📡Watazamaji wa Sci-Fi movies mtakuwa mmewahi kutana na zile simu ambazo ni kioo tu lakini zinafanya kila kitu.
Huenda huko ni mbali sana kufika labda 2050 huko. Twende mpaka 2030 ambapo nadhani huenda tutakuwa na simu zisizo na button yoyote, headphone jack wala tundu la chaji.
📡Unakumbuka iPhone X ilikuja na notch 2017? ikawa mwanzo wa kubadili muundo wa display za simu. Hapo tayari iPhone hazikuwa na port ya earphone
Oppo F9 ikawa simu ya kwanza kuja na teardrop screen na kumpa mtumiaji nafasi ya kutumia screen nzima.
Na sasa kuna Hole Punch.
📡Hizo zote ni jitihada za kuboresha namna ambavyo tutaweza tumia simu zetu. Leo hii ukipewa simu yenye screen za zamani na bezels kubwa unaona kama wanakuonea.
Najua si mimi tu ninaye tegemea simu kutokuwa na bezel, notch au hole punch natemea vyote vikae chini ya screen.
📡Simu ya miaka ijayo itakuwa nyembamba sana. Pia zitakuwa na wireless charge yenyewe kabisa tofauti na hizi za sasa.
True wireless charge ni ile ambayo unaweza kuwa umeshika simu mkononi lakini bado inapeleka chaji. Ukiwa popote ndani ya chumba chako unaweza chaji simu.
📡Mpaka hapo unaona kuna uhitaji wa kuwa na port ya chaji? Fikiria unakua na true wireless charge ya 120W. Yani ndani ya dakika 10-20 simu inajaa kutoka 0% -> 100%
Hakuna kulia tena kuhusu cable kukatika.
Tuachane na chaji. Kuna earphones.
Ni soko halijapewa heshima yake.
📡Unajua kwamba Airpods za Apple pekee zimefikisha mauzo zaidi ya $10 Billion?
Kama hao ni Apple pekee inakuaje tukiunganisha pamoja na mauzo ya wireless earphone za kampuni nyingine?
Hii ina maana gani?
📡Watu wengi wanaacha kutumia wired earphone. Aidha kwa sababu ya ufahari au kwa sababu hawataki kuachwa na teknolojia.
Yote kwa yote, hii itapelekea kuondoa kabisa port za earphone mara baada ya hizi wireless earphones kuweza kukaa na chaji kwa saa 12 za kutumika.
📡Kama hatuna port yoyote kwanini pia tusiondoe button?
Aah! haiwezekani sasa tutawasha vipi simu zetu na kuongeza au kupunguza sauti? 😂
Sasa hapo...Hapo ndipo pressure sensor zitakuwa na umuhimu (Kwa sauti ya professor wa money heist).
Tupo tayari kwa haya yote?
📡Hapo sasa sio kwamba buttons zimeondoka kabisa ila tu hatuna tena zile mechanical buttons unazoweza bonyeza.
Mfumo wake hautatofautiana sana na namna unatumia screen ya simu yako sasa hivi. Hivyo sio kitu cha kushangaza sana.
Vipi nikikwambia hata hii sio kitu kipya?
📡Mwaka 2019 HTC walikuja na simu iliyoitwa HTC Exodus 1. Button za simu hii ziliendana kidogo na kitu ninachokwambia hapa kuhusiana na button za simu zijazo.
📡Hizi mbwembwe zote ni kwa ajili ya nini sasa?
Kwako wewe muhimu ni kuwa na kifaa cha mawasiliano. Mwingine kuwa na simu yenye camera bora au uwezo mkubwa.
Ukiacha kwamba ni mashindano ya kiteknolojia na mauzo. Mara ngapi umedondosha simu ikavunjika au kuingia kwenye maji?
📡Nadhani imekukuta au imewakuta watu wengi. Hii ni moja ya sababu simu zitabadilika kiasi hicho.
