WHO is '๐“๐€๐‹๐ˆ๐๐€๐'? WANATAKA NINI HASA AFGHANISTAN?

#๐•ฟ๐–๐–—๐–Š๐–†๐–‰:
Ifahamike, walikuwa yatima ktk kambi za wakimbizi Pakistan.
Je, wana uhusiano na AL-QAEDA? #Tragedy:UINGEREZA & URUSI kuchezea kipigo cha Mbwakoko.
โœด๏ธChimbuko
๐Ÿ“กWalio nyuma yao?
๐Ÿ“‹Tofauti yao na MUJAHIDINA..
Vita vya Marekani nchini Afghanistan vimedumu kwa takribani miaka 20. Nimeona watu wengi wakitoa maoni juu ya Jeshi la TALIBANI kuchukua nchi Lkn wengi hawana historia juu yake. Wengine wanasema Rais wa Marekani @JoeBiden mefanya 'makosa' kuondoa majeshi yake.
BIG NO __Hapana.
Wengi tusichojua ni kwamba, huu ulikuwa ni uhalifu wa kivita na DICK CHENEY, aliyekuwa Vice President wa G. W BUSH na DONALD RUMSFELD, Kiongozi Mkuu wa Ulinzi kipindi cha Vita ya IRAQ (alishafariki), ndio walioiingiza Marekani kwenye shida hii unaiona Leo, kisa wanamtafuta OSAMA
Hebu tuangalie KWA UFUPI nini chanzo cha Vita hii na haya yote yanayoendele kutokea nchini Afghanistani.

LET'S GO...๐Ÿ‘‡

#Miaka 100 iliyopita, baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia (WWI) kumalizika, Dola ya Uingereza ilikuwa imekua sana kuliko nchi yeyote duniani (1921).
Nchi ya UINGEREZA ilikuwa imetawala eneo kubwa sana kwa takribani 23% inayokaliwa na idadi yote ya watu ulimwenguni.
#Kiufupi ilikuwa ni himaya kubwa kuliko zote ambazo ulimwengu umewahi kuona, kabla au tangu ya hapo. Na ndiyo ilikuwa kileleni kwa idadi kubwa ya makoloni.
Baada ya Uingereza kushinda ktk Vita vya Kwanza vya Dunia (WWI) vilivyomalizika mwaka 1918, ilikuwa pia na jeshi kubwa ktk makoloni yote iliyokuwa imewahi kuystawala. Hivyo, Uingereza ulikuwa UTAWALA USIOGUSWA kote ulimwengu kijeshi. Utagusaje Wababe wa Dunia๐Ÿ˜‚?
GUSA UONE MOTO๐Ÿ’ฃ
Ingawa sahv inatanguliwa na nchi nyingi baada ya maendeleo ya sayansi na teknolojia yaliyopelekea utengenezaji wa silaha mpya za kivita na za kisasa kabisa Duniani. Hivyo macho yake ilielekezea kusini. Hivyo, Ardhi ya INDIA ilikuwa "Kito cha thamani" kwa Dola ya Uingereza.
Baada ya kuzigusa Urusi (zamani Umoja wa Kisovieti) China, na Falme za Ufaransa na maeneo ya huko Indo-China (Vietnam n.k) ilielekeza majeshi kusini. Hivyo Uingereza ilikuwa na nguvu zaidi INDIA, Lkn ilipojaribu kupambana na AFGHANISTAN mnamo 1919, ilishindwa vibaya mno.

Why?๐Ÿ‘‡
Utajiuliza kwanini Wababe wa Dunia wakapigwa!!! Ukizingatia Uingereza haikuwa 'busy mahali pengine'. Kingine Vita vya Kwanza vya Dunia vilikuwa vimemalizika km mwaka mmoja uliopita. Hivyo Hakukuwa na kitu kingine chochote kinachoendelea!!

Lkn ilichezea..ilikuwaje?

Rt๐Ÿ”„ Twende
That was most and ever Tragedy to happen. Kushindwa kwa Uingereza nchini AFGHANISTAN kulishangaza sana. Yaani Falme kubwa kabisa iliyokuwa na watu wengi, haijawahi kutokea na jeshi lenye nguvu zaidi kwa WAKATI WOTE (kipindi hicho) imepoteza kwa nchi ndogo kama AFGHANISTAN...!!!?
Baada ya kupoteza huko Afghanistan, Falme ya Uingereza ilianza kuipoteza baadhi ya vita na ufalme ukaanguka.
Ni wazi kwamba AFGHANISTAN iliweza kusimamisha Himaya kubwa na yenye nguvu zaidi kuwahi kutokea duniani. Kwahiyo @ayubu_madenge usiione hivyo hii nchi ni hatari sana kaka.
Au, tunaweza kusema AFGHANISTAN ilitoa kipigo cha kwanza cha Mbwakoko kwa nchi ambayo ilikuwa haijawahi kupigwa.

#Twende miaka 60 mbele...

Ktk miaka 42 iliyopita, mnamo 1979, bado kulikuwa na shirikisho la Umoja wa Kisovieti (mojawapo iliyokuwa ktk muungano ni Urusi ya sasa).
Wasovieti walikuwa na jeshi kubwa ulimwenguni wakati huo ukipima kwa ukubwa wa ktk masuala ya ulinzi na usalama.
Jeshi la Wasoviet lilikuwa kubwa kwa idadi ya wanajeshi kuliko lile la #NATO, ukijumlisha muungano wa majeshi barani Ulaya, ukaongeza Marekani pamoja na Canada.
Naam..!!

WaSoviet walikuwa na jeshi kubwa sana, walikuwa wanamiliki Vifaru zaidi ya 40,000 huku nchi zote za NATO zikiwa na Vifaru 24,000 ukijumlisha na akiba zote za Marekani.
#Ninaomba pia nisisitize hili kwa wasomaji wangu na watu wote mnaonifuatilia...
Ukupima ukubwa wa Jeshi la NATO mwishoni mwa miaka ya 1970, ilionekana kwamba endapo NATO ingejaribu kupambana na majeshi ya Umoja wa Kisovieti, NATO ingepoteza vita ktk shambulio la WaSoviet kwa muda wa masaa 72 pekee tu. Huo ni utafati uliofanywa mwaka 2004 (jaribu kutafuta).
Ulaya yote ilitetemeka ikaogopa endapo watakuja siku moja kuvamiwa na WaSoviet.

Let's Go...

