My Authors
Read all threads
PARASITE: Ngoja leo tuhame kutoka Amerika kwenye zile filamu mnazozielewa na kuzikubali hadi pale korea ambapo leo tutakodolea macho filamu matata iliyopata TUZO za kumwaga na hasa ile tuzo kubwa ya OSCAR ACADEMY AWARD kwa mwaka 2019 kwa ufupi ni kusema hii ndo filamu bora kwa
mwaka 2019. Kuwa filamu bora na tuzo bwelele ndo iliyonifanya niitafiti kwa kupitia majalada mengi ya filamu duniani, pia nilifanikiwa kusoma ripoti mbalimbali za wachambuzi wa filamu duniani na mwisho niliweza kuitizama huku nikijiuliza nini hasa kilichopo kwenye filamu hii
hadi kupata tuzo zote hizo.

Ufutao ni ufupisho wa yale niliyojifunza kuhusu filamu hii. Filamu hii ilizinduliwa kwenye maonyesho ya filamu ya mwaka 2019 yaliyojulikana kama "Cannes Film festival" yaliyofanyika 21 May 2019 na ambapo ikawa filamu ya kwanza ya kutoka Korea Kusini
kushinda Tuzo ya PALME d'Or na ikawa filamu ya kwanza kushinda kura za makubaliano ya pamoja (unanimous vote) baada ya ile ya Blue is the Warmest Colour (Amerika) katika maonyesho ya filamu ya mwaka 2013

Picha hii iliongozwa na Bong Joon-ho na kuandikwa na yeye pia akishirikiana
na Han Jin-won na kuzalishwa na CJ Entertainment, wahusika walikuwa Song kang-ho, Lee Sun-kyun, na wengineo, picha hii ilipata uchambuzi chanya na kuwekwa kwenye Orodha ya picha bora za mwaka 2010 hadi 2019, Filamu hii ilitengenezwa kwa bajeti ya Dola za kimarekani zipatazo
milioni 11 ($11 Million), na kuweza kuingiza zaidi ya Dola za kimarekani zipatazo milioni 210 ($210 million) Duniani kote na kuifanya kuwa filamu ya Kikorea ya kwanza yenye maingizo makubwa sana kuliko filamu yoyote nchini Korea.

Baadhi ya tuzo ambazo filamu iliweza kupata ni
pamoja na tuzo ya The 92nd Academy Awards: Best picture, Best Director, Best Original screen play, na Best International feature Film. Ilikuwa picha ya kwanza ya Kikorea kupata tuzo ya Academy Award Recognition na ikawa picha ya kwanza isiyozungumza kiingereza kushinda picha Bora
ya Mwaka, pia iliweza kujizolea Golden Global Award for Best Foreign language Film na BAFTA Award for Best Award Not in English Language na ikawa picha ya kwanza isiyo ya Kiingereza kushinda Screen Actors Guild Award for Outstanding Performance by a Cast in a motion picture.
Kwa
Kwa sifa hizo hapo juu lazima utakuwa na hamu ya kujua ni nini hasa picha hii imebeba hadi itusue kwa kiasi hicho. Ngoja nikupe vitu

Kwa kuielewa picha hii kwanza yatupasa kuijua famlia ya wasionacho (The have nots) hii ni familia ya Kim, Baba (Ki-taek), Mama (Chung-sook) Binti
Ki-jung na kijana wao (Ki-woo) walikuwa wanakaa kwenye nyumba za hali ya chini kwenye basement ( Semi-Basement apartment) sijapata kiswahili chake fasaha, walikuwa wa kipato kidogo cha vikazi vidogo vidogo vyenye malipo madogo madogo sana hasa zile za kukunja mabox ya pizza. Siku
moja ambapo ndipo zali la mentali linaanza kwa kuja kwa rafiki wa mtoto wao wa kiume aliyeitwa Min-hyuk mwanafunzi wa chuo ambaye alikuwa anasafiri nje ya nchi na hivyo akaona awaachie kipande cha jiwe wanafamilia hao kwa maana aliamini kwa yoyote atakaye limiliki jiwe hilo basi
Afya yake itaimalika. Pamoja na kuwaachia jiwe hilo bado anampa rafiki yake mchongo wa kumfundisha kiingereza mtoto wa kike wa familia ya kitajiri ya bwana Park (The haves) aliyeitwa Da-hye, na hapa ndipo hasa kiini cha filamu hii kilipolala na ndio filamu inapoanza. Kevin
Ki-woo)akajifanya kuwa na Elimu ya chuo ambayo hakuwa nayo,dada yake aliyekuwa msanii alimtengenezea cheti cha kugushi. Hapo ndipo familia ya Kim ikaanza kujipenyeza kwenye familia ya Park kwa kila mmoja akitoa mapendekezo bora kumuhusu mwenzie anayetakiwa kuja huku wakijifanya
hawajuani lkn wakionekana kuwa wafanyakazi stadi sana kwenye kazi zao.

