My Authors
Read all threads
Ukizungumzia tamthilia kali za madawa ya kulevya katika ulimwengu wa Tamthilia itakuwa dhambi kubwa Sana kuacha kuitaja NARCOS() ambayo inamzungumzia Gaidi wa dawa za kulevya aliyefanya ulimwengu kuchanganyikiwa kutokana na madhara ambayo dunia ilishuhudia
kutokana na ukatili wa huyu jamaa

Watu wengi Duniani kama kawaida hasa wadau na wapenzi wa filamu na Tamthilia huangalia tamthilia na kuzichukulia kama vitu vya kufikilika na kuburudisha, Lakini Wengi walioitazama Tamthilia ya NARCOS na wale wanaotegemea kuangalia Tamthilia hii
waelewe kwamba kila wakionacho kwenye tamthilia hii ni Historia ya kweli ya kumuhusu muuza madawa ya kulevya aliyejulika kama PABLO ESCOBER

Simulizi hii ya leo itaangazia Maisha ya Gaidi huyu aliyewahi kuishi kunako mwaka 1949 hadi 1993

Pablo Emillio Escober Gaviria alizaliwa
1, Decemba 1949 huko Rionegro Colombia na alilelewa na kukua katika mji wa Medellin, alisoma kwa muda mfupi ktk chuo cha Universidad autonoma latinoamericana cha Medellin, lkn aliacha chuo pasipo kumaliza wala kupata cheti, na baadala yake akaanza kujihusisha na vitendo vya
kiharifu, na uharifu wake wa kwanza aliufanya pale alipoiba jiwe la thamani linalowekwa kwenye kaburi kama nguzo na kulisaga na kwenda kuuza unga wake na baada ya hapo baadae pablo pamoja na mwenza wake Oscar Benel Aguirre kwa ushirikiano wakaanza uharifu mdogo mdogo wa mitaani
wakiwa wanauza sigara za magendo, na ticket za bahati na nasibu za kugushi na hakuishia hapo pia alijihusisha na wizi wa magari aliendelea na shughuli hizi hadi kufikia mapema katka miaka ya 1970 akanza kufanya kazi na wazee wa magendo ya madawa ya kulevya na watekaji wa watu na
baadae kudai malipo ili kuwarejesha watu hao.

Kuanzia mwaka 1975 Pablo akaanza kutengeneza madawa ya kulevya yaliyojulikana kama Cocaine na kuanza kuyasambaza kwa kutumia ndege na wakati huo walikuwa wanapeleka madawa kwenda Panama na pale njia za kuingiza madawa amerika
zilipopatikana ikamlazimu Pablo kuongeza ndege ambapo alinunua ndege zipatazo kumi na tano(15) kwa ajili ya kufanya usambazaji wa madawa.

May 1976 Pablo na wenzake wakiwa wanatokea Ecuador kurudi Medellin wakiwa na mzigo mzito wa kilo 18 wa white paste, walikamatwa na kuwekwa
May 1976 Pablo na wenzake wakiwa wanatokea Ecuador kurudi Medellin wakiwa na mzigo mzito wa kilo 18 wa white paste, walikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi, Pablo akanza figisu zake za kutaka kuwahonga majaji lkn majaji walikataa hongo, baada ya vita vya kisheria ya muda mrefu,
na hakuna ufumbuzi Pablo akaona isiwe shida kwani kesi iliwategemea sana polisi waliowakamata, basi Pablo akamlisha kikosi chacke cha mauaji kuwatafuta na kuwaua polisi wote wawili na wakauliwa, baadae kesi hii ikafutwa

kutokaa taarifa kutoka kwa kaka yake Roberto Escobar
alisema hapa ndipo Pablo alipojifunza kushughulika na mamlaka za nchi kwa kuwahonga au ikibidi kuwaua kabisai
Roberto alisema Pablo alijiingiza kwenye madawa ya kulevya baada ya kuona kwa kipindi hicho hapakuwepo himaya ya wauza madawa (drug Cartels) na hivyo kufanya biashara ya
Dawa kuwa hatari sana kwa sababu hapakuwepo mtu wa kulinda maslahi ya wauza dawa pia, Pablo akaona eneo hili lilikuwa halijaguswa na lilikuwa lenye faida zaidi, akaona vyema kama akilimiliki yeye.

