa zama za Vita Baridi.

OTTO VON amekuja kunganisha upya Ujerumani mnamo 1990 ikapelekea majeshi ya USSR kuachia nchi za Ulaya na mwishowe kuanguka kwake.
📋Rising of Cold War

💨#Ifahamike ndicho kipindi nchi za Afrika zilikuwa zikitafuta uhuru, USA ilikuwa ikitoa msaada na USSR nayo kwa namna yake. Kila mmoja alitumia nafasi hiyo kuweka mizizi yake kwa nchi hizi kwa kutumia njia mbalimbali.

💨In Other words Cultural Diplomacy
Mataifa haya (Urusi na Marekani) yalianza kushindana kipindi cha vita baridi kutokana bado Africa ilikuwa na rasilimali nyingi.

Lakini kwa Afrika macho makubwa yalikuwa ktk nchi za:

📋 DR-CONGO

📋 ANGOLA

📋 EGYPT
Mwalimu Nyerere alipata kusema kuwa utajiri walionao Wazungu umepatika Afrika na uhusiano mkubwa na umaskini uliokithiri kwa Waafrika.

Haya yote tumefundishwa katika historia, kuanzia katika shule za msingi, sekondari hadi vyuoni.

ILA hapa ni kukumbushana tu.
Madhila ya ukoloni, ndiyo yaliyosababisha Waafrika kutafuta njia ya kujinasua na janga hili. Viongozi wa Afrika, kuanzia Mfalme Haile Sellasie wa Ethiopia, Patrice Lumumba wa Congo, Kwame Nkurumah wa Ghana, Julius Nyerere wa Tanzania, Jomo Kenyatta wa Kenya na .....
Nelson Mandela wa Afrika Kusini kwa kuwataja wachache kila mmoja kwa namna yake, na wakati mwingine kwa umoja wao na kushirikiana, walitengeneza mipango wa kulikomboa bara hili.
Kipindi cha harakati za ukombozi wa Afrika kilikuwa kipindi cha “Vita Baridi” au “Vita vya Maneno”

Yaani mashindano ya mataifa makubwa kupingana bila ya kupigana kati ya Magharibi yaliyoongozwa na USA na yale ya Mashariki yanayofuata siasa za kisoshalisti yaliyoongozwa na Urusi.
Maendeleo ya Afrika yaliathiriwa pia na vita baridi. Kwa jumla kila upande ulijaribu kuvuta nchi changa za Afrika upande wake.

Kama serikali ilipatana na upande mmoja, upande mwingine mara nyingi ulikuwa tayari kusaidia wapinzani wa ndani kwa msaada wa silaha na pesa.
#MFANO: Wapigania uhuru ktk makoloni ya Ureno kama vile Msumbiji na Angola walipata msaada wa SILAHA na PESA kutoka nchi za Magharibi kwa sababu Ureno ilikuwa upande NATO.

HIVYO, ulipokuwa mpinzani wa wakoloni (mataifa ya magharibi) ulionekana Mkomunisti na wakala wa Wasovyeti.
Hiki ndio kupindi ambacho madikteta wengi wa Afrika walipata usaidizi na kushirikishana na USA!

USA ilifanya hivyo kujisafisha kutokana na Urusi ilikuwa inaitangaza vibaya, kuwa ina sura ile ile ya kikoloni ndio maana kwa mara ya kwanza (Cold War 1989) Urusi iliibuka mshindi.
#Nirudishe nyuma namna Marekani ilivyotumia muziki kujiimarisha duniani hasa Barani Afrika ambapo viongozi wengi wa Waafrika wakaamua kushirikishana nayo.

Mwl. Nyerere hakukubali siasa za Marekani ndio miongoni mwa viongozi ambao hawakukubaliana na siasa zake!!

Let's Go👇👇
Miaka 60 iliyopita, majira ya kuchipua 1958 kijana mdogo kutoka California aliyeitwa DARIUS BRUBERCK alikuwa akitembea mitaa ya Warsaw (Poland). Alikuwa akitetemeka, ilionekana bado km majira ya baridi na theluji ilikuwa imeganda mashimo ya risasi yaliyopeperusha majengo ya mji.
Poland ilikuwa nchi ya Kisovyeti na DARIUS alikuwa sehemu ya ujumbe uliopangwa na USA State Department.

Jukumu lake kuangalia fursa za tamaduni za kigeni BILA kusababisha shida yoyote. Kipindi hicho kilikuwa mwanzo wa jaribio la diplomasia ya utamaduni/Cultural Diplomacy.
Kijana huyu alikuwa akiambatana na BABA yake, mpiga 'kinanda' maarufu leo hii watu especially huko makasani na kwenye bendi utasikia wanakiita kinanda Kwa jina lingine la "🎹keyboard🎹".

Baba yake alijulikana kama DAVE BRUBECK na alikuwa Balozi wa muziki ya miondoko ya JAZZ!!
Idara hiyo ya kijasusi nchini Marekani (State Department) haikulenga "maonyesho" hayo ya muziki, kwamba ionyeshe dunia na nchi hizo jinsi muziki wa Marekani ulivyo maarufu BALI ilitaka kwa kupitia huo muziki iwashinde wapinzani wake kiitikadi ktk Vita Baridi (strategy)!!!
Robo ya maonyesho 12 ya mwanzo ya DAVE BRUBECK, ilipangwa kwanza ifanyike huko Poland ili Marekani iweke mizizi yake ktk taifa hilo na mwishowe eneo lote la nchi za Kisovyeti.

