📡Zima hizi settings za windows 10 haraka sana

5 Oct Microsoft waliachia windows 11, lakini hatutegemei watumiaji wake watakuwa wengi kwa sababu ya vigezo vinavyohitajika kuweza tumia Windows 11.

Kuna zaidi ya PC 1 billion zinazotumia windows 10 mpaka sasa duniani.

#HabariTech Image
📡Kati ya watumiaji hawa kuna wengi wasiofahamu baadhi ya settings ambazo zinakusanya taarufa zao, zinawafanya waone matangazo mengi au kufanya PC zao ziwe pole pole.

Ukiacha madhaifu ubora wa Win10 ukilinganisha na zile za nyuma, bado ina madhaifu mengi unakutana nayo kila siku Image
📡Kati ya hayo ni pamoja na kutokuwa na uhuru wa usiri (Privacy) wako, spidi ya OS na urahisi wa kutumia.

Leo tuchambue baadhi ya settings ambazo ni vyema ukaziweka off ili uendelee kutumia Win10 yako kwa raha.
📌File Sharing Update

Hii ni setting ambayo inakuruhusu kupakua updates za Win10 kutoka kwa PC nyingine na sio kwenye server za Microsoft moja kwa moja.

Japo utapakua kutoka kwa PC nyingine unapokuwa umeunganishwa kwenye internet au LAN.
📡Ubaya wake ni pale ambapo PC nyingine zenye windows 10 zitaweza pakua updates kutoka kwako pia. Hii itafanya PC yako kuwa slow kwa kiasi inapotumia mtandao.
📡Kuizima setting hii nenda kwenye

Settings -> Update & Security -> Advanced Options -> Delivery Optimization kisha hapo ndani zima “Allow Downloads From Other PCs” Image
📌Notifications zinazokera

Kupata notifications kwenye Win10 huwa ni jambo nzuri pale inapokuwa notification ya msingi.

Kuna zile zinakera kama za VLC kila ikibadili nyimbo au video kwenye playlist yako.
📡Kutoa notifications za hivi nenda hapa
Settings -> System -> Notifications & Actions
Ukifika hapo scroll kwenda chini utakuta orodha ya program zinazoleta notification. Zima zile usizozihitaji. ImageImage
📌Matangazo ya Start Menu

Ukizingatia vizuri start menu yako utaona kuna apps zipo pale hujawahi zipakua. Hayo ni matangazo kutoka kwa Microsoft.

Wanajitahidi sana kutangaza apps zao zilizopo katika Microsoft Store ili zipakuliwa kwa wingi au kupata watumiaji wengi zaidi.
📡Unaweza toa haya matangazo kwa kufanya hizi
Settings -> Personalization -> Start
Hapo zima hii kitu “Show suggestions occasionally in Start” Image
📌Matangazo yanayokulenga kutoka kwa Third-Party apps

Katika kuupiga mwingi na Win10, Microsoft wanakufatilia sana unafanya na apps unazotumia kwenye Win10.

Wanaangalia mapendeleo(Preferences) yako katika apps unazotumia na vitu unavyoperuzi mtandaoni.
📡Kufanya vizuri zaidi wanakupa mpaka ID yako binafsi ya matangazo kupitia Microsoft account yako.

ID hiyo ndiyo inatumia kukuonyesha matangazo yanayokulenga wewe kulingana na namna unatumia Win10.
📡Fanya hivi kuzima hii
Settings -> Privacy -> General: ukifika hapo zima hii “Let apps use advertising ID to make ads more interesting to you based on your app activity (Turning this off will reset your ID). Image
📌Cortana kutaka kukujua zaidi

Cortana ni A.I ambayo ni msaidizi wako binafsi kwenye Win10. Kama msaidizi bianfsi anavyotakiwa kumjua bosi wake vizuri basi ndivyo Cortana alivyo.

Cortana anajifunza kukujua wewe kwa kukusanya taarifa zako kedekede.
📡Vitu kama sauti yako, namna unaongea, namna unatype, historia yako ya vitu umeandika kwenye PC yako na mengineyo.

