#DondooZaDaktari | #USUGU WA #DAWA

➡️ #Antibiotiki ni dawa zinazotumika kutibu maambukizi ya bakteria.

➡️Usugu wa antibiotiki hutokea pale bakteria wanapotengeneza usugu dhidi ya aina flani ya dawa.

➡️USUGU hufanya dawa kushindwa kufanya kazi

#AntimicrobialResistance
Matumizi holela ya dawa aina ya antibiotiki huchangia usugu wa dawa kutokea.

Bakteria wanapopata usugu husababisha
➡️Kutokupona ugonjwa hata baada ya kutumia antibiotiki ambazo zimekuwa zikitibu ugonjwa huo
➡️Kuongezeka kwa gharama za matibabu
➡️Kifo
Unatengeneza tatizo usugu wa dawa iwapo
➡️Humalizi dawa ulizoandikiwa na daktari
➡️Unatumia dawa zisizo na ubora/feki
➡️tumia dawa zilizoisha muda wake wa matumizi
➡️Unakula nyama, maziwa, mayai au damu yenye masalia ya antibiotiki kutoka kwa mifugo iliyotibiwa
➡️Unatumia antibiotiki bila ushauri wa daktari
➡️Unatupa kiholela wa mabaki ya dawa za antibiotiki

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Dr. Norman Jonas

Dr. Norman Jonas Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @NormanJonasMD

29 Oct
#DondooZaDaktari | Leo ni siku ya #KIHARUSI #WorldStrokeDay

➡️Tatizo la dharura la kiafya ambalo ni moja ya magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo.

➡️Mitindo ya maisha na Lishe ni vitu vinavyochangia wagonjwa wanaopata stroke kuongezeka

➡️Kiharusi huacha ulemavu au kifo Image
➡️KIHARUSI hutokea pale seli za ubongo 🧠 zinapokufa kutokana kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo hivyo kukosa hewa ya oksijeni na virutubisho.

➡️Kiharusi kikihusisha mshipa wa mkubwa wa damu kwa wastani mgonjwa hupoteza seli za ubongo (neuroni 1.9) kila dakika. Image
KUNA AINA KUU MBILI ZA KIHARUSIBrain

1️⃣Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo

2️⃣Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo

🗒️80% ya watu wanaopata kiharusi hutokana na kuziba kwa mishipa ya damu kwenye ubongo. Image
Read 10 tweets
27 Oct
#DondooZaDaktari | Ugonjwa wa kisukari unaongezeka kwa kasi hata katika nchi zetu maskini.

✍️Kisukari hutokana na mwili kushindwa kutumia glukosi (sukari)

➡️Kisukari ndio sababu kuu ya:
- Kiharusi
- Upofu
- Ugonjwa wa kudumu wa figo
- Shambulio la moyo
- Watu kukatwa miguu Image
➡️Kwa mwaka 2019, takribani vifo millioni 1.5 Duniani vilichangiwa moja kwa moja na tatizo hili la kisukari.

➡️ Kuanzia mwaka 2000 hadi 2016, kuna ongezeko la 5% la vifo katika umri mdogo (premature death) kutokana na kisukari. Image
➡️ Mlo sahihi
➡️ Mazoezi ya Mwili
➡️ Kudhibiti Uzito
➡️ Kuepuka sigara na pombe

Ni baadhi ya mitindo ya maisha inayoweza kusaidia kuzuia kisukari au kupunguza athari ya kisukari aina ya pili.
Read 4 tweets
7 Jul
#CORONA --- #UVIKO19 UZI 👉 Je dalili kwa sasa ni zipi? Zimebadirika ? Picha ya ugonjwa ukiambukizwa ni ipi kwa sasa?
DALILI HUTOFAUTIANA KULINGANA UKALI WA UGONJWA?
✍️Tafiti kuhusu makali ya ugonjwa wa Korona-19 (UVIKO-19) yameonyesha makundi 3 ya wagonjwa

1. Ugonjwa usio mkali (81 kati ya 100)

2. Ugonjwa mkali maana mtu anahitaji oksijeni au 50% limeshambuliwa na ugonjwa (14 kati ya 100)
3. Ugonjwa mahututi maana mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi au ogani muhimu kama moyo, figo , ini kufeli

✍️HATARI YA KIFO: Kwa wastani vifo hutokea kwa asilimia 2.3 ya watu waliopata maambukizi kumaanisha asilimia wanopata maambukizi ya Corona 97.7 hupona
Read 18 tweets
25 Feb 20
Inaweza tokea katikati ya usingizi mtu hasa mtoto akawa na tabia ya kutembea,kuongea au kufanya vitendo vingin akiwa usingizini

Hii ni SLEEPWALKING

Hutokea zaid kwa watoto hasa wavulana,inahisiwa hutokea kwa sababu mfumo wa ubongo kudhibiti msawaziko wa kulala/kuamka haujakomaa
Tabia ya kutembea au kuongea usingizini ikianza kwa mtu mzima inahusishwa na msongo mkubwa wa mawazo muda mwingine aina ya kifafa

🔵Tatizo la kutembea usingizini hutembea katika familia; 45% ya watoto wanaotembea usingizini pia na wazazi wao walitembea usingizini
Inaweza tokea katikati ya usingizi mtoto akaamka anapiga kelele,akazubaa kama Dakika 10 bila kujua nini kinaendelea akarudi usingizini kama hakijatokea kitu. Kesho akiamka hajui nini kilitokea.

🔵Hii ni SLEEP TERROR ni tatizo ambalo  huambatana tatizo la kutembea usingizini
Read 9 tweets
28 Jan 20
THREAD | MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO

KWANZA : Vidonda vya tumbo hutokea pale mfumo unaolinda kuta za tumbo unaposhindwa kazi hivyo asidi ya tumbo kuchoma kuta na kuleta kidonda/mchubuko.

🔵 Sababu kuu huwa ni maambukizi ya H. Pyroli na Dawa kundi la aspirin
Mtu mwenye vidonda vya tumbo hupata shida kama:
1️⃣Maumivu makali ya tumbo yanayochoma mara nyingi eneo la chini ya chemba ya moyo
2️⃣Tumbo kujaa gesi
3️⃣Kiungulia
4️⃣Uchovu huweza kutokea kama kuna upungufu wa damu kutokana na vidonda
5️⃣Kinyesi cheusi humaanisha vidonda vinatoa damu
Vidonda huweza kutokea tumboni au kipande cha kwanza cha utumbo

✍️Kidonda kilicho tumboni husababisha maumivu makali mara tu mtu anapokula;

✍️Kidonda kikiwa kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo husababisha maumivu mtu anakuwa na njaa, maumivu huisha mtu akila
Read 14 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(