MAUAJI YA RAIS WA HAITI

#OnJuly07, 2020 🇭🇹

#Story ina part A na B

📋Historia ya Haiti

📋Mauaji ya Rais @moisejovenel

👩‍💻Unajua tangu ipate uhuru imeongozwa zaidi ya marais 49, kati yao 9 ndio walimaliza vipndi vyao bila kupinduliwa/kuuawa wakiwa madarakani?
#Thread|Story🕒👇 ImageImageImage
Usiku Julai 7 watu wenye silaha walivamia makazi binafsi Rais @moisejovenel wa Haiti na kumuuawa. N MAUAJI yaliyoshtua Haiti, ingawa bado haijulikani nani aliyeajiri wauaji na kwanini, lkn mercenaries wa Colombia na Marekani walikamatwa kufuatia mauaji yale.
RT iwafikie wengi👇
Turn on Notification..

Naona 📱 iko Low baada ya nusu saa hv nitarudi kukiwasha.

Hii nchi ni mapinduzi, kuuawa, kutiwa sumu ukiwa madarakani mpk le👇 ImageImage
PART A

#HISTORIA Ya HAITI

#Uzi umechangiwa na maombi ya wanaTOT namimi nimechagua kuuleta👇

Taifa la HAITI lilivumbuliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1492 na Mfanyabiashara na Mpelelezi wa Italia kama alivyo fahamika kwingineko CHRISTOPHER COLUMBUS.

RT @omari_manyama ImageImageImage
👩‍💻#Inaaminika COLUMBUS ndiye aliyegundua njia ya usafiri kutoka bara Ulaya especially Spain mpk bara Amerika

Alipofika eneo hilo akapaita Island Hispaniola [Little Spain] Stori hii inaanzia mbali hivyo chukua #popcorn kabisa ili usichoke

Niwaombe pia Rt ndio support yenyewe!!
Mwaka 1496 Mtawala wa Spain kipindi hicho akaanza kuitawala kikoloni maeneo ya taifa hilo na makao makuu yalikuwa #Santo_Domingo ulipo sahv mji mkuu wa JAMHURI YA DOMINIC

Mnamo mwaka 1697 Ufaransa akachukua akampiga Spain kisha akajimilikisha maeneo yote na kuitawala rasmi Haiti
Vuguvugu la kutafuta uhuru lilianza mnamo mwaka 1791 baada ya Marekani kujipatia Uhuru (1776)na raia wakazi nyingi za Amerika wakachoka kutawaliwa.

Mwaka 1801 Toussaint Louverture (mtumwa) akajitangazakama General Governor wa Haiti na 1802 wafaransa wakaanza kurejea makwao. Image
Mnamo Januari 01, mwaka 1804 nchi hii ikapata uhuru na mtu mweusi Jean-jacques Descalines akajitangaza mtawala wa Haiti kipindi hicho ilikuwa bado ktk mfumo wa tawala za kifalme.Descalines akatawala kimabavu akaanza kuua wapinzani Nov 17,1806 baada ya miaka 2 tu akauwawa na waasi ImageImage
Nchi ikavurugika mpk ukatokea mgawanyiko wa kimaeneo utawala wa kusini iliitwa Etat d'Haiti ikawa chini ya watu weusi wenye mchanganyiko wa kizungu (Mullatos) na upande wa kaskazin pakajiita Republique d'Haiti ikawa chini ya watu weusi (Blacks) kwa kipindi cha karibia mwaka mzima Image
Mnamo Februari 17, mwaka 1807 akatokea mtu mmoja mweusi mbabe aliyeitwa Henri Christophe akajitangaza Mfalme wa Haiti na akatangaza asitokee mbwa yeyote ajikweze mbele yake atamnyoa mapema asbh. Utawala wake ukatawala Haiti kwa kipindi kirefu takribani karibu miaka 13. Image
Mnamo March 18, 1811 akapitisha sheria yw utawala wa kifalme na akajitangaza Mfalme rasmi kisha akamteua mwanae Jacques-Victor Henry kuwa Kamanda Mkuu wa Jeshi. Raia wakafura wakataka kumuua na Oct 08, 1820 akajiua mwenyewe Ikulu na siku 10 baadae mwanae pia akauawa na raia. Image
Kabla ya kifo cha King Henri nchi ilikuwa chini ya kiongozi wa mapinduzi Boyer Jean-Pierre (Mullato).Aliiunganisha Haiti lkn aliondoa Blacks ktk uongozi.
#Ndiye Rais pekee alitawala kwa kipindi kirefu zaidi (25yrs), alikimbia nchi Feb 13,1943 kwnd Jamaica wananchi walipoandamana. Image
Nchi ikapitia ktk kipindi cha mpito kweli kwani kila aliyeingia madarakani hakuiongoza nchi kwa zaidi ya mwaka mmoja

List iko hv___

Riviere Herard 1843/44 alipinduliwa
Philipe Guirrier 1844/45 akafia Ikulu
Jean L.Pierrot 1845/46 alipinduliwa
Jean B Richie 1847/48 alifariki
Kipindi Jean B. Richie akiugua kwa sumu aliyopewa akiwa madarakani kiongozi mkuu wa jeshi Faustin Soulouque alikuwa akiongoza nchi. Na Richie alipofariki akashika nchi kwa mwaka mmoja.Mwaka 1849 akajitangaza mtawala mpya akatawala kwa miaka 12 na 1859 alikimbia mapinduzi ya nchi Image
Mwaka 1859 Fabre Nicholas Geffrard alikuwa kiongozi mkuu wa jeshi akashika nchi na kilichopelekea apindue nchi ni binti yake kuuawa.Akatawala Haiti kwa muda mrefu (8yrs) kidogo.Mmwaka 1867 mapinduzi yaliyoongozwa na Meja Sylvain Salnave yakamuondoa madarakani akakimbilia Jamaica. Image
Meja Sylvain Salnave akaongoza kati 1867/1869 akapinduliwa na rafiki yake Nissage Saget, akawa mafichoni asionekane. Baadae Rafiki akamdanganya arudi wajenge nchi alitua tu mjini Port-au-Prince akakamatwa.Alikutwa na hatia ya mauaji Januari 15,1870 alinyongwa kweupe watu wakiona. ImageImage
Jean-Nicolas Nissage Saget akaongoza Haiti km kiongozi wa mpito kwa miaka minne (1870/74) ilipofika April 1874 bunge la nchi likaketi ili kuchagua rais akakubali akaridhika na muda wake akaachia madaraka bila mapinduzi na Mei 20 alihamia Saint-Marc alipoishi mpk kifo chake (1880) Image
Bunge likamchagua Michel Domingue atawale vipindi viwili tofauti yaani (miaka 8) lakini hakumaliza. Aliongoza miaka miwili (1874/76) tu akatengeneza uhasama na mataifa ya magharibi akaandamwa na April 1876 alijiuzulu na kwenda uhamishoni Jamaica, ambako alikufa mwaka 1 baadaye. Image
Changamoto ilianzia alianza alipokamata wapelelezi wa nchi waliogundua harufu ya ufisadi miongoni mwao ni Pierre Théoma Boisrond-Canal, Generals Brice, Pierre Monplaisir Pierre wapinzani wake wakuu.Brice na Monplaisir waliuawa gerezani lkn Boisrond akakimbilia ubalozi wa Marekani
Ikapelekea tena mgogoro wa kidiplomasia kati ya Haiti na US baada ya kuua wamarekani wawili waliosemekana ni wakimbizi. Kiti cha Uongozi kikawa kigumu.

Boisrond alipoona Domingue amekimbia nchi akarudi Haiti akashikilia uongozi kwa mpito mpk Julai 17, mwaka 1879 alipojiuzulu. Image
Baada ya kuachia Lysius Feoicite Salomon akatokea bungeni.Alichaguliwa kwa7bu alikuwa waziri wa vyeo vingi serikali iliyopita.

Sababu nyingine iliyompa ushindi aliwahi kuisaidia kulipa mkopo wa Ufaransa. Ndio maans alipogombea akachaguliwa. Aliongoza kwa miaka tisa (1879/1888) Image
Salomon naye alipunduliwa. Machafuko yalianza 1886 baada ya kuchaguliwa kwa muhula wa II (miaka 7) kipindi nchi ikiandaa sheria kwa ajili ya #Katibampya, yakajirudia 1887/88 baada ya mji mkuu kutekwa na waasi  (Le Cap) akaona isiwe tabu akakimbilia Paris ambapo mauti ulikumkuta.
Bunge likachagua kiongozi mwingine kpnd hiki aliyekuwa waziri wa kilimo François Denys Légitime ndiye alipata kijiti. Akaongoza kwa pressure kabla hajamaliza muda miaka saba akajiuzulu. Aliongoza kati ya 1888/89 yaani mwaka mmoja tu baada ya kuona nchi ngumu akakimbilia Jamaica. Image
Bunge likaketi likamchagua Florvil Hyppolite. Huyu alikuwa kiongozi wa ulinzi na waziri wa usalama kipindi Denys alipokuwa madarakani. Huyu ndiye rais aliyeiongoza Haiti kwa maendeleo kidogo akaunganisha mji mkuu kwa mawasiliano ya simu. Alikosea tu alipoanza kuua wapinzani wake. ImageImage
Aliuawa na viongozi waliokuwa wameachwa na utawala wa Denys Legitime, akawa amekosea. Akatiliwa sumu akaanza kuugua mdogo mdogo akawa anashauriwa na mkewe aachie madaraka hasikii, siku moja akiwa njiani akielekea bungeni akaanguka pu kutoka kwenye farasi akafa. Aliongoza 1889/96. Image
Bunge likaogopa huenda ikatokea mapinduzi baada ya Rais kufariki, March 24, 1896 likamchagua haraka haraka aliyekuwa waziri wa vita Paul Tirésias Simon Sam, kuwa Rais wa Haiti. Akaongoza nchi kwa miaka 6 (1896/1902) siku chache akamilishe muhula wake akaandika barua ya kujiuzulu. Image
Nchi ikaongozwa kwa mpito na General Boisrond Canal (aliwahi kuwa rais 1876/79 kisha akakimbilia uhamishoni). Mwezi Disemba 1902 baada ya Sam kujiuzulu mzee Pierre Nord Alexis akiwa na miaka 80 akachaguliwa kuwa Rais wa Haiti (alikuwa waziri wa Vita). Image
Akaanza na kukamata viongozi wote waliowahi kula ama kutuhumiwa kwa ufisadi akawafunga gerezani.Baadae akaanza kuandamwa alipoona muda wake wa urais umeisha alikwenda uhamishoni Jamaica baadaye alihamia New Orleans (US) na familia yake, ambapo kifo kilimkuta akazikwa hukohuko.
Yeye aliongoza kati ya 1902/1908.

Ilitokea njaa maeneo ya kusini watu wakaandamana wakimtaka ajiuzulu + vitisho baada ya kuwaua watu 20 waliompinga kutokana na hio migomo ya njaa. Alifariki dunia Mei 01, mwaka 1910 na kuzikwa ktk makaburi ya  St. Louis huko New Orlea, Marekani.
Kwa Leo Tuishie hapa

Weka Notification ON

Kesho Muendelelezo, kumbuka ndio nipo miaka ya 1910's

Mengi mazuri yanakuja mbeleni

#Visa vitamu vipo mwishoni
Ndg kumekucha ww unayesoma huu #uzi nikuombe support yako kwa kurudi mwanzo kabisa juu u-retweet ili iwafikie wengi namm unakuwa umenipa moyo wa kuendelea kukuletea nyuzi kali kali

Tuendelee 👇

Mzee Alexis alipokimbia Haiti kuelekea USA, François C. Antoine Simon akashika nchi. ImageImageImage
Rais François C. Simon aliingia madarakan kwa mapinduzi,kwanza aliuteka mji mkuu wa Port-au-Prince alipoona Alexis kakimbia akajitangaza Rais.Yeye hakuwa na cheo chochote serikali bali alikuwa mhuni tu ktk mitaa ya mji na genge kubwa la walanguzi wa madawa ya kulevya nchi nzima
Alipoingia madaraka akasahau wahuni wake wa mtaani waliosababisha yeye kuingia madarakani. Akaanzisha program ya kuweka umeme ktk mitaa yote ya mji mkuu ili kukamata wahalifu akawa ameharibu.Mbaya zaidi akaweka sheria walio uhamishon wanaruhusiwa kurejea ili kujenga nchi pamoja. Image
Hakuishia hapo akaanza kodi mpya ktk mashamba ya miwa na migomba ya wazawa eti ndio uzalendo ili kujenga nchi.
Akaanza kuandamwa na mjukuu wa Rais wa kwanza wa Haiti (Dessalines) ENG. CINCINNATUS LECONTE. Huyu mjukuu alikuwa kwanza ana pesa halafu Waziri wa kazi na kilimo.
Ukumbuke Rais SIMON ndio ameingia madarakan 1908 ilipofika Feb 1911 CINCINNATUS akafanya jaribio la mapinduzi ili kumuondoa rais madarakan ikashindikana, akarudi maeneo ya vijijin akakusanya wakulima wapatao LAKI hv akaanza maandamano na mnamo Agosti 3, 1911 SIMON akakimbia nchi.
Akaingia CINCINNATUS LECONTE akashika nchi kisha bunge likampitisha kuwa Rais. Aliongoza kati ya 1911/12.
Ktk uongozi wake aliongeza mishahara walimu na minara ya simu. Alikosea alipopunguza idadi ya wanajeshi, akaharibu.Agosti 08, 1912 akalipuliwa na bomu akiwa ikulu akafariki. ImageImageImage
Ilikuwa ghafla nchi ikatetemeka, achilia rais lile bomu liliua zaidi ya watu 300 hata nyumba za viongoz waliokuwa wanaishi karibu na Ikulu zilianguka kwa mtikisiko.Bunge likaitisha kikao cha ghafla akachaguliwa TANCRÈDE AUGUSTE'S (alikuwa waziri wa ulinz na mfanyabiashara mkubwa) Image
Rais TANCRÈDE AUGUSTE'S akashika nchi, aliongoza kati ya 1912/13.

Huyu ndiye aliyejenga Ikulu mpya maana pesa alikuwa nayo (alikuwa mfanyabiashara). Ikulu ya kisasa ambayo ni imara na ndio inayotumiwa mpk sasa

Alifariki Mei 02, 1913 akiwa madarakani inasemekana alinyeshwa sumu. ImageImageImageImage
Akachanguliwa MICHEL ORESTE, huyu kipindi anachaguliwa nje ya bunge mitaani kulikuwa milio ya rasisi (waasi walikuwa wanataka nchi).
Aliongoza nchi kwa miezi 9 tu (1913 mei /Jan 1914) akaachia kwa kupinduliwa, akimbilia uhamishoni (New York).Hakupendwa kbs maana alikuwa mzungu. ImageImage
Akaingia ZAMOR ORESTE (alikuwa waziri wa Vita).

Alipoingia Marekani ikamlazimisha asikusanye mapato sababu sio kiongozi wa taifa.Akaweka mgomo, Lkn DAVILMAR THÉODORE (mkuu wa majeshi) akajitokeza kupinga urais wake eti sio halali. Alitawala miezi 8 tu (Feb1914-Oct) akapinduliwa Image
Rais DAVILMAR THÉODORE alikuwa mkulima wa zao la cocoa kaskazini mwa Haiti.
Aliwaambia wananchi waungane naye ktk mapinduzi ya kumng'oa ZAMOR kwa ahadi kuwa akiwa rais atanunua zao hilo kwa bei ya juu. Wananchi wakamuunga mkono na wakampindua naye akashika nchi kutawaliwa. Image
Aliposhika madaraka akasahau alitoa ahadi ya kununua cocoa zote kwa bei ya juu.

