My Authors
Read all threads
Thread: Majina/Miaka sio ya kweli.
Joseph alihitimu chuo mwaka 2011, akaanza kutafuta kazi kwa bidii kwa kutuma maombi sehemu nyingi. Ila zote hizo hakufanikiwa kupata, ila hakukata tamaa. Mwaka 2012 katikati kaka yake mkubwa alimsaidia kumconnect na rafiki yake aliyesoma nae
👇🏾
Kaka yake alichukua CV/vyeti vya Joseph na kumtumia rafiki yake ili amsaidie maana walitangaza nafasi ya kazi inayoendana nae(IT officer). Yule rafiki yake anaitwa Simon, alimsaidia Joseph na akaitwa kwenye interview kwa mara ya kwanza. Interview ilikuwa na round 3 za mchujo.
👇🏾
Usaili ulifanyika Morogoro, Mwezi 5 Joseph akaenda kufanya interview zake na alimaliza Salama. Mwezi 5 mwishoni alipigiwa simu na HR kuwa amefanikiwa kupata kazi(mkoani), anatakiwa kuanza mwanzoni kabisa mwa mwezi 6. Kampuni ile ni ya kimataifa, ilipofika siku Joseph akaenda.
👇🏾
Akapewa mkataba asome, alifurahi sana maana mshahara ulikuwa mzuri kulingana na ndo kazi yake ya kwanza. Akapewa pia Sera za kampuni baada ya kusaini mkataba. Alipomalizana na taratibu zote alianza kazi rasmi. Joseph alijiambia kuwa “lazima nifanye kazi nioneshe uwezo wangu”.
👇🏾
Joseph hakujua tabia ya boss wake, boss wake ni Simon(rafiki wa kaka yake). Simon anapenda uboss, anapenda kuonekana ni wa juu, anapenda kunyenyekewa. Joseph alijitahidi kujifunza mazingira ya ile office(Morogoro) maana ilikuwa yupo kwenye uangalizi kabla hajaenda kituo chake.
👇🏾
Siku moja Simon alifika ofisini, hakumuona Joseph, alianza kumtafuta, kuuliza Bila mafanikio. Baada ya saa 1 Joseph akatokea, basi Simon akaanza kumfokea kwa sauti kubwa mbele za watu kuwa ni mvivu, hataki kujifunza, anakaa tu. Joseph akajibu, AC inavuja server room Niko huko
👇🏾
Simon akaona aibu akazuga akaondoka, watu walishangaa. Na tangu siku hiyo uhusiano wa Joseph na boss wake ulikuwa mbovu. Joseph alianza kufanya kazi kwa uoga na boss wake akaanza kumkandamiza zaidi. Joseph alikaza kibishi maana maisha ya mtaani sio mchezo. Kazi zikaendelea.
👇🏾
Baada ya miezi 2, Joseph alipelekwa kwenye kituo chake cha kazi Tabora. Huko alikutana na watu wachache sana kwakuwa Tabora ndo branch ilikuwa mpya. Joseph alifanikiwa kusimamia miradi mingi kipindi cha mwanzo na alifanikiwa kutengeneza marafiki ofisini na nje. Maisha ya Amani
👇🏾
Mkurugenzi wa Tabora alitokea kuelewana na Joseph, wakawa wanampa Hadi kazi za idara tofauti asaidie. Ila boss wa Joseph alikuwa hajui hayo yote kwakuwa Joseph alifanya kazi yake kwa ufanisi. Joseph alipendwa sana Tabora, watu wakaongezeka kwenye ofisi ya Tabora.
👇🏾
Ofisi ya Tabora ilikuja kuwa kubwa na maarufu kuliko ya Morogoro. Jina la Joseph likakua sana, watu walivutiwa nae. Boss wake akazidisha manyanyaso, Yaan hata Joseph asipopokea simu boss anamfokea kama mtoto. Joseph alivumilia Hadi ilipofika hiyo siku aliposema “SASA BASI”.