Kwa Afghanistan hatuhitaji kuhesabu Jeshi la Wanamaji, kwa7bu Afghanistan ni nchi iliyozungukwa na ardhi.Kikosi cha jeshi la angani Afghanistan kilikuwa na marubani wanaoteleza ktk anga.
Nchi ilikuwa inamudu vita vyote angani na ardhini. Jeshi lake la mwaka 1979 lilikuwa lenye nguvu zaidi kuwahi kutokea. Kwanza mitambo mipya ya silaha ktk historia, vifaru vinavyoweza kuzuia mionzi ya nyuklia au gesi ama silaha za kibaolojia.

RT๐Ÿ”„ iwafikie wengi..
Na lingeweza kupigana na wanajeshi karibia milioni 1 kwa wkt mmoja wakiwa ndani ya magari na vifaru vya kisasa.
Baada ya kuona Jeshi la Marekani ikipigana huko Vietnam WaSoviet waliweza kujifunza kutumia ndege na kutambua udhaifu wao. Ilikuwa rahisi sana kuwaangusha chini.
WaSovieti walirusha ndege angani maili 24 juu, ikawa helikopta ya kwanza yenye BULLET-PROOF. Chombo kilichokuwa salama kwa kiasi chake km Kifaru, imagine!! kikarushwa juu angani.
Hii ilikuwa silaha hatari kutoka kiwandani haijawahi kutokea kutokana na maendeleo ya teknolojia.
Lilikuwa jeshi kubwa kutengenezwa lenye nguvu na lisiloshindwa. Likiwa angani hatari, likishuka ardhini usiguse, likaingia nchi ya Afghanistan mnamo 1979.

Miaka kumi baadaye mnamo 1989, likapoteza na kufurushwa vibaya nchini kutoka Afghanistan baada ya kushindwa vita.
Wataalamu wengi wa masuala ya kivita mnamo 2001 walionya, kwamba vita nchini Afghanistan vitakuwa vya muda mrefu na vyenye umwagaji damu na pengine majeshi ya Marekani hayawezi kushinda.
Walisema angalau kidogo vinaweza kudumu kama ilivyokuwa vita vya Marekani nchini Vietnam (miaka 10) au Umoja wa Kisovieti huko Afghanistan (miaka 10).

Watu walio wengi walisema hakika Marekani haiwezi kushinda.
Ilikuwa rahisi kuona kwamba mnamo 2001, wakati Dick Cheney, Rumsfeld & W walipoamua kuvamia Afghanistan, kulikuwa na Maendeleo ya KITEKNOLOJIA, ambayo yangeweza kubadilisha uwanja wa vita. Silaha nzito na za kisasa pamoja na ndege zisizokuwa na rubani (drones).
Labda hiyo ilionyesha kungekuwa na ushindi na majeshi ya Marekani yangefanikisha hilo.Mpk mwaka 2004, kulikuwa na ushahidi wa wazi kwamba hapatakuwa na ushindi kwa Marekani dhidi ya Afghanistan. Utakumbuka kwamba Wataalam wengi ktk masuala ya kivita Marekani walikubaliana wkt huo
Tangu mwaka 2004 kumekuwa ni vita ya Kisaikolojia sasa ya kutafuta namna Marekani itajiengua kutoka ktk vita hii.
#Isipokuwa wachache kutoka Grand Old Party (GOP) au Republican ndio walioona kabisa vita ya Afghanistan ni km mchezo wa kamari muda wowote Marekani inaweza kupoteza..
Zamani kabla ya vyama vya Democratic na Republican kuundwa kulikuwa na chama kimoja cha DEMOCRATIC-REPUBLICAN PARTY, ingawa baada ya kugawanyika Republican kiliendelea kujiita wakongwe (GOP),
Katika uchaguzi wa Rais wa mwaka 2008, @BarackObama alitangaza Sera zake, ikiwemo kuvitoa vikosi vya majeshi ya Marekani nchini IRAQ na AFGHANISTAN. Lkn kwa mpinzani wake John McCain yeye alitaka majeshi ya Marekani kubakia ktk nchi zote mbili.
OBAMA akashinda, akayaondoa majeshi nchini Iraq, lkn kwa Afghanistan hakuondoa Jeshi lote. Alipunguza wanajeshi kiasi wengine wakabaki. Ktk uchaguzi mwaka 2012 mgombea wa chama cha Republican ROMNEY akakubaliana na OBAMA, kwamba Marekani inapaswa kuondoa vikosi vyake Afghanistan.
Mnamo 2016 TRUMP wa Republican na HILLARY CLINTON wa Democratic, wote wakaahidi kuviondoa vikosi vya Marekani kutoka Afghanistan
@DonaldJTrumpJr akashinda, Lkn alivunja AHADI yake. Hz ndio siasa za Marekani, wagombea hawatoi sera za barabara au madawati ni maisha ya Wamarekani Tu
Ktk uchaguzi wa Rais mwaka Jana (2020) JOE BIDEN aliahidi ataviondoa vikosi vyote vya majeshi ya Marekani kutoka nchini Afghanistan & TRUMP naye akaahidi vivyo hivyo, lkn kutokana alikuwa ameshavunja ahadi mwanzo alishindwa vibaya BIDEN akachukua nchi.

Kwann Trump alishindwa?๐Ÿ‘‡
#SABABU:
Kila mtu nchini Marekani alijua kwamba vita vya Afghanistan vilianzishwa kimakosa, wanajeshi wengi wa Marekani wanakufa huko uwezekano mkubwa wa kushindwa ktk vita hii ulikuwa mkubwa. Na taratibu waliona wataangukia ktk mikono vikosi vya Wa-TALIBAN ndio maana alishindwa.
Lkn Chama cha Republican wao waliahidi tangu 2012 kuwa watayaondoa majeshi yao AFGHANISTAN.
Bila shaka mlimsikia Rais @JoeBiden msimamo wake ni ule ule wa kuviondoa vikosi huko.Hata juzi nilimwambia ndg yangu @ayubu_madenge kuwa asitegemee kauli ya mabadiliko ktk press ya BIDEN.
Kwahiyo, Republican kumlaumu JOE BIDEN kwa kusafisha hili dhoruba ya miaka nenda miaka rudi itakuwa UJINGA. Ni sawa na mtu atengeneza silaha, yatokee mauaji halafu atokee kulaumu waliofanya mauaji, kwanini ulitengeneza? Ili waweke mapambo au watumie kwa vitendo?