Baadae bendi hiyo ilikwenda Ulaya Mashariki, Mashariki ya Kati, Asia ya kati na Bara Hindi.
📋Ziara nyingine zilipangiwa wakongwe wa Jazz akiwemo GERRY MULLIGAN na DIZZY GILLESPIE kupiga tarumbeta ktk maadili ya Amerika ktk nchi makoloni ya Ulaya, Afrika na Asia.

💨Lengo likiwa bado moja tu, kufuta siasa na itikadi za kikomunisti kwa njia yeyote ile inayowezekana.
Huko Poland, watazamaji walitumia tamaduni zao zilizopitishwa na Serikali ya Kisovieti kama vile style za BALLET na OPERA.

📋Mwanzoni muziki wa Jazz ulishamiri Poland ktk miaka 1930, na baada ya USSR kuanza kuitawala kufuatia kumalizika kwa vita, muziki huo ulipigwa marufuku.
Baadhi ya redio zilipinga ukandamizaji huo, hata ilipofika saa ambazo muziki wa Jazz ulikuwa ukipigwa kupitia redio ya Sauti ya Amerika (VOA), zilikuwa zikinasa mawimbi na kusikiliza.

Kwahiyo maonyesho ya Brubeck ambaye ni miongoni mwa wacheza Jazz wa mwanzo ulikuwa live wanaona
Tamasha la kwanza la Brubeck lililofanyika SZCZECIN ktk mpaka kati ya Poland na Ujerumani Mashariki, lilipendeza sana.

Miaka 03 baada ya DAVE BRUBECK kuingia nchini Poland, Serikali ya Marekani ikaona kumbe matamasha ya muziki wa Jazz yanaweza kuwa silaha ya Vita Baridi.
Wakati huo, USA na USSR walijiona mataifa yaliyoendelea, hivyo ht muziki wao walitaka ionekane umeendelea. Walikuwa ktk mashindano na yalishika mioyo ya walimwengu.

Miaka ya 1956's, DIZZY GILLESPIE, alikuwa ameshafika Pembe yote ya Amerika (Balkans) na Mashariki ya mbali.
Bendi za Jazz zilizuru nje ya nchi kwa miaka mingi, lkn kwa msaada wa State Department, ambayo iliruhusu muziki huo kufikia maeneo ya kimkakati ambayo kijiografia hayawezi kuhisiwa ktk nchi husika kwamba majasusi wa Marekani (CIA), wanaweza kuyatumia maonyesho hayo kwadefeat.
Brubeck aliitangaza sana USA, ndipo rasmi ikaanzishwa JAZZ AMBASSADORS + Full ufadhili kwenda nchi nyingine

Waanzilishi wa mwanzo walikuwa

🎼 DIZZY GILLESPIE✔️
🎼 DUKE ELLINGTON✔️
🎼 BENNY GOODMAN ✔️
🎼 LOUIS ARMSTRONG ✔️

📡Safari hii walikwenda Iran, Pakistan & Turkey!!
Walienda ziara India, Lebanon, Greece, Yoguslavia, Africa (Ghana) walipirudi wakaishauri Serikali kutumia bendi ya DIZZY GILLESPIE ktk ziara.Kote walipoenda walikuwa wanalipwa na Serikali pesa ndefu

Hapa ndio tutaanza sasa kumfahamu Armstrong, pichani ni yeye na mke wake (Egypt)
ARMSTRONG NI NANI?

📋LOUIS DANIEL ARMSTRONG, alizaliwa Agosti 04, 1901 huko New Orleans (Louisiana). Alipewa jina la utani "Satchel Mouth" baadaye lilifupishwa kuwa "SATCHMO". Alifahamika miaka ya 50/60 akiwa mwanamuziki wa Jazz na mpuliza tarumbeta mahiri nchini Marekani.!!
Maisha ya utotoni mwake yalikuwa ya shida sababu walikuwa maskini. Hiyo ilitokana na baba yake WILLIAM ARMSTRONG kuitelekeza familia, ikamfanya aishi bila baba. Alilelewa na mama yake MARY ALBERT ARMSTRONG ambaye baada ya William kumuacha aligeukia kujiuza na kupelekea kifo chake
Baada ya mama kufariki, yeye na mdogo wake wa kike BEATRICE ARMSTRONG COLLINS, walilelewa na bibi yao aliyeitwa JOSEPHINE. Baadae alichukuliwa na familia iliyokuwa na asili ya Kiyahudi (Kanorfsky).

Akaishi hapo mpk alianza kujifunza kupiga Koneti (hii ni aina ya tarumbeta dogo).
Koneti ilikuwa ni tarumbeta yake ya kwanza kuinunua na ilitokana na pesa zake za mkopo ($5) alizopata kutoka ktk familia hiyo na angelipa kwa pesa kwa kufanya kazi ktk familia hiyo. Kwa kipindi hicho hakujifunza kwanza muziki alinunua akatunza mpk alipofikisha miaka 11
Alipokuwa mkubwa LOUIS alianza safari yake ya muziki kwa kusikiliza wanamuziki wa kizamani kila alipopata nafasi, na alijifunza kutoka kwa BUNK JOHNSON, BUDDY PETIT na JOE "King" OLIVER ambaye alikuwa kama mshauri wake na aliyempa uzoefu na zaidi alimjenga kijana Louis.
Baadaye alianza kuhudhuria live bendi zinazokuwa zinatumbuiza ktk meli za MTO MISSISSIPPI. Alijifunza muziki kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Kisha alianza kutembea na bendi ya 'The Wellregarded band' iliyokuwa inatumbuiza ktk meli za mto huo, ikamfanya kujifunza zaidi.
Uwezo na uzoefu wa kuandika na kupangilia kazi zake ulianzia hapo.

