"YOU ARE UNDER ARREST"

#Uzi

📌Je, wajua Leo ilikuwa siku ambayo sheria inayomlinda mhumiwa [Miranda rights/Warnings] anapokamatwa na vyombo ulinzi ilipitishwa huko marekani?

💨YES it's Miranda Vs Arizona case

📌 Historia yake

📌 Chanzo chake

📌Maamuzi ya kihistoria.

👇👇 ImageImage
Mnamo Juni 13, 1966 Mahakama Kuu ya Juu (Supreme Court) nchini Marekani ilitoa uamuzi wa kihistoria juu ya taratib za uendeshaji kesi za jinai mahakamani.Uamuzi huo ulitokana na kesi ya Miranda Vs Arizona kwamba watuhumiwa wa kesi wanazo haki zao kabla ya kuhojiwa wawapo kizuizin Image
Nadhani ulishawahi kusikia maneno haya

1. Una haki ya kukaa kimya.

2. Chochote unachosema kinaweza, na kitatumika, kama ushahidi mahakamani.

3. Una haki ya kuwa na wakili.

4. Ikiwa hauwezi kumudu gharama za wakili mahakama, itamteua mmoja kusimamia kesi zako

Tuendelee 👇 Image
Hapa nchini sheria inayoratibu uendeshaji wa mashauri ya makosa ya jinai yanayohusu watu wazima iko chini ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 1985 kwenye sura ya 20. Lkn zipo sheria nyingine mbalimbali ambazo zinahusiana na uendeshaji wa mashauri ya makosa ya jinai.
Halikadhalika, ili kukamilisha utaratibu wa uendeshaji wa mashauri ya jinai kuna Sheria ya Ushahidi ya mwaka 1967, sura namba 6, inayoelekeza aina ya ushahidi, taratibu za kutoa ushahidi. Lengo langu sio hili bali ya kukuletea chanzo cha sheria hizi na taratibu za uendeshaji kesi Image
#Chanzo ni Miranda v. Arizona case, 384 U.S. 436 (1966)

Miranda vs. Arizona case ilikuwa kesi kubwa iliyofuatiliwa na kusisimua ulimwengu wote kutoka ktk Mahakama Kuu ya Jimbo la Arizona nchini Marekani.
RT. @Mangiwakwanza @biturojr @adamlutta @IAMartin_ @Gaspinho15 @Nkololotz Image
Kesi hii ilihusisha tuhuma za binti mmoja kubakwa na baadae ikaonekana polisi wa mjini Arizona wakiwa wamemfikisha kijana kwamba ndiye alihusika na jinai ile na kisha akahukumiwa kutokana na taarifa iliyolewa na polisi kwamba alikiri kufanya tukio lile.
@CarolNdosi @jtemba321 Image
HISTORIA

Mnamo Machi 2, mwaka 1963 katika mitaa ya Phoenix, huko Arizona nchini Marekani. Ikiwa ni mida ya usiku binti mmoja Patricia McGee (sio jina lake halisi) mwenye umri wa miaka 18 akiwa barabarani kuelekea nyumbani akitokea kwenye ukumbi wa sinema alikokuwa akifanya kazi Image
Ghafla alitokea mtu aliyekuwa kwenye gari na kumkamata kwa nguvu akamfunga mikono nyuma na kumlazimisha alale kwenye kiti cha nyuma.
Baada ya kuendesha kwa takribani dakika 20, alilisimamisha gari pembezoni mwa barabara mbali kidogo ya jiji na kumbaka. Image
Baada ya kumbaka alimlazimisha ampe pesa zake zote alizokuwa nazo la sivyo angemuua na kisha akamwambia alale tena kwenye kiti cha nyuma, kisha akamrudisha mjini na kumuachia maeneo ya karibu na nyumba kwao.
Binti yule alipofanikiwa kufika nyumbani na alichukua simu akawapigia polisi kuomba msaada, walipofika ndipo aliwaeleza mkasa uliomtokea na kuwaambia muonekano wa kisura, kiumbo wa mtu aliyemfanyia unyama huo na plate namba za gari kisha wakampeleka hospitali kupatiwa matibabu. Image
Polisi waliendelea na zoezi la kumtafuta mhalifu na siku chache baada ya tukio kutokea Patricia na binamu yake walikwenda polisi na kutoa taarifa ya kuona gari moja linalofanana na lile likiwa linapita mara nyingi ktk kituo cha mabasi ambapo alitekwa. Image
Polisi walifuatilia gari lile na kufahamu lilikuwa likimilikiwa na mwanamke aitwaye Twila Hoffman (29) aliyekuwa akiishi Mesa huko Arizona. Hoffman alikuwa ni mpenzi wa Miranda na wote walikuwa wakiishi pamoja. Image
Wakapata mkanganyiko wa kuendelea kutafuta mhalifu baada ya kujua mmiliki wa gari ni jinsi ya kike. Lakini hawakuishia hapo waliamua kwenda kwake Hoffman ili kumkamata na kwamba huenda anafahamu aliyefanya unyama ule kwa kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alitumia gari lake.
mnamo Machi 13 asbh Polisi walimbishia mlango Hoffman, akafungua na wakamweleza kilichowapeleka nyumban kwake. Baada ya kusikia polisi wapo ndani Ernesto Miranda kijana mwenye umri wa 24 na mwanafunzi wa Sekondari A-level kwa mujibu wa maelezo ya polisi akajitokeza kuzungumza nao Image
Miranda alifanya vile ili kunusuru penzi lake kwani alijua yeye ndiye anatafutwa akawaomba waondoke naye wakazungumzie kituoni. Kiufupi Miranda akakamatwa na polisi na moja kwa moja kituoni kwa tuhuma za uhalifu na jinai ya utekaji nyara, kumbaka na kumuibia binti Patricia. Image
CHUMBA CHA MAHOJIANO