Turudi ktk Uzi๐Ÿ‘‡
TALIBAN

Wakati vikosi vya majeshi ya TALIBANI vinachukua utawala Afghanistan (kwa mara nyingine tena), Tunahitaji kuiangazia TALIBANI kwa undani zaidi. Wengine wanasema Talibani wamewafukuza vibaraka wa Umoja wa Kisovyeti kutoka nchini mwao na wengine magaidi!!

Kipi ni kipi? ๐Ÿ‘‡
Kupata ukweli juu ya hili, hebu NIFUATILIE kwa umakini kabisa, ili tuangalie asili ya TALIBANI na MUJAHIDEEN, pamoja na PASHTU na Serikali iliyokuwepo madarakani kwamba ni akina nani.
Niliwahi kuandika mwaka 2016 kuhusiana na siasa za AFGHANISTAN, nikitahadharisha Serikali ya Magufuli dhidi ya vitendo vya kuwatenga Viongozi wa upinzani (ambao ni wawakilishi) ktk shughuli mbalimbali za Maendeleo nchini. Ikiwa ni miaka 5 iliyopita leo yanatokea niliyoandika.
Nimewahi kutembelea mataifa kadhaa ktk maisha yangu takribani nchi 8 hadi sasa. Ijapo bado sijaenda Afghanistan. Lkn nimewahi kukaa kwa majirani zao, Saudia Arabia na Omani, ambapo nilikutana na stori za Waafghanistan.
Sitaki kuelezea zaidi ilikuwaje nikafika huko lkn natumai wengi mna historia yangu, nimewahi kuandika hapa Uzi nikielezea My Life Story na nikagusia kwa uchache nilipokuwa Oman.

Hebu turudi Tuendeleee na Uzi..๐Ÿ‘‡
Tukiwa tunaendelea Ifahamike kuwa kuna baadhi ya watu ht kule Marekani waliosababisha vita ya TALIBANI na serikali ya Afghanistan pamoja na serikali ya Saudi Arabia na wanaojaribu kuzima ukweli usijulikane juu ya nani mwanzilishi na mnufaika

Kwahiyo, uzi huu ni muhimu na maalum
#ILI kuelewa mnyororo mpk vita ya TALIBAN nchini Afghanistani, Inatakiwa tuanzie chimbuko la kikosi hiki cha wapiganaji kilipoanzia.

Lkn kabla hujaendelea hapa chini. Naomba kuelewa km unakubali ninachokuletea kila siku ktk nyuzi mbalimbali.๐Ÿ™

Weka maoni yako bonyeza hapa ๐Ÿ‘‡
Tuendeleee..

Ktk historia ya Uchumi wa mwanadamu kwa miaka ya zamani, kulikuwepo na njia moja iliyokuwa muhimu na ilitumika kwa zaidi ya miaka 3,000 iliyopita. Barabara hiyo iliyoitwa SILK ROAD au Jade Road huko kwa wenzetu.

Uzi huu nimeandika na kuongezea maoni ya @tomiahonen
Njia hii iliunganisha ardhi kubwa zaidi maeneo ya EURASIA, eneo ambalo idadi kubwa ya watu ktk sayari ya Dunia walikuwa wakiishi.
Ndio njia iliyopitisha wafanyabiashara kutoka nchi za Ulaya kufanya biashara mpk China, na baadhi ya nchi zote zilizopo hapo katikati.
Maana ya EURASIA ni jina linalotumika kutaja kwa pamoja nchi zote za Asia na Ulaya.

Jina hilo linaunganisha maneno mawili:

"Europa"+"Asia" = EURASIA

Kiuhalisia mabara ya Ulaya na Asia yako pamoja kama nchi moja na hakuna bahari inayoyatenganisha.
Kwahiyo, Ulaya na Asia haziitwi mabara kwa7bu za kijiografia bali kwa7bu za kihistoria na za kiutamaduni tu. Utaratibu huu unatokana na WAGIRIKI wa Kale ambao ni watu wa kwanza kuigawa Dunia ktk sehemu 3: Ulaya, Asia na Afrika) na kuweka msingi wa ugawaji wa dunia kwa mabara.
Wataalamu wengi wa jiografia wanakubaliana kwamba mass (tungamo) ya nchi kavu inayojumuisha Ulaya na Asia ina tabia zote za bara moja na hivyo hutumia jina la "EURASIA".
Karibu eneo lote liko juu ya bamba la Ganda la Dunia (Gandunia) lile lile (Bamba la Ulaya-Asia)

Tuendeleee..
Haya mambo ya kijiografia ktk sayansi Tuachane nayo tuendeleee na stori yetu.๐Ÿ‘‡

#SILK_ROAD sio kwamba ni barabara moja tu, hapana, hizi ni njia nyingi za hiyo barabara. Upande mmoja wa njia hiyo ilikuwa ikielekea maeneo ya India. Mwingine Uchina mpk upande mwingine mpk ITALY...
Kwa upande wa kuelekea mpk INDIA, ilipitia ktk safu za milima, kupita kichochoro kimoja kilichoitwa KHYBER. Ilikuwa njia muhumu kwa wafanyabiashara kusafirisha bidhaa haraka. Ukilinganisha umuhimu wake kwa leo basi ni sawa na Mfereji wa SUEZ (Suez Canal) kwa nchi za Kaskazini.
Ukitizama hiyo njia ya KHYBER ilivyokuwa inapitia milimani kwenda India, unaweza kuona jinsi ilivyokuwa fursa nzuri kwa MAHARAMIA. Hivyo, eneo hilo lilikuwa chini ya udhibiti wa Maharamia yenye nguvu. Maharamia hao walitoka ktk kabila lililoishi huko milimani liitwalo WaPASHTUN..
Ukichukua eneo la mikoa ya MOROGORO na DODOMA ndio ukubwa wa eneo hilo ambalo lilikaliwa na maharamia hao.

Kwa hiyo, kwa karne nyingi, hao watu wa jamii ya PASHTU (PASHTUN) walikuwa wanatoza ushuru kutoka kwa wasafiri waliokuwa wakipitia njia hiyo iliyokuwa ikipita SILK Road.
Na hakuna nchi iliyokuwa na uwezo wa kuchukua mkoa huo kutoka kwao. Hata Mfalme Alexander Kiongozi mkuu wa kabila na iliyokuja kuwa Milki ya GENGHIS KHAN huko Uchina, hakuna hata 1 zilizofanikiwa kuchukua eneo hilo kutoka kwao. Kila walipojaribu walichezea kipigo.
Ukawa msingi thabiti kwa wao kujenga himaya yenye nguvu.