🎼Miaka hiyo kulikuwa na mwanamuziki aliyeitwa JOE 'king' OLIVER alikuwa maarufu sana. Baadae OLIVER aliondoka New Oleans 1919, Louis akachukua nafasi yake ktk bendi ya "Kid Ory's band", iliyokuwa hapo mjini
Nikurudishe nyuma Machi 19, 1918
kabla LOUIS hajaanza rasmi muziki alimuoa DAISY PARKER, binti aliyekuwa mzaliwa wa mitaa ya Gretua (Louisiana).

Wakapata mtoto mmoja CLARENCE ARMSTRONG. Waliachana mwanao akiwa na miaka 03, hivyo ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu.
Mnamo 1922 Louis alijiunga na "Creole Jazz Band" iliyokuwa mjini Chicago baada ya kupata mualiko wa bahati kutoka kwa OLIVER. Hii ilikuwa bendi ya Oliver na iliyokuwa bora na kali mjini Chicago, mwanzoni mwa miaka ya 1920 na wakati huo mji wa Chicago ulikuwa ndio makao ya Jazz.
Louis alitoa rekodi zake za kwanza na wakati huo akiwa akipuliza tarumbeta kwenye bendi ya Oliver mwaka 1923 Louis alifurahi kufanya kazi na Oliver, na akafanikiwa kupata mwanamke aliyekuwa mpiga Piano aliyeitwa LIL HARDIN ARMSTRONG, akamuoa.
@ArmstrongHouse walimpenda sana LIL na alimfanya ajisikie kuwa mtu muhimu zaidi katika bendi hiyo, lkn walitengana baadae 1924, bila kugombana kwa sababu LIL alianza kumuona LOUIS amekuwa maarufu, ziara kila mji akaona kabisa ndoa yao haitadumu. Wakaachana kiroho safi.
Mwaka huo huo aliotengana na Lil aliamua kuelekea New York City. Alipohamia akajiunga na kundi la Fletcher Henderson Orchestra, iliyokuwa ni bendi bora ya Wamarekani wenye asili ya Afrika kwa wkt huo. Akiwa hapo alianza kupiga tarumbeta kwa mitindo tofauti ambao ulivutia sana
Aina yake ya upulizaji ilimuambukiza mwanamuziki mwingine, COLEMAN HAWKINS ambaye baadae alikuja kuwa kiongozi ktk bendi hiyo. LOUS akawa maarufu baadae na kila alipokuwa akienda watu walijazana. Ukizingatia kipindi ndio Afrika na mataifa mengine yalikuwa yakipigania Uhuru.
Nyimbo zake nyingi ziligusia harakati za kudai haki za raia kutoka kwa wakoloni na nchi nyingine dunia. Asili ya muziki huu wa Jazz ni Afrika na watumwa kutoka Afrika Magharibi waliopelekwa Amerika ndio walianza kuumba huko mitaa ya kimaskini New Orleans.
Hivyo LOUIS alikuwa na mvuto wa aina yake na toka wakati huo alitoa rekodi nyingi kwa kushirikishana na rafiki zake wa zamani wa New Orleans, CLARENCE WILLIAMS na waimba Blues na Jazz km DUKE ELLINGTON. Alifariki Julai 07, 1971 kutokana na maradhi ya Moyo (kifo chake kina utata)
Kwahiyo kipindi LUOIS hajafariki, kulikuwa na vita ya kimya kimya iliyoitwa Cold War na ndipo Marekani iliona inaweza kuwatumia wanamuziki kufanya ujasusi na LOUIS ARMSTRONG alikuwa miongoni mwao.

Tuendeleee sasa.....👇👇
Mpiga tarumbeta huyo alizuru mara nyingi sana barani Afrika miaka 1959/60.

Kwake ilikuwa ni ngumu kufahamu hili lakini ukweli ni kuwa ziara zile zilizoku zikipangwa na majasusi wa Marekani ili kuitangaza nchini hiyo zilikuwa na siri nyuma yake..na sio nyingine ni kujipambana na
nchi za Umoja wa Kisovieti ikiwemo Urusi iliyokuwa imejikita Afrika na Sera za Ujamaa, huku Wachina wakiwa na Ukomunisti

Nimeelezea Idara ya "State Department" ktk #Uzi wa Vyombo vya Ulinzi, Usalama na Intelijensia vya Marekani.Kuupata Bonyeza hii link 👇
📋STATE DEPARTMENT ilikuwa inafanya hivyo kwa lengo la kujenga uhusiano kati ya Marekani na nchi za Afrika zilizokuwa zimetoka kutawaliwa na wakoloni.

📋LOUIS ARMSTRONG alikuwa miongoni mwa mabalozi wa JAZZ Ambassadors na alipangiwa ziara nyingi tu.
#Lakini mwishoni mwa 1950, ilikuwa kipindi ambacho harakati za kutetea haki za raia zimeshika kasi sana, kutokana na mapigano ya kujitafutia Uhuru hasa barani Afrika.

Mnamo Mei 1956 LOUIS ARMSTRONG alitembelea mji wa Accra, Ghana wakati huo ikiwa koloni la Uingereza.
Mnamo Oktoba 1960, alifuta ziara zake zilizopangwa aende Umoja wa Kisovieti ili kuzuru Afrika.

