My Authors
Read all threads
HELIOS AIRWAYS FLIGHT 522
NDEGE YA WAFU
: Katika ulimwengu huu wa Sasa ambao karibu Kila kitu kimerahisishwa kutokana na maendeleo makubwa ya kiteknolijia yanayofanywa na wajuba tuna waita magenious, ukianzia kwenye mawasiliano, uzalishaji na usafirishaji yani Ni Mambo yamekuwa
mtelezo tu wenyewe tukisema dunia inakuwa Kijiji. Hasa tukiangalia Katika ishu za usafiri siku hizi Yani raha tu kwenda bara, taifa ama mkoa mwingine ni chap tu mfuko wako ukiwa unaruhusu, Mzee baba unachana mawingu dakika sifuri uko kwenye ardhi ya wakoroni. Pamoja ya kwamba
usafiri wa anga ni rahisi na waharaka lakini unaweza kuwa ndo njia ya usafiri yenye risk na hatari zaidi, Yani kwenye ndege ikikosewa kubonyezwa button moja tu Basi kinachofuata Ni majanga na majonzi ya wapendwa wa watu kupoteza maisha na kuacha vilio.
Iki ndo kilichotokea kwenye ndege ya shirika la Helios Airways ndege namba 522. Ambapo ndege hiyo ilipewa jina la ndege ya wafu(Ghost Plane). Ndege Hii ya abiria ambayo ilikuwa na ratiba ya kuruka kutoka Larnaca, Cyprus kuelekea Prague , Czech Republic ikiwa inatakiwa kutua kwa
muda katika mji wa Athens, Greece. Ndege hiyo ilianguka August 14,2005 na kuua watu wote 121 abiria na wahudumu walio kuwa kwenye ndege hiyo. Baada ya kukosa hewa ya kutosha na kupelekea watu wote kulala na kuacha ndege ikijiongoza yenyewe. Ilikuwa ni ajali mbaya zaidi kutokea
nchini Greece katika usafiri wa anga.

Nini kiliikumba ndege Hii Hadi kupelekea watu kukosa hewa ya kutosha na kuanguka. Ndege hiyo ilipo wasili kutoka London ikiwa inaendeshwa na rubani Hans Jurgen Merten mwenye umri wa miaka 59 ambaye amekuwa akifanya kazi ya urubani kwa zaidi
ya miaka 35 akiwa na jumla ya masaa 16,000 ya kuruka na ndege na jumla ya masaa 5500 akiwa na ndege Aina ya Boeing 737, pembeni yake alikuwepo rubani Pampos Charalambous umri miaka 51 ambaye amefanya kazi katika shirika la Helios kwa miaka 5 akiwa na jumla ya masaa 7,549 ya
kuruka na ndege na jumla ya masaa 3,991 akiwa na ndege aina ya Boeing 737.

Ndege hiyo ilipo wasili kutoka London asubuhi ya siku hiyo wahudumu waliokuwemo mwanzo walitoa taarifa juu ya kuganda kwa kifuniko Cha mlango (door seal) pamoja na kuwepo kelele za ajabu katika upande wa
kulia wa mlango wa dharura. Wakaomba mlango huo ufanyiwa uchunguzi wa uhakika. Uchunguzi ukafanywa na engineer wa uwanjani apo ambaye pia alichunguza mfumo wa hewa wa ndege hiyo kuona Kama ulikuwa unavuja, Sasa ili kuweza kufanya uchunguzi katika mfumo huu bila kuhitaji kutumia
engine za ndege inabidi kuswitch kutoka katika "auto" na kuwekwa "manual" , lakini baada ya engineer kumaliza uchunguzi wake akasahau kuurudisha mfumo huo katika "auto".

Baada ya ndege hiyo kurudi katika utendaji wahudumu wake walifanya check up ya mfumo huo wa hewa katika
nyakati tatu tofauti, kabla ya ndege kuanza kuruka(pre-flight procedure), baada ya ndege kuwashwa (after-start check) na baada ya ndege kuruka (after take-off check) ,waswahili usema siku ikifika imefika hakuna kusalimika. katika nyakati hizi zote tatu hakuna mtu aliegundua
kulikuwa na makosa katika setting za mfumo wa hewa wa ndege hiyo, ndege hiyo iliruka mnamo saa 9:07 mfumo wa hewa ukiwa bado umewekwa manual badala ya auto.

Ndege hiyo ilipo anza kupanda juu kiwango Cha hewa ndani ya ndege kilianza kupungua na ilipo vuka altitude ya feet 12,040
Sawa na mita 3,670 mlio wa kuashiria kupungua kwa hewa ndani ya ndege ilianza kulia, mlio huo ulitakiwa kuwa tahadhalisha marubani wasiende juu zaidi, lakini mlio huo wa tahadhari ukachanganywa na mlio mwingine wa tahadhali unaotokeaga endapo kukiwa na hitirafu katika mfumo wa
ndege kuruka na mlio huo utokea ndege ikiwa bado iko chini lakini marubani wakashangaa kusikia mlio huo ndege ikiwa tayari angani, kumbe milio hiyo ilikuwa ikifanana.