Raia wakasanda wamuue wakaandamana wakiongozwa na mkulima mwenzao JEAN VILBRUN GUILLAUME SAM.Akatisika sana mpk Jeshi la USA likaingia Haiti likajichotea pesa $500,000 Benki kuu na hakuwafanya kitu ImageImage
Ndipo Jeshi la Ufaransa likarejea Haiti kwa ajili ya ulinzi wa Benki kuu na kuanzia Januari 1, 1915 Haiti ilikataa kutambua sarafu ya marekani nchini humo. Pesa hizo zilikwenda mpk leo hazijawahi kurudishwa ndipo SAM akashika nchi kwa mbinde ilikuwa Februari 15 mwaka 1915
Akaingia madarakani VILBRUN GUILLAUME SAM. Akaongoza miezi michache akaanza kupingwa vikali na wasomi wakiongozwa na DR #ROSALVO_BOBO. Mbaya zaidi Julai 27, 1915 alipoamuru kunyongwa wafungwa 167 wa kisiasa akiwemo na rais wa zamani ZAMOR ORESTE dunia ikamgeukia asipate pakutokea Image
Wananchi wakaandamana wakimtaka aachie ngazi.Alipoona hali imekuwa ngumu akakimbilia ubalozini (France Embassy).

Waasi (mullato) wakavunja ubalozi wakamtoa nje na kumpiga sana mpk wakamuua kisha wakatundika mwili wake ktk geti la ubalozi na kwa wiki 2 nchi ilikuwa ktk machafuko. ImageImageImage
#STORY zaidi ya VILBRUN SAM unaweza kuipata ktk kitabu cha WEIRD TALES "Thus Spake the Prophetess" (1924) by ARTHUR J. BURKS au ktk filamu ya "Emperor Jones" iliyochezwa na EUGENE O'NEILL

Aliongoza kwa miezi mitano tu (March4-July 27 1915).

Ndipo Marekani ikaivamia Haiti rasmi Image
Habari za mauaji zilimfikia Rais wa Marekani kwa kipindi kile WOODROW WILSON akatoa amri @USNavy ziivamie Haiti (Julai 28, 1915)
Nchi nzima ikawekwa chini ya ulinza hata DR BOBO akatulizwa. Wanajeshi wa Marekani wakakalia mji mzima wakaitawa Haiti kwa miaka 19 mpk Agosti 1934. ImageImageImageImage
KABLA hatujaenda huko 1934 hebu tuangalie marais waliowekwa na USA kipindi ikiwa imeikalia kwa mabavu HAITI👇

Sudré Dartiguenave 1915/22-FTime
Louis Borno 1922/30 -FTime,
Eugène Roy 1930 (Dark) -FTime,
Sténio Vincent 1930/41 -FTime. ImageImageImageImage
#Wengine

📋Elie Lescot 1941/46-Overthrown
📋Leon Estime 1946/50-Overthrown
📋Frank Lavaud 1946-Overthrown
📋Paul Magloire 1950/56-Overthrown
📋Francois Duvalier 1957/71-Died inOffice
📋Jean-Claude (mtoto wa👆) 1971/86-Overthrown
📋Leslie F Manigat 1988 #mwanamkePekee-Overthrown ImageImageImage
Turn On Notification📌🔔

#Nikirudi

👩‍💻UDIKTETA RASMI HAITI

📋🎼Hapa nitamzungumzia #DUVALIER 🎤
📋🎼Aliyetawala urais ukawa mzuri akajipitisha kuwa Rais mpk kifo.
📋🎼NitaGUSIA kwa uchache waliyowafanya hao niliowataja hapo JUU!!

MUHUMU 🔔 | FOLLOW ME
KISHA RETWEET HUU UZI ImageImage
#Muendelezo🔥

MORNING ALL__&&

Leo ni nitagusia viongozi baadhi baada ya Marekani kuikalia kijeshi Haiti (1915/34)

📋Historia yao,
📋Waliyofanya,
📋Walivyoboronga & mwisho wao💣
#USIACHE KU-LIKE & RETWEET ile tweet ya mwanzo kabisa kule JUU kabisa iwafikie wengi
Twende chap👇👇 ImageImageImage
Ikumbukwe @USMarineCorps waliingia na kuikalia Haiti baada ya wazungu (mullato) kumuua JEAN VILBRUN GUILLAUME SAM akiwa ikulu mnamo July 28, mwaka 1915. Nchi ikajikuta ikawa ktk hali ya mpito na marais wengi ni walipewa kutawala na serikali ya Washington (hachaguliwa na raia)
Wapo niliowataja hapo JUU kwa uchambuzi zaidi nitagusia baadhi.

#From 1915's___________TO 1922

LOUIS BORNO (1922/30)

Alimpokea Philippe Sudré Dartiguenave akaongoza miaka 8 kwa mihula miwili na ktk utawala wake alijitahidi kuigusa Jamii. Alipoingia alikuta deni kubwa la taifa Image
Deni lilikuwa kubwa sawa na Budget ya serikali kwa miaka minne. Akachukua $ 23M akalipa madeni yote ya nchi.

Akajenga miundombinu:
📋Barabara 1700km,
📋Madaraja 189,akajenga shule, hospitali,visima na kukarabati majengo ya umma, PAMOJA na kuweka mfumo mpya ☎️Automatic Dialling
Ndiye Rais wa kwanza kupitisha Lugha asili za nchi hiyo #Haitian_Creoles ktk Mfumo wa Elimu, akafuta kifaransa.

#KOSA:Alikataa kuandaa mazingira ya uchaguzi ujao kuwa huru na wa haki.Baraza lake la mawaziri lote lilikuwa la chama chake (mawaziri 21) na muhula wake wa 1 ukaisha.
#April 21, mwaka 1926 akachaguliwa TENA. Uchaguzi ulifanyikia ndani kwake (kipindi hicho Bunge ndio lilikuwa linachagua rais. Upinzani ulimpinga vikali kutokana na siasa zake.
Akaanza kufunga wakosoaji na waandishi wa habari waliomkosoa na wengine aliwafyekelea mbali kwa kuwaua.
📋GHAFLA ukatokea mtikisiko wa kiuchumi "The Great Depression 1929's" uliotikisa dunia especially US Stock Market Crash ukapelekea sera za kiuchumi Marekani kubadilishwa na ikajiondoa kuifadhili kiuchumi Haiti. Maandamano ya wakulima yakaanza kutokana hali ngumu ya maisha.
#Akaona raia watamuaa akaachia nchi lkn hata hivyo muda wake ulikuwa umeisha. Nchi ikarudi mikononi mwa @USMarineCorps Rais JOHN H. RUSSELL (USA) akamteua kiongozi kukaimu urais kwa mpito.

#Mei 15, 1930 EUGENE ROY mtaalum wa Bank ndiye aliteuliwa kuongoza nchi mpk Nov 18, 1930.
EUGENE ROY (1930/1941)

Awali alisome sheria na kuhitimu Law school akiwa mdogo sana (19yrs Old).
#Alipoingia madarakani aliruhusu raia kuchagua wawakilishi ktk BUNGE la nchi hiyo!! Lkn alikutana na uongozi mgumu sana.Alitawala muda wake ukaisha na Mei 15, 1941 akaachia madaraka ImageImageImage
ELIE LESCOT (1941/1946)

📋Kitaaluma alikuwa Mfamasia💊

#Yeye aliingia ktk siasa 1911 baada ya kufiwa na mke. Aliwahi kuwa Balozi wa Haiti (Dominica). Nchi ilimlemea na 1944 kidogo tu apinduliwa, waasi wakakamatwa. Maandamano yaliendelea akaachia urais na kukimbilia uhamishoni. Image
DUMARSAIS ESTIME (1946/50)

#Alizaliwa ktk familia maskini, wazazi wake walifariki akiwa mdogo (9yrs OLD), Akasomea sheria, Akawa waziri wa elimu 1937/40.Ktk uongozi wake alirudisha waafrika serikalini lkn alipinduliwa Mei 10,1950 kabla ya muda wake kuisha akakimbilia JAMAICA!! Image
FRANCK LAVAUD

#Alikuwa Mkuu wa Majeshi baada ESTIME kukimbia nchi yeye ndio aliongoza taifa kwa mpito mpk uchaguzi ulipofanyika.

Tofauti na viongozi wengine wa majeshi huyu hakuwa na tamaa aliongoza nchi kuanzia Januari 11 mpk Aug 16, mwaka 1950 akawapa wenye nchi madaraka. Image
PAUL MAGLOIRE (1950/56)

Baada ya Gen. LAVAUD kurudisha madaraka kwa raia, uchaguzi ukapangwa mwishoni mwa mwaka na MAGLOIRE akagombea na Desemba 06,1950 Alichaguliwa kuwa rais. Ktk uongozi wake alikuta nchi ikiwa na mashamba makubwa ya kahawa yaliyokuwa yanamilikiwa na serikali. Image
#Akauza kahawa na Fedha alizopata akajenga Nchi.

Aliongeza barabara, akakarabati miji & huduma za jamii. Ni ktk utawala wake Haiti ilionekana #kivutio cha watalii kuliko nchi yeyote Amerika. Mwaka 1954 kimbunga HAZEL kikaipiga vibaya mno nchi ikapelekea miundombinu kuharibika. ImageImageImageImage
🌀Kimbunga kiliharibu Haiti, nchi wahisani wakatuma Fedha za misaada ikasemekana zimeibiwa wananchi wakafura, kumbuke muhula wake ulikuwa umeisha akawa anataka kugombea TENA!! akapoteza umaarufu.
#Mnamo Dec 06, 1956 akajitokeza akasema hatagombea uchaguzi ujao maandamano yakaisha
Baada ya Magoire kukimbilia uhamishoni JOSEPH PIERRE-LOUIS alijitangaza RAIS wa mpito ktk redio.
#Alitangaza pia uchaguzi mkuu utafanyika April 1957 na kuamuru LOUIS DEJOIE aliyekuwa mgombea urais (alifungwa na Magoire) kuachiliwa huru pamoja wafungwa wote wa kisiasa nchini humo ImageImage
Januari 1957 PIERRE-LOUIS alikamata mali (majengo, duka) za rais wa zamani Magloire.
Alikaimu urais kwa muda mfupi (Dec 12- Feb 03,1957).
Bunge likamshtukia likamchagua FRANCK SYLVAIN (Lawyer) kuongoza nchi kwa muda, aliongoza kwa siku 56 naye akaondolewa na kupewa DANIEL FIGNOLÉ ImageImage
DANIELaliapishwa Mei 25 kushika nchi kwa muda.

#Yeye alichaguliwa kwa7bu ya umaarufu wake mji mkuu Port-au-Prince na siku anapokula kiapo kulikuwa maandamano Lkn walposikia kiongozi mwingne kachaguliwa walisogea viwanja vya Ikulu, akahutubia wanachi kuahidi kuongeza mishahara. ImageImage
Ingawa DANIEL FIGNOLÉ alimuahidi FRANKLIN D. ROOSEVELT (aliyekiwa rais wa 32 Marekani) kupingana na siasa za kikomunisti waziwazi Lakini siasa zake zilimfanya akatiliwa shaka kumbuke ilikuwa kipindi cha Cold War na sababu kubwa ilionekana akiunga mkono siasa za nchi za kisovieti.
ALLEN DULLES Mkurugenzi wa CIA ndiye aliyefanya uchunguzi na kumgundua kisha akawambia Rais Dwight D Eisenhower (aliyekuwa rais wa US kwa kipindi hicho), kwamba DANIEL FIGNOLÉ alikuwa na mwelekeo wa siasa kali za mlengo wa kushoto.

Hivyo Marekani ikakataa kuitambua serikali yake
Rais EISENHOWER akamuita Balozi wa Ufaransa ikulu kwamba kumwambia ana wasiwasi kwamba FIGNOLÉ huenda mwishowe anaweza kuwa #ARBENZ mwingine, akimaanisha Rais wa Guatemala aliyeondolewa baada ya miaka mitatu kuchaguliwa ktk mapinduzi yaliyotekelezwa na CIA.
#Fignolé hakuongoza km matarajio yake yalivyokuwa.

Ikiwa ni siku 19 tu baada ya kuwa Rais kikosi maalum wakiwa pamoja na Mercenaries wa US kiliingia Ikulu akamkamatwa na kulazimishwa kwa mtutu kutia saini barua ya kujiuzulu, kisha wakamuingiza ktk gari na kumtoa nje kimya kimya
#Ilikuwa June 14, mwaka 1957 nchi ikarudishwa chini ya utawala wa kijeshi chini ya ANTONIO THRASYBULE KÉBREAU aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza kuu la Kijeshi nchini humo. Akaongoza nchi mpk 22 Okt 1957 ulipofanyika uchaguzi na aliyekuwa waziri kazi François Duvalier akashinda Urais Image
FRANÇOIS DUVALIER (1957/71)

Alichaguliwa kuwa rais wa Haiti mnamo Trh 22 Oktoba 1957 na raia wengi sababu kubwa ni alikuwa mweusi.
#KwaUfupi:
DUVALIER alizaliwa 14 April 1907 mjini Port-au-Prince na wazazi Duval (Baba) na Ulyssia Abraham (mama) aliyekuwa mwokaji mikate. ImageImageImage
Baba alipofariki shangazi yake Madame Florestal akamchukua kuishi nae.
Shangazi akamsomeshs na mwaka 1934 alihitimu Degree ya udaktari #Haiti_University. Akafanya kazi za udaktari ktk hospitali kadhaa za umma.Baadae akajiunga na Chuo Kikuu cha Michigan akisomea Public Health
Mnamo 1943 akawa anaishi US akifanyia kazi shirika moja lililokuwa linajihusisha kudhibiti kuenea kwa magonjwa yanayoambukizwa ktk ukanda wa kitropiki km vile Typhus, Malaria na magonjwa mengi.

#Huko ndiko alipata jina la "PAPA DOC" (alipewa na wagonjwa aliokuwa anawahudumia)
#Nimechagua kumuelezea FRANÇOIS DUVALIER kwa sababu ktk uongozi wake ndipo tutakuja kupata chanzo cha mauaji ya Moïse aliyekuwa rais wa Haiti kilichotokea hivi majuzi usiku wa Julai 07, 2021 siku ya Jumatano akiwa kwenye makazi yake binafsi mjini mkuu wa nchi hiyo Port-au-Prince.
Mnamo 1946, Duvalier alimuunga mkono rais DUMARSAIS ESTIMÉ ndipo akateuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa taasisi zinazotoa huduma za afya nchini. Mwaka 1949, aliteuliwa na kuwa waziri wa afya na kazi, Lkn MAGOIRE alipofanya mapinduzi (1950) aliacha uwaziri na kufanya shughuli binafsi.
Mwaka 1954 DUVALIER aliacha kazi shughuli za kutibu akajificha maeneo vijijini kukwepa serikali ya Magloire. Mnamo 1956 serikali ya Magloire ilikuwa inaelekea kushindwa kabisa kuongoza nchi, akiwa mafichoni Duvalier alitangaza kugombea urais na Dec 1956 aliibuka kutoka mafichoni
#Katika kampeni ya urais mwaka 1957 wagombea walikuwa wawili DUVALIER na LOUIS DÉJOIE (mfanyabiashara wa kaskazini). Mpk kampeni kufanyika Haiti ilikuwa imeongozwa na viongozi watano bila kudumu. Duvalier aliahidi kuijenga upya na kuiboresha nchi na vijijini walimuunga mkono Sana
François Duvalier akachaguliwa kuwa RAIS Trh 22 Septemba 1957

#Alipata kura 679,884 dhidi ya 266,992 za mpinzani wake DÉJOIE. Ijapokuwa ktk uchaguzi huu udanganyifu ulikuwa mwingi na vitisho kwa wapiga kura. Baada ya kuchaguliwa tu wafuasi wengi wa Déjoie walikimbilia uhamishoni ImageImageImage
#DUVALIER akawapandisha vyeo watu weusi na kuwaweka wengine vyeo vizuri ktk utumishi wa umma na Jeshini.
Mnamo Julai 1958 maafisa 03 wa jeshi waliokuwa uhamishoni wakiwa na mercenaries 05 raia wa marekani walingia Haiti ili kumpindua DUVALIER, Bahati mbaya wote #waliuawa.!!! ImageImage
Baada ya kuzuia mapinduzi hayo utawala wake ukabadilika ukawa wa kiimla na kidikteta.
Mwaka 1959 akaunda kikosi chake cha siri alichokiita #Tonton_Macoute. Kikaanza kuua wapinzani wake unaambiwa kilifanya mauaji mpk Wahaiti waliogopa sana hakuna aliyejiita ni mpinzani hadharani Image
Mwaka huo huo kwa mgongo wa #uzalendo akafukuza viongozi wa kidini na maaskofu wote wa kigeni wa @RomanCatholic (hakubakiza hata mmoja) na GHAFLA akaugua ugonjwa wa shinikizo la moyo na kisukari akampa madaraka mkuu wa kikosi chake hicho cha mauaji Clement Barbot akaenda kutibiwa
Aliporejea kutoka Hospitali akamkamata CLEMENT BARBOT akamfunga kwa tuhuma kuwa kipindi anaugua huyu mwamba alikuwa anapanga njama za kumpindua. Mwaka 1963 BARBOT alipotoka Jela akaanza harakati za kumuondoa DUVALIER madarakani kwa kuteka watoto wake ili kumshinikiza aachie urais
Kile kikosi chake 'The Tonton Macoute' kikaingia mtaani kusaka watoto wa mkuu wao. Taarifa zikamfikia zikieleza maeneo BARBOT alipojificha na kufanya watoto wake mateka, ndani ya masaa 4 Barbot akapatikana na kuuawa, Duvalier akaagiza kichwa chake kiletwe aone aage marehemu. Image
Muhula wa kwanza ktk utawala ukaisha akiwa anaogopeka sana.