📋Akishirikiana na bendi yake ya ALL-STARS, alizuru nchi za Zaire (DRC), baadae akarudi Ghana, kisha Nigeria, Kenya na Uganda na mnamo 1961 alizuru Sierra Leone na Guinea (Conakry).
#Inshort: Huyo ndio LOUIS DANIEL ARMSTRONG, mwanamuziki ambaye aliwika miaka 50/60's. Hebu sasa tuangalie vitu 02:

📡 Historia ya Mauaji ya Patrice Lumumba

📡Kisha tuangalie connection ya ARMSTRONG, CIA, Rais wa Marekani pamoja Uingereza na UBELIGIJI zilivyoshiriki mauaji yake
Zaidi ya miaka 60 sasa imepita tangu alipouawa kijana mdogo, mrefu, mwembamba, miaka 36, Mzalendo wa kweli na baba wa watoto wanne, aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), PATRICE EMERY LUMUMBA.

Mauaji haya yaliyogubikwa na utata mwingi.
#Kabla sijaendelea nikurudishe nyuma.

📡Mnamo Alhamisi ya Juni 30, 1960, Congo ilijipatia uhuru kutoka kwa Ubelgiji.Kijana PATRICE LUMUMBA akiwa na miaka 35, akawa Kiongozi wa jamhuri hii mpya.

📡Lakini hali ya amani na utulivu nchini humo ilikuja kutoweka muda mfupi baadaye.!!
Kikosi cha waasi kikazua vurugu kiasi kwamba mpk Ubelgiji ilipeleka jeshi lake kulinda raia wake

Siku chache baadaye, Julai 11, 1960, Jimbo la Katanga lililokuwa likiongozwa na MOISE KAPENDA TSHOMBE likajitenga, @UmojaWaMataifa
ukaingilia kati kwa kutuma jeshi la kulinda amani.
Siku ya Jumanne ya Januari 17, 1961, miezi sita tu baada ya uhuru wa DR-Congo, Patrice Lumumba aliuawa katika Jimbo la Katanga😢

📋Februari 13, maofisa wa Jimbo la Katanga wakatangaza kifo cha Lumumba, lakini hakuna aliyewaamini. Hata wao hawakuziamini taarifa walizotoa.
Lawama zikaanza kumiminika kutoka pande zote za dunia.

Urusi iliwashutumu mabeberu na kuitaka Marekani iondoe watu wake Congo, lkn pia ikamtaka aliyekuwa Katibu Mkuu wa @UmojaWaMataifa, DAG HAMMARSKJOLD, kujiuzulu kwa sababu alionekana kuwa kibaraka wa wakoloni. Ilikuwa simanzi!
Jijini Moscow nchini Urusi watu waliandamana baada ya kupata taarifa za kuuawa kwa Lumumba.

📋Ktk Jiji la Beijing, China, kulifanyika maandamano makubwa ya watu waliokadiriwa kuwa zaidi ya 100,000. Katika nchi mbalimbali raia walivamia balozi za Ubelgiji na kufanya uharibifu.
Ndani ya mwaka mmoja tangu kuuawa kwa Lumumba, Umoja wa Mataifa ulifanya uchunguzi na baadaye ikabainika kuwa hata Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA) lilishiriki katika njama za kumuua Lumumba.

Katika ukurasa wa 198 wa kitabu “The African Liberation Struggle: Reflections”
cha GODFREY MWAKIKAGILE, kinasema jasusi wa Marekani aliyeitwa STEPHEN ANDREW LUCAS, ambaye alikuja Tanzania na kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikuwa Congo akifanya kazi chini ya mkuu wa CIA, LARRY DEVLIN, wakati Lumumba alipokamatwa na kuuawa.
Mwingine aliyekuwa Congo na baadaye akaenda Zanzibar ni FRANK S. CARLUCCI.

Siku ya mauaji Lumumba alikuwa wengine wawili waliokamatwa na kuuawa pamoja naye; JOSEPH OKITO (alikuwa Naibu Spika wa Bunge la Congo) na MAURICE MPOLO (alikuwa Waziri wa Vijana na Michezo).
Watatu hao walisafirishwa kwa ndege kutoka Kinshasa hadi mji mkuu wa Kalonji wa Bakwanga (sasa unaitwa Mbuji-Mayi).

Wakiwa kwenye ndege aina ya DC-3, wote watatu waliteswa kikatili na walinzi wa Congo. Ndege ilipowasili anga la Bakwanga, rubani hakuweza kutua kwa sababu uwanjani
hapo kulikuwa kumetapakaa matanki ya ujazo wa galoni 55.

Rubani aliamua kwenda kutua Uwanja wa Elisabethville (sasa Lubumbashi), na ndege ilipotua, PATRICE LUMUMBA alikuwa anakaribia kuzirai kutokana na maumivu.
Ndani ya ndege walikuwa wakiteswa mbele ya Kamishna wa Ulinzi wa Congo, FERDINAND KAZADI na Kamishna wa Mambo ya Ndani wa Congo, JONAS MUKAMBA.

📋Walipofikishwa Lubumbashi walipelekwa kwenye nyumba jirani na Uwanja wa Ndege wa Luano na kuendelea kuteswa.
📋PATRICE LUMUMBA, alipigwa mpk uso wake uliharibiwa kiasi cha kutotambulika kutokana na vipigo na nguo zake zikiwa zimetapakaa damu, alisimamishwa kwenye kichuguu kikubwa huku akimulikwa na taa za magari.
Kwa amri ya Moise Tshombe, rais wa jimbo la Katanga ambaye naye alikuwa akipokea maelekezo kutoka Brussels, Lumumba aliteswa. Kikosi cha mauaji kilimtoa Lumumba katika nyumba alimokuwa akiteswa na kumsafirisha kwa mwendo wa dakika 45 hadi Katanga.
Hapo aliuawa na kikosi cha mauaji kwa kupigwa risasi kwa amri ya Kapteni wa Ubelgiji, Julien Gat.

