"PIGA PICHA..☁️🙄"

Piga picha uko bar na machizi wako wawili mnakula stori za hapa na pale..ni kama saa tatu,tatu na nusu hivi..bar haijajaa vizuri ila ugiza flani na mziki wa kueleweka ndo unakufanya uendelee kuagiza moja moja...
Piga picha kwamba Ghafla unaona kwa mbali kiwiliwili cha mtu kinakuja uelekeo wa bar..kila kinaposogea ndo unazidi kukiona vizuri..unaanza kuona nywele zilizofungwa kwa style yao inaitwa ponytail ya juu..unywele uliomwagika mpaka matakoni kwa jinsi unavyojitokeza pembeni ya mwili
Mwendo wake unakuvutia kidgo..so unaamua kukazia jicho kuona je ni mpita njia?na ni nani?maana ww ni mtoto wa hiko kitaa..
Mara anapinda kuingia bar..hapo ndo machizi nao wanapomwona..kama kawaida kuna miguno ya wana inatawala na huku macho yenu yakiulizana "umeona kitu kile??"
Anaingia moja kwa moja counter..hakai..anasimama..
Anaagiza lite moja..inafunguliwa..haicheleweshi..anaipeleka mdomoni na kuanza kuidigida..
Anaishusha ipo nusu...ndipo ana survey..unabahatika kuona sura vizuri..akili inawaza "kazuri zuri,kanalika haka"
Kati ya machizi waliopo mmoja ni bro ako..anakuangalia usoni akicheki jinsi unavyo piga hesabu zako maana anakujua..
"Dogo,amua haraka either uende au ntaenda mimi"..
Anakuweka njia panda hadi mkojo unakubana..ukiangalia counter,dogo kanyanyua la pili anamalizia..
Ananyanyuka..
Machizi wanakuangalia kama "oyaa fanya fasta fara we"..
Manzi analipia na kuanza kuondoka kurudi alipotokea...
"Liwalo na liwe" unaanza mfukuzia kwa step za haraka kidgo..
Unatembea huku unawaza mbona amekaa kidgo na kuondoka..labda malaya tu alikua anasaka akaona hamna ishu
Ila mbona alifika pale kama mtu mwenye stress au kiu kama kaagiza ki apple punch na kukipiga na kuondoka zake..unashindwa muelewa..ila ntajua nikifika..
Unapokaribia unamwita "sister samahan"..mara ya pili anageuka ila hasimami..unaamua kuongeza mwendo na kumfikia
"Mambo,mbona umekuja na kuondoka mapema hvyo,kuna mtu ulikua unamsubiri?"
Anakuangalia kama anakushangaa "No,nilikua nna ham na bia moja tu basi"
Huku akiondoka unaona tonge linaniponyoka hili ntarudje kule mikono mitupu..
"Unaonekana una stress maana sio kwa ulivyoipiga ile bia"
Unaona kama anataka kusmile.."kisa ile bia ndo umeona nna stress..hata mi nipo sawa tu"
"Unaenda wap sasa kwani..tunaweza kurudi tuongeze mbili tatu,ya pili itatuliza kiu vzuri maana hata mi najuaga moja haitoshi"
Manzi anakwambia alikua amekuja check kuna birthday ya frnd ake
Ila ameambiwa wamebadilisha kiwanja so ndo anataka kwenda..unaamua ku offer kumpeleka maana ni mwendo kidgo..unamwomba akusubiri ukachukue gari mwende..anasita sita ila kama kawaida anakubali..unarud unakimbia kuomba gari la bro..bro hakufelishi si mafuta utaweka..
Unamfata mtoto..mnapelekana hadi kiwanja kingine na unajua jina lake Latipha..mnafika unakuta kweli kib'day kina happen..mnapoingia mzuka wa rafki zake unampokea kwa shangwe kama alikua hana mpango wa kuja..huku wakiulizana kwa macho "whos the guy,mbona hatumjui"
Anaonekana mnywaji kwa gambe linavyotembezwa..umetengwa kimtndo japo unahusishwa kwenye vijipart vya hapa na pale..wanapolewa kidgo unapigwa touch za hapa na pale na waliokuwepo maana pia umecover bili kadhaa..kama saa tisa na nusu watu wanaamua kuhama kiwanja
Latipha na mmoja wa manzi waliokuwepo uliomsikia kwa jina la Natasha wanaamua kuondoka na wewe..japo wote lengo lao ni kwenda kulala maana hali zao sio poa..unaamua kuwarudsha huku unajilaumu..latty yupo mbele mwenzake nyuma wanabwabwaja na kuchekacheka..vibe kubwa kwao
Laty anachukua sim yako anakwambia utoe lock..anaandika namba yake huku anakwambia ntafute kesho tuongee vzuri "niko wasted sasa hivi..nisogeze tu home plz" anakuelekeza hadi anapoishi..anashuka na kufungua mlango wa nyuma na kujarbu kumvuta mwenzake ambae amepitiwa flani
Anafanikiwa..
Unashangaa mlango wa mbele umefunguliwa na natasha anabwagwa mbele..
"Naomba umfikishe kwao plz atakuelekeza..home kwetu noma"
Huku akimpiga piga mashavu kama kumuamsha huku akimwambia utamwelekeza.
Inakuchekesha kidgo kuona mlevi na mlevi mwenzake wanapeana support
Unawaza "atleast kashanipa namba haina shida"
Latipha anakuelekeza kidgo huelew vizur ila unaona si manzi yupo tukifika atanielekeza vzur "mlevi hapotei kwao"
Safari inaanza..unapofika maeneo uliyoelekezwa unaanza kumuamsha..kama kawaida watu wakilewa wanavyosumbua..laty hapatkan
Hatimae Anashtuka..anakuangalia kwa jicho legevu huku anatoa nywele za wigi zilizotapakaa usoni.."nielekeze kwenu nkupeleke.."
Anakuangalia af anasmile..kwa sauti ya kilevi anakwambia "Nikwambie kitu.....twende kwako tukalale sitamwambia latipha,cant go home niko hivi wataniua"
Anakushika mkono..unachek mwili wake ulivyonawiri..mapaja yanavyoita..jinsi anavyokuangalia..unapatwa na joto..hamu iliyopotea inarud kwa nguvu. akili inacheza..home huwez mpeleka so destination lodge moja karibu na kitaa..unaona leo sitoki kapa..hela zilitumika zitalipiwa na mtu
Mnafika unalipia chumba,unampandsha hadi ghorofa ya tatu kwa tabu sana..mpka kumlaza kitandan jasho linakutoka kichwan pombe inaanza kuisha..mtoto amejaa sawia.
Unapombwaga na yeye ndo anaulaza kimoko..na kwa jinsi ulivyochoka unaona acha niulaze tu na mimi ntamalizana nae asubuh
Unachek saa..saa 4:37..miguu chini..unapitiwa.
Unashtuka kengele ya breakfast inavyopigwa..saa 8:01..unamwangalia manzi kajitapikia..nguo..mikononi hadi nywele.."duh,pombe kama hamziwezi msiwe mnazinywa"

