My Authors
Read all threads
Thread: (No names as usual)
Jamaa yangu anaishi Tabora, anafanya kazi. Mpenzi wake anaishi Arusha, anafanya kazi. Mwaka 2012 alikuwa na mpango wa kumchumbia, kutokana na sababu kadhaa wakasogeza hadi 2013. Jamaa yuko njema kiuchumi na mpenzi wake yuko njema pia.
👇🏾
Mnamo mwaka 2013 ambapo ilitakiwa wachumbiane jamaa akapata mchepuko Tabora pale kazini kwake. Jamaa akawa mkweli akamwambia mchepuko kuwa ninamchumba wangu tayari yuko Arusha, mchepuko akasema “haina shida maana hata mimi ninamchumba wangu yupo Dar”. Wakaanza mahusiano yao.
👇🏾
Walikubaliana kuwa watapeana muda wa Kila mmoja kuwasiliana na mchumba wake. Long distance si unajua simu ndo mawasiliano pekee. Jamaa alikuwa anamjali sana yule mchepuko na sometime akawa anamlipia bills kadhaa. Mapenzi yakawa motomoto Tabora, wote wakawa na furaha.
👇🏾
Mwezi 3, 2013 mchepuko aliombwa na mchumba wake aende Dar akae wiki moja. Jamaa alimkatia ticket ya ndege mchepuko na kumpa hela ya matumizi ya Dar. Mchepuko alipewa show nzuri usiku ule, kesho yake ndo akaenda Dar. Jamaa aliendelea na maisha Kama kawaida, hadi aliporudi.
👇🏾
Aliporudi alimtoa na kumpeleka Mwanza kuenjoy maisha. Walipokuwa huko mchumba wa jamaa aliumwa, akawa anampigia simu kila wakati ili kujua status. Mchepuko ulivumilia ila ikabidi amwambie “tumekuja Mwanza kuenjoy, weka simu pembeni baby”. Jamaa akamwambia ni mchumba wangu huyu
👇🏾
Mchepuko kwa Mara ya kwanza ukaanza kuona wivu, jamaa alikuwa anaongea na mchumba wake kwa mahaba ya hali ya juu. Ile vacation ikaisha, wakarudi Tabora. Mchepuko alikuwa huru kuja kwa jamaa muda wowote maana hakuwa na mwanamke tofauti Tabora. Anakuja anapika wanakula, wanalala
👇🏾
Mwezi 5, 2013 mdada akaanza kuwa na hisia na jamaa Kama utani. Akaanza kumuuliza maswali jamaa, akaanza kumfuatilia jamaa, kumpangia kuongea na simu. Jamaa alivumilia, akawa anakwepa ugomvi. Siku moja, mchepuko alipigiwa simu na mchumba wake, akaipotezea simu na hakumpigia.
👇🏾
Mchepuko aliombwa tena na mchumba wake kwenda Dar, akataka kukataa jamaa akamlazimisha. Akamkatia ticket ya ndege kama kawaida na pesa. Mchepuko akiwa kule akawa anampigia simu jamaa. Jamaa akanishirikisha mimi, nikamwambia “kaka kuwa makini unamchumba wako, kumbuka hilo”.
👇🏾
Mchepuko aliporudi, jamaa alikaa kama wiki 2 akaenda Arusha kwa mchumba wake. Alikaa huko wiki 2, mchepuko alikuwa anapiga sana simu. Jamaa alijitahidi kumuelewesha ila alikuwa ameshapenda na alikuwa haelewi. Inaonekana mchepuko alipata huduma hadi akawa anamuonea wivu mwenzie
👇🏾
Jamaa aliporudi Tabora alimuelewesha mchepuko kuwa awe na heshima na mchumba wake. Siku mbili baadae mchepuko akaomba msamaha na mapenzi yakaendelea. Kumbe mchepuko alishaanza kugombana na mchumba wake akijua atakuwa na jamaa moja kwa moja.
👇🏾
Upande wa mchumba wa jamaa waliahirisha tena tukio la uchumba kutokana na ratiba zao Hadi mwaka 2014 katikati. Mchepuko alipewa za chini chini kuwa jamaa anataka kumvalisha Pete mchumba wake. Mchepuko akaona kama anazidiwa akili maana lengo lake ni aolewe yeye na jamaa.
👇🏾
Mwezi wa 8, 2013 jamaa alipigiwa simu na mchumba wake akiwa analia sana na alikuwa anamlalamika kamsaliti. Jamaa akampoza kwa sauti nzuri, akamwambia amuelezee ishu nzima. Mchumba wake akaanza kutoa stori kuwa alipigiwa simu na mwanamke wake wa Tabora akamwambia anamimba yake.
👇🏾
Kumbe yule mchepuko alitafuta namba ya mchumba wa jamaa akampigia simu kumwambia aachane na mchumba wake, amefuma msg zao za mapenzi kwenye simu ya mpenzi wake(jamaa). Pia kwasasa anamimba yake na anategemea kujifungua. Jamaa hakupanic na alimtuliza na kumwambia atulie kwasasa
👇🏾
Jamaa alimwambia ukweli wote kuwa ndio ni mchepuko wake na aliomba sana msamaha. Siku iliyofuatia jamaa alimfuata yule mchepuko, alimchana sana. Akamwambia aache kuwasiliana na mchumba wake, uhusiano wao pia umeisha. Mchepuko alilia sana na akawa anahaha haelewi afanyeje.
👇🏾
Jamaa akapanda ndege kwenda Arusha, akaenda akamuomba msamaha mpaka wakaelewana. Kabla hajaondoka alimwambia mchumba wake atamvalisha Pete mwaka huohuo, anaahirisha ratiba zake zote. Wakakubaliana hilo then jamaa akarudi Tabora. Mchepuko hakuacha kuomba msamaha Kila siku.
👇🏾
Mwezi 10, 2013 jamaa akamvalisha Pete mchumba wake kimyakimya. Mwezi wa 12 akamuoa, akarudi zake Tabora. Mchepuko alikuja kuoneshwa picha za harusi na rafiki zake akachanganyikiwa. Hakuweza kufanya kazi, aliacha kwenda kazini, akataka kujiua. Jamaa alisema hajihusishi tena.
👇🏾
Mke wa jamaa hakuwa na makuu, alifanya mambo yake kimyakimya pia. Marafiki wa mchepuko walimlaumu sana na kumwambia “UMESHINDWA KULA NA KIPOFU”. Mchepuko alibaki kujuta kwanini alifanya yale wakati jamaa alikuwa anampa mahitaji yake, anamjali na kumpa huduma kali usiku daily.
👇🏾
Mchepuko alipopata ahueni, akawa anampigia simu mchumba wake. Mchumba wake alishaambiwa stori nzima, na yeye alishaamua kumpotezea maana alikuwa haoni future kwa huyo mdada. Akamwambia anampenzi mpya, yeye aendelee na huyo wa Tabora tu. Mwanamke alibaki analia na kujuta.
👇🏾
FUNDISHO: Kama Huwezi kuchepuka, usichechepuke. Asilimia kubwa ya wanawake wakichepuka wanahamishia mapenzi yote kwa mchepuko na kuharibu kwa mpenzi wake. Mchepuko ukishauambia unamtu wako, hawezi kuweka future kwako. Mwisho, unakosa kotekote.
***Asante***
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Philipo Bethuel👨🏽‍💻

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!