My Authors
Read all threads
SABABU KWANINI HARMONIZE AMEONDOKA WCB

Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu Harmonize aondoke WCB kumekuwa na sitofahamu nyingi kuhusu kwanini konde boy ameondoka WCB

Tuwekane sawa kidogo inekuwa ngumu sana kuujua ukweli kwasababu sio WCB wala Harmonize amekuwa tayari
Kulizungumzia hili sababu zao binafsi huku WCB kama taasisi inalinda siri za kibiashara huku Harmonize akilinda heshima yake asije kuonekana mbaya kwa mashabiki lundo wa WCB(public sympath)

Swali linabaki kwanini aliondoka WCB?
WCB ikiwa recording lebel kubwa na ikiwa na kila kitu nikiwa namaanisha kifedha,managers wenye uzoefu mkubwa wa zaidi ya miaka 20 kwenye game ya kiwanda cha bongo fleva huku wakiwa na ushawishi mkubwa wa kumfanya msanii mdogo kuwa mkubwa ndani ya siku moja pamoja na
Kuwa na kamati ya fitina(promotion strategies) mtu kama mkubwa Fella yule Dj wa Radio ya mkoani huko wewe unaemchukulia poa kila siku ana uwezo wa kumtumia elfu 50 ya vicha ahakikishe msanii wake
Anapigwa hata mara3 kwa siku, mfano Babu Tale ana uwezo wa kuhakikisha CD ya nyimbo ya msanii wake inafika Afrika mashariki ndani ya siku moja kila radio unayoijua na usioijua wewe

Lakini swali linabaki pale pale uwezo wote huo wa WCB lakini Harmonize kwanini aliondoka WCB?
Sababu zipo zaidi ya 10 ila nitaangazia sababu kadhaa kuu za Harmonize kuondoka WCB

Kama mgeni nikukaribishe kwenye uzi huu maarufu ujulikanao kama #sanukanachapo shuka na mimi mpaka mwisho
SABABU ZA KUONDOKA

Sababu ya kwanza kabisa iliomfanya Harmonize kishindwana na WCB ni ‘kiburi’
Harmonize ama Jeshi anavyopenda umwite ni msanii bora wa mwaka 2018-2019 huki ngoma yake ya Kwangaru alimshirikisha boss wake Diamond ikiwa moja ya ngoma bora za muda wote
Huku ikivunja record kibao kwenye mziki wa bongo, Harmonize alianza ingiea na kiburi baada ya kuanza kupata mafanikio akawa hamsikilizi mtu yeyote labda Diamond pekee
Unapozungumzia mafanikio ya Harmonize huwezi kuacha kulitaka kijan la Ricardo Momo yeye ndiye
Aliemfanya Harmonize kuwa hapa leo, kuna mtu atasema chapo mbona humtaji sallam Sk aliempeleka Harmonize south Africa ku shoot ngoma yake ya kwanza kabisa!
Ila mtu atakeniuliza swali hilo na mimi nitamjibu kwa swali kuwa unamjua aliewasiliana na Harmonize hadi
Kuja WCB? Yes anaitwa Ricardo Momo huyu ndiye aliemuonesha radio na Tv zote Tanzania mlango uko wapi nani wakumuona ukiwa unataka interview kwa kifupi ricardo Momo ndiye aliemtengeneza Harmonize ukiachana na boss Diamond
Ila cha kushangaza walikuja kuzinguana na Harmonize na kutokuwa washikaji tena na ikabidi Harmonize atafutiwe manager mwengine aitwae Mr. Pua ambae kama ulikuwa hujui huyu jamaa ndiye aliemfungulia Harmonize youtube channel yake ambayo mpaka kufikia mwaka 2018
Ilimuingizia Konde boy zaidi ya milioni 360. Ila nae wakaja kubwagana kwa kebei nyingi huku Harmonize akidaiwa kuwa alikuwa jeuri na asie msikivu tena kama awali wakati anatoka alikuwa very humble