Unashtuka unapoona kitu...Macho yalivyomtoka..unashikwa na ganzi
Shughuli ya kumwamsha inaanza..unahisi kama mavi yanataka kukutoka,tumbo linauma,jasho linakutoka balaa..kila unachojaribu hamna kitu..unawaza apa nisiharibu sana hali..unapiga mapokezi kuomba msaada..unapiga kwa bro na marafiki wawili..huwezi ata elezea zaidi ya kuwaambia waje
Kwakweli hakuna msaada mkubwa unaotolewa zaidi ya polisi kupigiwa..unaamua kukaa chini ukutani..huamini kama ni kweli..bro na bestfrnd wako wanafika unajaribu kuwaelezea huku chozi linakudondoka..ndo faraja iliyobaki..lisaa linapita..askari wanaingia watu wanatolewa unabaki wewe
Wachache wanahojiwa na latipha anatafutwa,process zinazingatiwa mpaka pale unaposikia
"Kijana..nyanyuka"
Unageuzwa huku askari akisema maneno ambayo hata husikii kwa mawazo zaidi ya pingu zinazobana mikono yako..
Chozi linakudondoka huku ukivuta pumzi ndefu
"MUNGU NISAIDIE"
PIGA PICHA kisha ujue
"LIKIJA HALIGONGI HODI"

Ndo kilichomsibu mwanangu Amani
Atlast yuko huru..