Dakika kadhaa baadae milio pamoja na taa kadhaa za tahadhari ziliwaka katika chumba Cha marubani, pia ziliwaka
Taa za tahadhari kwenye mfumo wa upoozaji wa ndege kuonyesha kulikuwa na kiwango Kidogo Cha hewa kilichokuwa kinaingia na kutoka katika feni za kupoozea ndege, milio Hii ilisindikizwa na kuwaka kwa taa kuu ya tahadhari. Taa ya kuonyesha kiwango Cha oksjeni katika maeneo ya abiria
nazo ziliwaka ndege hiyo ikiwa imefika altitude 18,000 sawa na mitaa 5,500. Vitolea oksjeni kwa abiria vilifunguka automatically ndege ilipofika usawa huo.

Muda mfupi baada ya taa hizi za tahadhari kuwaka rubani wa ndege hiyo aliwasiliana kwa njia ya radio na waongoza ndege wa
Helios na kutoa taarifa kwamba, mlio wa kutahadhalisha kuwepo na tatizo katika mfumo wa ndege kuruka ulikuwa ukilia na pia vifaa vya kupoozea ndege pamoja na vile vya ziada vilikuwa vimezimika, baada ya muda akafanikiwa kuongea na engineer wa uwanjani apo na ambaye aliifanyia
uchunguzi ndege hiyo kabla ya kuruka ambapo engineer huyo alimuuliza rubani "can you confirm that the pressurization panel is set to AUTO" lakini muda huo tayari rubani huyo alikuwa ameisha Anza kupatwa na kitu kinaitwa "Hypoxia" (Hali ya kupoteza utambuzi wa Mambo kutokana na
kukosa hewa ya oksjeni ya kutosha) hivyo alishindwa kujibu swali alilo ulizwa ye akasema "where are my equipment cooling circuit breakers". Na hayo ndo yalikuwa mawasiliano ya mwisho kufanywa na ndege hiyo.

Ndege hiyo iliendelea kwenda juu zaidi Hadi kufikia feet zinazo kadiliwa
34,000 sawa na mita 10,000. Mamlaka za anga za Nicotis zilijaribu kuwasiliana na ndege hiyo bila mafanikio. Ndege hiyo ilivuka mipaka ya anga ya Cyprus FIR (flight information Region) na kuingia Athens FIR bila ya kufanya mawasiliano na mamlaka za Athens, kumbuka muda huo wote
ndege Hii ilikuwa ikijiongoza yenyewe,hivyo hakukuwa na mawasiliano yoyote yalifanywa kwenda mamlaka za Athens , majaribio 19 yalifanywa na mamlaka za Athens kuwasiliana na ndege hiyo bila mafanikio kutoka saa 10:12 Hadi saa 10:50. Ndege hiyo ilienda kuelea angani kwa kujiendesha
yenyewe (auto-pilot) kwa dakika zinazokadiliwa 70.

Ndege za kivita F-16 mbili zililuka kutoka uwanja wa jeshi wa Hellenic baada ya kutaarifiwa habari za ndege ya Helios ndege namba 522. Ndege hizi zakivita ziliambiwa kwenda kuangalia Ni nini kimeipata ndege hiyo. Ndege hizi
mbili walikutana na ndege hiyo saa 11:24 na kujaribu kuangalia ndani yake ambapo walimuona rubani mmoja akiwa kalala hajitambui uku kiti Cha rubani wa pili kikiwa wazi. Pia walitoa taarifa kwamba vifaa vya oksjeni kwa ajili ya abiria vilikuwa vikining'inia.

Saa 11:49 muhudumu
wa ndege Andreas Prodromous alionekana kuingia katika chumba Cha marubani akiwa ndo mtu pekee aliekuwa na fahamu katika ndege hiyo na Andreas inaaminika alikuwa na fahamu kwasababu alitumia vimitungi vya oksjeni ya ziada kwa ajili ya wahudumu wa ndege. Andreas alikaa kwenye kiti
Cha rubani na kujaribu kuiongoza ndege hiyo, Andreas alikuwa na mafunzo ya kuendesha ndege na alikuwa na leseni kabsa lakini tatizo likaja hakuwa kapitia mafunzo ya kuendesha ndege Aina ya Boeing 737. Wapelelezi wa ajali za ndege walisema uzoefu wa Andreas ulikuwa Ni mdogo kuweza
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with RashY Grinch

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!