#Mwaka 1963 akafanya akiwa mgombea pekeyake baada ya kuenguliwa wagombea wenza wa upinzani, matokeo ya uchaguzi yakatangazwa ikaonekana ameshinda kwa kura 1,302,748 sawa na 93.6% akaapishwa kuongoza kwa muhula mwingine ImageImage
Baada ya kuapishwa kwa mara ya pili JOHN F. KENNEDY akaitembelea Haiti (1963) ikiwa ni baada ya miaka mingi nchi hizo zikiwa ktk kutoelewana. JFK aliporudi akatangaza kumsaidia DUVALIER misaada mbalimbali ikiwemo ya kifedha kwa7bu Duvalier alilionekana kupingana na siasa za Cuba.
Msaada wa kwanza ulikuwa Fedha kiasi cha US$ 15M Lkn pesa hiyo inasemekana aliiweka ktk A/c yake binafsi, baadae akatangaza kuwa Marekani ni vibaraka akavunja uhusiano. FIDEL CASTRO alipoona Duvalier ameachana na siasa za USA akamtumia US$ 4M km msaada wa kujenga uhusiano wao.
Unaambiwa fedha hizo aliweka kwenye A/c binafsi na inasemekana alijipendekeza baada ya JFK kuuawa.

Mnamo April 24, mwaka 1966 Mfalme wa Ethiopia HAILE SELASSIE. Akatunukiwa Necklace (mkufu) wa heshima wa JEAN-JACQUE DESSALINES (alikuwa rais wa kwanza Haiti ilipopata uhuru 1804) ImageImageImage
Mfalme HAILE SELASSIE alikwenda kuitembelea Haiti kuzungumza na DUVALIER kuhusu mpango wake wa kujitengenezea katiba iliyompa nguvu ya kutawala mpk kifo (President for life 1964).

Ijapokuwa hakufanikiwa ktk hilo

Mwaka 1967 ukatokea mlipuko mkubwa Ikulu ila hakudhuruka.
siku chache baadaye Duvalier alihotubia Taifa kisha alisoma karatasi ya mahudhurio ya maafisa wa jeshi majina 19 wakaonekana hawapo (absentees) baada ya kusoma orodha yote alisema kuwa wote wamepigwa risasi, means amewaua na ilisemekana ktk mlipuko uliotokea Ikulu ndio walihusika
April 28, 1969 DUVALIER alianzisha kampeni ya kuwaondoa Wakomunisti wote nchini.Akatunga sheria mpya iliyopiga marufuku shughuli za Kikomunisti bila kujali ni za aina gani kwamba zinatishia usalama wa taifa.Waliopatikana wakifanya shughuli hizo waliuawa, na kunyang'anywa mali zao
Mbabe FRANÇOIS DUVALIER alifariki dunia April 21,1971 akiwa hajamaliza muda wake kwa ugonjwa wa moyo na kisukari wiki moja baada ya kusherekea miaka 64 ya kuzaliwa kwake na mwanawe JEAN-CLAUDE DUVALIER almaarufu kwa jina #Baby_Doc akiwa na miaka 19 akamrithi km Rais mpya wa Haiti ImageImageImage
Tunaweza kusema ktk utawala wake 14yrs madarakani alitengeneza matabaka baina ya watu weusi na weupe na wataalam wengi walihamia mataifa ya nje.
KiNGINE alijenga uwanja wa ndege alioupa jina François Duvalier Airport ambao sasahv unaitwa Toussaint Louverture International Airport ImageImageImage
JEAN-CLAUDE DUVALIER (1971/86)

#Nickname "Baby Doc"
Alizaliwa 4 July 195, alimrithi baba yake baada ya kifo chake mwaka 1971.Alipochukua madaraka maelfu waliuawa na kuteswa,wengi walikimbia nchi.Aliishi maisha ya kifahari (harusi iliyogharimu US$ 2M) huku raia wakifa kwa umaskin ImageImageImageImage
***Alizaliwa 4 July 1951
#Let's GO!!

Muendelezo wa Part A

"BABY DOC" na vitimbi vyake baada ya kumrithi #Papa_Doc💣
📋Ufisadi
📋Utawala wake
📋Majaribio kupindua n.k
Tukimaliza hii Game of Thrones ANDIKO LA MOÏSE 🔥ndio litafuata.

#MUHIMU:FOLLOW ME & RETWEET #uzi huu 'll be Your Appreciation TO-ME!!🙏 Image
#Ikumbukwe ktk Utawala wa Baba yake Wahaiti wengi walikimbilia uhamishoni especially waliokuwa hawamuungi mkono Duvalier.
Mwishoni mwa 1978 Jean-Claude Duvalier (Baby Doc) alivamiwa akiwa ktk ziara ya maeneo ya kaskazini mjini Cape St. Nicholas, bahati mbaya ikawa kwao wakauawa!!
Jaribio lingine lilifanyika mwaka 1980.

#Kikosi cha wanajeshi (mullatos) kutoka uhamishoni kilitia nanga pwani kutoka Dominica kwa boti ndogo. Lengo kumpindua BABY DOC, lkn kilipigwa vibaya mno na TONTON wakisaidiana na jeshi la Haiti.

#Tafadhali unayesoma huu Uzi FOLLOW ME 🙏
#Mwaka 1982 kikundi cha watu 17 kikiongozwa na mmiliki wa karakana ya TORTUGA iliokuwa pwani ya Haiti kilijaribu mapinduzi wote walikamatwa na kupigwa risasi hadharani
#Ukandamizaji wa kisiasa kwa wapinzani ulikiwa mkubwa ndio maana unaona kulikuwa na majaribio haya ya mapinduzi
Mnamo 1980 "Baby Doc'' alimuoa MICHÈLE BENNETT, binti msomi na mtoto wa mfanyabiashara mkubwa wa zao la kahawa nchini Haiti.

#Unaambiwa alitumia gharama ya US$ 2M kufanya sherehe na kuingia ktk kitabu cha Guinness of World Records km harusi ya gharama kubwa zaidi kuwahi kufanywa ImageImage
#Mwaka 1984 ulifanyika uchaguz wa wawakilishi viti 59 vya Bunge, hakuna wagombea wa upinzan walioruhusiwa kushiriki uchaguz huo.Hata majina ya viongozi wa vyama pinzani waliokuwemo bunge lililopita yalifutwa ktk karatasi za kupigia kura na kutishiwa kukamatwa kwa makosa ya uhaini
Hata GRÉGOIRE EUGÈNE kiongozi wa chama kikuu cha upinzani ambaye awali alikuwa uhamishoni New York alizuiwa kurudi. Wengine km SILVIO CLAUDE alikamatwa na kuteswa pamoja na wafuasi wake 70. Ni raia wachache waliopiga kura na serikali ilikataa kusema hata idadi ya waliopiga kura.
Mikutano michache iliitishwa kupinga uchaguzi iliofanyika lakini Baby Doc alifungua vikosi vyake vikawafurusha mitaa yote na kila aliyeonekana kupinga uchagizi alikamatwa na kufunga kifungo cha maisha gerezani.
Hata jumuiya za kimataifa zilipojaribu kupaza sauti alizipa masikio.
Tuendelee 👇👇
Uongozi wake uligubikwa na ukandamizaji, mauaji, uminywaji wa demokrasia na kukosekana kwa uhuru wa kisiasa.
#Haiti ilijikuta likirudi miaka 300 nyuma, wasomi wengi walikimbia nchi, idadi ya wasiojua kusoma na kuandika ikaongezeka, hali ngumu ya maisha na magonjwa yakaongezeka.
Sekta ya utalii iliharibiwa na wagonjwa wa UKIMWI waliongezeka.
#Mwaka 1985 wakulima walikuwa wakizalisha 43% tu ya kahawa iliyolimwa miaka ya 1960's. Barabara za miji ziligeuka kuwa makorongo, umeme ndio usiseme kabisa, ushuru wa ovyo na kiholela pamoja na ufisadi ukashamiri.
#Mwanzoni mwa Februari mwaka 1986 ghasia ziliongezeka ktk miji yote nchini mpk jeshi lilizidiwa kutokana na machafuko makubwa. BABY DOC Akaogopa, akaona maisha yake yapo hatarini akakimbilia Paris kwa ndege ya kubeba mizigo ya Marekani, yeye na familia yake na wasaidizi wake 17
Ufaransa ilimpa hifadhi ya muda, lakini baadae ilikitaka chama cha Duvalier kumtafutia mahali pengine pa kukimbilia. Ubaya ni kuwa hakuna nchi yoyote iliyokubali kuwahifadhi.
Alijaribu kuomba Political asylum lkn hakukubaliwa, akaishi uhamishoni tena maisha ya kifahari.
Mnamo 19 Juni 1990 alipewa talaka mke wake MICHÈLE BENNETT.
Alipoteza utajiri wake mwingi baada ya kugawana mali na mke wake mwaka 1993.

Akiwa Paris raia mmoja alifungua kesi mahakamani na kumshitaki Jean-Claude Duvalier km #mhamiaji haramu lkn mashtaka yake yalitupiliwa mbali
Mnamo 1998 GÉRALD BLONCOURT mpiga picha raia wa Haiti, alimshitaki ili akamatwe huko Paris, Lkn wizara ya mambo ya ndani Ufaransa ilisema haiwezi kufanya hivyo kwa7bu ya sheria mpya (Schengen Agreement act) iliyotungwa karibuni imekufuta udhibiti wa mpaka kati yake nchi zingine
#Ktk siasa za Haiti baada ya kukimbia tuweke PAUSE kidogo ili nimalizie kuelezea historia ya huyu mwamba JEAN-CLAUDE DUVALIER alimaarufu "Baby Doc"

Mwaka 2004 alitajwa kwenye jarida moja nchini Marekani kuwa miongoni mwa viongozi wala rushwa duniani "Global Corruption report"
Akishika nafasi ya 6 kwa kuiba zaidi ya US$ 800M nyuma ya viongozi wengine wawili SLOBODAN MILOSEVIC (3rd President of Yugoslavia) 1997/2000 na ALBERTO FUJIMORE (President of Peru) 1990/2000.

Mwaka 2007 Uswizi ilikataa kumfungulia akaunti zake za Benki alizokuwa amehifadhi pesa.
Mwaka 2010 mahakama ya Uswizi ikakubali kufungulia akaunti zake, na kipindi hiki kilikuwa cha kampeni Haiti, baadae alitangaza kurejea nchini mwake ambapo wengi walihisi anataka kurudi ili agombee urais.
Mnamo 16 Januari 2011, Mbabe BABY DOC alirejea Haiti kutoka uhamishoni.
Alipotua Airport alisema "Today I returned to my homeplace, But I'm not here for Politics, I'm here for reconstruction of Haiti." Na siku moja baada ya kurejea alikamatwa akiwa hotelini kwa tuhuma za rushwa, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, kesho yake akatoka kwa dhamana.
22 Septemba 2011 taratibu za kisheria zilionekana kutokamilika kipindi hicho akiishi ktk nyumba moja ya kifahari Port-au-Prince lkn chini ya kizuizi cha kutosafiri nje.

#Mnamo Trh 30 Januari 2012, ilitangazwa Duvalier atafikishwa mahakamani kukabiliana na mashtaka ya ufisadi.
Kutokana na rais aliyekuwepo madarakani kutohudhuria mahakamani zaidi ya mara 3 kwa ajili ya kutoa ushahidi, Mahakama iliendelea kumpa dhamana kwa masharti ya kuripoti kila baada ya siku 60 mahakamani, na Feb 28, 2013 alifutiwa rasmi mashtaka ya kesi zake zote na kuachiliwa huru
DUVALIER alikuwa na uwezo wa kuongea Lugha kadhas kwa ufasaha, ambazo ni Kifaransa, Kihispaniola, Kiingereza na Lugha mama za Taifa lake 6 (Haitian Creoles.

Na mnamo Tarehe 04 Oktoba 2014 mwamba JEAN-CLAUDE DUVALIER almaarufu "BABY DOC'' alifariki dunia kwa maradhi ya moyo. ImageImageImage
Kufuatia anguko la serikali iliyoongozwa na JEAN-CLAUDE DUVALIER ambaye alikimbia nchi na familia yake mnamo 1986, Lut. Gen HENRI NAMPHY alichukua madaraka kama rais wa muda. Akaunda Baraza linaloundwa na raia 6 pamoja na wanajeshi, akaahidi kufanyika uchaguzi huru na wa haki.
#NAMPHY akaingia ikulu.

Wiki chache mwanzoni mwa uongozi wake Wahaiti walianza ghasia na uporaji.
Machi 1986 ghasia zikawa kubwa mji mkuu Port-au-Prince, ikapelekea waziri wa sheria akajiuzulu na Namphy akawafukuza mawaziri wengine 03 waliokuwa na uhusiano wa karibu na Duvalier.
Baraza jipya likapata wkt mgumu ktk kufanya maamuzi hasa kwenye kutekeleza majukumu yake kimamlaka kwa sababu ya migomo ya mara kwa mara na maandamano. Uchaguzi wa bunge uliofanyika Oktoba ili kuandaa rasimu ya katiba ulionyesha umma ndio una mustakabali wa kisiasa wa nchi hiyo.
Uchaguzi wa rais ulifanyika 1987 ukagubikwa na kasoro nyingi ikiwemo mauaji ya wapiga kura kadhaa.

#Atangazwa LESLIE MANIGAT ameshinda urais kwa 50.29%. Ijapokuwa ilionekana idadi ya wapiga kura ilikuwa chini ya 10%, Lkn wanahistoria huona uchaguzi huu ulikuwa wa kidemokrasia.
MANIGAT aliapishwa kuwa rais Februari 7, 1988 na akamteua MARTIAL CÉLESTIN kuwa Waziri Mkuu.
#Mnamo Trh 20 Juni 1988 HENRI NAMPHY akampindua tena MANIGAT kwa kisingizio kuwa hakushinda kihalali, akaongoza nchi kijeshi mpk Sept 17, mwaka 1988 alipopinduliwa na Gen. Prosper Avril.
GEN. PROSPER AVRIL alikuwa mdogo kiumri kipindi anaingia madarakani. Sababu iliyomfanya afanye mapinduzi ni mauaji ya St. Jean Bosco 1988 lkn hayakuwa ya kumwaga damu.
Gen Avril aliongoza kwa miaka miwili (1988/90). Akafanyia marekebisho katiba ya Haiti ya 1987 mnamo Machi 1989.
Marekani ikamtaka Gen. AVRIL kupambana na biashara ya madawa ya kulevya ndipo itampa misaada, akakamata wanajeshi waliokuwa wanahusika na ulanguzi wa madawa ikampelekea heshima na umaarufu wake kupungua. Mnamo April 1989 likatokea jaribio la mapinduzi akawakamata wote waliohusika
Makundi ya upinzani yakiongozwa na raia yakaanza kuandamana wakimtaka atimize ahadi yake ya kufanya uchaguzi. Hakujali sauti zao, ilipofika Januari 1990 alisafiri kwenda nchini Taiwan akiwa ziarani akapewa taarifa kuwa kuna watu wanataka kumpindua AVRIL akarudi nchini haraka sana
Baada ya maandamano makubwa ya umma, Avril akarudisha madaraka ya kuongoza nchi kwa mkuu wa majeshi Gen. HÉRARD ABRAHAM mwezi March 10, 1990. Akakimbilia uhamishoni huko Miami Florida baadaye alihamia Dominica alipokataliwa kuingia Haiti 1992, lkn mwaka 1993 alirudi kuishi Haiti.
Mwaka 1995 alikimbilia tena uhamishoni baada ya serikali kutaka kumkamata kufuatia mauaji ya maafisa wa serikali ktk uongozi wake.
#Alikuja kukamatwa mwaka 2001 muda mfupi baada ya JEAN-BERTRAND ARISTIDE kuchaguliwa kuwa Rais, kwa madai alikuwa anapanga njama dhidi ya serikali.
#Aliachiliwa huru 2002 baada ya Mahakama ya Rufaa kutoa kusema serikali haikuwasilisha ushahidi wa kutosha dhidi yake.

