My Authors
Read all threads
#Covid_19: HOFU Vs TAHADHARI. #UZI

Kuna mstari mwembamba kati ya kutia hofu na kuhabarisha, kutia moyo na kutoa tumaini la uongo.
Nayakumbuka maneno ya mwalimu wangu, "Usimwambie mtu atapona kama unajua hatapona wala hatapona kama kuna uwezekano akapona"
Mtanzania, Vuta Pumzi.😷
Siku chache zilizopita, niliandika #Uzi mrefu kuelezea kuhusu #coronavirus, naamini umewasaidia.
Juzi, Mh. waziri alipotangaza tuna mgonjwa, mlango wa waandishi wa habari na wasemaji wa sekta ya Afya ukafunguka. Kila mtu na lake. Nimejitahidi sana kurekebisha taarifa potofu. KAZI
HALI IPOJE DUNIANI? Kwa mujibu wa @WHO hadi tarehe 16/03/2020, kulikuwa na maambukizi jumla 167,511 na vifo 6,606 tangu mlipuko ulipoanza.
Huku @WHOAFRO wakiripoti kuwa hadi sasa idadi ya watu walioambukizwa barani Afrika imefikia 418.
Idadi ya waliopona inakadiriwa kuwa 80,000
Kutokana na takwimu hizo, inaonyesha wazi wengi wanapona na ni jambo jema.
Wataalamu wa takwimu wameonyesha kuwa kati ya 3-4% ya wanaoambukizwa ndio hufariki, wengi wao wakiwa na kingamwili dhaifu na magonjwa mengine.
Wengi wanajiuliza, kama ndivyo, kwanini tunasisitizwa yote
haya?
Unapotazama watu kwa jicho la NAMBA, ni rahisi sana kuona "mbona wanayakuza tu"
Lakini unapotazama kwa jicho la UTU, utaelewa kwanini tunahimiza kuchukua tahadhari.
Wengi wanasema wao wana kingamwili ngangari, hata wakipata watapona, wanasahau kuwa wakipata wataambukiza
wengine ambao kingamwili yao si nzuri na kuweza kuwasababishia vifo au kuumwa muda mrefu.

Katika janga hili, nimejifunza kitu.
Mwanadamu ana U-MIMI sana.
Tutakapoamua kuacha U-Mimi na kufuata U-Sisi, tutaona umuhimu wa kuchukua tahadhari.

Watu 6,000 kati ya 160,000 wanaonekana
wachache sana kwasababu tunaangalia NAMBA.
Tukiangalia kwa jicho la tatu:
-Tumepoteza nguvukazi ya watu 6,000
-Familia ngapi zimebaki yatima au wajane?
-Watu hawa 6,000 walikuwa na ndugu, jamaa na marafiki.

Hapo utagundua kuwa tunahitaji kuchukua TAHADHARI. Kuwalinda waliopo
kwenye hatari zaidi.

Lakini pia tukumbuke kuwa sisi ni nchi inayoendelea. Tahadhari zetu hazina budi kuwa kali zaidi kwasababu, mfumo wetu wa afya si imara kama nchi zilizoendelea, tuna muingiliano mkubwa wa watu hivyo uwezekano wa maambukizi ni mkubwa.
Jana Mh. Waziri alisema ukweli, tunachukua tahadhari kwasababu ukitokea mlipuko mkubwa, hatuna uwezo wa kuukabili.
Ni ukweli ambao wengi tunaufahamu lakini hatutaki kuukubali.
Kauli ya Mh. haikuwa ya kutia hofu, ilikuwa kuonyesha umma jinsi ilivyo muhimu kufuata tahadhari hizi.
Dhana nyingi potofu zinazosambazwa, m.f waafrika hatuwezi kuumwa/kufariki kwa ugonjwa huu, au Corona ni "mafua kama mafua mengine"
Ni namna ya watu kujipa moyo katika wakati ambao wana hofu, bila kufahamu kuwa usambazaji wa taarifa hizi unatuweka kwenye hatari ya mlipuko.
Naelewa, wengi tunaambiana "MSIPANIKI jamani", ni rahisi kusema ingawa tunafahamu ni asili ya mwanadamu kupata hofu anaposikia taarifa ya janga kama hili.

