THOUGH IT WAS SHORT BUT I'LL NEVER FORGET πŸ’”

Kuna wakati naona kama nilikua character wa hadithi nzuri ya mapenzi iliyoishia njiani, nawaza pengine Mwandishi wa ile hadithi yangu aliishiwa wino na hakuona haja ya kununua kalamu nyingine kumalizia story
#Thread
Kwa kawaida ikifika mwisho wa wiki hasa nyakati za jioni ni mida ya watu kutoka kwenda kuupa mwili pole baada ya heka heka za week ndio maana wengine huita FurahiDay japo kama hauna pesa unaweza kuamua tuu kubaki ndani kama Bulb, inaruhusiwa pia.
Ilikua Ijumaa moja jioni nikiwa home nimechill nikaona nikiendelea kukaa peke yangu naweza nikajikuta nawaaibisha ancestors kwa kutext maEx ovyo. So nikaona nipige mahesabu miguu inipeleke wapi jioni ile na karata ikaangukia kiunga kimoja wanaita IpoIpo.
Maarufu kwa kitimoto yake na jioni sana pakauaga na liveband & Karaoke
Nadhani kitu pekee kimekosekana hapa Moro ni bahari tuu ambayo kimsingi hatuihitaji,maeneo ya kufurahia yapo mengi yaani kimwili unawezakua chimbo hili la bata lakini roho iko chimbo jingine. micasa sucasa!!
So nikaingia bafuni kuosha hekalu la bwana maana mi sio jamii ya wale ambao birthday ndio bath-day zao.
T-shirt +jeans +boots ndio combo yangu perfect na kijicoat flani,nikachukua wallet yangu na pesa si corona ipo basi mask usoni since kuna Elon,Forbes wangeweza niita Noel-Mask
Sikuwa na haja ya kujiangalia kwenye kioo sikuna Mirror on the world anayojiangaliaga Lil Wayne bhana?
So,baada ya dakika kadhaa nikawa Mazimbu IpoIpo nikatafuta eneo zuri nikapoa nikiwa na bwia juice za wakubwa
Haikuchukua muda kama vile director wa movie akawa ndio karuhusu
Aliingia binti mmoja mrembo sana utadhani katengenezewa labaratory.Wallahi hata ungekua wewe unge-weweseka, nikahisi yawezakua baba yake ni Maulid maana kwa vazi lake la Kitenge na zile airpods sikioni ilitosha kuniambia hakua wale low hanging fruits
Nikajikaza kutokumwangalia
Lakini wapii uharisia wangu ukanigomea, ule mwendo wake, kigauni juu ya magoti,usoni kajipiga lamination wanaita makeup.Alikua Hot sana kidogo niombe wawashe feni mule ndani.
Sikuwahi kufanya kazi SACCOS lakini nikajikuta nimekua na Interest na yule dada.Akaenda kukaa pembeni
Nikiwa naendelea kunywa nashangaa naona binti yupo mwenyewe tuu almost 30 minutes. Nikaona isiwe kesi sana nijisogeze maana mie sio Freemason sikuona haja ya ku-sita-sita hata nikitoa Bocco fresh tuu kwanza mie shabiki wa Yanga.
Nilivyomfikia nikaanza kumchombeza kwa tahadhari
Maana huezijua jamaa yake yuko pembeni akakutengenezea clip ukajikuta unatrend mitandaoni
"Hey,bila shaka unaitwa Happy maana sio kwa tabasamu hilo ambalo nimeliona tangia umefika, kama sio hivo basi waitwa Waridi maana ingekua mchana vipepeo wangekufuata kwa jinsi ulivyopendeza"
Akabaki anashangaa, mi nikaendelea sikumpa time ya kuwaza cha kuongea yani ile back to back punch lines mpaka angekua bubu ange-bubujikwa kwa machozi ya furaha.
"Naitwa Noel, nilikua peke yangu nilivyoona uko mwenyewe nikaona sio mbaya nije hapa so that we can be alone together "
Ye akasema anaitwa Rhoda
Damn!! my dirty mind si ikaweka "U" nyuma ya Rhoda 😀
Akatoa airpods na kuweka simu mezani nilivyoona macho matatu nikajua ni Eye-phone sasa sijui ni trick yake kumchanganya adui.Hadhi, urefu, umri,unene kipato ni vitu sizingatii labda sikuambiwa jandoni
Nikaendelea bana " So Rhoda, Moro ni kwenu au ni umekuja kusoma" akasema yupo Intern kwenye moja ya bank hapa mjini. Kumbe kipindi mi napambania school fees yeye keshakua school free, unafikiri nilijali sasa??
Nikamuita waiter akamuanzishia Safari ya Savanna kupitia Kilimanjaro.
Story zikaendelea bana bia zishaanza kumuingia kila nachoongea anacheka kama kajiunga kifurushi. Akawa anamlaani bwana wake aliyemuahidi angefika pale na hakutokea.
Akawa ananiangalia sana akaniuliza "Noe, unaona nini ndani ya macho yangu" kiukweli nilichoona
Ilikua ni kope za bandia na wanja mweusi ila nikaona nimwambie angechopenda kuskia kwa wakati ule nikamwambia " licha ya weusi wa mboni zako but i can see the bright future in it, macho yamefit vizuri kwenye orbit, unaonekana imara sana Rhoda" basi akazidi kucheeeka
Moyoni nikajiona mshindi usiku ule maana kwa kuzoeana ghafla namna ile nilijua leo lazima nikalale usingizi-wa-Porno na yule mrembo ambaye akiongea kama anamumunya pipi
Ikafika mida kama saa nne na nusu akadai baridi nikasimama gentle as a man nikampatia koti langu siunajua tena!
Sasa akawa anaanza kusimama kucheza macho karembua Ozil sio Ozil,Fei Toto sio Fei Toto. Ikabidi nimchukue mpaka pembeni ukutani palipotulia ambapo kelele pekee zilikua mapigo yetu ya moyo, tumesogeleana ile distance hata vernier callipers isingeweza measure.
Akaanza kupumua kwa kasi pale mapacha wawili kifuani mwake walivyogusa kifua changu, nikaanza kubarizi anatomy ya ule mwili wake mkono unazunguka Mbezi, Kibamba, Kama Joke-et kidogo nifike Kisarawe Astaghafirullah. Sasa ghafla simu yake ikaita akawa kama katoka usingizini.
Akadai yule boyfriend wake anapiga wakaongea kama dakika moja ati jamaa yake yupo nje kaja na gari kumchukua.
Nadhani ukiachilia mbali maumivu ya kujikwaa kidole cha mwisho kwenye kona ya tranka, haya ni maumivu makali kwa mimi kuwahi kuyapata
Akatoa mkoba wake harakaharaka huku akinikabidhi business kadi yake nikamfuatisha kwa macho mpaka anaingia kwenye ile gari InayoSitiriTuu mwili wanaita IST.