#Alikamatwa tena na kushtakiwa kwa kuhusika na mauaji ya wakulima (1990) akahukumiwa. Aliachiliwa baada ya ARISTIDE kuondolewa madarakani ktk mapinduzi ya 2004
Lut. Gen ABRAHAM

Alikaimu urais wa Haiti baada ya Avril kuachia madaraka. Aliachia madaraka siku 3 baadaye. Ndiye kiongozi wa jeshi aliyeachia Ikulu kwa hiari yake mwenyewe.
Aliwahi kuzuia jaribio la mapinduzi na Roger Lafontant na July 02, 1991 alistaafu jeshi na kuhamia USA.
Muendelezo...!!

#Ikumbukwe Lt Gen. Abraham alishika nchi baada ya Gen. AVRIL kumuachia sababu alikuwa Mkuu wa Majeshi (kikatiba) lkn na yeye alikaa Ikulu siku 3 Tu akasema hawezi kuendelea kukaimu urais akaachia kiti, Taifa la Haiti likajikuta ktk wakati mgumu sana. ImageImageImage
#IMAGINE!! Rais kakimbia nchi, na aliyekaimu kuongoza nchi naye hataki tena hicho cheo.
Badala ya Haiti ikawa Hatia sababu ya madaraka. Ikabidi kikatiba aliyekuwa Chief Justice aongoze nchi.Ndipo mwanamama ERTHA PASCAL-TROUILLOT aliyekuwa Jaji mkuu kwa kipindi hicho akaimu urais. Image
ERTHA PASCAL-TROUILLOT (1990/91)

ERTHA alizaliwa Agosti 13, mwaka 1943 huko Pétion-Ville iko nje ya mji mkuu.
#Kihistoria ndiye mwanamke pekee mwenye asili ya Africa aliyewahi kuwa Rais ktk mataifa ya kizungu. Baba yake Thimbles, alikuwa mhunzi wa vyuma, alifariki akiwa mchanga
Mama yake Louise (néeDumornay) alikuwa mshonaji na mpambaji.

Ertha alikuwa mzaliwa wa 9 kati ya watoto kumi. Alipokuwa na umri wa miaka 10, yeye na kaka yake walijiunga na shule ya Lycée François Duvalier na huko ndiko alikutana na ERNEST TROUILLOT aliyekuja kuwa mme wake baadae Image
Ernest Trouillot alikuwa mkubwa kwake (he was 21yrs Old). Alipoanza chuo kikuu, alitamatani kuendelea na masomo ya sayansi lkn mpenzi wake alimshauri asomee sheria ili baadae aingie ktk siasa.
#Mnamo 1971 alipokea Degree yake ya sheria ktk Chuo cha Olecole de'Droit des Gonaïves. Image
Alikuwa wakili wa kwanza mwanamke nchini Haiti.

Akafanya kazi za kisheria kama Jaji ktk mahakama mbalimbali miaka ya 1980 wkt wa udikteta wa Duvalier. Mumewe alikuwa anafanya kazi Benki kuu, yaani ingekuwa ni BongoTz tungesema mme wake alikuwa mfanyakazi wa @BankOfTanzania. Image
Miaka 1975/88, alihudumu ktk mahakama mbalimbali za Serikali km Jaji hadi alipokuja kuteuliwa kuwa JAJI MKUU wa Mahakama ya Juu zaidi (Supreme Court) na kuwa mwanamke wa kwanza na mweusi kushika nafasi hiyo Haiti. Kileo leo namlinganisha na Jaji FABIANA PIERRE-LOUIS (New Jersey) ImageImageImage
#Unaambiwa Ertha Pascal alikuwa mwanamke mwenye akili sana, alitumia ujasiri wake kuamua kesi ngumu alipokuwa Jaji Mkuu. Aliolewa na ERNEST TROUILLOT miezi minne baada ya kula kiapo cha Uwakili, ambapo walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kike 'Yantha'. Mme wake alifariki mwaka 2018.
#Machi 13, 1990 alipewa jukumu la kukaimu kiti cha urais ili kufanya uchaguzi, kwa sababu aliaminika kuwa ndiye mtu pekee angeweza kuandaa na kuleta chaguzi zisizo na vurugu na kweli ikawa hivyo, ambapo JEAN BERTRAND ARISTIDE alichaguliwa kuwa rais kwa ushindi wa 67% ya kura zote Image
#Kwanza tu alipoingia Ikulu alifungua shule na vyuo kuendelea na masomo akiamini elimu ndiyo nyenzo muhimu zaidi kwa mwanafunzi, na siku hiyo hakulala usingizi kabisa kwani aliingia maktaba kupitia majina ya wagombea takribani 40 waliokuwa wanatarajia kugombea kiti cha urais. ImageImage
Kampeni zilifanyika kwa utulivu na amani ndani ya wiki 6 na wagombea 40 walijitosa, ambapo wakuu walikuwa watatu, Padri Jean Bertrand Aristide (bila shaka huyu alikuwa mhaya) wa chama cha FNCD, Marc Bazin wa NADP na Louis Dejoie wa NAIP (huyu ilikuwa mara ya tatu kugombea urais)
Mnamo 16 Dec, 1990 uchaguzi mkuu na wa kidemokrasia tangia Haiti ipate uhuru (1804) ulifanyika chini ya mwanamama Ertha Pascal. Jumla ya wapiga kura 1,640,729 sawa na 50.8% walijitokeza kupiga kati ya 3,271,155 waliojiandikisha kupiga kura na matokeo yalitangazwa Januari 20, 1991
Padre JEAN BERTRAND ARISTIDE wa chama cha FCND ndiye aliyeibuka mshindi wa Urais kwa kupata kura 1,107,125 sawa na 67.48 akifuatiwa na MARC BAZIN aliyepata kura 233,277 sawa na 14.22%

Mfanyabiashara LOUIS DÉJOIE yeye alipata kura 80,057 sawa na 4.88% licha ya kuwa alikuwa mzoefu
Mnamo Tarehe 07 Februari 1991 Padre JEAN BERTRAND ARISTIDE aliapishwa kuwa rais na mwanamama Bi Ertha Pascal-Trouillot akaumaliza mwendo wake.

#Unaambiwa yeye ndiye aliwafungulia njia wanawake, maana baadae wengi walijitokeza kugombea useneta, uwaziri na hata urais nchini humo. ImageImageImage
Cha kushangaza baada ya BERTRAND kuingia ikulu mwanzoni kulitokea jaribio la mapinduzi ambalo lilizimwa, Lkn Bi Ertha Pascal-Trouillot ndiye aliyekamatwa kwambs yeye ndiye alikula njama za kumpindua Rais.

Baadae aliachiliwa na alipotoka aliachana na siasi kisha akuondoka Haiti.
JEAN BERTRAND ARISTIDE

Alikuwa Padri kabla ya kuingia ktk siasa na ndiye Rais pekee aliyechaguliwa kidemokrasia kuliko viongozi wengine waliomtangulia nchini Haiti.

#Amekuwa madarakani:

📋Miezi 8 (1991)
📋Mwaka (1993/1994)
📋Miaka mitatu (2001/2004)

Ana historia ndefu sana👇 ImageImage
TURN ON NOTIFICATION AU RETWEET HUU UZI NA HIYO NDIO APPRECIATION YAKO KWANGU.

BAADA YA NUSU SAA NARUDI

TUMALIZIE PART A
📋Amenduliwa vipindi vyote
📋1st time, alikimbilia Marekani
📋Mzimu wa Baby Doc haumuachi
📋2nd time, akakimbilia Afrika ya Kati
📋Akapelekwa Africa kusini
📋Akaishi huko uhamishoni baadae akarejea Haiti..Yaani ni visanga na nusu.

📍Ilikuwaje?

📍Yupo wapi sahv?

RT & FOLLOW ME Image
ALISTIDE alizaliwa Trh 15 Julai 1953 ktk kijiji cha Port-Salut, Sud huko Haiti. Baada ya kuzaliwa baba yake alifariki dunia akiwa na miezi mitatu.
Baadaye alihamia mjini Port-au-Prince na mama yake na alipofikisha miaka 5 alianza shule kwa ufadhili wa kanisa la Roman Catholic. Image
#Alijiunga na Chuo kikuu cha Notre-Dame huko Cap-Haïtien mpk alipohitimu masomo yake ya dini mnamo 1974.Baadae akaenda masomoni huko La Vega (Rep.Dominica) kabla ya kurudi Haiti kusomea Falsafa ktk chuo cha Grand Séminaire Notre Dame na kozi ya Saikolojia ktk Chuo kikuu cha Haiti Image
Baada ya kuhitimu masomo yake mnamo 1979, Aristide alisafiri kwenda Ulaya akasoma tena nchi za Italia,Ugiriki kisha akaenda Beit Jala (Palestina). Alirudi nchini 1982 kwa kuwekwa kwake wakfu kama kasisi wa Salesian na aliteuliwa kuwa msimamizi wa parokia ndogo huko Port-au-Prince Image
Kati ya 1957/86, Haiti ilitawaliwa na udikteta wa familia ya François "Papa Doc" na Jean-Claude "Baby Doc" Duvalier. Nchi ikawa ktk vitisho na ukandamizaji mkubwa uliovumiliwa na maskini lkn ARISTIDE pekeake ndiye alikosoa utawala wa Duvalier km ilivyo @EmmausAskofu hapa nchini. Image
ALISTIDE hakuogopa uongozi wa kanisa lake huko Vatican na ukizingatia kanisa la Roman Catholic toka 1966 lilikuwa na mgogoro na utawala wa Duvalier kwamba halitateua Maaskofu kutoka Haiti.
Aliendelea kushutumu vikali utawala wa Duvalier kila siku ya jumapili ktk mahubiri yake. Image
Chini ya shinikizo la makasisi wa Salesian ilibidi ARISTIDE apelekwe nchi nyinginge kwa muda miaka mitatu huko Montreal. Mwaka 1985 upinzani mkali dhidi ya utawala wa Duvalier uliongezeka, ndipo Aristide akarudishwa kuhubiri Haiti.
Ktk mahubiri wiki ya Pasaka alitoa waraka uliojulikana "A call to holiness" uliotolewa ktk kanisa kuu la Port-au-Prince na baadaye kusambaa kote nchini Haiti. Ulituma ujumbe kwamba ilitangaza: "Njia ya Wahaiti wale wote wanaokataa utawala wa dhuluma ni njia ya haki na upendo."
ARISTIDE akaendelea na mapambano ikiwemo yale "Ti Legliz movement" ambayo alikuwa kiongozi, na mnamo Septemba 1985 aliteuliwa kwa kanisa la Mt. Jean Bosco kusimamia kigango pembezoni mwa mji huko Port-au-Prince kutokana na itikadi na mafundisho yake (adhabu) kwa waumini wa Roma.
Kutokana na kupungua kwa vijana kanisani, Aristide alianza kupanga kuhudumu ktk misa za vijana za kila wiki. Akaanzisha kituo cha kulelea watoto yatima cha mitaani mnamo 1986 kilichoitwa Lafanmi Selavi [Family is Life]
Alifundisha demokrasia kwa mgongo wa kuhudumia watoto akaanza kuandamwa. Alinusurika majaribio 4 ya mauaji, ikiwemo la ''st.Jean Bosco massacre on 11 Sept 1988" ambapo magaidi waliingia kanisani ktk misa akihubiri wakafyatulia watu risasi na kuua watu 13 na wengine 77 kujeruhiwa.
Yeye alinusurika akajificha.

Baadaye viongozi wa Salesian walimwamuru aondoke Haiti, lkn siku anaondoka makumi ya maelfu ya Wahaiti walizuia kuingia uwanja wa ndege, wakimlilia asiondoke. Mnamo Desemba 1988 ARISTIDE akaonekana alikaidi wito akafukuzwa kutoka jumuiya ya Salesian.
Barua aliyotumiwa alimshtukum kwa shughuli za kisiasa anazozifanya ni uchochezi wa chuki na vurugu kinyume na jukumu lake kama kasisi.