Harmonize huyu wa kwangaru alikuwa agusiki anaweza kumfokea manager mbele za watu
Kwa jambo ambalo alikuwa anaweza kumuita chobingo kifupi aligombna na managers wake hao kwasababu ya kiburi nikichokieleza hapo hawali ila alikwenda mbali zaidi akawa anavimbia kifua mpaka Babu Tale na Sallam Sk ambao ndio topo bosses nafikiri unanielewa sasa kiasi
Gani bwana jeshi kiburi kili mjaa. Wazee wa zamani wana msemo ukiona unagombana na kila mtu ujue una tatizo

Wazee mtakuwa mmelala naona tuendelee kesho ila nikiona mko macho basi tutaendelea kumbuka tupo kwanza sababu ya kwanza.
SABABU ZA KUONDOKA

Inaendelea ilipoishia....
Ukiona unagombana na kila mtu ujue una tatizo.

Sababu ya pili ya Harmonize kuondoka WCB ni ‘Uhuru’
Ilifika wakati Harmonize gari lilishawaka
Nakurudisha kidogo nyuma mpaka kipindi Harmonize ametoa EP yake
Ijulikanayo kama Afro Bongo iliotoka mnamo February 25,2019 ikiwa na ngoma kama kainama,tepete,show me what you got na niteke
Hizi ngoma na EP hiyo ndiyo iliomfanya Harmonize kuwa mkubwa.
umo ndani akiwa amemshirikisha msanii mkubwa na anayefanya vizuri Afrika ‘Burna boy’
Namamanisha kuwa Harmonize alikuwa mkubwa ila EP hii ilimfanya kuwa mkubwa sana Afrika mashariki na kati huju akijaribu kupenya Afrika ya mangharibi.

Tarehe iliotoka EP hiyo ama tuiite album(ili tuelewane) si tarehe Harmonize aliyopanga kutoka kwa album hiyo bali
Alitaka itoke week moja kabla, ila Sallam SK aligoma na kupanga siku kadhaa mbele wakati Konde boy alishaitangazia umma kuwa mzigo unadondoka week hiyo kitu kilichomuumiza sana Harmonize.
napose Harmonize aliitaji uhuru namanisha
Uwezo wa kuamua ngoma gani itoke kwa wakati upi kwasababu msanii anajua muda sahihi wa kutoka ngoma ila WCB walikuwa wakiwapangia wasanii ku rotate na kutoa muda pale managers wao watakapoamua
Hermonize ni kati ya wasanii wanaosikiliza sana nyimbo za zamani nikiwa
Namaana kuwa Harmonize ana playlist ya ngoma kibao za zamani hali iliomfanya kuhusudu kurudia nyimbo za zamani au kufanya collabo na wasanii wa zamani, utakuwa shahidi kuwa kuna kipindi Harmonize alikuwa na tendency ya kuachia ngoma na wasanii wa kitambo kama vile
Prof Jay,Ben pol na Qchief ila inasemekana alikuwa akiachia ngoma na kufanya collabo bila kushirikisha management, kwenye interview moja Sallam SK alisema kuwa “kuna wakati Harmonize alikuwa akitoa ngoma bila kutushirikisha na alienda mbali zaidi alikuwa aki
Mmanage Qchief bila baraka za WCB”
ila tunarudi palepale kuwa Harmonize kuondoka WCB alihitaji uhuru na kiu ya maamuzi kwani ilifika kipindi alijihisi yupo kama kifungoni.
kutokana na hii sababu Harmonize ilikuwa ngumu kubaki WCB.
Twende sababu ya Tatu👇
SABABU YA KUONDOKA