Hii kitu kwa baadhi ya watu inaweza kuwa a kutisha kidogo.
📡Unaweza mzima Cortana kwa kufanya hivi.
Ingia kwenye Settings kisha search “Cortana”, Katika majibu chagua “Change how you talk to Cortana”.
Ndani yake zima kila kitu ambacho kitakuwa on kwa muda huo. ImageImage
📌Apps zinazofanya kazi kwenye Background

Apps hizi ni zile ambazo hata usipozifungua zinaendelea kufanya kazi. Zinaweza pokea taarifa, kutoa notifications mpaka kupakua na ku-install updates.

Kwa hizi gharama za data hapa TZ ni vyema ukazima hizi kutunza bando uliyonayo.
📡Ingia Settings -> Privacy -> Background Apps
Hapo unaweza zima zote zisifanye kazi kwa kuzima “Let apps run in the background” au ukazima app moja moja kwenye orodha iliyopo chini. Image
📌Automatic Updates

Win10 huwa inapakua na ku-install updates yenyewe PC yako inapopata internet. Huwezi kuzima hii moja kwa moja na nakushauri usizime.

Updates huwa ni njia ya kuboresha ufanisi kazi wa PC yako na kuboresha usalama wa PC yako,
📡lakini kuna muda huwa tunahitaji kuzima updates hizi aidha bando halitoshi au updates zinaleta shida badala ya kuboresha.

Updates unaweza zima kwa siku 35 au chini ya hapo. Baada ya muda huo kuisha utalazimika kufanya update kwanza ndipo utaweza tena kuzima kupokea updates.
📡Kuzima feature hii ingia
Settings -> Updates & Security -> Advanced Options kisha nenda kwenye pause updates na uchague unataka zima kwa muda gani.

Maisha ya Windows yanapendeza inapofanya kazi vizuri katika ubora. Kwa kufanya haya tunategemea utafurahia maisha na Windows 10. Image

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with HabariTech

HabariTech Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @HabariTech

11 Oct
📡Hakuna Tesla iliyotengenezwa China kuingia nchini India.

Hivi karibuni waziri wa usafiri wa barabara nchini India amesem, aliongea na Elon Musk na kumuomba kwamba Tesla kwa za india zitengenezwe nchini India.

Maalumu kabisa hakutaka Tesla za China kuwepo India.

#HabariTech Image
📡Akongea katika "India Today Conclave 2021", waziri huyo alisema kwamba, Gari za umeme zilizoundwa na Tata Mottors zina ubora unaokaribiana na zile za Tesla.

Hivyo Tesla za kuuzwa India inabidi zitengenezwa ndani ya India na sio China na kuuzwa kutoka India kwenda nchi jirani. Image
📡Sambamba na hilo alisisitiza kuwa, Tesla watapata sapoti yoyote wanayohitaji kutoka serikali ya India.

Tesla waliomba kupata punguzo la ushuru wa kuingiza gari za umeme India. Mpaka sasa hawajafikia muafaka na serikali ya India kuhusiana na maombi haya yote.
Read 5 tweets
28 Sep
Unaijua simu isiyo na tundu la chaji wa earphone?

Ni kama uhalifu vile namna kampuni za simu zinaleta mabadiliko mapya kila kukicha.

Apple alianza kwa ondoa headphone jack kwenye iPhone 7 na matoleo yaliyofuata na baadae Samsung akafuata.

Kuna cha zaidi? Ndiyo 🧵

#HabariTech
📡Watazamaji wa Sci-Fi movies mtakuwa mmewahi kutana na zile simu ambazo ni kioo tu lakini zinafanya kila kitu.

Huenda huko ni mbali sana kufika labda 2050 huko. Twende mpaka 2030 ambapo nadhani huenda tutakuwa na simu zisizo na button yoyote, headphone jack wala tundu la chaji.
📡Unakumbuka iPhone X ilikuja na notch 2017? ikawa mwanzo wa kubadili muundo wa display za simu. Hapo tayari iPhone hazikuwa na port ya earphone

Oppo F9 ikawa simu ya kwanza kuja na teardrop screen na kumpa mtumiaji nafasi ya kutumia screen nzima.

Na sasa kuna Hole Punch.
Read 17 tweets
18 Sep
Njia rahisi kutunza UZI za twitter uweze zisoma kwa muda wako.