Hawa PASHTU, wao ni Waislamu, lkn kama wale Waislamu wa nchi jirani ya IRAN (ambao wengi WASHIA), lkn kwa PASHTU ni wale Answar Sunni wenyewe, kwahiyo mara nyingi huungana na Saudi Arabia na kupingana na Iran.
Ktk miaka 200 iliyopita, Dola kuu zilizokabiliwa pande zote kwa kutumia njia hii ya KHYBER zilikuwa: Dola ya Uingereza (huko India, Kusini) na Dola ya Urusi (Kaskazini). Hivyo, nchi ya Afghanistan iliibuka kama taifa la kimkakati na ulinzi kati ya maeneo haya mawili.
Eneo hilo lipo umbali wa kilometa 8 Magharibi mwa njia iliyokuwa ikipita Khyber

Ingawa eneo la Afghanistan ni kubwa zaidi kuliko eneo linalokaliwa na PASHTU, lkn wao wenyewe wanaishi eneo la ukubwa karibu kilomita za mraba 160,000 sawa na uchukue Singida, Dodoma na Morogoro.
Kabila hili limetapakaa mpk nchi jirani ya Pakistani. NUSU ya wakazi wote wa AFGHANISTAN ni kabila la Pashtu na wanaishi zaidi ktk majiji ya PESHAWAR, KABUL QUETTA na KANDAHAR. Hakuna kabila lingine kubwa zaidi hilo nchini humo, kwa hivyo watu wa Pashtu wanaongoza kwa idadi kubwa
Idadi ya watu wote Afghanistan ni karibu milioni 32. PASHTU wenyewe ukijumlisha na wale waoishi Pakistani idadi yao inakadiriwa kusa zaidi ya milioni 50 hivi.
Kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1800, watawala wa Afghanistan walikuwa wakiwachanganya sana watawala wa Urusi na Uingereza, wao kwa wao, yaani Serikali ya Afghanistan ilikuwa inaunga mkono kwa muda, yeyote ambaye alikuwa dhaifu kati yao.
#Kiufupi, PASHTU walikuwa ni mabingwa wa kujifanya wako upande wako, kumbe kwa ground wanakusoma tu wakiona umepata nguvu wanahamia upande wa pili.

Kila wkt Uingereza iliposhiba, ikajaribu kuichukua ardhi ya Afghanistan, mara zote walishindwa na mara ya mwisho ilikuwa mnamo 1921
Hata Warusi nao pia walipojaribu walichezea kipigo cha mbwakoko na kupoteza, mara ya mwisho wao ilikuwa mnamo 1989 (ukiwa Umoja wa Kisovieti). Hivyo Basi HAKUNA FALME hata moja uliyowahi kushikilia eneo hilo. Naam hao ndio WaPashtu ambao wanaunda nusu ya wakazi wote Afghanistan
MUJAHIDEEN (MUJAHIDINA) ni Akina Nani?

Hapa ndipo tunapokwenda kupata chimbuko la TALIBAN.