Aristide alikata rufaa juu ya uamuzi huo, akisema: "Kosa ambalo ninashtakiwa ni kosa la kuhubiri chakula kwa wanaume na wanawake wote".
Mwaka 1988 aliwahi kusikika akisema "The solution is revolution, first in the spirit of the Gospel, Jesus could not accept people going hungry. It is a conflict between classes, rich and poor. My role is to preach and organize." akizungumzia msimamo wake na mstakabali wa kanisa.
Mnamo 1994, ARISTIDE aliamua kustaafu upadri baada ya kutomaliza mvutano wa miaka mingi na kanisa lake juu ya ukosoaji wa viongozi waliopo madarakani na siasa kwa ujumla. Alipostafu, alimuoa MILDRED TROUILLOT, ilikuwa 20 Jan, 1996, na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili wa kike.
Akaingia ktk siasa kipindi hicho utawala wa Duvalier ulikuwa umeanguka. Na ktk uchaguzi uliofanyika mnamo Desemba 1990 JEAN BERTRAND ARISTIDE alichaguliwa kuwa rais mpya wa Haiti kwa 67% ya kura na ndio uchaguzi pekee unaotambuliwa kufanyika kwa demokrasia ktk historia ya Haiti. ImageImageImageImage
Siku chake baada ya kuapishwa, kulifanyika jaribio la mapinduzi dhidi yake na ROGER LAFONTANT (kiongozi wa #Tonton_Macoute ktk utawala wa Duvalier), aliyejitangaza rais baada ya Bi Ertha lkn baada ya idadi kubwa ya wafuasi wa Aristide kuandamana jeshi likazima mapinduzi. ImageImage
Mnamo Julai 31, 1991, LAFONTANT akamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali ya Haiti. Aliuawa baadae huko huko gerezani wakati wa mapinduzi mengine yaliyotokea mnamo Septemba 29, 1991.
Mwanzoni alifanya mageuzi makubwa na kupelekea kupata upinzani uliokosolewa na wasomi pamoja na wafanyabiashara nchini. Mwezi July Lt.Gen ABRAHAM aliyekuwa mkuu wa majeshi alistaafu kazi,ndipo akapiga marufuku viongozi kusafiri nje mpk hapo akaunti zao za benki zitakapochunguzwa
#Uhusiano wake na Bunge ulizorota baada kuchelewa kuteua mawaziri na mabalozi. Alipomteuazi rafiki yake wa karibu RENÉ PRÉVAL kuwa Waziri Mkuu alikumbana na ukosoaji mkali kutoka upinzani na kupelekea Bunge kutishia kupiga kura ya kutokuwa na imani na PRÉVAL mnamo Agosti 1991.
Hii ilisababisha watu wasiopungua 2000 kuandamana nje ya Ikulu wakitishia vurugu endapo atashindwa kufanyia maamuzi matakwa yao.
Rais ARISTIDE alipata wkt mgumu, akahisi kuangushwa endapo angeshambulia waandamanaji zaidi akaona anaweza kushtakiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu
Mnamo Sept 1991, Jeshi likafanya mapinduzi dhidi yake likiongozwa na Gen. RAOUL CÉDRAS ambaye alikuwa amepandishwa cheo na ARISTIDE kuwa Mkuu wa Jeshi. Aliondolewa rasmi madarakani 29 Sept, 1991 akakimbilia uhamishoni akanusurika kuuawa baada ya kuokolewa na ubalozi wa Venezuela.
Kwa mujibu wa katiba ya Haiti kifungu cha 149, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu zaidi (Supreme Court) JOSEPH NÉRETTE aliteuliwa kuwa kiongozi wa mpito mpk hapo uchaguzi utakapofanyika ndani ya siku 90, ijapokuwa aliyekuwa na mamlaka yenye nguvu ni mkuu wa majeshi Gen. RAOUL CÉDRAS. ImageImage
Waliongoza mapinduzi walikuwa ni Gen. CÉDRAS, PHILLIPE BIAMBYAND (kiongozi wa kijeshi) na MICHEL FRANÇOIS (Mkuu wa polisi).
#Uchaguzi ulipangwa, lakini ulifutwa chini ya shinikizo kutoka Marekani. ARISTIDE alisema mapinduzi dhidi ya serikali yake yalipangwa na serikali Marekani.
Wengine walioshutumiwa kuhusika na mapinduzi, ni maafisa wa shirika la ujasusi la Haiti (SIN), ambalo lilianzishwa miaka ya 1980 na kupewa ufadhili na Shirika la CIA ili kudhibiti biashara ya madawa ya kulevya, kwasababu inasemekana baada ya mapinduzi ufadhili wa CIA ulisitushwa
Operations ya kuwasaka wafuasi wa Aristide ilianzishwa kote nchini na EMMANUEL CONSTANT (alikuwa mtoa siri CIA kwa kulipwa toka 1992). Mnamo 1993, Constant alianzisha kikundi kilichoitwa FRAPH kwa mgongo wa kuchangia maendeleo ya Haiti lengo likiwa ni kuwaua wafuasi wa Aristide.
ARISTIDE akakaa uhamishoni Venezuela na kisha alikwenda Marekani, alifanya kazi ili kutafuta mahusiano mema na washirika kimataifa. Akiwa Marekani @UmojaWaMataifa uliwataka viongozi wa mapinduzi kuachia madaraka, ikawa pigo kubwa kwa uchumi wa Haiti uliokuwa tayari umeshaporomoka
George H W. Bush akiwa Rais akatoa msamaha na kuondoa kizuizi kwa kampuni za Marekani zilizokuwa zikifanya biashara nchini Haiti na alipokuja Bill Clinton akaongeza msamaha huo.
#Kwa kukufungua macho mapinduzi ya Aristide yalisababishwa na vita ya yake dhidi ya madawa ya kulevya
Ilikuwa ni biashara ambayo inawapa faida kubwa wafanyabiashara wengi kupitia kampuni nyingi za Marekani. Aristide alisema harakati zake za kukamata wafanyabiashara wa dawa za kulevya ndio zilisababisha mapinduzi na maafisa waliotekeleza tukio lile akiwemo CÉDRAS ni miongoni mwao.
Mwaka 1994 Jeshi la Marekani likashikilia nchi viongozi waliohusika na mapinduzi wakaogopa kukamatwa, ndipo Gen. RAUOL CÉDRAS ambaye aliongoza mapinduzi ya kumng'oa Rais JEAN BERTRAND ARISTIDE madarakani akiwa na familia yake akakimbilia uhamishoni huko nchini Panama. ImageImage
Kukatokea maandamano makubwa mjini New York yaliyoungwa mkono wafuasi wa ARISTIDE, inakadiriwa waandamanaji walikuwa zaidi ya watu 250,000. Waandamanaji waliendelea siku hadi siku wakimtaka BILL CLINTON atimize ahadi yake ktk uchaguzi, kwamba atamrudisha ARISTIDE nchini kwake. ImageImage
Kutokana na azimio namba 940 la kikao cha Baraza la usalama la @UmojaWaMataifa kilichoketi mnamo Julai 31, 1993 lilishawishi Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini Haiti na Rais BILL CLINTON mnamo 05 Oktoba, 1994 alimrudisha ARISTIDE nchi kwake ili kumalizia muda wake wa uongozi. Image
Alipokelewa na watu wafuasi wake wengi sans na ARISTIDE mnamo mwaka 1996 alipewa Tuzo na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa. (UNESCO) kwa ajili ya kutoa elimu ya namna ya kupigania Haki za Binadamu. ImageImage
#Aliporejea Haiti aliendelea kuongoza nchi kama Rais na ilipofika Oktoba 30, 1996, JEAN BERTRAND ARISTIDE alivunja chama chake cha zamani cha Organisation Politique Lavalas (OPL), kwa kile alichokiita kukiweka mbali na watu akaunda chama kipya cha kisiasa cha FANMI LAVALAS (FL).
Kuhusu ARISTIDE tuishie hapo kwanza.

Hebu turudi nyuma kipindi ambacho Marekani ilikuwa inashikilia nchi baada ya mapinduzi yaliyotekelezwa na Gen.RAOUL CEDRAS. Baada ya mapinduzi JAJI JOSEPH NERETTE ndiye alikaimu urais, akaongoza kutoka Trh Okt 08, 1991 mpk June 19, mwaka 1992 Image
Kisha akachaguliwa MARC LOUIS BAZIN (aliyekuwa mshindi wa tatu uchaguzi wa 1990)

BAZIN alikuwa ni Afisa wa @WorldBank na aliwahi kufanya kazi @UmojaWaMataifa na Waziri wa Fedha na Uchumi kipindi cha Dikteta wa Jean-Claude Duvalier.

Yeye alikaimu kutoka June 1992 mpk June 1993 Image
Kisha ÉMILE JONASSAINT ambaye alikaimu kati ya June 1993 na Oktoba 12,1994 na kuachia kiti aliporejea ARISTIDE. Mzee huyu ndiye aliyemshinikiza Aristide kuachia madaraka (1991) na alikuwa mwenyekiti wa Bunge la Haiti mwaka 1987. Alifariki dunia Oktoba 24, 1995 akiwa na miaka 82. ImageImage
Tuendelee sasa👇

Baada ya kurudi aliongoza Haiti na kipindi akiwa na chama kipya cha FL.
#Ijapokuwa alikutana changamoto kadhaa lkn alijitahidi kupambana nazo na alifanikiwa kuunganisha watu nchi nzima na kuondoa matabaka yaliyokuwa yamesababishwa na matukio ya miaka ya nyuma
Aliongoza miaka 6 na muhula wake wa kwanza ukaisha.

Mnamo 26 Nov, 2000 ulifanyika uchaguzi mkuu.Baadhi ya vyama vya upinzani vilitengeneza muungano ulioitwa Convergence Démocratique lkn vilisusia uchaguzi huo kutokana na matokeo ya uchaguzi wa Bunge ulikipa FL viti vingi bungeni
Mwaka 2000 watu walijiandikisha wengi lkn waliojitokeza kupiga kura ni watu 2,871,602 sawa na 50% na sababu kubwa ilikuwa ni kujitoa kwa muungano wa vyama vya upinzani (CD)

#Matokeo yalitangazwa na JEAN-BERTRAND ARISTIDE alishinda urais kwa kupata kura 2,632,534 sawa na 91.67 %
HELLOW TOT

RT #Uzi huu (kule juu mwanzoni) ili niumalizie.

Ktk uchaguzi huu kila jumuiya ya Kimataifa ilisema la kwake.
#MFANO: Marekani ilisema ni 10% walipiga kura, Waangalizi wa Kimataifa wao walisema ni 50% huku CNN ilisema ni 60% na zaidi ya 92% walimpigia kura Aristide.
MUHULA WA PILI (2001-2004)

JEAN BERTRAND ARISTIDE aliandelea muhula wa II wa uongozi na kuitaka Ufaransa kuilipa Haiti Fedha kiasi cha US$ 21BIL, pesa ambayo ililipwa na Haiti kiasi cha Faranga 90M za dhahabu mwaka 1847 km adhabu ya mali zilizoachwa na mkoloni huyo nchini kwake.
Naomba nikupe HISTORIA ya HUO MKOPO (US$ 21BILLIONS)

NDG @Fundi_Ntapanta alijaribu kugusia kuwa mojawapo ya sababu inayoipelelea Haiti kubakia ktk umaskini mkubwa na ndiyo hupelelea wanafanya maandamano mara kwa mara tangia wapate uhuru mpk leo.

Nikuombe RT Iwafikie wengi sana.
#Kwanza, IFAHAMIKE kwamba ktk miaka ya 1800 (Colonialism era) Island Hispaniola (Haiti) ilikuwa ni moja ya mataifa machache yaliyokuwa yana uchumi mkubwa kutokana na uzalishaji ktk mashamba makubwa (Large Plantations) ya kahawa, Migomba na chai kwa sababu ilikuwa watu wengi sana. ImageImageImage
Mwaka 1804 Haiti ilipata uhuru kutoka kwa mkoloni (France), nchi nyingi zilikuwa zinafaidika na watumwa waliokuwa wanazalisha mazao mbalimbali Taifa hili. Hazikufurahia kabisa.

Hata THOMAS JEFFERSON aliyekuwa rais wa Marekani ktk miaka hiyo alisitisha kuipatia Haiti misaada.
#Mnamo Oktoba 1806 Haiti iligawanyika kutokana na kifo cha JEAN-JACQUES DESSALINES aliyekuwa mtawala baada ya nchi hiyo kupata uhuru aliyenyongwa akiwa IKULU.
📋Kusini ikawa chini ya Wahaiti wenye mchanganyiko na wazungu (Mullatos)
📋Kaskazini ikawa chini ya Watu weusi (Blacks) ImageImage
📋Mullatos (Southern Parts) ikaongozwa na ALEXANDRE PETION na,

📋Blacks (Northern Parts) ikaongozwa na KING HENRY CHRISTOPHE.

Na wote hawa awali walikuwa viongozi walio-ongoza majeshi (Generals) ya mapinduzi kipindi cha Haiti kujitafutia uhuru kutoka kwa mkoloni (Ufaransa) ImageImageImageImage
Ufaransa bado haikutaka kukubali kuichia koloni lake la Haiti, ikabuni mbinu nyingine mpya ya kuinyonya nchi hiyo.

#Mnamo 1815 Mfalme wa Ufaransa (kwa kipindi hicho) KING LOUIS XVIII, akatuma makamishina wa3 Haiti ili kuwataka viongozi wake kwa hiari waachie uongozi wa nchi hiyo Image
🎼KING HENRY CHRISTOPHE (Black) aliyekuwa Kiongozi wa eneo la kaskazini alikataa kuirudisha ktk mikono ya wakoloni na kurudi utumwani.

🎼 ALEXANDRE PETION (Mullato) aliyekuwa Kiongozi eneo la kusini walipokuwa wazungu wengi akakubali kukaa chini na hao Makamishina wayazungumze.
PETION alikubali kuilipa Ufaransa ili Mfalme wake aiachie ardhi ya Haiti.

KING LOUIS XVIII aliyekuwa mtawala wa Ufaransa alikuwa ni mtawala mpya akimfuata KING NAPOLEON.

#Huyu NAPOLEON mnamo mwaka 1803 aliuza koloni lake LOUISIANA kwa nchi ya Marekani kwa Faranga 15Millions. Image
#HIVYO, ALEXANDRE akakubali kulipa pesa sawa na zile NAPOLEON alizouza Louisiana.

Taarifa kwamba Mtawala wa Eneo la kaskazini KING HENRY amekataa kuachia madaraka zikamfikia LOUIS XVIII
Mfalme LOUIS XVIII akakataa kupokea Ofa aliyopewa na PETION maana alikuwa anataka HAITI Yote.
#Ukumbuke, kipindi hiki ndio United States ilikuwa inaimarika kiuchumi kuliko taifa Lolote. Na ili uonekane Taifa Lenye Uchumi mkubwa basi inatakiwa uwe na hifadhi kubwa ya Almas, Dhahabu, mashamba makubwa na viwanda. Marekani vyote hivi ilikuwa navyo kumbuka ilipata uhuru 1776.
#GHAFLA, mtawala wa Eneo la kusini ALEXANDRE PETION akafariki dunia kwa Ugonjwa wa Manjano.Akaingia JEAN PIERRE BOYER, alipofariki HENRY CHRISTOPHE wa kaskazini akaunganisha maeneo ya kusini na kaskazini ikawa nchi moja Haiti. Akaendeleza mpango wa Petion kuhusu kuilipa Ufaransa Image
KING HENRY wa Kaskazini alifariki mwaka 1820 kwa kujiua mwenyewe kwa kujipiga risasi IKULU.

Mnano 1824 KING CHARLES X akaingia madarakani km mtawala mpya wa Ufaransa. Mnamo 17 April 1825 akatuma kikosi cha wanajeshi nchini Haiti ili kulazimisha JEAN-PIERRE BOYER kuachia madaraka Image
Jeshi lilikuwa meli 14 za kivita na mizinga 500 pamoja na makamishina (viongozi) wawili.

#Walifika nchini Haiti mnamo 11 Julai 1825 na ilibidi Rais JEAN-PIERRE BOYER awaombe wakae chini wazungumze, ndipo akakubali kusaini mkataba kuilipa Ufaransa Faranga 150Mil za dhahabu. Image
#Ufaransa iliilazimisha Haiti ilipe pesa hizo kwa sababu:
📋Fidia ya watumwa,
📋Fidia ya mashamba,
📋Fidia ya nyumba ilizojenga nchini humo.
Rais JEAN-PIERRE BOYER akakopa baadhi ya benki za Ufaransa na @Citibank ya Marekani US$ 30Millions sawa na Faranga 60M za dhahabu Akalipa!! ImageImage
Pesa yote iliyokuwa inadaiwa ni 150Mil Gold Francs sawa na bajeti ya miaka 10.

Deni likabaki Francs 90M (US$21BIL).

Ufaransa ikaendelea kuidai deni lililobaki na kila mwaka Serikali ya Haiti ilikuwa inalipa US$ 9Millions.

#Mnamo 1838, Ufaransa ilituma tena Jeshi lenye meli 12
Rais alikuwa STENIO VINCENT, naye alikaa chini na viongozi waliokuwa wametumwa kuiwakilisha Ufaransa. Walizungumza mpk mwisho wakakubaliana kulipa deni lililobaki. Rais akasaini mkataba wa kulipa "Treaty of Friendship" (1838) kwa amani.

Haiti iliendelea kulipa huo mkopo mpk👇
Mnamo 1920 LOUIS BORNO aliingia madarakan akalipa mkopo wa US$ 23M uliokadiriwa sawa na Budget ya miaka 4.

#Mkopo wote wa Haiti ulimalizika kulipwa na Rais DUMARSAIS ESTIME (1947), Lkn alipoingia dikteta Duvalier alianza kukopa, na mpk sasa Haiti inadaiwa zaidi ya US$ 1.25BIL
Hilo ni deni la nje (External Debit) Tu.