Twitter ni social media pendwa ambayo uhusiano wa watu unaendeshwa kwa mazungumzo ya tweets. Tweets zimekaa kwenye muundo rahisi mtu kusoma.

Bahati mbaya ni rahisi pia tweet kukupotea kama hukuitunza.

🧵#HabariTech
Ushakutana na uzi za @JemsiMunisi au @TOTTechs ?

Unakuta ni uzi flani hivi zina flow matata. Unajiuliza sasa zikipotea hizi nazipata vipi tena?

Usipate tabu tena. Leo nitakupa njia 5 ambazo zinaweza kukusaidia kutunza tweets/uzi unazokutana nazo hapa twitter.

Kana flow eeh!
1. Twitter Bookmark

Hii feature watumiaji wengi wa twitter huwa hawazingatii au hawaijui. Kwa wanaoijua ukifungua bookmark zao utakuta madini ya kutosha huko.

Kuiweka tweet kwenye Bookmark

Gusa "Share" kwenye hiyo tweet unataka save kisha chagua "Add tweet to Bookmark".
Read 11 tweets
15 Sep
Whatsapp itapokea update mpya.

Whatsapp ni mtandao wenye watumiaji takribani 2 billion dunia nzima. Mtandao huu umekuwa maarufu kwa sababu umerahisisha sana mawasiliano kwa njia ya Internet.

Hivi karibuni huenda Whatsapp web ikabaki kujitemea bila uhitaji wa Mobile version. Image
Whatsapp Web ni version ya Whatsapp ambayo hutumika kwenye browser za computer au kwenye app ya Whatsapp ya Windows au MacOS.

Whatsapp web inabeba text, zile zile ambazo unazion kwenye simu yako. Kwa maana hiyo inatumia akaunti yako ile ile. Image
Ili utumie Whatsapp Web ilikuwa ni lazima ile ya kwenye simu iwepo online na ya PC pia iwepo online.

Hili litabadilika hivi karibuni baada ya Whatsapp kuanza fanyia kazi version ambayo haitahitaji zote mbili kuweo online.
Read 7 tweets
8 Sep
Websites zilizojificha kwenye 60,000,000,000 TB za data kwenye internet.

Internet ni kijiji kimoja kikubwa sana kinachozidi kukua kila sekunde. Kama unavyojua maisha yetu kijijini ni ujamaa.

Kuna hizi website kadhaa ni muhimu sana zinaweza boresha uwepo wako mtandaoni.

🧵
1. Soap2Day

Huwa una bando la kutosha na unaweza vumilia matangazo yasiyo na mpangilio? Tumia hii website ya soap2day kuangalia movies mtandaoni.

Hapa hauna haja ya kumiliki akaunti ya netflix ni mwendo wa ski ads na press and play.

wvw.ssoap2day.to
2. Temp Mail

Kuna huduma unahitaji kujaribu kama inakufaa, lakini hutaki kutumia email yako ya kila siku?

Tempmail ipo kukupa email utakayo tumia kwa muda mfupi kukamilisha zoezi hilo.

Ukiingia kwenye page hii utakuta email ipo tayari kwa ajili yako.

temp-mail.org/en/
Read 6 tweets
1 Sep
Afrika Bila Internet kwa muda usiojulikana.

African Network Information Centre (AFRINIC) taasisi ambayo toka mwaka 2005 ilipewa mamlaka ya kusambaza anawani za kimtandao (IP addresses) barani Afrika ipo hatarini kushindwa kuendelea kufanya kazi.

UZI 🧵
#habarinews
Kila kifaa kinachotumia mtandao kina anwani iitwayo IP Address. Anwani hii inakutambulisha wewe mtandaoni.

Anwani hizi ndizo ambazo zinatambulika mtandaoni na si jina la simu, website au PC unayotumia.
website kama ya @RednetCompany unaweza ifikia kwa kutafuta rednet.co.tz lakini computer yako inapoingia mtandaoni itatafuta 162.214.100.22.

Namba hii ni anwani ambayo mtandao inatambua kama ni miliki ya @RednetCompany
Read 20 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(