Alihojiwa na wapelelezi maswali mengi kwa muda wa masaa mawili bila kuwepo Wakili wake, ambapo baadae alikiri kutenda uhalifu huo. Baada ya hapo wapelelezi walimleta mwathiriwa ndani ya chumba polisi mmoja wao alimuuliza Miranda "huyu ndiye mtu aliyembaka?" Image
Miranda alimwangalia na kusema "Ndio, msichana alikuwa huyo" akakiri na kisha kusaini kwa maandishi.

Karatasi ile ilisema "haya ni maelezo yangu binafsi na nakiri nimeyatoa kwa hiari na haki zangu nazielewa,hivyo maelezo haya yatumike mahakamani kama ushahidi na sio vinginevyo"
Maelezo yale yalichukuliwa kama ushahidi mahakamani ingawa hakukuwa na haki maalum zilizoorodheshwa kwenye karatasi ile kama yanavyosema.Akasomewa mashataka mahakamani na alihukumiwa kwa uhalifu huo na Mahakama ya Arizona kutumikia kifungo cha miaka 20 mpk 30 jela.
@rollymsouth Image
Baadaye, Wakili wake Alvin Moore alihisi kwamba kukiri kwake Miranda hakukuwa na ukweli kutokana na ukweli kwamba hakuwa anafahamu haki yake ya kimsingi ya kuwa na wakili atakaye mwakilisha na aidha kwamba maneno yake ya awali yangeweza kutumika kama ushahidi wa maneno dhidi yake Image
Baada ya miezi 6 Wakili Alvin aliamua kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Jimbo la Arizona kwamba hakukubaliana kuwa kukiri kwa maandishi ya mteja wake na kuongeza kuwa huenda maelezo yalitokana na kulazimishwa, hivyo akaisisitiza mahakama ktk uamuzi ilioutoa kuangalia hilo. Image
Rufaa ya kesi hii katika Mahakama kuu ndiyo ilibadilisha kabisa utaratibu wa uendeshaji wa kesi za jinai nchini Marekani nadhani hata ktk nchi nyingi duniani.

Katika rufaa Wakili Alvin alihoji Mahakama maswali yafuatayo.

"Je! Taarifa yake [Miranda] ilitolewa kwa hiari?" na Image
Je, "Alipewa kinga zote za haki zake zinazotolewa na Katiba ya Marekani kwa kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji kesi mahakamani?"

Rufaa yake ilijibiwa na Mahakama Kuu ya Arizona mnamo Aprili 1965 kwamba kukiri kwa Miranda kulikuwa halali na kwamba alikuwa akijua haki zake.
Baada ya uamuzi huo kutolewa ndipo kesi ya Miranda ilianza kuvutia macho watu mbalimbali ikiwemo mawakili wa kimataifa. Kutokana na kuchukua sura mpya ktk Jimbo la Arizona, Robert Corcoran ndipo aliibuka na ACLU (American Civil liberties Union) Umoja wa Uhuru wa Kiraia wa Amerika Image
Wakili Corcoran akaamua kuivalia njuga kesi hii akaenda kwa wakili mwenzie mashuhuri wa kesi John J. Flynn, akatafuta mtaalam mwingine wa sheria na katiba, John P. Frank, wote kwa pamoja kusaidina katika kukata rufaa kwa Mahakama ya Juu kabisa nchini Marekani. @Nkololotz Image
Wakili Frank Katika muhtasari wake kwa niaba ya Miranda, aliandika,

"Siku ni hii leo kutambua umuhimu wa kufanya marekebisho ya sheria sita.