Mtawala wa Kikomunisti MOHAMMED DAOUD KHAN, aliingia madarakani nchini Afghanistan kwa kumuondoa Mfalme MOHAMMED ZAHIR SHAH mnamo 1973. Akaunganisha Afghanistan na Umoja wa Kisovieti.
WA-PASHTU wakaona sasa watapoteza endapo lao litachukuliwa na Urusi, wakaanzisha vita vya msituni (Guerillas wars) dhidi ya Serikali ya Afghanistan. MUJAHIDEEN (Mujahidina) walikuwa mashujaa wa dini la Kiislamu dhidi ya serikali ya Kikomunisti iliyokuwa madarakani.
Mwanzoni WAPATSHU waliungwa mkono na Saudi Arabia. Wakapata misaada kutoka kwa jamaa zao WaPashtu waliokuwa mpakani maeneo ya Pakistan. Kpnd Umoja wa Kisovieti ulipoivamia Afghanistani mnamo 1979, majeshi ya MUJAHIDINA yalikuwepo na yalipigana kunisaidia serikali ya Afghanistani.
Wasovieti waliivamia Afghanistan kwa7bu tangu awali walikuwa wanatamani kuchukua ardhi yao. MUJAHIDINA hawakujali serikali iliwasaliti huku ndani walikuwa na vita vya wenyewe baina ya makundi. Wakaungana Wakavamia WaSovieti wkt huo wakiungwa mkono na Saudi Arabia na Pakistani.
Waingereza waliona waunge mkono MUJAHIDINA dhidi ya Urusi (Wasovieti) kutokana na historia (mahasimu).Wakawapa wapiganaji silaha, chakula na magari ya kivita. Marekani ilikuwa ndio imetoka kupoteza vita na Vietnam, so ilitoa msaada kidogo, Fedha na mafunzo SAUDIA ndio ilisaidia
Kutokana na safu za milima ilivyokaa maeneo walioishi PASHTU na ukizingatia kwakarne nyingi walizoea mapigano. MUJAHIDINA walikuwa wanakwenda Afghanistan kupigana na kisha jioni kurudi kupumzika upande wa pili wa mpaka Pakistan kujipanga upya na kuandaa mbinu za kuwapiga Warusi.
Hivyo, Majeshi ya Kisovieti yalishindwa kabisa kuvamia upande wa Pakistan ili kupigana nao ama kuwaondoa.
Hii ilisababisha kambi nyingi za wakimbizi upande wa Pakistan. Ikiwemo kambi za MAFUNZO namna ya kupigana vita. Walifundishwa na nani? Majeshi ya Saudi Arabia na Pakistani.
Zikaanzishwa shule kwa mgongo wa kuwaelimisha vijana kujiunga MUJAHIDINA. Serikali hiyo hiyo ya SAUDIA ndio ilianzisha shule za dini zenye msimamo mkali zikaitwa 'MADRASA' ili kufundisha Sharia kuu (fundamentalist Sharia law).
Wapiganaji wa MUJAHIDINA waliajiri wanajeshi wa Kiislam, kutoka maeneo mbalimbali kuja kupigana ili kulikomboa taifa lao la Kiislamu la Afghanistan kutoka kwa waliowaita wao wavamizi (Wakomunisti) na wasioamini Mungu.
Mmoja kati ya wajitolea wengi kutoka nchi za nje ni OSAMA BIN LADEN aliyekuwa mshirika mkuu wa Marekani mwenye asili ya Saudi Arabia.Uvamizi wa majeshi ya Kisovieti nchini Afghanistan ulidumu kwa kipindi cha miaka 10, Lkn hawakuwahi kupata udhibiti na ushindi kamili ktk nchi hiyo
Wasaudia akiwemo OSAMA BIN LADEN na Wapakistani waliwaunga mkono MUJAHIDINA tangu mwanzo. Uingereza na Falme za Kiarabu (UAE) wao walisaidia mwanzoni. Marekani ilikuja baadaye, ndipo wakawapa makombora ya kutungua ndege za kivita. Kupindi hicho OSAMA hajaanza kuitwa Gaidi na USA
Marekani ilisaidia kwa7bu ilikuwa ikipinga sera za kikomunisti tangu zamani. Wapiganaji wa MUJAHIDINA walikuwa hodari na walitumia akili sana haijawahi kutokea, na ktk miaka 10 waliliondoa jeshi kubwa la Kisovieti lilikuwa na nguvu zaidi ulimwenguni kote kwa kipindi hicho.
Licha kuwa na idadi ndogo ya silaha kulinganisha na Wasovieti, umoja wao uliwasaidia hatimaye Wakashinda mchana kweupe na wazi. Majeshi ya Umoja wa Kisovyeti yakaondoa kutoka nchini Afghanistan mnamo mwaka 1989, tena bila mbwembwe wala vitisho vyovyote.
Ulikuwa mshangao wa wengi, serikali ya kikomunisti ya Afghanistan ya MOHAMMED NAJIBULLAH ikashikilia uongozi kwa zaidi ya miaka mitatu kabla ya kulemewa na wapiganaji wa MUJAHIDINA waliokuwa umiliki ktk baadhi ya majimbo. Ukumbuke Mfalme alipinduliwa na Kiongozi wa Kikomunisti.
Baadhi ya VIONGOZI wa MUJAHIDINA walishindwa kukubaliana juu ya muundo wa utawala, machafuko yakaibuka. Nchi ikawa tena na makundi yaliyoundwa. Umoja ukasambaratika kila mmoja akachagua wapi alekee, tatizo udhibiti nn? Uongozi wa baadhi ya wilaya ambazo hazikugawanywa awali.
Baadhi ya MUJAHIDINA walitaka kupanua shughuli zao kuongeza mapambano ya Kiislamu ktk maeneo mengine ya dunia, kama vile ISRAEL na KASHMIR.
Yakajitokeza mashirika kadhaa kushirikiana nao kuendeleza matarajio hayo.
Moja ya haya mashirika ni AL-QAEDA, lililoundwa na OSAMA BIN LADEN na mkutano wa kwanza ulifanyika 11 Agosti 1988. OSAMA alitaka kuanzisha shughuli zisizo za kijeshi maeneo mengine ya Dunia, Lkn rafiki yake AZZAM akataka kubaki kampeni za kijeshi tu.
Baada ya ABDALLAH YUSUF AZZAM kuuawa mwaka 1989, makundi yaligawanyika huku idadi kubwa wakijiunga na shirika la OSAMA BIN LADEN. Mnamo Novemba 1989, ALI MOHAMED (Sergeant wa vikosi maalum vya Fort Bragg, Marekani) alisomea mambo ya kijeshi na akahamia SANTA CLARA (California)
MOHAMED ALI alisafiri kwenda Afghanistan kisha Pakistan na ashirikiana kwa usiri na BIN LADEN.

Mwaka mmoja baadaye, mnamo 08 Novemba 1990, Shirika la Kijasusi FBI, Lilivamia nyumba moja ktk mitaa New Jersey ya mmoja WA washirika wa Al-Qaeda aliyeitwa MOHAMMED EL SAYYID NOSAIR.
akukutwa na ushahidi wa mipango mikubwa ya kigaidi, pamoja na mipango ya kulipua majumba marefu ya Jiji la New York. Akapatikana na hatia ya kuhusika na ulipuaji wa bomu mnamo 1993 ktk World Trade Center na kwa mauaji ya RABBI MEIR KAHANE yyaliyotokea Novemba 05, 1990.
Mnamo mwaka 1991, ALI MOHAMMED alisaidia kumhamisha OSAMA BIN LADEN kutoka Sudan kwenda Afghanistan.
Nimejaribu kuelezea kwa ufupi, mengi nimeacha yasubili Uzi mwingine maana hapo sijagusia kwa undani AL-QAEDA, lkn zile sehemu muhimu nimegusia kiasi chake.
TALIBAN

Wapiganaji wa Taliban HAWANA uhusiano wowote na mapigano yoyote ya hapo awali, ht wkt AFGHANISTAN ilipokuwa imevamiwa.WALA hawana uhusiano wowote na uvamizi wa Urusi au Umoja wa Kisovyeti. TALIBAN haikuwepo.Kikundi hiki kilizaliwa BAADA ya majeshi ya Kisovieti kuondoka.
KABLA ya uvamizi wa majeshi ya Kisovieti mnamo 1979 Afghanistan ilikuwa ktk Vita vya wenyewe kwa wenyewe, (nitakuja kuielezea siku nyingine). Kwahiyo ile vita ilisitishwa kwa miaka 10, ili kuwaondoa Warusi, ndipo vita ya wenyewe kwa wenyewe vikaanza tena waking'ang'ania majimbo.
Hapo ndipo kikundi cha wanamgambo chenye misimamo na Itikadi kali cha TALIBAN kilipoundwa. Wakitaka kuibadili nchi ya Afghanistan kuwa nchi inayofuata mfumo wa Sharia za kiislam na kuwa taifa linalotawaliwa kwa kufuata mifumo ya Itikadi za kidini wakifuata misimamo ya AL-QAEDA.
Maana ya neno 'TALIBAN' linamaanisha 'Wanafunzi' kwa lugha ya kabila la PASHTUN.