Hivyo basi, Baada ya Rais JEAN BERTRAND ARISTIDE kurejea madarakani mwaka 2003 alianza kudai Serikali ya Ufaransa irudishe Fedha kiasi cha Faranga 90M za dhahabu sawa na US$ 21Millions ilizolipwa na Haiti kutoka 1825 mpk 1947. Image
Kutokana na hilo mnamo 26 Februari 2004 kulitokea tena mapinduzi yaliyomuondoa madarakani JEAN BERTRAND ARISTIDE. Baraza la Usalama la @UmojaWaMataifa ambalo Ufaransa ni mwanachama wa kudumu, lilikaa kikao baada ya ombi kutoka @CARICOMorg kutuma Jeshi kulinda amani nchini Haiti
Ufaransa ilikataa kupeleka Jeshi lake na siku tatu baadae ARISTIDE alijiuzulu, muda mchache baada ya @UmojaWaMataifa kupiga kura kwa kauli moja kutuma wanalinda amani Haiti
Mwaka 2015 licha ya Rais FRANÇOIS HOLLANDE (France) kusamehe madeni Haiti alisema hawezi kulipa fedha hizo.
Tuendelee_______&&

JEAN-BERTRAND ARISTIDE baada ya kuchaguliwa muhula wa II

#Miaka ya 2001 na 2004 vikundi vya waasi wanajeshi wa zamani wa nchi walitekekeleza mauaji kadhaa kwa raia, maafisa wa serikali pamoja na wanachama wa LAVALAS chama kilichokuwa kinaongozwa na ARISTIDE.
Februari 2004 akauawa AMIOT METAYET kiongozi wa genge la magaidi baada ya majibizano makali ya risasi na polisi wa Haiti huko Gonaives. BUTEUR METAYET (kaka yake Amiot) alimlaumu Rais Aristide kwa mauaji ya ndugu yake, kisha ndipo akajiunga na kikosi cha mapinduzi.
Kikosi hicho kilikuwa kinaitwa "Revolutionary Artibonite Resistance Front" kilichokuwa na magaidi, wanajeshi walioasi, walanguzi wa madawa ya kulevya kikiongozwa na GUY PHILLIPE mwanajeshi aliyewahi kuwa mkuu wa Polisi zamani pamoja na LOUIS JODEL CHAMBLAIN wa kikosi cha FRAPH.
Waasi walianzia kudhibiti maeneo ya Kaskazini na kisha wakazingira mji mkuu Port-au-Prince. Marekani ikamtaka ajiuzulu kuepusha mauaji ya raia wasio na hatia.
Mnamo 28 Februari 2004 akiwa na bodyguard wake FRANZ GABRIEL akakimbia nchi kwa msaada wa ubalozi wa Canada na Ufaransa.
Kikosi maalum wamevalia nguo za jeshi la Marekani ndicho kiliwapeleka Airport lkn wakiwa chini ya ulinzi wa usalama wa Canada. Baada ya Aristide kuondolewa Haiti, matukio ya uporaji na mauaji viliisha. Nchi ikawa chini ya polisi wa Haiti, pamoja na waasi wenye silaha.
Rais ARISTIDE akasafirishwa mpk Central Africa, kisha familia yake ikasafirishwa kutoka Haiti kwenda huko ikisindikizwa na SHARON HAY-WEBSTER aliyetumwa na P. J PATTERSON waziri mkuu wa Jamaica, ambapo baadae serikali ya Jamaica ilimpa hifadhi kabla ya kusafirishwa Africa Kusini.
ARISTIDE baadaye alisema kuwa Ufaransa na Marekani zilihusika na kile alikiita "utekaji nyara" ambao ulimchukua kutoka Haiti kwenda Afrika Kusini kupitia Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo baadae maafisa walisema hifadhi yake ya kisiasi ilipitishwa na Marekani, Ufaransa na Gabon.
Mnamo 1 Machi 2004, mbunge wa Bunge la Marekani, MAXINE WATERS (D-CA) pamoja na rafiki yake Aristide, RANDALL ROBINSON, walisema kwamba ARISTIDE aliwaambia kuwa alilazimishwa kujiuzulu na wanajeshi wa Marekani waliokuwa na silaha kisha wakamteka nyara yeya pamoja na mlinzi wake.
ARISTIDE UHAMISHONI (2004-11)

Mwaka 2004 baada ya kupelekwa uhamishoni nchini Africa kusini pamoja familia yake, alikaribishwa vizuri tena mawaziri kadhaa, wanadiplomasia 20 akapewa mlinzi maalum aliyekuwa analipwa mshahara na serikali ya Afrika Kusini. ImageImage
ARISTIDE aliishi na familia yake ktk nyumba ya serikali mji mkuu Pretoria. Akiwa kusini alijiunga na Chuo Kikuu cha Afrika Kusini akisomea lugha ya Kizulu na Trh 25 Aprili 2007, alitunukiwa shahada ya uzamivu (PhD) katika lugha za Kiafrika. Aliishi huko kwa kipindi kirefu sana.
Mnamo 21 Desemba 2007, akiwa @SouthAfrica kuelekea maadhimisho ya uhuru wa Haiti, ARISTIDE alihotubia ikiwa hotuba yake ya nne tangia aishi uhamishoni, ambapo alikosoa uchaguzi wa urais mwaka 2006 uliompa RENE PRÉVAL ushindi na kudai ulikuwa uhaini ktk serikali ya watu wa Haiti. Image
"Since the election, some high-ranking members of Lavalas have been targets for violence. Lovinsky Pierre-Antoine, a leading human rights organizer in Haiti and a member of Lavalas, disappeared in August 2007, his whereabouts remain unknown."
"Like many protesters, he [Wilson Mesilien coordinator of the pro-Aristide 30 September Foundation] wore a T-shirt demanding the return of foundation leader Lovinsky, a human rights activist and critic of both U.N. and U.S involvement in Haiti who disappeared in August." Alisema.
Mnamo 2 Agosti 2006 ktk mkutano na maafisa wa Idara ya Usalama nchini Marekani, mwanadiplomasia wa zamani wa Guatemala EDMOND MULET, wakati huo akiwa Mkuu wa MINUSTAH alihimiza Marekani kuchukua hatua za kisheria dhidi ya ARISTIDE kuzuia asipate kibali cha kurudi Haiti.
Kwa ushauri wa MULET, Katibu Mkuu wa UN @KofiAnnan alikubaliana nao na kumtaka Rais THABO MBEKI kuhakikisha ARISTIDE haondoki nchini humo mpk hapo hapo atakapopewa taarifa nyingine.

Balozi wa US nchini Haiti alisema ktk uchaguzi wa 2004 km ARISTIDE angekuwepo angeshinda urais.
Baada ya aliyekuwa rafiki wa zamani wa Aristide, RENÉ PRÉVAL kuchaguliwa kuwa rais wa Haiti mwaka 2006, mnamo Desemba 16, 2009, waandamanaji maelfu waliandamana wakitaka Aristide arudishwe Haiti na kupinga kutengwa kwa chama cha Aristide cha Fanmi Lavalas kwenye uchaguzi uliopita Image
Mwanzoni kabisa mwa mwaka 2010 kukatokea Tetemeko kubwa la Ardhi.

Mnamo Januari 12, 2010, Aristide alituma salamu za pole kwa wahanga wa tetemeko la ardhi huko Haiti masaa machache tu baada ya kutokea, na akasema kwamba alitamani kurudi nchini mwake ili kusaidiana kuijenga nchi.
Mnamo Februari 2011, Aristide alitangaza atarudi Haiti ndani ya siku chache baada ya serikali ya Haiti kuondoa vizuizi kwake kwa kupokea hati yake ya kusafiria kwenda nchini humoHaiti.

#Rasmi Trh 17 Machi 2011, ARISTIDE aliondoka uhamishoni nchini Africa kusini na kuelekea Haiti ImageImage
Rais @BarackObama wa Marekani alimuomba rais JACOB ZUMA kuchelewesha kibali cha ARISTIDE kurudi Haiti (asiende kabla ya uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20), ambapo chama cha Aristide kilizuiwa kushiriki uchaguzi huo akihofia kurudi kwake kunaweza kuleta vurugu.
Lkn kutokana na maandamano makubwa Haiti aliruhusuwa kuondoka kwenda nchini kwake.

#Na siku ya Ijumaa 18 Machi 2011, akiwa na mke pamoja na wanae na walinzi wake waliwasili ktk uwanja wa ndege Port-au-Prince na kulakiwa na maelfu ya wafuasi mithili ya @TunduALissu alivyokuja. ImageImage
Alihutubia umati mkubwa uliokuwa uwanja wa ndege na kusema:

"Kutengwa kwa Fanmi Lavalas ni kutengwa kwa Wahaiti. Mapinduzi ya mwaka 1804, yalikuwa ya kumaliza utumwa nchini. Je, Leo mnaweza kumaliza vifungo vya uhamishoni na mapinduzi ya kisiasa, kipindi hicho amani ikitawala?". Image
Baada ya Aristide kurudi Haiti aliacha kujihusisha na siasa.

Mnamo 12 Sept 2014, Aristide alitumiwa waranti ya kukamatwa na JAJI LAMARRE BELZAIRE kwa ajili uchunguzi wa ufisadi.Lkn Mawakili wa Aristide na wafuasi wa FL walihoji uhalali wa amri ya jaji chini ya sheria za Haiti.
#inasemekana ktk uchaguzi wa urais wa 1991, 2000, 1995 na 2006, idadi ya watu waliopiga kura ilikuwa karibu 60-70%. Lkn ktk miaka iliyofuata kutokana tetemeko la ardhi la 2010, idadi ya waliojitokeza ktk chaguzi ilipungua sana hadi 20% na ndio kipindi mrengo wa kulia uliongezeka.
Hebu tutizame kilichofanyika ktk utawala wake.

📋Aliboresha huduma za afya,
📋Aliongeza uelewa ktk kielimu,
📋Alitetea haki za binadamu,
📋marufuku kuvunja haki za binadamu,
📋Alizuia majeshi kuonea raia,
📋Alihubiri uhuru raia popote alipo,
📋Aliongeza mishahara mara mbili,
#KINGINE:

📋Aligawa chakula familia maskini
📋Aligawia wanavijiji boti za uvuvi,
📋Alijenga makazi ya bei rahisi,
📋Alipunguza Ufisadi serikalini,
📋Alijenga S/Msingi mpya 195
📋Alijenga Sekondari mpya 104 (awali zilikuwa 34),
📋Watoto 72% walijiunga na shule
📋Madaktari 573
Mengine__&&

📋Alipunguza urasimu ktk nchi,
📋Aliongeza 55% Adult Literate rate
📋Watu (adults) wazima zaidi 300,000 walipata elimu bure.
📋Alipunguza vifo kwa watoto wachanga
📋Alipunguza utapiamlo na
📋Alipendekeza jeshi la raia (civilian police force).
JEAN-BERTRAND ARISTIDEyupo mpk sasa nitaelezea mbele anachofanya. Tuishie hapo hebu turudi tuangalie alivyopinduliwa 2004 kwa mara ya pili nani alishika nchi na ilikuwaje.

BONIFACE ALEXANDRE

#Alikaimu kwa muda Urais wa Haiti kutoka 2004 hadi 2006 baada ya Aristide kuachia urais ImageImage
Alizaliwa 31 July 1936, alilelewa na mjomba wake, Martial Célestin. Akasomea sheria, akatumikia mahakama kadhaa Port-au-Prince kwa takribani miaka 25 kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji ktk Mahakama Kuu (1992). Mwaka 2002 Rais Aristide alimteua kuwa JAJI MKUU wa Mahakama ya Juu zaidi
Kufuatia Alexandre kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu zaidi (Supreme Court) alikaimu urais kwa muda. Wkt wa uongozi wake shirika @amnesty liliripoti matumizi mabaya ya nguvu kwa polisi, mauaji ya kiholela, utekaji nyara na watu 40 na zaidi walifungwa bila kufikishwa mahakamani.
Alimteua GÉRARD LATORTUE kuwa waziri mkuu wasaidiane kuongoza nchi na aliachia madaraka 14 Mei 2006 baada ya RENÉ PRÉVAL kushindi wa uchaguzi wa rais Februari 2006 na kuapishwa kuwa rais wa Haiti.

Alexandre alikuwa mpwa wake waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo, MARTIAL CÉLESTIN. Image
RENÉ PRÉVAL

Prevail ni rais wa pili nchini Haiti kuondoka madarakani kwa kumaliza kwa kipindi chake cha uongozi bila kuuawa au kupinduliawa. Alizaliwa April 17, 1943 huko Marmelade, akasomea kilimo ktk chuo cha Gembloux kisha akajiunga na chuo kikuu cha Leuven nchini Ubeligiji. ImageImage
Alipotoka Leuven Belgium alijiunga na chuo kikuu cha Pisain Pisa huko Italia ambako alisomea Geothermal Sciences. Baadae aliondoka Haiti na familia yake mwaka 1963. Baba yake pia alikuwa mtaalam wa kilimo na waziri wa kilimo ktk serikali ya Gen. MAGLOIRE mtangulizi wa Duvalier.
Aliondoka Haiti kwa sababu historia yake ya zamani kisiasa (alikuwa mpinzani), Baba yake Prevail pia aliwahi kufanya kazi na mashirika ya @UN barani Afrika. PRÉVAL alikaa uhamishoni mpk alipomaliza muda wake dikteta Jean-Claude Duvalier, ndipo alirudi nchini Haiti.
Aliishi huko Brooklyn (NYC) takribani miaka mitano akifanya kazi kama mhudumu wa mkahawa. PRÉVAL aliporudi Haiti alipata kazi ktk Taasisi ya umma ya Rasilimali za Madini (National Institute of Mineral Resources). Mwaka 1988 alifungua kiwanda cha kuoka mikate mjini Port-au-Prince.
Wkt PREVAIL akiendesha kampuni yake, alikuwa anajihusha ktk shughuli za kisiasa na kutoa michango kama vile mikate ktk kituo cha watoto yatima cha JEAN-BERTRAND ARISTIDE na kuimarisha uhusiano wao.Baada ya uchaguzi 1990 ambao ARISTIDE alishinda, PRÉVAL aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu
Nafasi aliyohudumu kutoka Februari 13 hadi Oktoba 11, 1991, alipokimbilia uhamishoni kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Septemba 30, 1991.
Mnamo Desemba 6, 2009, PRÉVAL alimuoa ELISABETH DÉBROSSE DELATOUR aliyekuwa mjane wa LESLIE DELATOUR, Gavana wa zamani wa benki kuu ya Haiti.
Aliongeza wake wawili, Bi GUERDA BENOIT na SOLANGE LAFONTANT, ambao wote baadae waliachana.

#Mnamo mwaka 1996 Préval alichaguliwa rais kwa kipindi cha miaka 5 kwa kura 88% akiwa rais wa pili kuchaguliwa kidemokrasia ktk historia ya miaka 191 tangia Haiti kuwa taifa huru.
Muhula wa II aligombea tena km mgombea wa #Lespwa ktk uchaguzi wa urais wa mwaka 2006.

Matokeo ya uchaguzi yaliyotolewa mnamo Februari 9 yalionyesha kwamba alishinda kwa 60% ya kura, lkn baadae matokeo yatangazwa upya kwamba awali walikosea ikaonekana alipata kura chini ya 50%.
lkapelekea kutolewa maamuzi kwamba uchaguzi urudiwe upya. Siku chache baadae kulizuka maandamano mjini Port-au-Prince na baadae miji mingine ya Haiti.

PRÉVAL alidai kulikuwa na udanganyifu ktk zoezi la kuhesabu kura akataka atangazwe mshindi wa urasi ktk duru ile kwanza kabisa.
Waandamanaji waliharibu miji kwa matukio ya uhalifu ikiwemo kuchoma hoteli ya kifahari yenye hadhi ya nyota 5 (Montana Hotel) iliyoko Pétion-Ville, wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ya awali. Na Feb 16, 2006, RENÉ PRÉVAL alitangazwa mshindi wa urais kwa 51.15% ya kura. ImageImage
Mnamo Mei 14, mwaka 2006 alikula kiapo cha urais na baada ya kuapishwa alisisitiza umoja, akisema kwamba mgawanyiko umekuwa shida kuu ya Haiti na kuwaomba wananchi waungane kufanya kazi pamoja.

