#DondooZaDaktari | Ugonjwa wa kisukari unaongezeka kwa kasi hata katika nchi zetu maskini.
✍️Kisukari hutokana na mwili kushindwa kutumia glukosi (sukari)
➡️Kisukari ndio sababu kuu ya:
- Kiharusi
- Upofu
- Ugonjwa wa kudumu wa figo
- Shambulio la moyo
- Watu kukatwa miguu
➡️Kwa mwaka 2019, takribani vifo millioni 1.5 Duniani vilichangiwa moja kwa moja na tatizo hili la kisukari.
➡️ Kuanzia mwaka 2000 hadi 2016, kuna ongezeko la 5% la vifo katika umri mdogo (premature death) kutokana na kisukari.
➡️ Mlo sahihi
➡️ Mazoezi ya Mwili
➡️ Kudhibiti Uzito
➡️ Kuepuka sigara na pombe
Ni baadhi ya mitindo ya maisha inayoweza kusaidia kuzuia kisukari au kupunguza athari ya kisukari aina ya pili.
Kwa wale wenye kisukari tayari.
Kisukari hutibiwa na madhara yake yanaweza kuepukika kwa kuzingatia:
➡️Mlo sahihi
➡️Mazoezi ya mwili
➡️Matumizi sahihi ya dawa za kisukari bila kukosa ➡️Kuzingatia mahudhurio ya kliniki na upimaji bila kukosa.
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
➡️Tatizo la dharura la kiafya ambalo ni moja ya magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo.
➡️Mitindo ya maisha na Lishe ni vitu vinavyochangia wagonjwa wanaopata stroke kuongezeka
➡️Kiharusi huacha ulemavu au kifo
➡️KIHARUSI hutokea pale seli za ubongo 🧠 zinapokufa kutokana kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo hivyo kukosa hewa ya oksijeni na virutubisho.
➡️Kiharusi kikihusisha mshipa wa mkubwa wa damu kwa wastani mgonjwa hupoteza seli za ubongo (neuroni 1.9) kila dakika.
KUNA AINA KUU MBILI ZA KIHARUSIBrain
1️⃣Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo
2️⃣Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo
🗒️80% ya watu wanaopata kiharusi hutokana na kuziba kwa mishipa ya damu kwenye ubongo.
Matumizi holela ya dawa aina ya antibiotiki huchangia usugu wa dawa kutokea.
Bakteria wanapopata usugu husababisha
➡️Kutokupona ugonjwa hata baada ya kutumia antibiotiki ambazo zimekuwa zikitibu ugonjwa huo
➡️Kuongezeka kwa gharama za matibabu
➡️Kifo
Unatengeneza tatizo usugu wa dawa iwapo
➡️Humalizi dawa ulizoandikiwa na daktari
➡️Unatumia dawa zisizo na ubora/feki
➡️tumia dawa zilizoisha muda wake wa matumizi
➡️Unakula nyama, maziwa, mayai au damu yenye masalia ya antibiotiki kutoka kwa mifugo iliyotibiwa
Inaweza tokea katikati ya usingizi mtu hasa mtoto akawa na tabia ya kutembea,kuongea au kufanya vitendo vingin akiwa usingizini
Hii ni SLEEPWALKING
Hutokea zaid kwa watoto hasa wavulana,inahisiwa hutokea kwa sababu mfumo wa ubongo kudhibiti msawaziko wa kulala/kuamka haujakomaa
Tabia ya kutembea au kuongea usingizini ikianza kwa mtu mzima inahusishwa na msongo mkubwa wa mawazo muda mwingine aina ya kifafa
🔵Tatizo la kutembea usingizini hutembea katika familia; 45% ya watoto wanaotembea usingizini pia na wazazi wao walitembea usingizini
Inaweza tokea katikati ya usingizi mtoto akaamka anapiga kelele,akazubaa kama Dakika 10 bila kujua nini kinaendelea akarudi usingizini kama hakijatokea kitu. Kesho akiamka hajui nini kilitokea.
🔵Hii ni SLEEP TERROR ni tatizo ambalo huambatana tatizo la kutembea usingizini
THREAD | MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO
KWANZA : Vidonda vya tumbo hutokea pale mfumo unaolinda kuta za tumbo unaposhindwa kazi hivyo asidi ya tumbo kuchoma kuta na kuleta kidonda/mchubuko.
🔵 Sababu kuu huwa ni maambukizi ya H. Pyroli na Dawa kundi la aspirin
Mtu mwenye vidonda vya tumbo hupata shida kama:
1️⃣Maumivu makali ya tumbo yanayochoma mara nyingi eneo la chini ya chemba ya moyo
2️⃣Tumbo kujaa gesi
3️⃣Kiungulia
4️⃣Uchovu huweza kutokea kama kuna upungufu wa damu kutokana na vidonda
5️⃣Kinyesi cheusi humaanisha vidonda vinatoa damu
Vidonda huweza kutokea tumboni au kipande cha kwanza cha utumbo
✍️Kidonda kilicho tumboni husababisha maumivu makali mara tu mtu anapokula;
✍️Kidonda kikiwa kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo husababisha maumivu mtu anakuwa na njaa, maumivu huisha mtu akila