, 19 tweets, 9 min read
MATUKIO YA WANAUME KUJIUA: Tutafunika kombe mwanaharamu apite hadi lini? #Thread

Wiki chache zilizopita, vyombo vya habari vilipambwa na habari kuhusu wanaume kuongoza kwa matukio ya kujiua.
Jambo hili bado halijapewa uzito sahihi.
Ungana nami💭
#AfyaYaAkili
#DaktariMwandishi 👣
Wanaume wapo kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya akili kutokana na msongo wa mawazo.
Vihatarishi huanzia kwenye uchumi, ulevi, aina ya kazi wanazofanya na majukumu yanayowakumba.
Mfumo wa maisha unamshinikiza mwanaume kubeba majukumu mengi na wakati huo huo kumlazimisha
asionyeshe hisia waziwazi kama ishara ya "uanaume".
Hivyo basi, wanatembea na mizigo mikubwa ambayo baada ya muda akili zao hushindwa kuhimili na kukata tamaa.
Kuanzia mtoto wa kiume akiwa mdogo anapoumia anaambiwa, "wanaume hawalii" hivyo anakua akiamini kuwa mwanaume kuonyesha
hisia ni dalili ya UDHAIFU.
Ndio maana hawaongelei matatizo wanayokumbana nayo, na hata wanapoyaongelea wanayadogosha ili kuhakikisha uanaume wao una nguvu.
Utamaduni huu umesababisha watoto wa kiume kutoripoti pale wanaponyanyaswa kijinsia, jambo linalowaweka kwenye hatari zaidi
ya kupata magonjwa ya akili.

Zaidi ya hayo, anategemewa aweze kuijali familia yake, wazazi wake na hata wakwe zake. Hii inazidi kumuweka katika shinikizo, kufanya kila aliwezalo kuwaridhisha wote.

Wanaume wengi hutumia vilevi kama njia ya kukimbia matatizo yao. Ulevi ni sehemu
ya magonjwa ya akili, na huwaweka kwenye hatari ya kupata sonona na magonjwa ya muda mrefu kama vile shinikizo la juu la damu, kisukari, kiharusi n.k
Magonjwa haya ya muda mrefu nayo huchangia kudidimiza #AfyaYaAkili zaidi.

Tofauti na wanawake ambao wanapoelezea shida zao,
jamii inakuwa tayari kuwasikiliza, kuwasaidia na kuwahurumia, wanaume wanapojieleza jamii inawaangalia kama wanajidekeza na wadhaifu.
Hivyo wanaume wanakosa msaada wa kijamii.

Licha ya watu kulalamika kuhusu wanawake wa siku hizi kupenda pesa kuliko hapo mwanzo, kiini cha tabia
hii hutokana na jamii ambayo tangu mwanzo imekuwa ikitumia wanawake kama kitega uchumi, hivyo mchumba mwenye mali zaidi ndiye anayefaa.
Leo vijana wa kiume wanapata msongo wa mawazo kwasababu ya tamaduni hii. Waswahili wanasema, "ukipanda maembe usitegemee kuvuna mihogo"
Tatizo jingine lililoibuka hivi karibuni, ni maumbile ya sehemu za siri na nguvu za kiume, kuwa kipimo cha "uanamume"
Ingawa ni ngumu kukubali, lakini hili limewafanya wanaume wengi kutafuta dawa mbalimbali kuonyesha uanaume wao.
Wengi hupata msongo wa mawazo kutokana na hili.
Mapokeo mengi tunayoyakumbatia ndio yanayomuumiza mtoto wetu wa kiume leo.

Watoto wa kiume pia wanalelewa kuwa "mwanamke atakushindaje?"
Hii inaleta msuguano kati ya wanawake na wanaume, hasa wanapokuwa katika mazingira ya kushindana na wanawake.
Enzi zimebadilika, na wanaume
hawajaandaliwa kuyakubali mabadiliko haya. Hii inaongeza matatizo ya mahusiano ambayo ni kichocheo kingine cha magonjwa ya akili.

Utamaduni wa wanaume kuhisi wana haki dhidi ya wanawake pia ni tatizo. Hii imewaingiza katika matatizo mengi, hasa katika zama hizi ambapo mwanamke
anawezeshwa kumfanya awe na uhuru wa kiuchumi.

Mwanaume anayeonekana kama amepitwa kiuchumi au kiustadi na mwanamke, anadharauliwa na jamii. Anaonekana hafai. Hii si sawa!

Mambo haya na mengine mengi yanawaweka kwenye msongo kupelekea sonona na magonjwa mengine ya akili.
Waswahili wanasema, "Mficha maradhi, kifo humuumbua".
Wanayaficha maradhi, maumivu, matatizo na shida zao ili kulinda "uanaume" wao na kutulinda sisi.

Magonjwa mengine ya akili huwafanya wawe watenda makosa. Magonjwa ya kingono, kama vile wale wanaobaka watoto wadogo au wazee,
Wanaoridhishwa na maumivu ya wengine hivyo kufanya ngono zenye hatari (sadism) n.k na hata magonjwa ya utu kama Antisocial personality disorder huwafanya kuvunja sheria.
Jamii inawalinda wasishikwe na mkono wa sheria, hiyo haiwasaidii zaidi tunaharibu kizazi kijacho.
Mfumo uliopo si rafiki kwao. Wakati umewadia wanaume kuonyesha hisia lisiwe jambo la aibu. Wanaume ongeeni. Fungukeni. Elezeeni matatizo yenu. Tembeleeni vituo vinavyotoa huduma za #AfyaYaAkili kupata msaada mnaohitaji.

Jamii nayo iwe tayari kuwasaidia kwa kushirikiana katika
majukumu mbalimbali ya kiuchumi na kifamilia, badala ya kubweteka na kutegemea walishe ukoo wao na wakwe zao.

Ulevi si starehe, uzinzi na uasherati pia unachangia wanaume kujiua. Licha ya wao kuonekana kuongoza kwenye matukio ya usaliti, pale mahusiano/ndoa yanapovunjika, athari
kubwa huwakumba kihisia. Wengi hawajaandaliwa kuweza kulea familia (watoto) kinyumbani, hivyo wanalazimika kuingia kwenye mahusiano mengine ambayo huweza kuwa hatarishi kwao.

Mpaka wanaume watakapoamua kubadili mfumo huu, tutaendelea kuwazika kwa magonjwa ya akili ambayo
yanaepukika kabisa.
Uanaume haupimwi kwa uwezo wa mwanaume wa kuficha hisia, uwezo kiuchumi, ukubwa wa maumbile yao au nguvu za kiume.

Tuendelee kubadili mifumo ili kuepusha vifo vya kujiua. TUWAOKOE!
#AfyaYaAkili ni muhimu kwa maendeleo ya jamii.
ALAMSIKI💭
#DaktariMwandishi 👣
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Kuduishe Kisowile

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!