Simu zikiweza fika huko zitakuwa imara zaidi na hata uwezekano wa kuingia maji utakuwa mdogo mno.
Hiyo itakuwa ni True Waterproof phone.
Picha za chini ya maji zitakuwa nyingi.
📡Naota ndoto za mchana au hizi ndizo zitakuwa simu za badae? Binafsi naamini ndipo tunakoelekea.
Mabadiliko ya hivi tushaanza kuyaona kwenye baadhi ya simu.
Labda hapo baadae tutaanza hata tumia holograms kama zile za Tony Stark (Iron Man).
📡Mfano wa portless phone ni ile ambayo @Xiaomi walituletea concept yake.
Whatsapp ni mtandao wenye watumiaji takribani 2 billion dunia nzima. Mtandao huu umekuwa maarufu kwa sababu umerahisisha sana mawasiliano kwa njia ya Internet.
Hivi karibuni huenda Whatsapp web ikabaki kujitemea bila uhitaji wa Mobile version.
Whatsapp Web ni version ya Whatsapp ambayo hutumika kwenye browser za computer au kwenye app ya Whatsapp ya Windows au MacOS.
Whatsapp web inabeba text, zile zile ambazo unazion kwenye simu yako. Kwa maana hiyo inatumia akaunti yako ile ile.
Ili utumie Whatsapp Web ilikuwa ni lazima ile ya kwenye simu iwepo online na ya PC pia iwepo online.
Hili litabadilika hivi karibuni baada ya Whatsapp kuanza fanyia kazi version ambayo haitahitaji zote mbili kuweo online.
African Network Information Centre (AFRINIC) taasisi ambayo toka mwaka 2005 ilipewa mamlaka ya kusambaza anawani za kimtandao (IP addresses) barani Afrika ipo hatarini kushindwa kuendelea kufanya kazi.
Utakubali kuhudumiwa na Muuguzi Roboti Hospitalini?
UVIKO-19 umebadilisha sana mwenendo wa maisha yetu ndani ya miaka 2 iliyopita. Nani aliwaza kwamba leo hii kufanya kazi kutoka nyumbani ingekuwa ni kitu kinachopewa kipaumbele hivi?
🧵
Katika jitihada za kuokoa maisha ya watu wengi zaidi duniani, tumeona uundaji wa roboti ambao wanachukua nafasi za wauguzi katika hospitali.
Kampuni ya Hanson huko Hong Kong imekuja na roboti huyu mwenye muonekano wa kibinadamu.
Amepewa jina la "Grace".
Hanson robotics kwa wale msioifahamu, ni kampuni ile ile ambayo ilimtengeneza Sophia. Roboti mmoja maarufu sana duniani.
Sophia alipewa uraia wa Saudi Arabia. Na sasa Hanson robotics wanatuletea Grace.
Grace atahusika zaidi kutoa huduma kwa wagonjwa wa UVIKO-19 hospitalini.
Kutaka kutupia PC ni ili kuboresha ufanisi wa kazi na kuongeza spidi ya kufanya kazi.
Bahari mbaya Windows huwa si rafiki kwetu siku zote katika hili. Unaweza hitaji kukamilisha kazi haraka, lakini windows ikakufedhehesha.
Somo la leo ni jinsi ya kuongeza spidi ya win10.
UZI
Windows 10 imeboreshwa sana ukilinganisha na matoleo ya nyuma ya Windows. Inafanya vizuri sana kwa PC ambazo zimekidhi vigezo, shida huwa kwa PC za kizamani.
PC hizi hazina uwezo mzuri kubeba hii OS, hivyo mara nyingi watumiaji wake huwa wakilalamika kuhusu ubora wa Win10.
Twende moja kwa moja kuangalia ni kwa namna gani tunaweza ongeza spidi ya Win10.
MUHIMU: Hacks hizi ni zile anazoweza fanya mtu yeyote.