Mei 17 alimteua tena Bw. JACQUES-OUDOUARD ALEXIS kuwa Waziri Mkuu ktk Muhula wa Pili.
Baada ya kuchukua madaraka ofisi, PRÉVAL alisaini mkataba wa makubaliano ya mafuta na nchi ya Venezuela, baadae alisafiri kwenda Marekani, Cuba na Ufaransa. Alijitahidi kutoa misaada kwa watu masikini na aliungwa mkono sana haswa ktk maeneo maskini zaidi ya mjini Port-au-Prince.
Ingawa maskini wengi walidai kwamba Rais wa zamani ARISTIDE aruhusiwe kurudi, pamoja na wafanyabiashara waliofukuzwa na serikali ya LATORTUE. Préval aliahidi kujenga mfumo mkubwa wa barabara ambao utaongeza biashara na usafirishaji kote nchini.
Haiti chini ya PRÉVAL ilishirikiana kidiplomasia na kindugu na mataifa mengine ya Amerika Kusini. Ushirikiano ambao ulipelekea nchi hiyo kupata msaada mwingi ambayo walihitajika, hata mgogoro wa kidiplomasia na Venezuela uliisha kabisa zikaanza kushirikiana ktk masuala mbalimbali
Urafiki wao na rais wa Venezuela HUGO CHÁVEZAND ulipelekea nchi hizo kuingia makubaliano ya kiuchumi ambapo Venezuela kuijengea Haiti mitambo minne ya kufua umeme (mtambo wa megawatts 40, 30, na miwili ya megawati mbili 15). Jingine ni usafishaji wa mafuta mapipa 10,000 kwa siku.
Misaada ya Venezuela kwa Haiti kihistoria ilianzishwa kipindi Haiti ilipopata uhuru baada SIMÓN BOLÍVAR na kutoa wanajeshi wake kusaidia ukombozi wa nchi nyingi kipindi cha kutafuta uhuru toka kwa mkoloni kwa bara zima la Amerika Kusini.
FIDEL CASTRO, RAUL CASTRO na pamoja na viongozi wengine wakidiplomasia wa Cuba kama Makamu wa Rais ESTEBAN LAZO HERNANDEZ waliishukuru Haiti kwa kupiga kura mfululizo ktk Mkutano Mkuu wa @UmojaWaMataifa kufuatia vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba.
Mahusiano ya kidiplomasia ya Préval na mataifa mengine ya Amerika Kusini yalifungua fursa nyingi za kiuchumi kwa Haiti. PRÉVAL alikutana na viongozi wengi km vile FIDEL CASTRO, EVO MORALES wa Bolivia, MARTÍN TORRIJOS wa Panama, na LEONEL FERNÁNDEZ wa Jamhuri ya Dominica.
Uhusiano na Dominica uliimarishwa kutokana na PRÉVAL kufuta migogoro ya kisiasa baina yao iliyosababishwa na watangulizi wake. Dominica ilikuwa Taifa la kigeni la kwanza kuizuru Haiti, kisha Préval aliitembelea Marekani ambapo George W. Bush alimpongeza kwa kuchaguliwa tena.
Mapema Aprili 2008, ghasia kubwa zilizuka juu ya gharama kubwa ya chakula, tangu mwaka 2007 bei za vyakula km vile mchele zilipanda kwa karibia 50%. Wakati ghasia hizo zikiendelea, waandamanaji walishambulia ikulu ya rais Aprili 8, lkn vikosi vya @UN viliwatawanya ktk eneo hilo.
Mnamo Aprili 9 rais PRÉVAL alijaribu kutuliza ghasia kwa kuzungumza na waandamanaji, ambapo alisema:
"bei kubwa ya chakula ni shida kote ulimwenguni, lkn na shida hiyo haitatatuliwa kwa kuharibu maduka". Kisha akaamuru Polisi wa Haiti na wanajeshi wa UN kuzuia vitendo vya uporaji
Licha ya waandamanaji kudai kuondolewa ushuru wote wa uagizaji wa chakula, lkn PRÉVAL alisema asingeweza kufanya hivyo kwa7bu pesa zinahitajika sana.
Na kuahidi kuongeza uzalishaji wa chakula nchini Haiti ili nchi isitegemee uagizaji kutoka nje, lkn hilo halikutuliza ghasia.
Mnamo Aprili 12, Bunge la Seneti lilipiga kura kumwondoa Waziri Mkuu ALEXIS ktk nafasi hiyo kwa sababu alikuwa hasaidii wananchi wake kutokana na kupandisha kodi kwa vyakula, na rais PRÉVAL naye akatangaza kuwa bei kwa kila kilo 23 za mchele itapunguzwa kutoka US$ 51 hadi US$ 43.
PRÉVAL aliongeza kuwa mchele huo utafadhiliwa na misaada ya kimataifa na sekta binafsi ilikuwa tayari kupunguza bei kwa US$ 3. Akaahidi kwenda kutafuta msaada nchini Venezuela ktk kuboresha hali ya uchumi.

#Mnamo Januari 12 mwaka 2010 Taifa hilo likakumbwa na tetemeko la ardhi
Tetemeko ambalo lilikuwa na ukubwa wa magnitude 7.0 halijawahi kutokea tangia nchi hiyo ipate uhuru. Makadirio idadi ya vifo ni kati ya watu 100,000 hadi 316,000 na wakijeruhiwa ndio wengi zaidi. Watu walipoteza makazi maana nyumba nyingi zilianguka vibaya hata ikulu ya rais. ImageImageImageImage
Préval na mkewe walifanikiwa kuondoka kwenye jengo kabla ya nyumba hiyo kuanguka. Ripoti za awali zilisesha wanadiplomasia hawakusiliana na Rais PRÉVAL, na hivyo kuhofia huenda atakuwa kaangukiwa kifusi cha nyumba yake. Baadae ripoti zilisema walinusurika na wapo kisiwa salama. Image
Inakadiriwa watu zaidi ya milioni 3 waliathiriwa na tetemeko hilo na makazi 250,000 na majengo 30,000 ya kibiashara yalianguka. Mbaya zaidi nchi ilikuwa na deni kuwa la Taifa, ukiongeza umaskini na hali duni ya makazi ambayo ilichangia idadi ya vifo vingi kutokana na janga hilo.
Tetemeko lilisababisha uharibifu mkubwa ktk nchi yote ya Haiti. Majengo maarufu ya kihistoria yaliharibika vibayasana, mojawapo ni Ikulu ya Rais, Jengo la Bunge, makao makuu ya mji mkuu WA Port-au-Prince, pamoja na magereza kuu. Image
Miongoni mwa waliouawa ni Askofu Mkuu wa mji mkuu Port-au-Prince JOSEPH SERG MIOT na kiongozi wa upinzani MICHA GAILLARD. Makao makuu ya Balozi wa Kudhibiti Amani wa @UmojaWaMataifa Haiti (MINUSTAH), iliopo mji mkuu, yalianguka na kuua watu wengi akiwemo Hédi Annabi Mkuu-MINUSTAH
Miundombiju ya mawasiliano, vifaa vya usafiri wa anga, ardhi, na baharini, hospitali, na mitandao ya umeme viliharibiwa na tetemeko la ardhi, ambalo lilikwamisha juhudi za uokoaji na misaada. Unaambiwa vyumba cha kuhifadhia maiti vilizidiwa kwa makumi ya maelfu ya miili.
Nchi nyingi zilituma misaada ya kibinadamu, zingine zikaahidi fedha na kutuma timu za uokoazi na vifaa vya matibabu, wahandisi na wafanyikazi wa misaada. Ktk historia moja ya mchango uliochangiwa live ulirushwa 22 Januari, ulioitwa "Hope for Haiti Now" ulikusanya US$ 58M kwa siku
Zoezi la uokoaji lilikwama kutokana kuchelewa kwa usambazaji misaada, vurugu na uporaji.Mnamo Januari 22 @UmojaWaMataifa ulibaini kuwa hatua ya dharura ya operesheni ya misaada lkn siku iliyofuata Haiti ilisitisha rasmi utafutaji wa manusura.Haiti ilichangiwa US $ 5.3B km msaada
Baada ya Tetemeko la ardhi mataifa mengine yaliisamehe Haiti madeni iliyokuwa inadaiwa. Mojawapo ni:
💰 @WorldBank 2.1B (Deni Lote)
💰 @imfcapdev 757M
💰 France US$ 77M
💰 Venezuela 257M
💰@idabank 1.20B
Baada ya hapo ndipo uchaguzi wa mwaka 2010 ulifanyika.

Nini kilitokea?

TURN ON NOTIFICATION & RT THIS THREAD
#Good Evening!!

#Leo nimeona nimalizie Part A [historia ya Haiti]

#Muendelezo:Baada kutokea Tetemeko la Ardhi (2010) hali ya umaskini iliongezeka na kulitokea mlipuko wa UGONJWA wa Kipindupindu. Rais RENÉ PRÉVAL alikuwa amemaliza muda wake wa uongozi hivyo aliachia madaraka.
Kawaida uchaguzi wa Haiti ulikuwa ukifanyika Trh 28 Februari ktk mwaka wa uchaguzi. Lkn Tetemeko lilitokea Januari hivyo ikawa ngumu uchaguzi kufanyika. Ukasogezwa mbele bila siku maalum na baadae Novemba 28 iliamuliwa km Trh rasmi ya kufanyika uchaguzi wa urais na wabunge.
Taarifa ilitolewa kuwa 07 Agosti 2010 itakuwa siku ya mwisho ya kupokea fomu za wagombea nafasi ya urais na Agosti 17 ORODHA rasmi ya wagombea itatangazwa na Tume ya Uchaguzi.Kutokana na kazi ya kupitia majina yote ya wagombea ili kuhakiki taarifa zao orodha ilitolewa 19/08/2010.
Mojawapo wagombea urais walikuwa @mirlandemanigat (mke wa rais wa zamani), mwanamuziki @wyclef, @leslievoltaire na MICHEL MARTELLY (mwanamuziki)
Kutokana na sheria za uchaguzi ikiwemo la mgombea kukaa nchini kwa muda usiopungua miaka 5 @wyclef aliondolewa ktk kinyang'anyiro hicho ImageImageImage
Orodha ilikuwa na majina ya wagombea 38 lakini Chama cha Fanmi Lavalas (FL) cha JEAN-BERTRAND ARISTIDE licha ya kuwa uungwaji mkubwa kutokana na umaarufu wake huku yeye akiwa bado uhamishoni Afrika Kusini baada ya kukataliwa kukataliwa hati yake ya kusafiri kurejea nchini Haiti.
Kampeni zilianza, maswali mawili kwa wagombea ilikuwa ni kitu gani watafanya ili kujenga upya Taifa la Haiti baada ya kutokea Tetemeko la ardhi mwanzoni mwa mwaka huo na kupelekea kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu miezi miwili kabla ya uchaguzi.
Kura za maoni ilionesha wagombea wanaungwa mkono km ifuatavyo

#Okt2010:
📋Mirlande Manigat (RNDP) 23%
📋Charles Baker (Respect) 17.3%
📋June Celestin (Unity) 7.7%

#Nov2010:
📋Charles Baker 24.4%
📋Mirlande Manigat 17.5
📋Juene Leon (EL) 14.6%
📋Michel Martelly (Peasant) 14.1%
Siku ya kwanza ya upigaji kura, Martelly na Manigat na wagombea wengine walishutumu matokeo ya awali kuwa ni batili kabla hata zoezi la kupiga kura kumalizika. Shutuma zilimuangukia JUDE CELESTIN aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la Ujenzi aliyeungwa mkono na rais RENÉ PRÉVAL.
Kufuatia maandamano na madai ya upinzani kwmb uchaguzi haukufanyika ktk haki, na Bunge kuendelea kubaki licha ya muda wake kuisha trh 7 Februari, Rais René Préval alivunja bunge na kuagiza Tume ya Uchaguzi kuendesha zoezi la uchaguzi vzr, na yeye akakaa pembeni kuepuka lawama.
Wengine waliiona serikali kuwa haijajiandaa kufanya uchaguzi kufuatia tetemeko la ardhi ambalo liliwaacha zaidi ya watu milioni 1 ktk kambi za muda huku wengine wakiwa hawana vitambulisho vya kupiga kura.
Pia kulikuwa na hofu huenda uchaguzi ukaitupa nchi ktk mzozo wa kisiasa.
Hata kabla matokeo ya Uchaguzi kutangazwa, mizozo na mivutano ilikuwa mingi.
Kutokana baadhi ya wagombea kupinga awali matokeo ya uchaguzi, Jumuiya za Kimataifa zilihofia kutokea machafuko nchini humo. Hivyo vikosi vya usalama vya vilipewa mafunzo maalum na vikosi vya kigeni.
@UmojaWaMataifa ulipiga kura ya kuongezea muda mamlaka ya @MINUSTAH kuendelea kubakia nchini humo kutokana na hofu ya ukosefu wa amani. Hii iliongeza nguvu ya maandamano ktk miji mbalimbali na vitendo vya kuchoma bendera ya Brazil iliyokuwa na idadi kubwa ya wanajeshi MINUSTAH.
Wagombea waliokuwa na nguvu ni mwanamuziki MICHEL MARTELLY na mwanamama na Prof. MIRLANDE MANIGAT mke wa LESLIE MANIGAT aliyekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo.
Baadae Bi HILLARY CLINTON aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Marekani wakati huo alienda Haiti kuweka mambo sawa. ImageImageImage
Mpaka @HillaryClinton kwenda Haiti, ni kutokana na watu wawili kuuawa katika mapigano ya risasi za moto kati ya wafuasi wa vyama upinzani huko Aquin, na wengine kujeruhiwa ktk siku za mwanzo kabisa baada ya kuanza zoezi la kupiga kura na kupelekea kuenea kwa vurugu nchini kote.
MARTELLY alipata umaarufu kwa7bu alikuwa mwanamuziki mkubwa nchini Haiti, yaani Martelly ungemlinganisha na @HEBobiwine wa Uganda. Alikuwa na watu wengi vijana na maarufu. Alitangaza kuwa hatoshiriki marudio ya uchaguzi endapo CELESTIN atashiriki km mgombea.

Pichani ni MARTELLY ImageImageImageImage
Mnamo Dec 10, Tume ilitangaza matokeo. MIRLANDE MANIGAT (RPND) alipata kura 336,878 sawa na 31.37%, wa Pili JUDE CÉLESTIN (Unity) aliyepata kura 241,462 sawa na 22.48% wa tatu MICHEL MARTELLY kura 234,617 sawa 21.84%.
Manigat na Martelly waliyakataa isipokuwa CÉLESTIN aliyakubali
Kufuatia makubaliano yaliyofikiwa mwishoni mwa Desemba 2010 ili kufikia suluhu kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza ktk mchakato wa kuhesabu kura, iliafikiwa kurudiwa zoezi la kupiga kura tena mwezi Februari mwakani (2011) kwa7bu hakuna mgombea aliyefikisha 50% ya kura zote.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi PIERRE-LOUIS OPONT alihutubisa Taifa na kuomba angalau muda wa mwezi mmoja ili kuandaa zoezi la kurudia kupiga kura nchini humo. Pia aliomba mashirika ya Mataifa likiwemo @OAS_official la Marekani kusaidia ktk kukamilika kwa marudio ya Uchaguzi huo.
OAS ilipendekeza Manigat na Martelly warudishwe ktk marudio, huku Célestin aliyekuwa mshindi wa pili akitupiliwa mbali. Tume ilikataa mapendekezo awali, lkn baadae ilikubaliana nayo na kutangaza Jan 19, 2011 kuwa siku ya kupiga kura na wawili hao ndio walirudishwa kugombea urais. ImageImage
Ulitokea mvutano mkubwa baina ya Célestin na Tume, Lkn kutokana na shinikizo la kimataifa alikubali kujiondoa rasmi ktk marudio ya uchaguzi 26/01/2011. Kampeni za duru ya pili zilianza rasmi Alhamisi 17/02/2011. Kutokana na mvutano huo na kila mgombea alichagua pa kuanzia kampeni
Bi @mirlandemanigat yeye alifungulia kampeni zake ktk hoteli alipozungumza na wana habari na kuweka bayana mipango yake ya baadaye. MARTELLY alianzia mitaa ya Cap-Haïtien, mji wa pili kwa ukubwa nchini Haiti, ambapo alifungua kwa muziki mnene huku akicheza stejini na wafuasi wake ImageImageImageImage
Baadae Michel Martelly alikwenda kufanya kampeni huko Miami huko Marekani, ambako ni makazi ya idadi kubwa ya wahamiaji kutoka nchini Haiti.

Kura zilipigwa na matokeo ya raundi ya kwanza yalitangazwa Feb 03, 2011, na baadae matokeo ya pili na ya mwisho yalitangazwa 20/03/2011 ImageImage
Na 4 April 2011, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi PIERRE-LOUIS OPONT, alimtangaza mwanamuziki MICHEL MARTELLY kuwa mshindi wa urais ktk marudio ya uchaguzi wa rais, kwa kupata kura 716,986 sawa na 67.57% dhidi ya mpinzani wake MIRLANDE MANIGAT aliyepata kura 336,747 sawa na 31.74%. ImageImage
Rais MARTELLY aliapishwa kuwa Rais Tarehe 14 Mei 2011 na kwa mara ya kwanza ktk historia ya Haiti, Rais aliye madarakani alikabidhi madaraka kwa mpinzani kwa amani.
Waziri Mkuu aliyekuwepo madarakani JEAN-MAX BELLERIVE, alijiuzulu ili kumruhusu Martelly kuchagua PM wake mwenyewe. ImageImageImageImage
Martelly aliahidi mageuzi na mchakato wa ujenzi baada ya Tetemeko. Mnamo Agosti 2011, alitangaza mpango wa kurudisha Jeshi la Taifa. Mpango uliokuwa wa kutatanisha, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa na wasiwasi juu ya kurudi kwa jeshi lililofanya ukatili mwingi huko nyuma Image
MICHEL MARTELLY (2011/2016)

#Alizaliwa 12 Februari 1961 huko Cote de Fer nchini Haiti.
Martelly ni mtoto wa MARIE MADELEINE MARTELLY (née De Pradines) na GERARD MARTELLY Mtendaji wa kampuni Mafuta ya Shell Oil. Martelly baada ya kuhitimu masomo High school alijiunga na jeshi. Image
Hakumaliza mafunzo ktk Chuo cha Jeshi, alifukuzwa baada ya kumpa ujauzito binti wa Jenerali. Mwaka 1984 aliondoka Haiti na kwenda nchini Marekani, ambako alifanya kazi ktk kampuni ya ujenzi akiwa saidia fundi. Baadae alijiunga na chuo cha maendeleo ya jamii huko huko Miami.
Kilikuwa cha dikteta JEAN-CLAUDE DUVALIER aliyekuwa amejitangaza rais mpk kifo, baadae Duvalier alipinduliwa akakimbilia uhamishoni.Mwaka 1987 MARTELLY alirejea Haiti akiwa na mchumba wake SOPHIA SAINT-RÉMY ambaye walioana baadae huko Florida, mwaka 1988 alirudi tena nchini Haiti ImageImage
Aliporudi Haiti alifanikiwa kuanzia Label ya muziki, akawa anatumbuiza ktk maeneo mbalimbali ktk kumbi za huko Pétion-Ville na Kenscoff na baadhi ya mitaa ya mji mkuu wa Port-au-Prince. Mnamo mwaka 1991 alifungua Night Club yake ambapo viongozi wengi walikuwa wanakuja kumsikiliza ImageImageImageImage
Mwaka 1992 alijiunga na maandamano, mwaka 1995 jina lake lilitajwa miongoni mwa watu waliotakiwa kuuawa na Utawala uliokuwepo lkn alinusurika.