Sababu ya tatu ni Pesa vs Mzungu
Harmonize alianza kubadirika baada ya kuanza ku date na sarah mtoto wa kiitaliano ambae kuhusu hela kwao kuna mfeleji una kinga tu nikiwa na maana marehemu baba yake na Sarah alikuwa na hela sana so wameachiwa
urithi wa pesa chafu, unawajua ma don wa kiitali, kama umecheki filamu inaitwa Godfather utakuwa unanielewa basi dingi wa Sarah alikuwa kwenye hizo mbanga.
Konde boy anatoka maisha ya kawaida tu kuna uwezekano hata maisha aliyonayo sasa hakuwai hata
Kuyaota ,kifupi ukichukua hela za muziki ukachanganya na za Sarah Harmonize kwa sasa ana hela nyingi,hata Diamond aliwai kukili hilo kuwa “pale WCB msanii mwenye hela ni harmonize”
Kwa jeuri ya pesa Harmonize alinunua gari zote kama anazo miliki boss wake hata uo mjengo
Ambao unakaribia kuisha ambayo ni ghorofa sio wa kitoto. Wana saikolokia wanasema kuwa hakuna kitu cha hatari kama kumiliki pesa nyingi ukiwa na umri mdogo hicho ndicho kilicho mtokea Harmonize jeuri ya pesa hakukuwa na mtu wa kumwabia kitu bali Diamond pekee
Ilifika kipindi Babu Tale na Sallam walikuwa hawana sauti kwake mfano wakati anaenda Nigeria kufanya baadhi ya collabo alipaswa kwenda na Babu Tale ila Harmonize alikataa akasema anataka kwenda na Sallam Sk kitu ambacho kilimuuzi sana Babu Tale na kusababisha
Hadi Diamond kuingilia kati na kumcheki ila Harmonize kwenye simu kulikoni ila Harmonize akamjibu Mondi kuwa hafeel kiwa confortable akiwa na Tale sababu ana maneno ya kuudhi(Tale alishaona mabadiriko ya Harmonize kwaio muda mwingi alikuwa akimkumbushia kuwa asijisahau)
Harmonize akaendelea kujizatiti zaidi akafuta email ya Sallam Sk Kama booking email na kuweka ya kwake yeye kwamba show zote zipitie kwake kwenye page zake za instagram na mitandao mengine.
Harmonize akaanzisha kundi lake liitwalo Konde gang na ku waajiri watu wote muhimu kwa
Lebel kama mpiga picha,assistant manager(mchopanga) aliweai kuwa mtangazaji wa Dizzim Tv ya Sallam na Babu Tale na wengine wengi kifupi Harmonize alikuwa na full management kitu ambacho baadae kilikuja kuwa kirusi kwa WCB kwani Konde gang ikawa kubwa sana mpaka
Harmonize akawa kwenye show za wasafi akawa anaenda na Bus binafsi la Konde gang badala ya wasafi festival tour bus, pia akafanikiwa kuwa na kampuni ya kutengeneza video ya Zoom Production ambayo badae Diamond aliingia tamaa nakuwa mbia, ila zoom production founder ni
Harmonize na si Diamond. Hivyo kuwa na Kampuni ya video production Harmonize alikuwa na uwezo wa kufanya video vile atakavyo ndio maana akawa anafumua tuu mangoma badala ya kusubiri mpaka WCB watoe hela ya ku shoot. So vyote hivyo ila bado kwenye show WCB wakawa
Wanataka asilimia zao za hela ya show sasa Harmonize akicheki video nafanya kwa hela yangu na studio ya recording chini ya bonga anafanya kwa gharama zake kwanini hawalipe WCB? Mwisho wa siku akaona anaweza kufanya kila kitu mwenyewe hawezi kubali kuwanufaisha watu
Ambao wemakaa tu kusubiri kukinga pesa za burebure ndio maana Konde boy akaamua kusepa. Nafikiri twende sababu ya 4 sasa na leo zote zinaisha hapa hapa kesho tunaanza mambo mapya karibuni #sanukanachapo 👇👇👇
SABABU YA KUONDOKA