Mafanikio makubwa ya Pablo yalitokea baada ya mahitaji ya cocaine nchini Merekani
kuwa makubwa sana, hapo Pablo akanza kutengeneza njia na mbinu, na kubuni aina ya usafiri wa kuingiza mzigo nchini Amerika, na kutengeza mtandao wa kusambaza dawa nchini Amerika hasa Florida kusini, California na sehemu zingine za nchi hiyo, pablo na mwenzake Carlos Lehder (hawa
wawili kwa pamoja ndo waliunda hii Medellin Cartel) wakaanzisha njia mpya ya kupitia visiwa vya bahama kwenye kisiwa cha Norman's Cay ambacho kilikuwa km 350 kutoka kusini mwa pwani ya Florida kisiwa hiki sehemu kubwa yake ilimilikiwa na Carlos Lehder ikiwa na uwanja wa ndege wa
km 1, bandari, mahotel, majumba, boti na wakajenga nyumba ya barafu(Refrigirated warehouse) kwa ajili kuhifanzia Cocaine ili zisiharibike kuanzia mwaka 1978 hadi 1982 kisiwa hiki kilitumika kama njia kuu ya kusafirishia madawa ya kulevya. Baadae pablo alinunua eneo lenye ukubwa
wa eneo za mraba zipatazo km 20, ambapo alijenga nyumba ya kifahari ikiwa na eneo la wanyama (zoo), akatengeneza ziwa (lake), bustani za kutisha, sehemu za siri na sehemu za kujificha yeye na familia yake haikuwa sehemu ya kawaida kabisa ilikuwa kama kufuru

Pablo inasemekana
Alikuwa anaingiza Amerika kiasi cha tani zipatazo 70 hadi 80 kwa mwezi huwenda usielewe ukubwa wa hiki kiwango, hiki kiwango ni sawa na kusema ukiwa na magunia yenye kilo 100 utahitaji jumla ya maguni 800 ya kilo 100 kupata tani 80 hii ina maana jamaa alikuwa anaingiza magunia
800 Cocaine kwenda kuumiza watu nchini Amerika ndo maana anaitwa gaidi wa dawa za kulevya (Narcoterrorist). Inasemekana mzigo mkubwa ambao Pablo alishawahi kuusafirisha kwa mara moja ulifikia kilo 23000 sawasawa na magunia ya mahindi 230 ukiwa umechanganywa na vipande vya samaki
vya samaki kwa mara moja kwa kutumia boti, na baadae akaanza kutumia Nyambizi (submarine) mbili kusafirishia madawa katika uzito mkubwa, huyu alikuwa mwanaume bwana na kati asiye na mfano.
Kufikia mwaka 1982 akachaguliwa kuwa mwakilishi wa chamber of representative of Colombia na
pia alikuwa mwakilishi wa serikali ya Colombia ktk kumuapisha rais wa Spain Felipe Gonzalez.
Baada ya haya yote Pablo akaanza kufahamika Duniani kote na dawa zake kufika Mexico, Puerto Rico, Dominican Republic, Venezuela and Spain

Shambulio la mahakama kuu ya Colombia
lililofanyika mwaka 1985 Inaaminika lilifanywa kwa udhamini wa Pablo ambapo kikundi cha wanamgambo wenye mlengo wa kushoto waliivamia mahakama kuu ktk shambulio la mzingo lilifahamika kama M-15, hawa watu walilipwa kuingia mahakamani na kuchoma nyaraka zote za kesi na karatasi
zote zilizohusu kikundi cha wauza madawa ya kulevya waliotakiwa kushikwa na kupelekwa Amerika (Los Extraditables) na Serikali ya Colombia, Shambulio hili liliua nusu ya majaji waliokuwa wanajadili hoja hiyo kisheria na kuangalia mikataba kati ya Colombia na Amerika. Mateka
waliochukuliwa walitumiwa kama njia ya kuwezesha kupata majadiliano ( negotiations) na kuzuia kabisa mpango wa serikali wa kuwapeleka watu Amerika

Kipindi wakati biashara za Pablo zilpokuwa kileleni Medellin Cartel ilikuwa inaingiza kwa siku dola za kimarekani zipatazo milioni70
kwa siku ambazo ni sawa TShs bilioni 175 kwa siku kwa rate exchange ya leo, na alikuwa anasafirisha tani 15( kilo 15,000) kwa siku hii ni sawa na magunia 150 yenye kilo 100 za dawa za kulevya, Pablo alikuwa anatumia dola 1000 za kimarekani kwa siku kununua vifungushio vya pesa
Rubber bands). Wakati huo huo kila mwaka asilimia 10 ya hela zote zilikuwa zinaliwa na Panya kwa kuwa zilikuwa zinahifadhiwa kwenye maghala
Kuna wakati Pablo aliulizwa ni kwa jinsi gani anaweza kuifanya biashara hii alijibu ni rahisi watu hawana hela na wanahitaji hela
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!