📌Aliyemfyatulia risasi ni askari wa Ubelgiji, kanali CARLOS HUYGHE. Mwingine aliyeshiriki kuwafyatulia risasi na kuwaua Okito na Mpolo ni kapteni JULIEN GAT.
📌Kupoteza ushahidi

Baada ya kuuawa kwa risasi, miili ya watatu hao ilizikwa eneo walilouawa. Kwa hofu kwamba kaburi la Lumumba lingegundulika na baadaye lingeweza kugeuzwa kuwa eneo la heshima, Wabelgiji na vibaraka wao waliamua kupoteza ushahidi ili mwili wake usionekane.
Siku ya Jumatano Januari 18, ikiwa ni siku moja baada ya mauaji hayo, miili ya kina Lumumba ilifukuliwa na kupelekwa ndani zaidi msituni na kuzikwa upya karibu na mpaka wa Rhodesia (Zimbabwe) na Congo.
Usiku wa Jumapili ya Januari 22 ndugu wawili wa Ubelgiji Kamishna wa Polisi wa Ubelgiji, GERARD SOETE na ndugu yake walikwenda tena kufukua miili ya Lumumba, Okito na Mpolo.

Safari hii walikuwa na shoka na misumeno. Wakaikatakata miili yao ikawa vipande vipande, kisha..
Wakayeyusha kwa tindikali iliyokuwa imejaa kwenye pipa la Petroli la LITA 200.

😢SOETE akachukua koleo akang’oa meno mawili ya Lumumba kwa ajili ya ukumbusho, yakapelekwa huko UBELIGIJI.

Baada ya kupata stori hiyo jinsi alivyouawa hebu tuangalie chanzo mpk kuuawa kwake👇
Kabla hatujaenda huko, nafanyia kazi pia MSG za DM.

WATU WANNE wameniambia hawamfaham PATRICE LUMUMBA.

Hivyo, acha nimchambue kwanza ndio Tuendeleee. Nitajaribu kudosoa nyuma ili umfaham vizuri.

LET'S GO👇👇
Katika robo ya mwisho ya karne ya 19, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Ureno ziligawana bara la Afrika, lakini Mfalme LEOPOLD II wa Ubelgiji ndiye aliyeichukua Jamhuri ya Congo na kuitawala.
Leopold II alikuwa mfalme wa Ubelgiji kuanzia 1865 hadi 1909.

📋Alimfuata baba yake LEOPOLD I aliyekuwa mfalme wa kwanza baada ya kuanzishwa kwa taifa hilo, na miongoni mwa watawala ukiacha na HITLER alivyoua wazungu zaidi ya 10M, huyu naye aliuawa Waafrika zaidi ya 15M..!!😢
Tuachane na hayo ijapo yaumiza.

📋Mnamo 1884 (Berlin Conference), USA ilitambua Congo chini ya mfalme huyo. Mkutano wa Berlin uliigawa Afrika ktk maeneo ya kiutawala.

📋Ingawa LEOPOLD II aliitawala Congo na kufaidi utajiri wa rasilimali zake lkn hakuwahi kuikanyaga nchi hiyo.
Vuguvugu la nchi za Afrika kujipatia uhuru lilianza ktkt ya karne ya 20.

Kipindi hicho MTU aliyekuja kuwa gumzo kubwa ktk historia ya nchi hiyo ni PATRICE EMERY LUMUMBA aliyezaliwa Julai 2, 1925, wazazi wake wakiwa FRANÇOIS TOLENGA OTETSHIMA (baba) na JULIENNE WAMATO LOMENDJA.
Patrice Lumumba, alizaliwa ktk familia ya Kikatoliki, pia ni kabila la "Batelela".

📋Alisoma shule za misheni na watoto wa wazungu, alikuwa smart sana kichwani. Kiasi siku moja kiongozi wa mji alienda kumuona. Baada ya kuhitimu masomo yake, alipata kazi ya ukarani wa posta.
Kazi hiyo ilimfanya ahame Kinshasa (wakati huo ikiitwa Leopoldville) kutokea Kasai.

Baadaye alipanda cheo na kuhamishiwa posta ya Kisangani (wakati huo Kisangani ikijulikana kama Stanleyville). Maisha yake ya kisiasa yalianza 1955 alipoanza kushiriki harakati za kisiasa.
Jina lake halisi ni ELIAS OKIT’ ASOMBO.

📋Kwa mujibu JONATHAN REYNOLDS ktk kitabu chake, “30-Second Twentieth Century: The 50 Most Significant Ideas and Events, Each Explained in Half a Minute” (page 1885), maana ya jina hilo ni “Mrithi wa aliyelaaniwa, ambaye atakufa mapema”.
“Baba yake alitaka Patrice Lumumba, awe katekista,” anaandika JOHANNES FABIAN ktk kitabu chake cha “Remembering the Present: Painting and Popular History in Zaire”.

📋Lakini baada ya kuelimika kiasi fulani, hakufuata njia hiyo aliyoitaka baba yake.
📋Kielimu:

Aliwahi kufukuzwa chuo cha kidini kwa7bu hakufuata sana mambo ya dini. Baadaye alijiunga na taasisi ya Kikatoliki ya TSHUMBE-SAINTE-MARIE ambako pia alifukuzwa ndani ya mwaka. Baadaye tena alijiunga na Chuo cha Kimethodist cha utabibu, lkn huko napo pia alifukuzwa!
Baada ya hapo alirejea kijijini kwao na kufanya kazi yoyote aliyoipata huku akisoma karibu kila kitu alichokikuta ktk maktaba moja iliyokuwa kijijini pale ya WEMBO-NYAMA.