Mnamo 2004 kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa Aristide, rafik yake GÉRARD LATORTUE, aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu.
Mwaka ajikita ziadi kusaidia watoto yatima. Mwaka 2007 kulitokea Global financial crisis (2007/08) akapoteza fedha zake zaidi ya US$ million moja ktk mkopo, alipoteza mali mara 3 kwa kufungiwa. Mnamo 2010 MARTELLY aligombea Urais wa Haiti katika uchaguzi mkuu na akashinda urais. ImageImage
Alifaidika na umaarufu wake kama mwanamuziki, na alifanya mikutano ya muziki na kuvutia umati mkubwa na vyombo vya habari viliyomriopoti sana kampeni zake. Alipata pia msaada wa Bill Clinton (Mjumbe Maalum wa UN kwenda Haiti) na msaada wa Waziri wa Mambo ya Nje Hillary Clinton.
Mnamo April 04, 2011alishinda Uchaguzi na May 14 alikula kiapo na kuwa mpya wa Haiti. Mwezi Septemba alitengeneza Taasisi ya kumshauri Rais. Februari 2012 waziri mkuu GANNY CONNILE) aliondolewa na kura ya Bunge. Mwezi na April alianza kushutumiwa kutokena na ufisadi. Image
Maandamano dhidi ya hali ngumu ya maisha na rushwa viliongezeka

Mnamo 14 Dec 2014, LAURENT (aliyekuwa waziri mkuu) alijiuzulu akamteua EVANS PAULO. Maandamano yaliendelea huku waandamanaji wakimtaka MARTEL ajiuzulu urais na Januari 13, 2015 alisema muda wake madarakani umeisha.
Kwa siku 4 maelefu ya waandamanaji ktk mji mkuu Port-au-Prince yalikuwa makubwa mpk ilibidi Polisi kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya raia. Ndani ya masaa 48 nchi ilikuwa imeharibika vibaya akazungunza na wana habari na kutangaza kukubaliana na waandamanaji kuunda serikali
#Mnamo Dec 27, 2015 kulifanyika Uchaguzi mkuu ambao @moisejovenel alishiriki na kushinda kiti cha Urais.
#The End of "Part A"👆

KESHO nitamalizia "Part B"
'Mauji ya JOVENEL MOISE kwa undani ZAIDI!!!
📋Alipozaliwa
📋Siasa na Urais
📋Mauaji yake

#MUHIMU:RT THIS THREAD & FOLLOW ME ImageImageImage
JOVENEL MOÏSE

Alizaliwa trh 26 June 1968 huko Trou du Nord, Haiti.
Mwaka 1974 wazazi wake walihamia Port-au-Prince alipoendelea na masomo ktk s/msingi Ecole Nationale Don Durélin, baadaye alijiunga na sekondari ya Lycée Toussaint Louverture na kisha ktk chuo cha Canado-Haïtien. ImageImageImage
Mnamo 1996 alimuoa mwanafunzi mwenzake MARTINE MARIE ÉTIENNE JOSEPH. Mwaka huo huo, waliondoka mji mkuu na kuhamia mji wa Port-de-Paix kupambana na kilimo cha ndizi maeneo ya vijijini. Alianza na mtaji mdogo, baadae alifungua Duka la JOMAR AUTO PARTS (spea za gari) lipo mpk leo. ImageImageImage
Akakuza mradi wa kilimo kwa uzalishaji wa ndizi ktk shamba lake lililokuwa na ukubwa wa Ekari 25. Mnamo 2001 akashirikiana na kampuni ya Culligan kuanzisha kiwanda cha maji ya kunywa na kuyasambaza maeneo yote ya mji mdogo wa Nord.

Mnamo 2012 alianzisha kampuni ya Agritrans SA👇 ImageImageImage
AGRITRANS ulikuwa mradi mkubwa wa kilimo cha ndizi huko Trou du wenye mashamba ya hekta 1,000 akapewa jina la "Banana Man". Serikali ilimuondolea kodi ya ardhi 15yrs, mkopo US$ 6M na wengine walimchangia US$ 10M.
Akaahidi ajira 3,000 ingawa mpk 2015 alikuwa ametoa ajira 600 pekee ImageImageImage
Mwaka 2015 aliteuliwa kuwa mgombea wa urais chama cha Haiti Tèt Kale Party (PHTK).
Ktk kampeni zake Moïse alitumia hoja ya kilimo cha bio-ikolojia kama injini ya kiuchumi kwa Haiti, ambayo idadi kubwa ya wakazi wake ni wakulima na zaidi ya 50% hutokea maeneo ya vijijini. ImageImageImage
Alionesha pia kuunga mkono sera zilizoshindwa kutimizwa na Rais aliyetoka madarakani Michel Martelly
📋Elimu,
📋Huduma za afya,
📋Umeme na
📋Ajira kwa vijana
Hii ilimfanya apate 32.8% ya kura ktk duru ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika Okt 15, 2015 ambapo wagombea 54 walishindana. ImageImage
Kikatiba hakuna mgombea aliyefikisha 50% ya kura zote, hivyo iliamualiwa mshindi wa kwanza na wa pili JUDE CÉLESTIN kurudia uchaguzi.
Ghafla yaazuka maandamano ya maelfu wakipinga kutorudiwa kwa uchaguzi uliokuwa ufanyike June 2016 na kupelekea kufutwa uchaguzi ktk duru ya pili. ImageImageImage
Februari 2016, Rais Michel Martelly akung'atuka madarakani baada ya kipindi chake kuisha, nchi ikabaki mikononi mwa Bunge. Ndipo Bunge likafanya uchaguzi wa kumpata kiongozi wa muda, akachaguliwa JOCELERME PRIVERT kuwa Rais wa mpito hadi hapo uchaguzi mpya utakapofanyika ImageImage
Mnamo 20 Novemba 2016, uchaguzi mpya ulifanyika na wagombea 26 walishiriki. Waliojiandikisha ni 6,189,253 sawa na 18.11% ya idadi raia wote nchini Haiti. Wiki moja baadaye, Tume ya Uchaguzi ilitangaza matokeo ya urais na JOVENEL MOÏSE alishinda kwa kura 590,927 sawa na 55.67% . Image
Mpinzani wake JUDE CÉLESTIN alipata kura 207,988 sawa na 19.57%, akifuatiwa na JEAN-CHARLES MOÏSE 11.04% na Bi MARYSE NARCISSE wa Fanmi Lavalas (FL) chama chake JEAN-BERTRAND ARISTIDE aliyepata 8.99%.

#Na mnamo 07 Februaria 2017 JOVENEL MOÏSE aliapishwa tkwa kipindi cha miaka 5 ImageImageImage
Changamoto zilianza baada ya viongozi wa upinzani kutoa tamko kwamba miaka yake mitano ya uongozi inapaswa kumalizika kuanzia siku mtangulizi wake alipotoka madarakani, licha ya kwamba yeye aliapishwa mwaka 1 baadae, hivyo akadai muda wake utaisha 2022.

Ndipo mgogoro ulianza👇 ImageImageImage
Mnamo 7 July 2021 majira ya usiku, JOVENEL MOÏSE aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ktk makazi yake binafsi huko Pétion-Ville na mke wake kunusurika kifo baada ya kupigwa risasi mkononi na watu waliofahamika kuwa makomando kutoka nchini Colombia wakishirikiana na wamarekani. ImageImageImage

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with JAPHET MATARRA

JAPHET MATARRA Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Eng_Matarra

18 Aug
WHO is '𝐓𝐀𝐋𝐈𝐁𝐀𝐍'? WANATAKA NINI HASA AFGHANISTAN?

#𝕿𝖍𝖗𝖊𝖆𝖉:
Ifahamike, walikuwa yatima ktk kambi za wakimbizi Pakistan.
Je, wana uhusiano na AL-QAEDA? #Tragedy:UINGEREZA & URUSI kuchezea kipigo cha Mbwakoko.
✴️Chimbuko
📡Walio nyuma yao?
📋Tofauti yao na MUJAHIDINA..
Vita vya Marekani nchini Afghanistan vimedumu kwa takribani miaka 20. Nimeona watu wengi wakitoa maoni juu ya Jeshi la TALIBANI kuchukua nchi Lkn wengi hawana historia juu yake. Wengine wanasema Rais wa Marekani @JoeBiden mefanya 'makosa' kuondoa majeshi yake.
BIG NO __Hapana.
Wengi tusichojua ni kwamba, huu ulikuwa ni uhalifu wa kivita na DICK CHENEY, aliyekuwa Vice President wa G. W BUSH na DONALD RUMSFELD, Kiongozi Mkuu wa Ulinzi kipindi cha Vita ya IRAQ (alishafariki), ndio walioiingiza Marekani kwenye shida hii unaiona Leo, kisa wanamtafuta OSAMA
Read 114 tweets
11 Aug
𝐅𝐀𝐇𝐀𝐌𝐔 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐉𝐈𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐈𝐊𝐎𝐀🇹🇿

#𝕿𝖍𝖗𝖊𝖆𝖉:
Tanzania ni nchi iliyoko Africa
Jina "𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚" lilipatikana kwa mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 na 𝐌𝐨𝐡𝐚𝐦𝐞𝐝 𝐈𝐪𝐛𝐚𝐥 𝐃𝐚𝐫 ndiye aliyelibun.Hivi unafaham asili ya jina la mkoa wako?
Ktk kipind cha 𝐔𝐤𝐨𝐥𝐨𝐧𝐢 Tanzania ilikuwa na utawala wa majimbo 8, Lkn baada ya #𝐔𝐡𝐮𝐫𝐮 mikoa ilianzishwa kwa miaka tofauti na mpk Leo hii ninavyoandika #Uzi huu 𝐌𝐢𝐤𝐨𝐚 31 imeanzishwa kutoka pande zote Visiwani na Tz Bara.Najua ulishawahi kujiuliza asili ya Mkoa wako
Kila Jina unalosikia lazima kuna chimbuko ambalo ndio Asili ya jina hilo. Aidha, yawezekana limetoholewa ktk lugha za kigeni na kuchukuliwa kutokana na matumizi yake, muonekano, lugha za asili ktk Eneo fulani, tukio ama hata tabia za watu wa eneo fulani na makosa ya kimatamshi
Read 158 tweets
29 Jul
FAHAMU MADINI YA ALMAS 💎 UTAJIRI & VITA YAKE

#Uzi:
📋Asili yake
📋Historia yake
📋Mgunduzi wake
📋Aina & Thamani yake
📋Vita yake duniani na Tanzania
📋🇹🇿 iligunduliwa lini na nani, wapi
📋DE BEERS & Msukuma wa Williamson DIAMONDS, aliyeipenda Mwadui hakuna wa mfano wake!!
🔄👇
Leo nimechagua kuzungumzia Maliasili za Taifa🇹🇿

#Maliasili ni vitu vinavyotokana na maumbile. MFANO:Wanyama, Misitu, Madini n.k kama ulikuwa hufahamu maliasili za nchi huchangia ktk utajiri wa nchi husika.Mojawapo ni South Africa, imenawiri kiuchumi kutokana na utajiri wa madini
Nafahamu ulishawahi kujiuliza, Almasi ni nini? Iko iko je? au Almasi zinatengenezwa na nini?

LEO nakupa Jibu:

#ALMASI: Ni kito Adimu chenye thamani kubwa sana Duniani. Kito hiki ni kigumu sana kushinda Metali au madini yote Duniani. Asili yake hutengenezwa na Carbon (C) 99.95%
Read 96 tweets
27 Jul
FAHAMU MVUMBUZI WA TELEVISION (📺)

#Yes_____&&
#Thread|story🕐
Any sufficiently Advanced Technology is indistinguishable from MAGIC!! Binafsi huwa nasema Technology Is the Great ant💉dote to the Poison of Enthusiasm and Superstition💣
📋Asili ya TV
📋Historia yake
📋Uvumbuzi n.k
Televisheni (TV) au Runinga ni kifaa chenye kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.

Neno "Televisheni" linatokana na maneno mawili:
(i)Tele (Kigiriki)-kwa mbali sana na
(ii)Visio (Kilatini)-mwono.

RT @omari_manyama
kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza #Television limetoholewa kwa lugha ya Kiswahili "Televisheni".

Ugunduzi wa TV📺 ni kazi iliyofanywa na watu wengi mwishoni mwa karne ya 19.Karne ya 20 Watu mmoja-mmoja na makampuni yalishindana kuunda chombo kilichopiku teknolojia ya awali.
Read 37 tweets
17 Jul
On This Day

TWA FLIGHT 800 😭
#RIP !!
#The aviation disaster, a Europe-bound Boeing 747, Exploded and Crashed off Long Island,NY

#Thread|StoryTime
#AllpeopleDied
📜Gaddafi, SADDAM HUSEIN wahusishwa | kwa upande wa USA ulikuwa usiku usiosahaulika.

RT @omari_manyama let's go👇 ImageImageImage
#Ikiwa ni dakika 12 tu baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy (JFKIA) uliopo mjini New York, ndege [TWA FLIGHT 800] iliyokuwa ikielekea Italia kupitia Paris ililipuka ghafla juu ya Bahari ya Atlantiki na kuua watu wote 230 waliokuwemo ndani ya ndege Image
Tukio hili lilitokea Trh km ya Leo majira ya saa 02:31 usiku Jumatano mnamo Julai 17, 1966, ambapo ndege hiyo kubwa ya masafa marefu aina ya BOEING 747 alimaarufu TWA FLIGHT 800 ya kampuni ya Trans World Airlines [TWA] ililiripuka karibu na pwani ya Long Island na kuua watu wote. Image
Read 24 tweets
13 Jun
"YOU ARE UNDER ARREST"

#Uzi

📌Je, wajua Leo ilikuwa siku ambayo sheria inayomlinda mhumiwa [Miranda rights/Warnings] anapokamatwa na vyombo ulinzi ilipitishwa huko marekani?

💨YES it's Miranda Vs Arizona case

📌 Historia yake

📌 Chanzo chake

📌Maamuzi ya kihistoria.

👇👇 ImageImage
Mnamo Juni 13, 1966 Mahakama Kuu ya Juu (Supreme Court) nchini Marekani ilitoa uamuzi wa kihistoria juu ya taratib za uendeshaji kesi za jinai mahakamani.Uamuzi huo ulitokana na kesi ya Miranda Vs Arizona kwamba watuhumiwa wa kesi wanazo haki zao kabla ya kuhojiwa wawapo kizuizin Image
Nadhani ulishawahi kusikia maneno haya

1. Una haki ya kukaa kimya.

2. Chochote unachosema kinaweza, na kitatumika, kama ushahidi mahakamani.

3. Una haki ya kuwa na wakili.

4. Ikiwa hauwezi kumudu gharama za wakili mahakama, itamteua mmoja kusimamia kesi zako

Tuendelee 👇 Image
Read 35 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(