Chimbuko lake imetokana na wakimbizi wa Afghanistan ambao waliachwa YATIMA baada ya vita. Watoto hao walipelekwa huko KANDAHAR kwenye kambi za wakimbizi kufundishwa ktk shule za kiislam (Madrasa).
Viongozi watano wa juu kabisa ktk kundi hili la TALIBAN, walikuwa miongoni mwa wahitimu wa DARUL ULOOM HAQQANIA, moja ya shule ya Madrassa ktk mji mdogo wa Akora Khattak. Mji huo uko karibu na Peshawar nchini Pakistan, lkn sehemu kubwa umekaliwa na wakimbizi wa Kiafghanistan.
Taasisi hiyo ilionyesha imani kwa mafundisho yake na kuchangia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya elimu mambo mbalimbali Fedha walizokuwa wakipewa na baadhi matajiri wa biashara za mafuta kutoka Saudia.
Baadhi ya marafiki wa OSAMA wengi Wamarekani walitoa michango mingi kupitia benki za Kiislamu na mashirika yaliyokuwa yanatoa misaada na kuzipeleka moja kwa moja ndani ya Pakistan. Huku viongozi wengine wakiendelea kupewa mafunzo ili kurudi kuikomboa nchi yao Afghanistan.
MUJAHIDINA wengi baadaye walijiunga na WATALIBANI kupigana na kundi la lilijiita wakereketwa la MUHAMMAD NABI MOHAMMAD la Harakati za INQILABI kipindi cha uvamizi wa Urusi. Kundi hili pia ni moja ya makundi yaliyopata uaminifu kwa wapiganaji wengi Waarabu wa Kiafghanistan.
Ugomvi uliokuwa ukiendelea kati ya makundi mbalimbali na uasi na kutofuata sheria kufuatia kuondoka kwa Urusi, ilisaidia WATALIBANI, wakaongezeka na kupanua udhibiti wa wilaya kadhaa Afghanistan. Vijana hawa waliojiita wanafunzi wakaanzisha misingi zaidi ya himaya yao.
Awali OSAMA BIN LADEN alikuwa mtu aliyepewa heshima zote na mataifa haya mawili (Marekani na Saudi Arabia). Hata aliporudi kutoka vitani baada ya kusaidia vikosi vya MUJAHIDINA kuwashinda WASOVIETI alitunukiwa nishani ya juu ya kijeshi. Ndipo akapata ufadhili wa kwenda kusoma USA
#KwaUfupi: Chanzo cha OSAMA kuitwa Gaidi ni kwamba, mnamo Agosti 1990 IRAQ aliivamia KUWAIT kwa kigezo kuwa lilikuwa eneo la nchi yake. Baada ya Mfalme wa SAUDIA ARABIA kuona vile akaona inawezekana ndiye anayefuatia kuvamiwa kwa7bu sehemu baadhi alizokalia zilikuwa za IRAQ.
Kpnd hicho IRAQ ikiongozwa na SADDAM HUSSEIN. Hivyo Saudi Arabia ikaomba msaada kutoka Marekani ili kumsaidia ulinzi asije akavamiwa. Baada USA kuingia Saudia Arabia ndipo OSAMA akaenda IRAQ kumsaidia ulinzi SADDAM asiuawe na majeshi ya NATO kwa7bu SADDAM alikuwa mtawala ...
Anayefuata misingi ya Itikadi za Kiislam na kuhusu KUWAIT kweli lilikuwa eneo lake. Ndipo Saudi Arabia ikatangaza kumfuta Ukoo OSAMA BIN LADEN. Ikawa sasa ni vita kubwa akaanza kufadhili makundi yalikuwa yanapigania Uislam kwa nguvu ikiwemo IRAQ.

Ikatangazwa ni Gaidi anatafutwa
Kpnd hicho BILIONEA kutokana na biashara za mafuta. Alikuwa na Nguvu ktk nyanja zote. Tuachane na OSAMA turudi ktk TALIBAN.
Wengi wanaiona Saudi ni safi ktk hili la AFGHANISTAN kuliko IRAN wakidhani ndio mbaya, Lkn makundi km AL-QAEDA, TALIBAN yalianzishwa kwa mchango wa SAUDIA
Hivyo basi, TALIBAN haikuanzishwa kpnd cha Uvamizi wa Kisovieti, bali iliazishwa mwaka 1994 na makomando wawili marafiki wa Saudia, MULLAH OMAR & MULLAH ABDUL GHANI BARADAR. Wakaanzisha himaya yao waliyoiita Jamhuri ya Kiislam ya Afghanistan (Islamic Emirate's of Afghanistan).
Mwaka 1995 walikalia eneo la Herat linalopakana na Iran, kabla kuuteka mji mkuu na kutimua utawala wa Rais BURHANUDDIN RABBANI, mmoja wa waanzilishi wa MUJAHIDINA kipindi cha Uvamizi wa Kisovieti.
Mwanzoni mwa 1996 waliuteka mji wa KANDAHAR na baada kujiimarisha wakachukua udhibiti wa nchi ya Aghanistan ktk mji mkuu KABUL mnamo Septemba 1996, hii ilikuwa baada kushinda vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kufikia mwaka 1998, Taliban ilikuwa inadhibiti karibu 90% ya nchi ya Afghanistan

Ktk mazingira yaliyotafirisiwa ugaidi mkali na jinai dhidi ya binadamu, Afghanistan iliongozwa na viongozi tofauti chini ya MULLAH OMAR aliyekuwa kiongozi wa wanamgambo wa Talibani hadi mnamo 2001.
Marekani ilivamia baada ya OSAMA kuweka makazi nchini humo, ikimtafuta kwa kufanya ugaidi ikiwemo lile la kulipua Balozi zake Afrika Mashariki (1998). Na ktk miaka hiyo 5 ni nchi TATU pekee (Saudi Arabia, Pakistan na Falme za Kiarabu [UAE]) zilizoitambua serikali ya Afghanistan,.
Wkt Taliban walipodhibiti Afghanistan waliigeuza nchi kuwa taifa la kiitikadi na misimamo mikali inayofuata mfumo wa Sheria ya Sharia za Kiislam.
Majeshi ya Marekani na NATO yalipovamia mnamo 2001, ndipo TALIBANI ilirudi nyuma wakajificha mafichoni wakipambana kuuondoa uvamizi.
Wengi tulijua kuwa hakuna mtu anayeweza kuchukua eneo hilo. Ni kama ulikuwa ujumbe kuashiria kuangamizwa kikundi hicho.