📋Alikuwa akiitembelea mara kwa mara. Huko alikuwa akikutana na mwalimu wake wa awali, JOSEPH LOGONYA.
Baada ya kukaa kijijini kwa muda mrefu aliamua kuhamia mjini, na ndipo alipobadili jina, badala ya ELIAS OKIT' ASOMBO akajiita PATRICE LUMUMBA.

📋Maisha yake ya hapo mjini alikaa kati ya miaka 1943 hadi 1956.
Kabla hajaajiriwa Posta, alifanya kazi miezi 04 ktk kampuni ya kuchimba madini ya SYMETIAN mjini Kalima jimbo la Maniema.

Ilipofoka Julai 1944 ndipo aliondoka kwenda Kisangani kufanya kazi ya ukarani wa posta.

Baada ya muda wa kazi akawa anaenda shule iliyoitwa MARIST BROTHERS
Hiyo shule ilikuwa ya taasisi ya kidini (Catholic)

Kwa kuvutiwa na utendaji kazi wake na bidii ya kusoma, boss wake alimpandisha cheo, akampeleka kituo cha kilimo YANGAMBI ilikuwa karibu na Kisangani.

Mwaka 1947 alikubaliwa kujiunga na Chuo cha Posta cha Leopoldville (Kinshasa)
Kwa mujibu wa mwandishi JOHANNES FABIAN, Lumumba alifaulu mitihani yake kwa kupata 94.4% hapo chuoni na akapata ajira inayolingana na ya Wazungu waliokuwa wakifanya kazi Posta ya Congo.

Ikaenda mpk akawa ofisa mwandamizi wa posta, ndipo akaanza kufanya mihadhara na kuandika.
Baadae alioa mwanamke kutoka kijiji alichozaliwa, lkn inasemeka awali alikuwa na mademu wawili, mjoja kabila la "Waluba na mwingine Mcongo".

Mwaka 1952 alikutana na kuanzisha urafiki na mwanasosholojia Mfaransa, PIERRE CLEMENT.
Kwa mujibu wa kitabu “Lumumba: Africa’s Lost Leader” cha LEO ZEILIG, Lumumba na Pierre walishirikiana kufanya tafiti zilizomfumbua macho na kumfanya ajihusishe zaidi na harakati za kisiasa

📋Mwaka 1954 alikutana na mwanasiasa Mbelgiji, AUGUSTE BUISSERET akajiunga na taasisi yake
Alipoanza kujihusisha na siasa, wanasiasa wa Ubelgiji walianza kuona changamoto kali kutoka kwake. Mawazo ya kuanza kumdhibiti yalianzia hapo baada ya ‘umachachari’ wake kuanza kuonekana bayana.

Lumumba akaanza kuwakosoa mpk viongozi BILA uoga wowote akiwa huko huko Ubeligiji!!
Mnamo Julai 6, 1956, aliporejea kutoka Ubelgiji alikokuwa amealikwa na Buisseret kuzungumza ktk jumuiya yao, alikamatwa mara tu baada ya kushuka kwenye ndege akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya faranga 126,000 za Kifaransa za ofisi ya posta (alisingiziwa) ili asijiingie ktk siasa
Akapelekwa mahakamani, akahukumiwa kifungo miaka 02 gerezani, lkn baadaye adhabu ilipunguzwa na kuwa miezi 18.

Hata mwandishi WILLAME JEAN-CLAUDE katika kitabu chake, “Patrice Lumumba: The Congolese Crisis Revisited” anaamini kufungwa kwa Lumumba kulitokana na chuki na....
..fitina za ajira zilizotengenezwa na wazungu waliokuwa wakifanya kazi posta walipomuona anaelekea kuwazidi kitaaluma.

Ikiwa una tabia hiyo hapo Ofisini, punguza hiyo sio tabia nzuri😂😂
📡UMAARUFU WAONGEZEKA

Kifungo hicho kilimfanya aanze kupata umaarufu zaidi hata nje ya Kisangani. Akiwa gerezani aliandika kitabu akidai Congo inahitaji ukombozi kamili.

Alitoka gerezani Juni 1958, akiwa tayari amepoteza kazi ya utawala katika Posta ya Congo.
Kwa kuwa hakuwa na kazi nyingine Kisangani, aliamua kuhamia Kinshasa na kupata kazi ya usimamizi wa biashara katika kampuni ya bia ya Bas-Congo.

💨Uvumi ukaibuka kuwa bia aina ya Polar inayotengenezwa na Bas-Congo ilikuwa ikiharibu nguvu za kiume.
Alipambana na uvumi huo huku akijihusisha na siasa. Baadaye alijiunga na JOSEPH ILEO na JOSEPH NGALULA kuanzisha chama cha MNC (National Movement for Congo). Baada ya mwaka mmoja akawa kiongozi MNC.

Mnamo Agosti 1958 alichukua likizo na kwenda Brussels ktk harakati za kisiasa.
Mnamo Oktoba 5, 1958 alikiwakilisha chama hicho katika mkutano wa Waafrika uliofanyika Accra, Ghana.

Kitendo cha kuhudhuria mkutano huo kilimfanya afahamike kwa wengi waliokuja kuwa viongozi wa nchi za Afrika baada ya uhuru. BILA shaka wengi mnawafahamu, mojawapo KWAME NKRUMAH.
Mnamo Jumapili ya Januari 4, 1959 kulizuka ghasia za kisiasa katika Jimbo la Leopoldville. Ghasia hizo zilisababishwa na Waafrika waliotaka mabadiliko ya haraka.

Walitaka uhuru bila kukawia.