Nikaangaza kama kuna mtu kashuhudia, kweli bhana kuna meza mbili wote walikua wananiangalia ikabidi nikajiunge nao tuu
Nachoshukuru hawakunicheka wengi wao walinipa moyo mpaka pale nilipogundua yule dada kumbe alienda na koti langu. Kwaio pamoja na yote na koti kabeba??
Anyways kuna kuFall in love na kuna kuFall asleep,mimi nikachagua hiyo ya pili
Kinyoonge nikarejea home, hata sikuwahi kumtafuta

β€’ β€’ β€’

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
γ€€

Keep Current with Noe_Wenc πŸ’Š

Noe_Wenc πŸ’Š Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Vet_doctor87

3 Nov 20
AN OPEN LETTER TO YOU BROTHER πŸ“œ

Habari za siku kaka , imekua muda mrefu sana bila mawasiliano nadhani ni vile changamoto za maisha zinatuweka mbali lakini kwa kuwa tupo chini ya anga moja natumai ni suala la muda mimi na wewe kukutana
#Thread
Matumaini yangu umzima sana hasa kiafya na harakati zako za kila siku ,ningeweza kukutumia ujumbe mfupi wa maandishi ( sms) au kukupigia simu lakini nikaona kama barua kidogo ingebeba ujumbe na hisia zote zaidi ingekupa muda wa kuitafakari tofauti na ilivo meseji ambapo ingefutwa
Dear brother, nia na dhumuni la barua hii ni kukuuliza kwamba " vipi bado una ari ile ile ya utafutaji? Vipi malengo yako bado yako vile vile? bado una sababu ya kutafuta maisha?
itakua vema kama bado upo yule yule wa zamani aliyekua na malengo mengi sana na molari
Read 18 tweets
15 Oct 20
HAKUSTAHILI KUPITA NJIA NGUMU KIASI KILE
Wakati mwingine dunia inatuweka darasani kujifunza masomo ambayo hatukuwahi kuwaza kujifunza. Pengine hata mitihani ya hayo masomo hatujui itakuja lini
Tabasamu na uchangamfu wake vilificha mengi lakini hakustahili yale #Thread
Unaweza kuchagua marafiki lakini sio jirani maana wewe utajenga hapa ila atakaekuja kujenga pembeni yako hauwezi kumjua ,hivohivo kwenye kupanga chumba. Nilijikuta nimepanga chumba ambapo nyumba ya jirani waliishi familia nzuri na sisiti kusema nilivutiwa nayo kiukweli
Walikua na furaha muda mwingi .Wazazi walikua wa makamo ya miaka 34 na mtoto mdogo wa miaka 10, kutokana na uchangamfu wangu nikajikuta nimekua rafiki na baba wa hiyo familia ambaye alikua ameajiriwa kwenye kampuni moja hapa Mjini . Aliitwa Mr Beda , nilipenda sana kuwa nae hasa
Read 25 tweets
16 Jun 20
LET MY MIND SPEAK
So, hakuna kizazi bora kama kizazi chenye wingi wa maarifa na vijana wenye kuchangamkia fursa kila inapotokea.
SHORT THREADπŸ‘‡
My brother @veggiesfarmer once said " We are in knowledge economy,what you know is what will differentiate you and accelerate your growth, your growth will highlight your value and your value will elevate your worth.
Imekua muda mrefu nikitafuta platform ya kuweka kila kitu nlichokua nacho kichwani coz i've a lot man!! My head is about to burst!!
Nimekua nikiandika sana humu twitter but naona haitoshi
Read 9 tweets
8 Jun 20
WE CAN'T BE THE SAME!!