"Marekebisho ya sita ya sheria ya uendeshaji kesi za jinai yanahakikisha haki za washtakiwa wa jinai pamoja na haki ya kuwa na wakili. Image
"Pia katika mfuatano huo Marekebisho ya Tano ya sheria hiyo yanawalinda washtakiwa dhidi ya kulazimishwa kuwa mashahidi wa kesi zao wenyewe.

"Ingawa Miranda alikuwa ameandika taarifa ya kukiri kwake na chini ya taarifa alisema kwamba alikuwa anajua kabisa haki zake za kisheria"
"wakili wake alisema haki hizo hazijafafanuliwa wazi kwake. Hivyo chini ya shinikizo la kukiri akiwa kizuizini, kukiri kwake hakukupaswa kuchukuliwa kuwa alikubali kutenda kosa."
UAMUZI WA KIHISTORIA

Mahakama Kuu, chini ya Jaji Mkuu Earl Warren, ilikubali.Katika uamuzi wa 5-4, Mahakama Kuu ilibadilisha uamuzi wa Mahakama Kuu ya Arizona na kutangaza kwamba kukiri kwa Miranda hakuwezi kutumiwa kama ushahidi katika kesi ya jinai.

Pichani: Jaji Earl Warren Image
Maoni ya Jaji Warren yaliyoandikwa kwenye kurasa 60 pamoja na marejeo, yaliyotolewa Juni 13, mwaka 1966, kufafanua zaidi utaratibu wa polisi ktk utendaji wa shughuli zao na kuhakikisha washtakiwa wanafahamishwa wazi haki zao wanapokuwa wakizuiliwa (chini ya ulinzi) na kuhojiwa. Image
Baadae kesi ya Miranda ilirudishwa kusikilizwa tena mahakamani na kile kiapo alichokiri kutenda jinai kilitupiliwa mbali lakini wakati huu mahakama ilibadilisha mwenendo mzima wa utaratibu wa uendeshaji kesi za jinai na hii ilikuwa ni mahakama zote nchini Marekani.
Kwa mara nyingine kesi iliunguruma mahakamani, lkn kwa bahati mbaya mpenzi wake wa zamani, Twila Hoffman, alitoa ushahidi kwamba kipindi Miranda alipokuwa gerezani alimwambia kuwa alihusika kweli, na mnamo Oktoba 1967, Miranda akahukumiwa tena kuhukumiwa kifungo cha miaka 20-30. Image
Alibahatika kuachiwa kutoka jela kwa msamaha Desemba mwaka 1975 baada ya kukaa jela kwa miaka 8 lakini kuishi kwake hakukuwa kwingi mwezi mmoja tu baadaye mnamo Januari 31, 1976, aliuawa kwa kuchomwa kisu hadi kufa kutokana na ugomvi katika baa moja mitaa ya Phoenix. ImageImage
#Mwisho: kutokana matukio ya kesi hii muhimu Ernesto Miranda, kila mmoja wetu hasa hapa nchini inapaswa atambue kuwa ni lazima afahamishwe haki zake za kimsingi awapo kizuizini (chini ya ulinzi) na anapohojiwa.
#Ahsante
RT is caring
Cc. @franklin_tissa @INFLUENCERjr
@TitoMagoti ImageImage

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with JAPHET MATARRA

JAPHET MATARRA Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Eng_Matarra

27 Jul
FAHAMU MVUMBUZI WA TELEVISION (📺)

#Yes_____&&
#Thread|story🕐
Any sufficiently Advanced Technology is indistinguishable from MAGIC!! Binafsi huwa nasema Technology Is the Great ant💉dote to the Poison of Enthusiasm and Superstition💣
📋Asili ya TV
📋Historia yake
📋Uvumbuzi n.k ImageImage
Televisheni (TV) au Runinga ni kifaa chenye kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.

Neno "Televisheni" linatokana na maneno mawili:
(i)Tele (Kigiriki)-kwa mbali sana na
(ii)Visio (Kilatini)-mwono.

RT @omari_manyama Image
kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza #Television limetoholewa kwa lugha ya Kiswahili "Televisheni".