Sababu ya nne ni upendeleo na kutofatwa mikataba.
Wakati nahaidi kuachia uzi pia nilisema nitaeleza sababu za kuondoka kwa Harmonize na watu wengine waliokuwa WCB kama vile kifesi,Almasi zambele na Rich Mavoko hii inaweza isimguse saana sana Harmonize bali
Hao wengine niliowataja hapo juu itawahusu zaidi ila Mtiga nitamzungumzia wakati mwengine sababu hakuwa WCB bali alikuwa WASAFI MEDIA.
WCB kuna upendeleo sana na kukiukwa kwa mikataba kupindukia mfano Rich Mavoko japo alisemekana ni kati ya wasanii wavivu waliokuwa
Wanategemea sana manager bila kuji push mwenyewe ila kutofatwa kwa mikataba kulimuumiza sana mfano mktaba wake ulikuwa umeeleza wazi kuwa atafanyiwa video tatu kwa mwaka ila aliishia kufanyiwa video mbili, alafu wenzake wanafanyiwa hata video 5 ungekuwa wewe
Ungefurahi?, japo kifesi alieleza wazi aliondoka WCB ili kukaa mbali na anasa japo bado anafanya kazi kwenye events/harusi zenye bia nakadhalika ila kiundani sababu ilikuwa ni Lukamba safari zote ana safiri yeye tu wakati aliajiriwa kama videographer na Kifesi alisafiri kamaa
Mpiga picha ila mwisho Lukamba akawa anafanya vyote, Kifesi ndiye alie design logo ya WCB ofisi ikiwa sinza kibarazani kwa Diamond ila mwisho alionekana kama takataka na kuthaminiwa Lukamba mgeni, unaambiwa Diamond akimpenda msanii hafichi maaba atampendelea kwenye
Vingi utatazama tu jinsi Mbosso anavyopendwa atapigiwa promo kuliko msanii yoyote tena ya nguvu kitu ambacho si vyema, laikini pia WCB mishahara inatoka tarehe 40 😷
Nikiwa namaana kuwa wafanyakazi WCB kama Almasi zembele alisepa sababu ya upendeleo na kucheleweshwa kwa
Mishahara, Qboy msafi alifukuzwa sababu ya upendeleo pia kwa maana kosa alilofanya lilikuwa dogo kulinganisha na hukumu wakati pale WCB kuna wasanii wasio na adabu kama Harmonize ila walikaushiwa(double standard) japo Qboy nae alikuwa na madhaifu yake. Itaendelea part 2
SABABU ZA KUONDOKA WCB
Inaendelea iliposhia upendeleo na kukiukwa mikataba ambapo ma managers wa WCB uwa wanajinadi kuwa wanafanya kazi kwa mikataba ukweli ni kuwa sheria za mikataba zinakiukwa ilapia elimu nayo inakuwa kikwazo japo wana uzoefu nikiwa na maana kuwa
Hakuna manager wa WCB ambae amesoma mwenye elimu kubwa ni Babu Tale ambae amesoma form four Makongo baadae akasomea cheti chuo cha bandari,Fela la saba na Sallam Sk hakumaliza form four licha ya yote hayo wanaiongoza taasisi kubwa kama WCB kwaio uswahili,ubabe na
Ukosefu wa busara unaachangia sana kuyumbisha lebel ya WCB ambapo inaendeshwa ki uzoefu tu si kiutaalam. Nafikiri tuendelee na sababu ya tano chapchap tumalizane kabisa 👇👇👇
SABABU ZA KUONDOKA WCB