Kevin ndiye aliyempendekeza dada yake kuja kumfundisha uchoraji mtoto wa kiume wa tajiri Park, na dada alipoajiliwa naye kazi yake ilikuwa kumleta baba kama dereva , siku anarudishwa nyumbani na dereva,
Jessica(Ki-jung) akavua Chupi yake na kuiacha kwenye kiti cha nyuma ambapo chupi hiyo inakutwa asubuhi na tajiri Park ambaye anakasirishwa sana na kitendo icho na kumfananisha mwanamke anayeweza kuacha Chupi kwenye gari ni kama mtumia madawa ya kulevya kwa sababu mwanamke anaweza
kupoteza heleni na vitu vingine vidogo vidogo wakati wa tendo la ndo likiendelea kwenye gari lkn sio rahisi mwanamke kusahau chupi hali iliyonyesha huyo mwanamke hakuwa vizuri na hii ni hatari kwa usalama,

kitendo kinachopelekea kufukuzwa kazi kwa dereva Alie onekana kuwa na
tabia za kufanya Mapenzi ndani ya Gari, na hivyo mpango ukafanikiwa, dada akampendekeza baba na baba akaajiliwa, kazi ikawa kumtoa mama aliyekuwa akihudumia kama mwangalizi wa nyumba (housekeeper) ili mama yao aweze kuchukua nafasi hiyo, baadae wakafanikiwa kuujua udhaifu wa mama
huyo, kuna tunda ambalo mama huyu alikuwa hali wala kulisogelea linampa hali ya mafua na kikohozi kikali (allergic to 🍑 peach) hapa palifanyika figisufigisu hadi mama akaonekana kuwa anaugua kifua kikuu na kuhatarisha maisha ya watu ndani na hivyo kufukuzwa na Kim akampendekeza
Mke wake kuajiliwa, Mama akaajiliwa na familia zima ya Kim ikawa imefanikiwa kujipenyeza kwenye familia ya Park na hii hali ndo ikachukua jina la picha hawa wanafamilia ya Kim ndo wakachukuliwa kama PARASITE sipati kauli ya kiswahili itakayobeba maana sawa au kwa kiswahili cha
mtaa tuwaite CHAWA

Mtiti unanza baada ya Park na familia yake kwenda pikiniki ya mahema(🏕️ camping) na hapa uhuru wa manyani ukatawala kwani familia nzima ya Kim ikahamia kwenye jengo la kifahari la Park, wakala, wakanywa wakalala hadi kwenye kitanda cha park Starehe ilidumu
hadi usiku mwingi wakati mama ambaye alikuwa housekeeper anarejea na kugonga hodi, wote wanapigwa na bumbuazi wakiwa hawajui mama huyu kafuata nini hapo muda huo wa usiku mwingi, akiwa anagonga akadai kuwa kuna kitu amesahau na anaomba aingie akichukue, na hapo mama housekeeper
(Moon-gwang) baada ya kuingia ndani akiwa hana jinsi inabidi amueleze ukweli Mama Kim wa kuwepo kwa chumba cha Siri ambacho alikitengeneza mmiliki aliyepita wa Nyumba hiyo na walipoingia huko ndani alichokiona mama Kim kilimshangaza hadi akataka kupiga simu polisi kwani humo
ndani alikutana na kitu ambacho hakukitegemea .....

Patashika ikawa kubwa mchezo ukaigeukia familia ya Kim baada ya familia hiyo kuanguka kutoka sehemu waliokuwa wakichungualia na kusikiliza mazungumzo kati ya housekeeper na mama Kim
Na walipofikika chini wakaanza kuitana mama
baba wakasahau kuwa walikuwa wameajiliwa kama watu wasiojuana na siri yao ikawa imetoka nje kwa uzembe ...
Mambo mengi hapa yalisemwa na vitu vingi vilifanyika lakini kwa kipindi hicho wakati haya yote yanatokea familia ya Park huko ilikoenda ikakosa sehemu ya kujenga mahema
kwani kulikuwa na mafuriko na watu wote waliambiwa waondoke na hivyo walikuwa njiani kurejea nyumbani ..naogopa kuendelea nisije haribu hii picha kwa wale ambao bado hawajaiona, kwani hapa sasa ndipo hasa utamu ulipo.
Picha iliweza kupata kiwango cha 8.6/10 katika viwango vya mtandao IMDb na kupata 99% katka mtandao wa Rotten Tomatoes

Pamoja na na Mafanikio haya yote picha hii story yake inaonekana KUIBWA kutoka kwenye filamu ya Kihindi iliyoitwa Minsara Kanna ya mwaka 1999 iliyotengenezwa
na P.L. Thenappan, hivyo mnamo tarehe 23 feb 2020 siku 4 zilizopita wakili wa Thenappan alimuandikia barua ya kisheria Director wa PARASITE ya kwa nini asimchukulie hatua za kisheria kwa kuiba stori

Siku filamu hii inaanza kuonyeshwa nchini Amerika kwenye kumbi 3 ilingiza jumla
ya dola 376,264 kwa siku moja

Utengenezaji wa filamu hii ulichukua siku 124 katika maeneo ya Seoul na Jeonju.
Uko Dodoma wala usiwaze sana unatoa wapi huu mzigo jongea mitaa ya mkabala na sido #cipherdotseriesandmovies mzigo tunao 1080p bila kusahau subtitle na wewe usisahau kibebeo chako..
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!