#DaktariMwandishi
🔅Unapataje kinga mwili ya asili?
Unapoumwa, mwili wako unatengeneza protini ziitwazo "antibodies" ambazo zinapigana na vimelea vya magonjwa,
Mwili una njia nyingi nyingine za kushambulia vimelea, na kwa pamoja zinawezesha kuushinda ugonjwa.
🔅COVID19 na HERD IMMUNITY
Wakati huu wanasayansi wanahaha kupata chanjo ya COVID19, hivyo kupata Kinga jamii kwa kutumia chanjo si
Wanaodhani tutumia KINGA JAMII inamaanisha tutegemee KINGA MWILI YA ASILI kwa sasa.
🔅Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa ili jamii ipate Kinga jamii kwa kupitia kinga mwili ya asili, inabidi 70-90% ya watu waugue ugonjwa huu. Kati yao 10-20% watapata madhara
🔅Je, nani anaweza kujenga kinga mwili ya asili dhidi ya COVID19?
Yeyote, lakini watu wenye kinga dhaifu wapo kwenye hatari kubwa ya kupata madhara makali ukilinganisha na wale wenye kinga ya kutosha wanapoambukizwa COVID19.
KINGA (IMMUNITY) ya mwili inajengwa na vitu vingi na kwa muda mrefu. Daktari mmoja alisema "Kinga mwili sio nguvu za kiume kuwa utakunywa kidonge iongezeke papo hapo"
Fahamu, kwasababu hupati magonjwa mara kwa mara haimaanishi
Nchi zinazoendelea zina vitu vifuatavyo ambavyo vinatishia kinga mwilini:
📌UTAPIAMLO - Hili si tatizo kwa watoto tu, hata kwa watu wazima. Kuanzia kwashakoo hadi uzito uliopitiliza, vyote vinakuweka hatarini kuwa na kinga dhaifu.
Hili ni tatizo kubwa.
📌UNYWAJI POMBE ULIOPITILIZA - Kiasi, aina na mlo unaoambatana na pombe vinaamua kama mwili wako utamaintain kinga au la.
📌SARATANI & KISUKARI- Ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa kwenye nchi zinazoendelea kama vile Saratani na Kisukari inashusha kinga
📌UTAMADUNI WA KUFUATILIA AFYA ZETU - Nchi zinazoendelea hazina utaamduni huu, hivyo uwezekano wa kuwa na watu wengi wenye magonjwa kama Saratani, Kisukari, UKIMWI ambayo yaanchangia kudhoofisha kinga lakini hawafahamu ni mkubwa.
📌Watu tofauti wanatengeneza kiasi tofauti cha antibodies
📌Haijulikani kiasi gani cha antibodies kinahitajika kujenga kinga mwili imara kiasi cha kutokupata maambukizi ya COVID19 tena.
📌Vipimo vya antibodies vinavyotumika ni tofauti
📌USUGU WA VIMELEA (ANTIMICROBIAL RESISTANCE)- Tatizo kubwa duniani ambalo
Infikirisha.
Unapoamua kutumia kinga jamii kwa kutegemea kinga mwili ya asili, inamaanisha wapo watakaofariki, wanaweza kuwa wengi, sana.
📌VIFAA VYA KUJILINDA KWA WAFANYAKAZI WA AFYA
📌Nawa mikono
📌Epuka mikusanyiko
📌Vaa barakoa
📌Safisha nyuso (surfaces) za vitu
📌Elimu kwa jamii
📌Uonapo dalili, toa taarifa mamlaka husika
📌Usisambaze taarifa POTOFU
NAWASILISHA!
#DaktariMwandishi 👣