Ugunduzi wa TV📺 ni kazi iliyofanywa na watu wengi mwishoni mwa karne ya 19.Karne ya 20 Watu mmoja-mmoja na makampuni yalishindana kuunda chombo kilichopiku teknolojia ya awali. ImageImage
Read 37 tweets
8 Sep 20
FAHAMU KUHUSU JAPHET KIRILO

#Uzi

✴️Mtanzania wa Kwanza kuachia Ubunge kisa mashamba ya kahawa 1990's

✴️Akiwa 31yrs alikwenda mpk UN kutetea wakulima
✴️Huyu ndiye alisomesha Wameru wengi akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Gen. SARAKIKYA pamoja na Babaake @CarolNdosi👇
Kwanz kabisa ktk HISTORIA ya Ukombozi wa Tanganyika kutoka kwa Mkoloni Haiwezi KUMTENGA Kirilo Japhet

Tukiwa tunaendelea hapo juu Pichani ni Japhet Kirilo (kulia), akizungumza na mmoja wa viongozi wa serikali ya kikoloni Ralph Bunche..

Tuendeleeee👇👇
Katika historia kuna matukio mbalimbali yaliyofanyika kwenye taifa hili. Leo tumwangalie Kirilo Japhet ambaye alitoka katika Mkoa wa Meru (Arusha ya sasa). Historia tunayoandika hapa leo ni kutokana na andiko la kitafiti la Dk. Simeon Mesaki wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
Read 30 tweets
6 Sep 20
FAHAMU MAANA NA ASILI YA MAJINA YA MAJIMBO YA MAREKANI

#Uzi mfupi.

Marekani ilipata uhuru wake mwaka 1776 na kuwa Jamhuri rasmi mwaka 1789, ina jumla ya majimbo 50 na jimbo la mwisho kujiunga kwenye muungano wa Marekani ni jimbo la Hawaii.
Hawaii iliingizwa kwenye shirikisho rasmi mwaka 1960 baada ya marekebisho ya 15 ya katiba ya nchi hiyo (15th ammendment) na ni zao la sheria mpya iliyoitwa Hawaii Adimision Act, yaliyofanyika mwaka 1959, ili kuingiza jimbo la Hawaii katika shilikisho la muungano wa Marekani.⠀
Hawaii ndio jimbo la mwisho kujiunga na Marekani, na kukamilisha jumla ya majimbo 50 yanayounda Taifa la Marekani/United States of America (USA), ndio maana kwenye Bendera ya Marekani uwakilishwa na nyota 50 kuashiria jumla ya nchi (majimbo) 50 yanayounda umoja wa taifa hilo.
Read 29 tweets
21 Aug 20
VISA VYA MADINI YA TANZANITE

#Thread

✴️Manuel De' Souza Fundi Cherehani na mgunduzi halisi ila hakupewa heshima,

✴️Mzee Ngoma atangazwa mgunduzi ilihali sio

Twende chap...

💨Asili ya Tanzanite
💨Historia yake
💨Visa ktk ugunduzi wake
💨Thamani yake
💨Sababu ya kuitwa hivyo👇
Kila mwaka July 07 huwa ni siku maalum na ukumbusho muhimu sana, na huwa ninafanya sherehe ya Birthday kwa ajili ya Mimi na Baba yangu (sisi wawili tulizaliwa siku hii), Lakini pia siku hii ndio madini ya Tanzanite yaligunduliwa.

Mwaka huu pia nilifanya..

Turudi ktk uzi👇
Tunapozungumzia juu ya vito vya thamani, basi fikra zetu kwa mbali hutupeleka ktk vito vya asili na bila shaka huwezi kukosa kuwazia madini ya Almasi, Emerald, Rubi na Lulu ila kama hufahamu Tanzanite ni moja ya madini ya asili na ghali sana na yenye historia tamu sana.

Twende👇
Read 58 tweets
12 Aug 20
MY LIFE

✴️TRUE STORY

#Thread...!!!👇

Leo nimeamka kukiwa na Baridi sana hapa Jijini Arusha nikakumbuka mbali (nikiwa Hamburg Ujerumani) nikawaza kushare nanyi historia ya maisha yangu itakuwa ktk sehemu Tatu
1. Sehemu I (kuzaliwa)
2. Sehemu II (Masomo)
3. Sehemu III (Maisha) Image
#SEHEMU I

Naitwa Japhet Matarra, nimezaliwa July 07, 1991 kijijini kwetu Machochwe Wilayani Serengeti.

Katika familia yetu mimi ni mtoto wa Tatu kati ya watoto 17 na FIRST BORN kwa Mama Yangu. Nilianza S/Msingi  mwaka 1998 hapo kijijini kwetu na kuhitimu Drs la VII mwaka 2005. Image
Baada ya hapo nilijiunga na masomo  ya sekondari mwaka 2006 ambapo nilichaguliwa kwenda shule ya kata (Machochwe sec) kama ilivyo kawaida vijijini na kayumba schools zetu na kuhitimu O-level mwaka 2009.

Hapa ndipo maisha yangu yalichange nitaelezea mbele ktk sehemu ya III Image
Read 163 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(