➡️Kisukari ni ugonjwa wa kudumu ambao hutokea pale kiwango cha sukari (glukosi) katika damu
kipo juu zaidi kutokana na kukosekana au mwili kushindwa kutumia homoni ya insulini
➡️Kiwango cha glukosi kikiwa juu kwa muda mrefu, husababisha madhara katika mwili
➡️Unapokula chakula, mfumo wako wa kumeng’enya hukichakata na kutengeneza glukosi.
➡️Glukosi inapoingia kwenye damu, husababisha kongosho lako kutoa homoni inayoitwa insulini.
➡️Insulini huzunguka mwilini na kuwezesha seli kupata glukosi ili kuitumia kuleta nguvu mwilini.
INSULINI NI KAMA FUNGUO YA GLUKOSI
➡️Inaruhusu glukosi kuingia kwenye seli.
➡️Wakati insulini haipo au imeacha cha kufanya kazi, glukosi katika mwili wako haiwezi kwenda mahali popote.
➡️Mwisho: viwango vyako vya glukosi katika damu vitapanda kuwa juu sana kupelekea kisukari
AINA ZA KISUKARI
➡️Kuna aina 3 za Kisukari zinazojulikana zaidi, ambazo ni:
• Kisukari aina ya kwanza (1)
• Kisukari aina ya Pili (2)
• Aina ya Kisukari kipindi cha ujauzito
KISUKARI AINA YA KWANZA
➡️Aina hii ya kisukari hutokea wakati mfumo wa kinga mwilini unashambulia kongosho na kusababisha lisiweze kutoa insulini ya kutosha.
➡️Aina hii huathiri zaidi watoto
UWEZEKANO WA KUPATA KISUKARI AINA YA 2
➡️Kila mtu ana kiwango tofauti cha hatari ya kupata aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari.
➡️Kiwango cha hatari kinahusishwa na mtindo wa maisha, umri, au sababu za kimaumbile (vinasaba).
VITU HIVI VINAKUWEKA KATIKA HATARI ZAIDI YA KUPATA KISUKARI AINA YA 2
➡️Unene uliokithiri
➡️Ulaji usiofaa
➡️kutokujishughulisha kimwili
➡️kuwa na umri wa miaka 45 au zaidi
➡️kuwa na historia ya ugonjwa wa kisukari aina ya 2 katika familia
BAADHI YA DALILI ZA KISUKARI
➡️kwenda haja ndogo mara nyingi sana, haswa wakati wa usiku
➡️kuhisi kiu kuliko kawaida
➡️kuhisi njaa mara kwa mara
➡️kuhisi uchovu sana
➡️kupungua uzito bila sababu
➡️vidonda kuchukua muda mrefu kupona uwezo hafifu wa kuona (kuona ukungu).
Watu wengi huishi na kisukari muda mrefu bila ya kutambua dalili hivyo ni muhimu kupima afya mara kwa mara walau mara moja kwa mwaka
KUDHIBITI KISUKARI
1⃣Shugurisha mwili (k.m kutembea) – zingatia mazoezi walau dakika 30 katika mazoezi ya kila siku ya wiki.
2⃣Zingatia lishe bora
3⃣Punguza uzito wako au dumisha uzito wenye afya kiadili
4⃣Punguza utumiaji wa chumvi
5⃣Tembelea kituo cha afya ya ugonjwa wa kisukari kupata uangalizi wa mara kwa mara ikiwemo kupima viwango vya sukari kwenye damu, shinikizo la damu, lehemu (cholesterol), figo,moyo, macho na afya ya meno
6⃣Angalia afya ya miguu yako-kila siku
7⃣Acha uvutaji wa sigara
➡️Tatizo la dharura la kiafya ambalo ni moja ya magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo.
➡️Mitindo ya maisha na Lishe ni vitu vinavyochangia wagonjwa wanaopata stroke kuongezeka
➡️Kiharusi huacha ulemavu au kifo
➡️KIHARUSI hutokea pale seli za ubongo 🧠 zinapokufa kutokana kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo hivyo kukosa hewa ya oksijeni na virutubisho.
➡️Kiharusi kikihusisha mshipa wa mkubwa wa damu kwa wastani mgonjwa hupoteza seli za ubongo (neuroni 1.9) kila dakika.
KUNA AINA KUU MBILI ZA KIHARUSIBrain
1️⃣Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo
2️⃣Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo
🗒️80% ya watu wanaopata kiharusi hutokana na kuziba kwa mishipa ya damu kwenye ubongo.
Matumizi holela ya dawa aina ya antibiotiki huchangia usugu wa dawa kutokea.
Bakteria wanapopata usugu husababisha
➡️Kutokupona ugonjwa hata baada ya kutumia antibiotiki ambazo zimekuwa zikitibu ugonjwa huo
➡️Kuongezeka kwa gharama za matibabu
➡️Kifo
Unatengeneza tatizo usugu wa dawa iwapo
➡️Humalizi dawa ulizoandikiwa na daktari
➡️Unatumia dawa zisizo na ubora/feki
➡️tumia dawa zilizoisha muda wake wa matumizi
➡️Unakula nyama, maziwa, mayai au damu yenye masalia ya antibiotiki kutoka kwa mifugo iliyotibiwa
Inaweza tokea katikati ya usingizi mtu hasa mtoto akawa na tabia ya kutembea,kuongea au kufanya vitendo vingin akiwa usingizini
Hii ni SLEEPWALKING
Hutokea zaid kwa watoto hasa wavulana,inahisiwa hutokea kwa sababu mfumo wa ubongo kudhibiti msawaziko wa kulala/kuamka haujakomaa
Tabia ya kutembea au kuongea usingizini ikianza kwa mtu mzima inahusishwa na msongo mkubwa wa mawazo muda mwingine aina ya kifafa
🔵Tatizo la kutembea usingizini hutembea katika familia; 45% ya watoto wanaotembea usingizini pia na wazazi wao walitembea usingizini
Inaweza tokea katikati ya usingizi mtoto akaamka anapiga kelele,akazubaa kama Dakika 10 bila kujua nini kinaendelea akarudi usingizini kama hakijatokea kitu. Kesho akiamka hajui nini kilitokea.
🔵Hii ni SLEEP TERROR ni tatizo ambalo huambatana tatizo la kutembea usingizini
THREAD | MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO
KWANZA : Vidonda vya tumbo hutokea pale mfumo unaolinda kuta za tumbo unaposhindwa kazi hivyo asidi ya tumbo kuchoma kuta na kuleta kidonda/mchubuko.
🔵 Sababu kuu huwa ni maambukizi ya H. Pyroli na Dawa kundi la aspirin
Mtu mwenye vidonda vya tumbo hupata shida kama:
1️⃣Maumivu makali ya tumbo yanayochoma mara nyingi eneo la chini ya chemba ya moyo
2️⃣Tumbo kujaa gesi
3️⃣Kiungulia
4️⃣Uchovu huweza kutokea kama kuna upungufu wa damu kutokana na vidonda
5️⃣Kinyesi cheusi humaanisha vidonda vinatoa damu
Vidonda huweza kutokea tumboni au kipande cha kwanza cha utumbo
✍️Kidonda kilicho tumboni husababisha maumivu makali mara tu mtu anapokula;
✍️Kidonda kikiwa kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo husababisha maumivu mtu anakuwa na njaa, maumivu huisha mtu akila