My Authors
Read all threads
FOR LIFE
Kama una unakazi unafanya basi iweke pembeni kidogo ili usome huu Uzi kwa mazingatio

Mwaka 1989 Isaac Wright Jr anakamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kuuza na kusambaza madawa ya kulevya, akiwa hana kumbukumbu yoyote ya uhalifu katika taarifa za polisi akiwa ni mtu wa
maisha ya Halali na akifanya Biashara zake halali bila tatizo. Baada ya kukamatwa kesi yake inafika mikononi mwa wakili wa serikali wa mji wa New Jersey Nicholas Bissell. Akijifanya kuibeba na kuisimamia sheria kuhakikisha wanapambana na tatizo la madawa ya kulevya katika mji
huo lakini kumbe chini chini alikuwa Ni mwalifu mkubwa tu kuliko ata watu alio wapeleka jela kwa mkono wake.

Mwaka 1991 Mwanasheria Nicholas Bissell anafanikiwa kumpa kifungo Cha maisha jela bwana Isaac Wright Jr kwa kosa ambalo hata hakufanya, Bissell alitumia mbinu zote chafu
kuhakikisha anafanikiwa Kwenye Ilo. Pamoja na kwamba alikuwa na elimu ya diploma tu Ila Isaac Wright alisimama Kama Mwanasheria Kwenye kesi yake mwenyewe hakutaka kuajiri mtu mwingine amtetee Kwenye kesi hiyo. Baada ya kuhukumiwa kifungo Cha maisha alipelekwa katika gereza la
ulinzi mkali (maximum security) 'New Jersey State Prison', akiwa jela Isaac Wright Jr alianza kujihusisha zaidi Kwenye masuala ya Sheria na kufanikiwa kupata kibali cha kufanya shughuli za kisheria ikiwemo kusimama mahakamani Kama wakili wa mtu. Kwa kutumia kibali hicho aliweza
kuwasaidia wafungwa wenzake zaidi ya ishirini katika kesi zao, ikiwemo kuachiwa huru kwa wale waliokuwa wamefungwa kimakosa na Wengine walifanikiwa kupunguziwa vifungo vyao.

Katikati mwa miaka ya 90s maisha ya Nicholaus Bissell yaliingia mushikeri, Mwaka 1996 alishitakiwa kwa
makosa mbalimbali ya kiharifu ikiwemo ubadilifu, rushwa na matumizi mabaya ya nafasi yake, hii ilipelekea kupewa adhabu ya kifungo cha ndani Bissell alikata kifaa cha kumonitor nyendo zake (monitoring bracelet) na kukimbia, lakini baadae polisi walifanikiwa kumpata katika mji wa
Nevada. Kwa kutaka kukwepa adhabu ya kifungo cha miaka 6 Hadi 8 Nicholaus Bissell aliamua kujiua.

Kutokana na Kifo Cha Bissell pamoja na kugundulika kwa makosa yake ya kiharifu, aliyokuwa anafanya nyuma ya mgongo wa kuwa Mwanasheria wa serikali kunaleta faraja Kwenye kesi ya
Isaac Wright Jr ambae alikuwa ameisha kaa gerezani kwa kipindi cha miaka Saba Sasa na ambaye alikuwa anafanya kila linalowezekana juu ya kesi yake. Kesi hiyo ilirudishwa mahakamani na kusikilizwa upya na safari Hii akafanikiwa kuachiwa huru baada ya ukweli kugundulika kuwa
alifungwa kwa kosa ambalo hakufanya. Baada ya kuachiwa huru Isaac alimaliza chuo na kwenda shule ya Sheria na kufaulu mwaka 2017 na sasa ni Mwanasheria alie kamilika.

Sasa sikia Hii Ni story ya Kweli ya maisha ya bwana Isaac Wright Jr , Siku Moja katika club moja iliyopo mitaa
ya Bronx Isaac alipata nafasi ya kukutana na 50 Cent, na alipo pata nafasi ya kupiga nae story aliamua kumpa story Hii ya maisha yake na kutoka pale 50 akawa kapata wazo jipya la kufanyia kazi na matunda yake ndo hii Tamithilia ambayo ipo mbele yetu na ambayo tunaingazia leo na
na hii si nyingine bali ni "FOR LIFE" Tamthilia iliyo beba maisha ya Isaac.

FOR LIFE Ni tamthilia ya kimarekani yenye maazi ya Sheria, Uharifu na Kusisimua ikiwa imetengenezwa na Hank Steinberg na 50 Cent akiwa Kama mmoja wa waandaaji wakuu. Ilianza kurushwa katika kituo Cha
runinga cha ABC February 11,2020 ikiwa imechezwa na star Nicholas Pinnock akijulikana Kama Aaron Wallace, mtu aliefungwa kwa kosa ambalo hakufanya, anakuwa Mwanasheria akiwa gerezani na kufanikiwa kuwasaidia wafungwa zaidi ya 20 katika kesi zao uku akipambana na kesi yake na huku
akiusaka Uhuru wake ili apate kuweza kuungana na familia yake. Aliweza kuyafanya haya yote kwa msaada mkubwa aliopata toka kwa mkuu wa gereza ilo (Warden) Safiya Masry nafasi iliyochezwa na Indira Varma.

Zikiwa zimeisha achiwa episode tatu mpaka sasa, series Hii Ina rate ya
7.3/10 Kwenye mtandao wa IMDb. Kama ni mpenzi wa tamthilia au filamu zinazoangazia mahangaiko ya watu weusi nchini marekani basi naamini Hii series itakufaa sana na utaifurahia sana.. Uzi huu umekujia kutoka Cipherdot Series and movies wakiwa wako jijini Dodoma.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!