Mh. Waziri Mkuu ametangaza kusitishwa kwa mikusanyiko mingi, shule zimefungwa. Tuyatendee kazi haya.
Tusipuuzie.
Viongozi wa dini, huu ndio wakati wenu kuwahimiza waumini wenu kutumia maarifa.
Badala ya kuwaaminisha kuwa ugonjwa huu haupo au vinginevyo.
Tafadhalini, kuweni wa mfano. Fungeni makanisa na misikiti. Elimisheni waumini wenu namna ya kuchukua tahadhari.
Wakati huu, mnahitajika.
Wengi wamekuwa na mawazo tofauti kuhusu kufungwa kwa sehemu za dini. Wakati huu ambapo hofu imewajaa wanataka kukimbilia huko kusema na Mungu.
Lakini tujifunze kitu hapa,
Malaysia juzi walirekodi wagonjwa wapta 41 kati yao 37 maambukizi yaliyotokea msikitini.
Seoul nao kari ya
maambukizi 74, 40 yaliyotokea kanisa mojawapo.
Hii inatuonyesha wazi kwanini kuna umuhimu wa kuacha mikusanyiko hii.
Imani zetu ni thabiti na Mungu hutusikia popote tulipo.
Viongozi wa dini wanaweza kuhubiri kupitia mtandao.

Mikusanyiko itaongeza maambukizi haraka, TUIEPUKE.
Nimepokea ujumbe na simu kutoka kwa familia, ndugu na marafiki.
Mama yangu ana hofu juu yangu.
Naamini ndivyo ilivyo kwa watu wengi.
Cha muhimu ni kuwatia moyo na kuwakumbusha kuchukua tahadhari.

WITO KWA WADAU WA SEKTA YA AFYA: Jamii inatusikiliza sasa kuliko wakati mwingine
wowote. Unachokisema, andika, shirikisha na unachokifanya kinachangia namna ambavyo wat uwanaokuzunguka wanachukulia jambo hili.
🔸Tusichoke kuelimisha umma
🔸Tusichoke kukemea taarifa potofu POPOTE tunapoziona
🔸Tuwe mfano kwa jamii katika kuchukua tahadhari
🔸Tuwe na utayari
Watanzania, huu ni wakati wa umoja.
Wakati wa kuonyesha utu.
Wakati wa kutumia maarifa.
Wakati wa KUWASIKILIZA WATAALAMU TU.
Taarifa SAHIHI zinapatikana @WHO @WHO_Tanzania @UmojaWaMataifa @CDCgov @wizara_afyatz @umwalimu @DocFaustine na vyombo vya habari VINAVYOAMINIKA.
Kwasababu mtu ana followers wengi, isiwe sababu ya wewe kuamini alichokiandika.
Kwasababu imetumwa na mtu fulani kwenye group whatsapp au imewekwa status, isiwe sababu ya wewe kuamini.
Vyombo vya habari vinafanya kazi kubwa ya kuhabarisha kila wakati, SIKILIZA.
Kuna namba zilizotolewa maalumu kutoa taarifa, zinaonekana hapo pichani, NI BURE.

Lakini pia, Mh. Waziri Mkuu ametaja maeneo yaliyotengwa maalumu kwa ajili ya wagonjwa watakaogundulika kuwa na ugonjwa huu.

Mtanzania, vuta pumzi ndani, shusha pumzi. USIOGOPE!
Ukweli ni kwamba, madhara ya gonjwa hili ni makubwa si kwa vifo au maambukizi bali kiuchumi, uzalishaji mali n.k
Ninafurahi kuona sehemu nyingi za biashara, taasisi mbalimbali zinafanya juu chini kuhakikisha watu wananawa mikono na kuchukua tahadhari.
Huo ndio umoja tunaoutaka!
Katika #Uzi uliopita niliwaambia, Mtanzania, upuka haya MATATU
🔸HOFU
🔸PROPAGANDA
🔸SIASA
Utayasikia mengi. Utayaona mengi. Utaaminishwa mengi.
Chagua kusikiliza wahusika wanaotakiwa kukupa taarifa SAHIHI.
UZUSHI KATAA!
#WeShallOvercome
#CoronavirusOutbreak
#DaktariMwandishi 👣
@threadreaderapp please unroll
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Kuduishe Kisowile

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!