My Authors
Read all threads
QUEEN & SLIM
Ngoja leo tuhame kabisa kutoka India na kurudi pale amerika ambapo nimegundua mavitu ya huko wengi wanayaelewa, leo ningependa tuiangazie filamu ya Kinyanyasaji iliyotengenezwa kuonyesha manyanyaso wayapatayo watu wa ngozi za kwetu huko America, filamu hii itakutia
simanzi kubwa sana kwa yale yanayotokea ndani yake ,kuonyesha hicho nilichokiongea hapo juu.

QUEEN na SLIM ni picha ya kimarekani iliyotoka mwezi Novemba, 2019 na kuzinduliwa Rasmi tarehe 14, Novemba (premiere), na kuanza kuonyeshwa kwenye majumba ya sinema nchini Amerika
kuanzia Novemba 27, 2019. Hii ni filamu ya kimapenzi yenye maonjo ya kiharifu na drama za kutosha, iliongozwa na muongozaji (director) Melina Matsoukas na kuandikwa na Lena Waithe kutoka kwenye story iliyoandikwa na James Frey na Lena mwenyewe. Filamu hii ilipata mrejesho chanya
kutoka kwa wakosoaji na wapanga viwango vya filamu duniani na kuweza kupata kiwango cha 83% kutoka mtandao wa Rotten Tomatoes na kupata 7.1/10 katika viwango vya mtandao wa IMDb na watazamaji wa kwenye majumba ya cinema waliipa filamu hii alama ya A- ( kutoka kwenye alama
zilizoanzia A+ hadi alama F) kwenye kura zilizoendeshwa na watu wanoitwa CinemaScore.

Story ya picha inaanzia pale ndugu yangu Slim anapokuwa na kidate cha mlo wa jioni na mdada aitwaye Queen ambaye ni wakili wa makosa ya uharifu (Criminal attorney). baada ya msosi Slim akiwa
anamrudisha Queen nyumbani wanakutana na msala ambao ndo unabeba kisa kizima Cha filamu hii. Kama ujuavyo wapenzi wakiwa pamoja kuna vitu vidogo vidogo vinaweza kutokea ktka maongezi vilivyopelekea gari yao kuyumba kidogo, na kwa bahati mbaya kitendo icho kilimvuta polisi wa
kizungu na kupelekea kuwasimamisha. Polisi huyu akamshusha Slim na kuanza kumnyanyasa huku ameshikilia bastola, hapa tunatakiwa tuelewe makuzi ya vijana hawa wawili moja kutoka familia zisizo za fujo na mmoja kutoka familia za kibabe, Mdada Queen kutoka zile familia za kitaa
akaona hii Hapana akatoka na simu yake akaanza kurekodi matukio hayo kwenye simu yake, polisi baada yakuona hivyo akajua hii noma na mkwala wake akampiga risasi Queen kwenye Mguu kitendo kilichomfanya mzee mzima Slim kumvaa polisi yule na baada ya purukushani Slim aliweza
kumnyang'anya silaha yule polisi na Kisha kumpiga risasi na kumuua.

Hapo sasa msala ukaiva black kamuua polisi wa kizungu, Queen akamwambia mzee mzima kuwa hapa mpango mzima ni kukimbia ama sivyo maisha yao yataishia jela, wakabidi waanze masafa ya kukimbia na kutoweka kabisa
kama ikiwezekana watoke nje ya nchi, siku ya kudead nyani bwana miti kweli huteleza, hawa wapendanao baada ya kutia gia za kutosha kiwese kwenye gari kikakata, ikabidi Waiache gari waombe lift na hapo ndipo msala wa pili unapotokea kwani pickup walioisimamisha ilikuwa ni ya mkuu
wa polisi(Sheriff) wa mji wa Kentucky wakiwa wamefika kituo cha mafuta ambapo Slim na Queen walikuwa wamebaki kwenye gari na polisi kuingia ndani ya kituo ambako inaokana kupata taarifa kupitia radio call aliyoivaa kiunoni za kuuwawa kwa polisi mwenzao na watu weusi wawili wa
kike na wa kiume, na hapohapo akawatambua kuwa abiria wake ndo hao waharifu,

Queen akashtukia msala kabla ya polisi kurudi kwenye gari, alipofika akashikiwa bastola na kuamrishwa kuendesha gari kurudi pale akina Slim walipoacha gari yao, walipofika hapo wanafanikiwa
kumtumbukiza kwenye buti la gari lao liloishiwa mafuta na wao kuchukua gari la huyu mjeda na kuelekea New Orleans Ambapo walikuwa wanaenda kumuona mjomba wao ambaye angewasaidia mpango mzima wa kutoroka, kufika huko mjomba akawa mgumu kuelewa somo, baada ya kupeana vipande vya
maneno na kukumbusha misaada ambayo ilishawahi kutolewa mjomba akalegea, Slim akashauri watorekee Cuba na mjomba akawaambia akiwa vitani Iraq aliweza kuokoa maisha ya bwana Shepherd ambaye ni mtu pekee angeweza kuwasaidia kutoroka kutokea Miami hadi Cuba.
Asubuhi wakiwa njiani kuelekea Florida gari waliloazima kwa mjomba lina haribika wanaamua kulipeleka gareji iliyokuwa inamilikiwa na mtu mweusi, siku ya pili Queen anatembelea kaburi la mama yake akiwa na Slim hali ya majonzi na ukaribu uliwapelekea hawa watu wafahamiane kwani
kwani hii siku Slim alimjua Queen (have sex) wakiwa ndani ya gari. Baada ya hapo Slim na Queen wanaenda kumuona Bwana Shepherd lkn majirani walivyowaona tu wakaita polisi.

Naomba niishie hapa Kama vipi Wazee maana mzigo una noga na ndo picha linaenda kuwaka so ili nisiharibu
filamu hii kwa maana baada ya hapa sasa filamu inaenda sehemu nisiyotakiwa kusimulia kwani nitakuwa nimemaliza picha nzima,

Filamu hii ilichaguliwa(nominated) kwenye awards zipatazo 42 🙌katka hizo filamu hii ilishinda awards 9💪na zingine 9 hazijatolewa maamuzi zipo kwenye
mchakato

Filamu ilitengenezwa kwa bajeti ya dola milion 17 hadi 20 na ilingiza dola 44.6
Picha hii iliingiza dola milion 1.7 kwa siku yake ya kwanza na siku ya pili iliingiza dola milioni 2.4 hadi kufikia mwisho wa wiki ikawa imeingiza dola milioni 11.9 zikiwa zimebaki
dola chache kurudisha hela ya uzalishaji.

GOOD NEWS mzigo uko tayari #cipherdotseriesandmovies tena in 1080p kabsa jisogeze zako mitaa ya mkabala na sido pale bila kusahau kibebeo Chako tu muhimu
Pata kuona hiki kipande kidogo.
Mtuwie radhi mtandao huku kwetu unasumbua sana tangu asubuhi tweet zinashindwa kwenda
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!