Sababu ya tano ni Fursa ya biashara, Diamond aliiiona fursa ya biashara kwenye mziki wa bongo fleva, Alikiba ameshindwa kabisa kuwa mshindabi wa kweli kwenye kiwanda cha bongo fleva licha ya ukweli kuwa ana king music yenye wasanii damu changa ambao
Walitarajiwa kuleta ushindani ila imekuwa tofauti, hakuna mtu atakaebisha kuwa WCB wamekuwa mabepari wamuziki kwenye soko zinaenda bidhaa zao tu mziki unapigwa ni wao tu,ikafika kipindi youtube on trending zinashindana video za WCB tu, mpaka sasa radio ambazo hazipigi nyimbo
Za WCB zikaanza kupoteza radha maana contents zipo WCB na radio uwazungumzii WCB nani atakuelewa? Vipindi vya top 20 hakuna ngoma ya WCB kisa tuu hawako nao sawa wakati ngoma kali zilikuwa WCB!
Halii hii ilisababisha kufa ama kuzimia kwa kipindi cha SHILAWADU
ambao walikatazwa kuwazungumzia WCB kabisa wakati umbea wote upo WCB. Sasa tunaelewana kiasi gani mziki wabongo ulipoteza ushindani na medi houses zilipoteza contents.
Diamond kuona hilo akakaa chini na Harmonize na kukubaliana kuwa atoke WCB aende kuanzisha
Lebel yake ili kuleta ushindani na wapige hela.
Kuna mtu atasema “Chapo umechanganyikiwa wewe hili linawezekana vipi mbona managers wanampiga majungu na fitina sikuizi konde boy?” Ningemjibu tulia wewe sisi ndio wataalam 😂
Iko hivi kuna WCB na kuna Diamond Platnumz
Ni vitu viwili tofauti, nikiwa namaanisha kuwa Harmonize ana bifu na WCB na sio Diamond. Mmmh sijui tunaelewana hapa?
Makubaliano ya Diamond na Harmonize yalikuwa nje ya WCB na Diamond kawekeza hela Konde gang nikiwa namaanisha yeye ndiye boss na manager mkuu wa
Harmonize Jembe ni Jembe ni mshikaji wa damu wa Diamond kabisa. Diamond aliona Harmonize ameshakuwa mkubwa kwanini isiwe biashara ndio maana mpaka leo Harmonize kwenye ngoma anaendelea kumtaja Diamond nikiwa na maana hawa jamaa wanatuchezea akiki zetu hakuna
Bifu kati yao bali bifu lipo kwenye uongozi wa WCB na mbaya zaidi WCB hawajui biashara ya Diamond na Harmonize.
Katika uzi huu kama umeufatilia sikuwai kumzungumzia tatizo la Harmonize na Diamond kwasababu hajawai kuzinguana hata kidogo nikiwa namaana Harmonize na
Jeuri yake anamuheshimu sana Diamond ndiye mtu pekee anaemsikiliza.
Mbona sasa alidaiwa pesa na WCB? Ndio alidaiwa pesa sababu mkataba uko hivyo na managers wa WCB wako after money na waliingiwa na hasira baada ya Harmonize kuandika barua na kumwachia mwanasheria
Wake amalizane na WCB kitendo hicho managers wa WCB waliona kama dharau walitarajia Harmonize atakuja waongee wamseme kama kawaida yao 😂 ila konde aliwakwepa na hakuwai kwenda tena WCB wala WASAFI MEDIA mpaka leo.
Na anachokisema Harmonize kuwa alishindwa kulipa
Pesa anazodaiwa WCB sio kweli kwamba aliuza nyumba Harmonize hela ya kuwalipa alikuwa nayo na hakuuza nyumba bali aliongea vile kwenye media ili apate huruma ya watu(public sympathy) wabongo wanapenda kusupport upande unaoonewa ndio maana watu walimsapport sana Diamond
Wakati wa bifu lake na Clouds media ndio wabongo tulivyo na jamaa wanalijua hilo 😂

Ila kitu ambacho Diamond na Harmonize wamekosea ni kumweka jembe ni jembe kama chief manager which is wrong, Jembe ni Jembe ni mfanya biashara mzuri ila hana uzoefu ku manage msanii
hivyo Harmonize ni jeshi la mtu mmoja na mastermind mwenyewe na hii ni kwasababu alikuwa karibu na Diamond hivyo alijifunza vingi chocho zote na namna ya kupambana.

Sababu zipo nyingi zaidi ya kumi ila nimeona kuangazia hizi kadhaa(5) hope mme enjoy uzi huu kwa wale ambao
Naweza kuwa nimewakwaza mniwie radhi ila naashukuru sana kwa kunipa muda wenu kwangu imenioa nguvu kuwa nachokiandika watu wanafatilia hivyo kwangu imekuwa changamoto ya kuboresha zaidi na zaidi.

-Mwisho

#sanukanachapo
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Chapo 🎧

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!