Vurugu zilizidi kusambaa maeneo mengine.
Pia mnamo Oktoba 23, 1959, maandamano makubwa yalianza baada ya mkutano wa hadhara wa MNC, na ilichukua siku takribani tano kutulia huku watu 30 wakiuawa wakuawa.

Mnamo Novemba Mosi, Lumumba alikamatwa na serikali ya kikoloni na kuhukumiwa tena kifungo cha miezi sita gerezani.!!
Tofauti na ilivyodhaniwa awali, kifungo hicho kiliongeza umaarufu ktk siasa

📡Chanzo cha kutaka auawe!!

📋Mnamo June 30, 1960 DRC ilipata Uhuru kutoka kwa Mbeligiji. Kipindi hicho Uwaziri mkuu ndio wenye nguvu, MNC ilikuwa moto ktk siasa, mwezi Mei nyuma kilishinda Uchaguzi.
Baada ya kushinda Uwaziri Mkuu alipewa Lumumba.

Ile siku Ubeligiji inakabidhi madaraka mfalme wa Ubelgiji, BAUDOUIN alihudhuria na kutoa hotuba yake. Mfamle alisifia Ubelgiji kuwapatia maendeleo Congo na kumwagia sifa babu yake, Mfalme LEOPARD II kwa kuwapa muongozo Wakongomani.
Ghafla sherehe ikaingia dosari baada ya Lumumba kuhutubia na kuwakasirisha Wabelgiji na mapebari wote walio hudhuria sherehe ile.

Unawaze kuitazama hotuba hiyo ya Patrice Lumumba kwa tafsiri ya lugha ya kiingereza kupitia link hii
Patrice Lumumba hakufurahishwa hata kidogo Wakongo kupewa uhuru kwa mashariti yaliyotolewa na mfalme huyo wa Ubeligiji.

Pamoja na kwamba hakuwekwa kwenye ratiba ya wazungumzaji wa siku ile, alisimama na kuhutubia ktk ukimbi ule wa 'National de Palace' na kutibua hali ya mambo.
"Tulizoea matusi,dhihaka na vipigo asubuhi,mchana na usiku, kw7bu sisi ni watu weusi..

"Tumeona ardhi yetu ikinajisiwa kwa sheria zilizowapendelea Wazungu na kuwabagua weusi. Hatujasahau kuwa sheria hazikuwa sawa kwa mweupe na mweusi, zilikuwa rafiki kwao na katili kwa wengine."
Baada ya kutoa hotuba ile, Lumumba alikwenda kukaa kwenye kiti chake huku akipongezwa kwa makofi na watu wengi waliokuwa wamehudhuria ukumbini pale wakasimama na kushangilia.

Mfalme BAUDOUIN na wageni kutoka nje walipigwa na butwa na kughadhibika na kutokana na maneno yake.
Lumumba alipopita mbele ya mfalme huyo alimwangalia na kumwambia, "Sisi sio nyani wenu tena." Kutokana na hotuba yake wabelihiji walimuona km mwenye siasa za Kikomunisti, ikaanza kutafuta namna ya kumuondoa madarakani na Chama chake cha 'The Movement National Congolais' (MNC).
Wkt huo JOSEPH KASAVUBU akiwa Rais, MOISD TSHOMBE akiwa Katanga na yeye akiwa Waziri Mkuu

Leo niishie hapa.

Kesho tuangalie mipango ya Wabeligiji kutaka kumuondoa madarakani....👇

📡Ilisukwa vipi?
📡Marekani ilihusikaje?
📡LOUIS alitumika vipi?

RT 🔄 Follow me @Eng_Matarra

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with JAPHET MATARRA

JAPHET MATARRA Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Eng_Matarra

13 Sep
FULL OPERATION MAPINDUZI YA RAIS (GUINEA)

#Thread

Baada ya TALIBAN nchin Afghanistan, habari sasa ni MAMADY DOUMBOUYA kiongozi wa kijeshi huko Guinea, kumpindua rais na kuchukua madaraka #Unadhani kikosi kidogo cha SFG kiliwezaje kudhibiti kambi za kijeshi na kumkamata rais?👇
Yes, mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa (French Legionnaire) aliyerudi nyumbani miaka 03 iliyopita na kuaminiwa na Rais ALPHA CONDÉ, ndiye aliyemsaliti na kumuondoa madarakani baada ya kutaka kuongoza nchi kwa muhula wa 03

MAMADY DOUMBOUYA ambaye ana cheo cha Kanali alionekana..
kwenye kituo cha Radio-Télévision Guinéenne(RTG), mnamo 5 Septemba majira ya saa 2 usiku, akiwa amevalia kofia nyekundu (Red Beret) ameweka bendera ya taifa hilo begani mwake, na kuzungukwa na wanajeshi wanane, akatangaza kuwa jeshi limechukua madaraka ya nchi.
Read 147 tweets
9 Sep
MAPINDUZI YA GUINEA TZ🇹🇿 YA SAMIA INACHAKUJIFUNZA

#UZI

Ilianza kama utani Mzee Condé hakuamini kijana wake mwenyewe aliyemlea, mwenye masters ya vita na cheo akampatia alipomwambia "simama juu hlf ukae chini" Unadhani ilikuwa rahisi kumpindua? Naam It's #Guinea:1958-Present👇
Sikuweza kuandika Uzi yalipotokea mapinduzi ktk nchi nyingine mbalimbali, lkn kwa yaliyotokea jumapili nchini Guinea nimeona niandike ili Watanzania tuone km kuna lolote la kujifunza. Nitaangazia upande wa kisiasa tu. Nitachambua kila kitu kuanzia uhuru hadi kutokea mapinduzi.
Maswali nayotaka kukujibu km ulijiuliza ni haya:👇

💨Historia ya Guinea ikoje?