#fanani ✍️ hapa

RT please 🙏@MarekaMalili @McinikaWaLamar
@gracemella95 @chibelube @YourFrenchFry @max_zitatu @timothynashon @Eric_Bernard94 @Kiganyi_ @mpambazi @sonnino123

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Urs truly✍️

Urs truly✍️ Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @crazyTanzanian

19 Mar
"ZINGATIA..☝️"
Retweet kwanza

Ni saa nne za usiku na mvua inanyesha tofauti na ilivyozoeleka ila naanza kuona mataa ya mji wa Dodoma..safari bado na njaa inauma..naona nikifika centre nisimame kidgo..stop ya kula ni Chako ni Chako kuna kuku wa kuchoma..nakula na kubeba nyingne..
Huwezi jua njian kuna mengi chakula muhimu..nakiwasha tena..napoanza kuitafuta Moro njiani malori mengi na ni usiku hvyo naenda kwa mwendo wa kawaida..nsije nkapunguza miaka ya kuishi..kamziki kwa mbali huku nasikia wiper zikifanya kazi kwa bidii ili tu nione uelekeo.
Baada ya kilomita 1..ndipo namwona
Koti kubwa likificha sehemu kubwa ya mwili wake zaid ya miguu iliyofunikwa na jeans nyeusi na raba..kanyoosha mkono kwa bidii kweli..
Nampita..ila baada ya kuona kuna basi dogo jingne pembeni na abiria ndani limesimama nikasimama
Read 20 tweets
20 Nov 20
"SIRI YANGU🤫"

Napiga pafu moja kutoka kwenye glass...mkono unanipiga begani,tuji bia tunanimwagikia kidogo kwa tshirt,,naangalia nyuma kuangalia ni nani huyu fa**..
Nakutana na cheko moja la kihuni..kumbe Jose,
"Mjinga umemwaga bia yangu"
Ananicheki kwa dharau..anaita muhudumu ananiongezea mbili...
Inabidi nimuulize "hii jeuri imeanza lini kapuku wewe..😅

Anantizama af sura inabadilika.."kuna hela nilikua nadunduliza nimtoe mtoto wa mtu ila acha tuinywee tu bia..atleast siku niseme na mimi nshawahi kukutoa"
Nakaa nae kwa masaa kadhaa..kwakua mwana anafanya kazi ya boda naona kabisa narudi gheto vizuri kabisa...
Muda unayoyoma...nakuja cheki saa saba na nusu..nanyanyuka huku nikiwaambia wana wengine "kesho nayo siku"
Napigwa vijembe kadhaa pale..sijali namshtua mwana anisogeze ghetto
Read 18 tweets
23 Oct 20
"NILILAMBA JOKERI🃏.."

Nipo kwenye gari nna hasira flani..nafungua whatsapp natafuta convo yetu mwanzoni kabsa..naandika "mnazingua"
Huyu ni rafiki angu wa kike,Ney, tumepanga kwenda premier ya movie flani ilikua inatoka af tuna ka dk 10 ianze,ameomba aje na rafiki zake wawili
Mi nipo na mchizi,ye ndo kamaindi mbaya. Kanimaindi mimi pamoja na huyo rafiki angu.."kubabeki,tunaenda kuanza movie nusu..si bora tukanywe bia tujue moja" 🤔nkawaza sio wazo baya ujue..
Mara nasikia milango inafunguliwa siangalii hata nyuma nawasha gari..
Nasikia sauti ya ney "kelvin,we are sorry" naongeza sauti ya mziki..
Mchzi anageuza shingo anawasalimu..naona kashalegea kuona vimwana,anaanza kuwapigisha stori pale
Njia nzima nipo kimya..hadi tunafika.
Wanashuka na mimi kma dereva nachek kma vitu vipo sawa kabla sijashuka
Read 17 tweets
15 Aug 20
"THUBUTUU...🤧"