Swali la msingi la kujiuliza ni nani aliye nyuma ya Wapiganaji wa TALIBAN kutoka mwaka huo 2001 mpk leo 2021? Jibu ni moja SAUDI ARABIA Bila Shaka.
Hili limeripotiwa mara kwa mara. Hata Idara za Usalama nchini humo zilijua hili lkn ikawa siri, na hii baada ya nyaraka za Serikali zilizovuja kuweka wazi mnamo 2009. Serikali IRAN inawaona TALIBAN kama maadui, hivyo SAUDIA ARABIA ndio iliyo nyuma kuwafadhili sababu za kidini.
Ukiangalia kabla ya miaka hii miwili iliyopita Marekani ilikuwa ikisigana na Saudi Arabia kutokana na Mauaji ya KASHOGI, Lkn ile kesi ilififishwa kiaina, kwa7bu huyo mwandishi alikuwa anatoa Siri nzito za SAUDIA iliyokuwa mshirika wake mkubwa + sakata la TRUMP kuachia wafungwa
Mpk hapo ukiniuliza TALIBAN ni akina nani?

Jibu nitakalokupa ni vuguvugu la wazalendo wa Afghanistan wenye msimamo mikali, lililoanzia katika nchi jirani ya Pakistani na kuanzia 1996/2001 walikuwa watawala, sema walitumia sheria za Kiislamu (Sharia).
Na Tangu uvamizi wa Marekani mwaka 2001, utawala wao uliangushwa na kundi hilo likageuka kuwa waasi nchini Afghanistani. Hali ilikuwa mbaya zaidi ktk kipindi cha Trump na ufisadi wake, akishirikiana na Saudi Arabia.
Trump pamoja na mambo mengine alitaka kuwaalika TALIBAN kwenye kambi moja inayoitwa Camp David mnamo Septemba 11, 2019. Trump ndiye ameipa nguvu Taliban. Na mwaka jana (2020) aliachilia Wapiganaji 5,000 wa Taliban KUTOKA GEREZANI.

Kuhusu VIONGOZI wa TALIBAN
...mnamo 2010 (wakati wa Obama) ni maswali ya kujiuliza na hapo ikitokea nitayaelezea ktk Uzi mwingine. Lkn kwa uchache ktk picha huyo namba 2 alikuwa kiongozi mwenza wa Taliban, anaitwa MULLAH AGDAR GHANI BARADAR alikamatwa na kupelekwa gerezani nchini Afghanistan
Halafu mnamo 2013 huyo namba 1 anaitwa MULLAH OMAR alifariki kwa ugonjwa wa kawaida (Taliban walifanya kuwa siri hadi 2015 waliposema), endelea kunifollow @Eng_matarra ili tuzidi kujifunza.
Lkn kwa kukudosea, Rais TRUMP alimwachia mwanzilishi mwenza wa Taliban, MULLAH ABDUL GHANI BARADAR mnamo 2018 kupitia mpango uliojadiliwa na Mike Pompeo akiwa mhalifu wa kivita.
Hakuna takwimu kamili za nguvu za jeshi la Taliban nchini Afghanistan. Lakini wachunguzi wanakadiria kuwa wapo karibu wapiganaji 150,000 ikiwa ni 50% chini ya jeshi la Afghanistan. Wapiganaji wa Taliban wanatawaliwa na ukoo wa Bashtun.
Lkn pia kuna wapiganaji wengine kutoka makabila mengine na nchi nyingine za Kiislamu. Kikundi hiki kimeundwa tofauti na vikundi vingine vya wapiganaji na ina uongozi wa kimfumo. Kundi linaongozwa zaidi na makamanda ambao walipigana dhidi ya Umoja wa Kisovieti ktk miaka ya 1990.
Makamanda hawa wana uzoefu wa jinsi ya kushambulia na njia rahisi za kushambulia miji muhimu nchini, na wameshinda vita hii kwa sababu wamekuwa wazoefu ktk mapigano ya msituni na milimani.
Wapiganaji wa Taliban wana silaha ndogo ndogo, lakini pia kuna silaha nzito.
Idadi kamili ya vifaa vyao vya kijeshi haijulikani.
Kiongozi wao anaitwa HEBATULLAH AKHUNDZADA alichukua uongozi wa Taliban nchini Afghanistan mnamo Mei 26, 2016, wakati alipoteuliwa na baraza la ushauri la harakati hizo.
Ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa Taliban na msaidizi wa karibu na mwanzilishi wake, MULLAH MOHAMED OMAR. Takwimu zinaonyesha zaidi ya wanajeshi 45,000 Afghanistani wameuawa ktk kipindi cha miaka mitano iliyopita. Naam hao ndio WaPashtu asili yake TALIBANI.

MWISHO____!!
MUHIMU _____________&&

RT๐Ÿ”„ kisha nifollow @Eng_matarra Tuendeleee kujifunza PAMOJA๐Ÿ™

Mwisho wa huu Uzi ndio mwanzo wa Uzi mwingine. Comment maoni Yenu hapo chini.

โ€ข โ€ข โ€ข

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
ใ€€

Keep Current with JAPHET MATARRA

JAPHET MATARRA Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Eng_Matarra

13 Sep
FULL OPERATION MAPINDUZI YA RAIS (GUINEA)

#Thread

Baada ya TALIBAN nchin Afghanistan, habari sasa ni MAMADY DOUMBOUYA kiongozi wa kijeshi huko Guinea, kumpindua rais na kuchukua madaraka #Unadhani kikosi kidogo cha SFG kiliwezaje kudhibiti kambi za kijeshi na kumkamata rais?๐Ÿ‘‡
Yes, mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa (French Legionnaire) aliyerudi nyumbani miaka 03 iliyopita na kuaminiwa na Rais ALPHA CONDร‰, ndiye aliyemsaliti na kumuondoa madarakani baada ya kutaka kuongoza nchi kwa muhula wa 03

MAMADY DOUMBOUYA ambaye ana cheo cha Kanali alionekana..
kwenye kituo cha Radio-Tรฉlรฉvision Guinรฉenne(RTG), mnamo 5 Septemba majira ya saa 2 usiku, akiwa amevalia kofia nyekundu (Red Beret) ameweka bendera ya taifa hilo begani mwake, na kuzungukwa na wanajeshi wanane, akatangaza kuwa jeshi limechukua madaraka ya nchi.
Read 147 tweets
9 Sep
MAPINDUZI YA GUINEA TZ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ YA SAMIA INACHAKUJIFUNZA

#UZI

Ilianza kama utani Mzee Condรฉ hakuamini kijana wake mwenyewe aliyemlea, mwenye masters ya vita na cheo akampatia alipomwambia "simama juu hlf ukae chini" Unadhani ilikuwa rahisi kumpindua? Naam It's #Guinea:1958-Present๐Ÿ‘‡
Sikuweza kuandika Uzi yalipotokea mapinduzi ktk nchi nyingine mbalimbali, lkn kwa yaliyotokea jumapili nchini Guinea nimeona niandike ili Watanzania tuone km kuna lolote la kujifunza. Nitaangazia upande wa kisiasa tu. Nitachambua kila kitu kuanzia uhuru hadi kutokea mapinduzi.
Maswali nayotaka kukujibu km ulijiuliza ni haya:๐Ÿ‘‡

๐Ÿ’จHistoria ya Guinea ikoje?