💨Kwnn mpk mapinduzi?

💨Col. Doumbouya ana nguvu gani

💨Kwann wananchi wamefurahia?

History repeats itself, 1st as Tragedy, second as Farce.
Just retweet 🔄 huenda siku
Uzi huu ukakukumbusha kitu
Read 211 tweets
18 Aug
WHO is '𝐓𝐀𝐋𝐈𝐁𝐀𝐍'? WANATAKA NINI HASA AFGHANISTAN?

#𝕿𝖍𝖗𝖊𝖆𝖉:
Ifahamike, walikuwa yatima ktk kambi za wakimbizi Pakistan.
Je, wana uhusiano na AL-QAEDA? #Tragedy:UINGEREZA & URUSI kuchezea kipigo cha Mbwakoko.
✴️Chimbuko
📡Walio nyuma yao?
📋Tofauti yao na MUJAHIDINA..
Vita vya Marekani nchini Afghanistan vimedumu kwa takribani miaka 20. Nimeona watu wengi wakitoa maoni juu ya Jeshi la TALIBANI kuchukua nchi Lkn wengi hawana historia juu yake. Wengine wanasema Rais wa Marekani @JoeBiden mefanya 'makosa' kuondoa majeshi yake.
BIG NO __Hapana.
Wengi tusichojua ni kwamba, huu ulikuwa ni uhalifu wa kivita na DICK CHENEY, aliyekuwa Vice President wa G. W BUSH na DONALD RUMSFELD, Kiongozi Mkuu wa Ulinzi kipindi cha Vita ya IRAQ (alishafariki), ndio walioiingiza Marekani kwenye shida hii unaiona Leo, kisa wanamtafuta OSAMA
Read 114 tweets
11 Aug
𝐅𝐀𝐇𝐀𝐌𝐔 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐉𝐈𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐈𝐊𝐎𝐀🇹🇿

#𝕿𝖍𝖗𝖊𝖆𝖉:
Tanzania ni nchi iliyoko Africa
Jina "𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚" lilipatikana kwa mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 na 𝐌𝐨𝐡𝐚𝐦𝐞𝐝 𝐈𝐪𝐛𝐚𝐥 𝐃𝐚𝐫 ndiye aliyelibun.Hivi unafaham asili ya jina la mkoa wako?
Ktk kipind cha 𝐔𝐤𝐨𝐥𝐨𝐧𝐢 Tanzania ilikuwa na utawala wa majimbo 8, Lkn baada ya #𝐔𝐡𝐮𝐫𝐮 mikoa ilianzishwa kwa miaka tofauti na mpk Leo hii ninavyoandika #Uzi huu 𝐌𝐢𝐤𝐨𝐚 31 imeanzishwa kutoka pande zote Visiwani na Tz Bara.Najua ulishawahi kujiuliza asili ya Mkoa wako
Kila Jina unalosikia lazima kuna chimbuko ambalo ndio Asili ya jina hilo. Aidha, yawezekana limetoholewa ktk lugha za kigeni na kuchukuliwa kutokana na matumizi yake, muonekano, lugha za asili ktk Eneo fulani, tukio ama hata tabia za watu wa eneo fulani na makosa ya kimatamshi
Read 158 tweets
29 Jul
FAHAMU MADINI YA ALMAS 💎 UTAJIRI & VITA YAKE

#Uzi:
📋Asili yake
📋Historia yake
📋Mgunduzi wake
📋Aina & Thamani yake
📋Vita yake duniani na Tanzania
📋🇹🇿 iligunduliwa lini na nani, wapi
📋DE BEERS & Msukuma wa Williamson DIAMONDS, aliyeipenda Mwadui hakuna wa mfano wake!!
🔄👇
Leo nimechagua kuzungumzia Maliasili za Taifa🇹🇿

#Maliasili ni vitu vinavyotokana na maumbile. MFANO:Wanyama, Misitu, Madini n.k kama ulikuwa hufahamu maliasili za nchi huchangia ktk utajiri wa nchi husika.Mojawapo ni South Africa, imenawiri kiuchumi kutokana na utajiri wa madini
Nafahamu ulishawahi kujiuliza, Almasi ni nini? Iko iko je? au Almasi zinatengenezwa na nini?

LEO nakupa Jibu:

#ALMASI: Ni kito Adimu chenye thamani kubwa sana Duniani. Kito hiki ni kigumu sana kushinda Metali au madini yote Duniani. Asili yake hutengenezwa na Carbon (C) 99.95%
Read 96 tweets
27 Jul
FAHAMU MVUMBUZI WA TELEVISION (📺)

#Yes_____&&
#Thread|story🕐
Any sufficiently Advanced Technology is indistinguishable from MAGIC!! Binafsi huwa nasema Technology Is the Great ant💉dote to the Poison of Enthusiasm and Superstition💣
📋Asili ya TV
📋Historia yake
📋Uvumbuzi n.k
Televisheni (TV) au Runinga ni kifaa chenye kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.

Neno "Televisheni" linatokana na maneno mawili:
(i)Tele (Kigiriki)-kwa mbali sana na
(ii)Visio (Kilatini)-mwono.

RT @omari_manyama
kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza #Television limetoholewa kwa lugha ya Kiswahili "Televisheni".

Ugunduzi wa TV📺 ni kazi iliyofanywa na watu wengi mwishoni mwa karne ya 19.Karne ya 20 Watu mmoja-mmoja na makampuni yalishindana kuunda chombo kilichopiku teknolojia ya awali.
Read 37 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(