Sijui ilikuwaje hadi nkasahau kuandika kuhusu hiki kisa..🤭
Nadhani kwasababu mchizi hakua mtu wangu wa karibu sana..ilikua ni kuonana kwenye vigenge vya stori na kitaa.

Ila siku tulijikuta wawili tu kwenye kota za tanesco anapokaa,chobingo moja yetu pendwa..
Mchizi aliitwa Saleh..
Tulisalimiana kiwana tukiulizana mishe zinaendaje na vijistori vya hapa na pale vya kupoteza muda.
Mchizi alitoa sigara mbili huku akiniuliza kama natumia..nilimjibu situmii hvyo aliiwasha yake akavuta pafu mbili kubwa..alitoa moshi nje af akabaki kaduwaa
Ilibidi nimuite mara mbili,aliposhtuka ilibidi ajicheke..nikamuuliza vipi asee mbona umeniacha peke yangu..
Nakumbuka alinambia
"aahh kmmk,nna kipengele kimoja hicho na sijui itakuaje" nkamwambia "nipange"
Alisita kidogo akaangalia sigara yake kidgo kisha akaanza kunipa stori
Read 26 tweets
27 Jun 20
"KARMA..🎭"

🌡Kama huna kifua basi usisome uzi huu haukufai maana mi natoa visa vya ukweli kama ifuatavyo...👇

Nipo na mwana ananionesha picha af ananiuliza "unaikumbuka hii"..naichek af nacheka ni picha ya kitambo kidgo,tukiwepo sisi na wasichana watatu..mmoja wao akiwa VERO
Vero mi nilimjua kipindi anatoka na mchizi wangu huyo..baada ya kukutana nae viwanja..tulikula sana bata za hapa na pale na huyu manzi,kipindi hicho anakaa mitaa ya sabasaba na wenzake.. walikua wamoto..kila weekend lazima niulizwe "shem leo wap!!nna rafki yangu nataka nikususie"
Kiukweli mchizi wangu alikua sio mtuliaji so wana tulikua tunajua saa yoyote kinaweza nuka..ila cha kushangaza haikua hvyo kwa muda mrefu..nadhani style za maisha ziliendana kiasi kwamba ilikua haiboi..
Basi hapo kati Vee kama nilivyokua namwita akapata mimba ya mchizi
Read 18 tweets
7 May 20
"LAANA...."🧞‍♂️

Wiki moja baada ya kuanza darasa la kwanza kutokana na umbo langu kua dogo kidgo kuliko wengne ilinipa ugumu maana nilishindiliwa uonevu wa kila namna..ila siku,mmoja wa wanafunzi alinikingia kifua..na si mwingine bali ni "MUDI" kama wengi tufupishavyo, jembe langu
Sikuwah kuonewa kuanzia siku hiyo na ndipo nilipojifunza ubabe..sikuwah kumwambiaga ila alikua kama kaka angu japo tulikua umri sawa ila kwa mwili wake na udogo wangu tofauti ilikua kubwa,alikua ndo rafiki wangu wa kwanza kishule shule. Alinifunza kujihami,kujilinda na ni yeye
alinifunza utukutu..asee shule nzma ilikua inamtambua. Kwa kila walimu walichomsema basi na mm nilihusika ila kwakua wengi hawakuamini mi kuhusika ivo mudi alichkua adhabu zote na hakuwah kunitaja. Ila nami nilihakikisha hafeli mitihani kwa njia yoyote na hakuwahi kuniangusha
Read 22 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!