Yawezakua nyuma yako ikawa mbele yangu, au mbele yako ikawa nyuma yangu. Hii haipingiki na ni ngumu kuikataa.
Safari ni moja ya wote tunapotaka kufika ijapokua tunatofautiana maana ya mafanikio na njia ya kuyafikia
T H R E A D πŸ‘‡πŸΌ
Tusichukuliane poa kabla hatujaijua kesho yako na yangu pia.

Imagine unafanya kazi kujinufaisha wewe peke ako lakini mimi napambana natafuta maisha kwa ajili yangu ya familia yangu pia kwahiyo ukiona sipigi hatua ya maendeleo usishangae HATUWEZI KUWA SAWA.
Wote tunaishi dunia moja chini ya anga moja.
Japo wewe unavaa kupendeza na kuwa mtu anaekwenda na wakati lakini mimi mwenzako navaa kujistiri tuu..Sikulaumu wala sikuonei wivu lakini priorities zetu zinatofautiana sana kuna vingi vya msingi kwangu kuliko kuvaa.Hatuwezi kuwa sawa
Read 12 tweets
28 May 20
AN OPEN LETTER TO MY CRUSH πŸ’Œ

Dear crush,
Nimetuma meseji lakini nachoambulia ni Bluetick lakini najipa moyo pengine unakuaga bize, nikipiga simu mara kadhaa nikikuta inatumika basi najipa moyo utakua unaongea na ndugu yako
Nimeona ni bora leo nikuandikie barua
T H R E A D πŸ‘‡ Image
I hope uko salama
Umekua furaha yangu kila nikikuona ukipita mwenyewe au na wenzio, umekua my mood changer maana nawezakua naskiliza reggae lakini ukipita tuu nahisi nachosikiliza ni blues.
Unaniweza sana dear crush maana simu yangu imejaa screenshots nyingi za picha zako
Wananicheka marafiki jinsi navyokosa kujiamini pale napokuona,
Huwezi amini umetawala kichwa changu nakumbuka ile siku tumekutana ulivonambia nimependeza ilibidi nipite dukani kwa Mangi ninywe soda kwa kujipongeza 😁
My dear, msonyo wako kwangu naona kama busu
Read 14 tweets
18 May 20
I ONCE EXPERIENCED THE POWER OF LOVE ❀

Nilidhani nguvu ya treni kuvuta behewa ndio nguvu kubwa kuwahi kutokea nikapingana na fikra hizo pale nilipowaza nguvu ya maji kunyanyua meli
Nlipingana na hayo pale nilipokumbana na nguvu iliyopo katika fikra za walopendana
T H R E A DπŸ‘‡
Binafsi sijizuii kupenda inapobidi japo haimaanishi siwezi kuishi bila mpenzi, naamanisha kisu changu kina kata vyoote lakini hakikati tamaa tuu
Nikimuhitaji mtu akaona siendani nae, naachana nae najiandaa kwa "come back " kubwa πŸ˜„
Ndio kilichotokea bana enzi hizo nasoma
High school nliwahi kumpenda mtu akahitaji mpaka niwe na funguo tatu " three keys" ya gari, ya nyumba na ya ofisi nkaona nisonge mbele kama injili maana local man ntavitoa wapi vitu ambavyo wengine wanapata wakistaafu πŸ˜‚

So baada ya mission hiyo kufeli nkapenda tena.Story began
Read 30 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(