๐Ÿ’จKwnn mpk mapinduzi?

๐Ÿ’จCol. Doumbouya ana nguvu gani

๐Ÿ’จKwann wananchi wamefurahia?

History repeats itself, 1st as Tragedy, second as Farce.
Just retweet ๐Ÿ”„ huenda siku
Uzi huu ukakukumbusha kitu
Read 211 tweets
11 Aug
๐…๐€๐‡๐€๐Œ๐” ๐€๐’๐ˆ๐‹๐ˆ ๐˜๐€ ๐Œ๐€๐‰๐ˆ๐๐€ ๐˜๐€ ๐Œ๐ˆ๐Š๐Ž๐€๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

#๐•ฟ๐–๐–—๐–Š๐–†๐–‰:
Tanzania ni nchi iliyoko Africa
Jina "๐“๐š๐ง๐ณ๐š๐ง๐ข๐š" lilipatikana kwa mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 na ๐Œ๐จ๐ก๐š๐ฆ๐ž๐ ๐ˆ๐ช๐›๐š๐ฅ ๐ƒ๐š๐ซ ndiye aliyelibun.Hivi unafaham asili ya jina la mkoa wako?
Ktk kipind cha ๐”๐ค๐จ๐ฅ๐จ๐ง๐ข Tanzania ilikuwa na utawala wa majimbo 8, Lkn baada ya #๐”๐ก๐ฎ๐ซ๐ฎ mikoa ilianzishwa kwa miaka tofauti na mpk Leo hii ninavyoandika #Uzi huu ๐Œ๐ข๐ค๐จ๐š 31 imeanzishwa kutoka pande zote Visiwani na Tz Bara.Najua ulishawahi kujiuliza asili ya Mkoa wako
Kila Jina unalosikia lazima kuna chimbuko ambalo ndio Asili ya jina hilo. Aidha, yawezekana limetoholewa ktk lugha za kigeni na kuchukuliwa kutokana na matumizi yake, muonekano, lugha za asili ktk Eneo fulani, tukio ama hata tabia za watu wa eneo fulani na makosa ya kimatamshi
Read 158 tweets
29 Jul
FAHAMU MADINI YA ALMAS ๐Ÿ’Ž UTAJIRI & VITA YAKE

#Uzi:
๐Ÿ“‹Asili yake
๐Ÿ“‹Historia yake
๐Ÿ“‹Mgunduzi wake
๐Ÿ“‹Aina & Thamani yake
๐Ÿ“‹Vita yake duniani na Tanzania
๐Ÿ“‹๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ iligunduliwa lini na nani, wapi
๐Ÿ“‹DE BEERS & Msukuma wa Williamson DIAMONDS, aliyeipenda Mwadui hakuna wa mfano wake!!
๐Ÿ”„๐Ÿ‘‡
Leo nimechagua kuzungumzia Maliasili za Taifa๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

#Maliasili ni vitu vinavyotokana na maumbile. MFANO:Wanyama, Misitu, Madini n.k kama ulikuwa hufahamu maliasili za nchi huchangia ktk utajiri wa nchi husika.Mojawapo ni South Africa, imenawiri kiuchumi kutokana na utajiri wa madini
Nafahamu ulishawahi kujiuliza, Almasi ni nini? Iko iko je? au Almasi zinatengenezwa na nini?

LEO nakupa Jibu:

#ALMASI: Ni kito Adimu chenye thamani kubwa sana Duniani. Kito hiki ni kigumu sana kushinda Metali au madini yote Duniani. Asili yake hutengenezwa na Carbon (C) 99.95%
Read 96 tweets
27 Jul
FAHAMU MVUMBUZI WA TELEVISION (๐Ÿ“บ)

#Yes_____&&
#Thread|story๐Ÿ•
Any sufficiently Advanced Technology is indistinguishable from MAGIC!! Binafsi huwa nasema Technology Is the Great ant๐Ÿ’‰dote to the Poison of Enthusiasm and Superstition๐Ÿ’ฃ
๐Ÿ“‹Asili ya TV
๐Ÿ“‹Historia yake
๐Ÿ“‹Uvumbuzi n.k
Televisheni (TV) au Runinga ni kifaa chenye kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.

Neno "Televisheni" linatokana na maneno mawili:
(i)Tele (Kigiriki)-kwa mbali sana na
(ii)Visio (Kilatini)-mwono.

RT @omari_manyama
kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza #Television limetoholewa kwa lugha ya Kiswahili "Televisheni".

Ugunduzi wa TV๐Ÿ“บ ni kazi iliyofanywa na watu wengi mwishoni mwa karne ya 19.Karne ya 20 Watu mmoja-mmoja na makampuni yalishindana kuunda chombo kilichopiku teknolojia ya awali.
Read 37 tweets
19 Jul
MAUAJI YA RAIS WA HAITI

#OnJuly07, 2020 ๐Ÿ‡ญ๐Ÿ‡น

#Story ina part A na B

๐Ÿ“‹Historia ya Haiti

๐Ÿ“‹Mauaji ya Rais @moisejovenel

๐Ÿ‘ฉโ€๐Ÿ’ปUnajua tangu ipate uhuru imeongozwa zaidi ya marais 49, kati yao 9 ndio walimaliza vipndi vyao bila kupinduliwa/kuuawa wakiwa madarakani?
#Thread|Story๐Ÿ•’๐Ÿ‘‡ ImageImageImage
Usiku Julai 7 watu wenye silaha walivamia makazi binafsi Rais @moisejovenel wa Haiti na kumuuawa. N MAUAJI yaliyoshtua Haiti, ingawa bado haijulikani nani aliyeajiri wauaji na kwanini, lkn mercenaries wa Colombia na Marekani walikamatwa kufuatia mauaji yale.
RT iwafikie wengi๐Ÿ‘‡
Turn on Notification..

Naona ๐Ÿ“ฑ iko Low baada ya nusu saa hv nitarudi kukiwasha.

Hii nchi ni mapinduzi, kuuawa, kutiwa sumu ukiwa madarakani mpk le๐Ÿ‘‡ ImageImage
Read 322 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(