Nilitazama nyuma na kukutana na kijana mrefu, maji ya kunde, mkakamavu, sura ya kazi kwelikweli.
Nikainuka, nikamtazama nisijue la kusema. FUATILIA #UZI
#DaktariMwandishi
Nikamsikia Afande akimuita yule aliyenisemesha, "Mbise, yatupie taulo baba."
Na huyo ndiye Afande wa kwanza kumfahamu, Afande Mbise.
Yeye ndiye aliyepewa jukumu la
Ilikuwa jioni, baada ya kukabidhiwa sehemu ya kulala na kula chakula cha usiku, Matron alitupeleka moja kwa moja hadi "uwanja wa damu", mbele alisimama yule kijana, Afande Mbise akiimbisha 'chenja'(nyimbo) mbalimbali za jeshi.
Moyoni nilikuwa na hofu
Na kwa sauti ya ukakamavu aliimba, "Lelelele amba, lelelele amba. Amba nalia, Amba lelelele amba. Amba nipo depo, amba lelelele amba."
Alikuwa na nyimbo zake alizopenda kwa mfuatano uleule.
Akimaliza "Amba", alifuata, "Aidama yoyoyoo"
Alikuwa mkali, wengi tulimuogopa.
Wiki zilikatika, tukiwa kwenye kombania zetu, hadi siku maafande wa kombania walipobadilishwa akaletwa Dcoy
Alitupa kazi kweli kweli. Madoso kama kawaida.
Naikumbuka siku ile, tumekunja ngumi, pushups za uganda juu, kwa dakika nyingi na hakika nilikuwa nimefika mwisho.
Mikono ilitetemeka, jasho jembamba lilitiririka usoni na kulowesha mchanga
Nikajitahidi lakini mwili ulikuwa umeshagoma, nikajiachia kama mzigo chini.
"Unakunja ngumi au nikubadilishie zoezi", akaniuliza.
Nikafikiria naweza kukubali kubadilishiwa zoezi halafu likawa gumu zaidi.
Kwa uoga nikasema, "nibadilishie zoezi afande."
Akauliza, "una uhakika?"
Nikasema, "ndio Afande"
Akasema, "haya nenda platuni namba 3 kaweke chenja ya morali"
Hilo likawa ndo
Nikamshukuru sana kimoyomoyo siku ile kwasababu kwakweli aliniokoa.
Siku zikayoyoma, tukamaliza kozi.
Siku ya kuondoka, nikaonana naye. Nikamkushukuru kwa miezi mitatu ya kujifunza mengi.
Sikuonana naye tena.
Tukawasiliana mara kwa mara kwenye whatsapp group, alikuwa
Mambo yalikuwa yanamuendea vema, alikuwa anajiendeleza kikazi.
Ilikuwa 2016, siku kama ya leo, SABA SABA, nikapokea taarifa kutoka kwa Afande Matron mmoja ameandika, "Rest In Piece Mbise"
Nilipouliza, nikaambiwa alipata ajali.
Tulisikitika sana. Mbise hakuwa
Sikuamini kwasababu nilitoka kuwasiliana naye masaa machache yaliyopita, akinieleza namna ya kujiunga jeshi na nafasi mbalimbali, wakati huo bado nina moto wa kurudi kulisaka "BakaBaka"
Hatukuwa naye tena.
Nyota imezimika.
Huyu alitulea tangu tukiwa wazalendo siku ya kwanza hadi siku tumemaliza kozi.
Aliacha alama maishani mwetu hakika.
"Alazwe Pema Peponi Kamanda", mashairi haya nayaelekeza kwa Marehemu Mbise.
Aamuaye ndo Mola, hawezi kukosea.
Lala Salama.
Tutakukumbuka Daima. @KachiwilePaul
#DaktariMwandishi