👇🏾
Miaka 3 baadae, Joseph aligombana vibaya sana na boss wake. Alimchana ukweli wote na kumwambia wewe ni mfanyakazi mwenzangu na sio kwamba kampuni ni yako hii. Tuheshimiane na tufanye kazi vizuri na sio kuzinguana. Simon alikasirika sana lakini hakuwa na jinsi huko aliko Moro.
👇🏾
Simon alipunguza manyanyaso Ila alitengeneza kinyongo kwa Joseph. Akaanza kumuwinda na kumtafutia visa. Joseph alikuwa makini sana, hakumpa nafasi ya kumuumiza. Kampuni hiyo ilitangaza kwenye ofisi zake zote duniani kuwa inafanya marekebisho na itawalazimu kupunguza watu.
👇🏾
Joseph hakuwa na wasiwasi maana alikuwa na uhakika nafasi yake iko Salama. Boss wake alijaribu kumhamishia Moro ili iwe rahisi kumuharibia, ila Joseph machale yalimcheza akakataa kwenda Moro. Simon akafeli tena. Ukafika muda wa kutangaza majina ya wale wanaopunguzwa kazini.
👇🏾
Simon alitumia mwanya huo Kama boss wa Joseph kumuumiza. Kiukweli Simon kwa siri alipendekeza jina la Joseph liwe miongoni mwa wanaopunguzwa bila kuangalia athari zake. Siku hiyo Joseph akaitwa Mbele ya HR/mkurugenzi na kuambiwa kuwa nafasi yake imepunguzwa na amepewa miezi 3.
👇🏾
Joseph haku-react na wala hakuonesha kushtuka. Alikubali na akasaini zile karatasi kwakuwa alikuwa anajua kwanini imekuwa vile. Watu wote pale Tabora walihamaki na kusikitika sana. Joseph aliendelea kufanya kazi Kama kawaida akisubiria miezi 3 iishe aondoke. Ila....!!!
👇🏾
Mkurugenzi mkuu(Mzungu) wa Tabora alienda kuongea na wakubwa zake kuhusu yale maamuzi. Alikasirika sana Kwanini wamuondoe mtu wa muhimu anayeijua kampuni na kazi vizuri Kama Joseph. Ila aligonga mwamba. Mkurugenzi akaapa kuwa hawezi kumuacha Joseph aondoke kirahisi hivo.
👇🏾
Kabla ya miezi mitatu walifanikiwa kumtengenezea nafasi nyingine Joseph na kumuweka. Boss wa Joseph alidhani kashammaliza Joseph Kumbe alikuwa amemtangaza zaidi na KUMUINUA. Joseph alitangazwa kwenye nafasi nyingine tofauti na cheo kikapanda mbali, Simon akabaki anashangaa.
👇🏾
Kumbuka Simon alifanya maamuzi yake kwa chuki bila kuangalia athari. Sasa jospeh alipohama tu, mambo kwenye Idara ya IT yakawa hayaendi tena. Ikabidi wamuhamishe mmoja kwenda Tabora lakini haikusaidia maana hakuna aliyekuwa anazijua kazi za Tabora kama Joseph. Simon anahaha...
👇🏾
Wakaanza kumpigia simu Joseph kumuomba msaada na kutaka kujua kazi zinafanywaje. Simon akawajibu kwa busara sana “Samahani ila mimi nipo idara tofauti siwezi kufanya kazi za huko, sera hairuhusu”. Simon tumbo joto na wazungu wameanza kukasirika Kwanini Joseph kaondolewa.
👇🏾
Joseph akapewa gari ya kutembelea na kampuni, akawa anaishi kwa raha kwenye kazi yake mpya, boss wake mpya ni mzuri hajapata kutokea kwake. Joseph amepata tena furaha ya kazi na maisha na wenzake yakarudi Kama kawaida. Upande wa pili Simon hana raha na anahangaika kurekebisha
👇🏾
FUNDISHO:
Usijimwambafy kama mbavu ni za mbwa koko. Ishi na watu vizuri katika sehemu zetu za kazi. Ongoza watu wa chini vizuri bila manyanyaso, hakuna ajuae kesho yake. Simon anaweza kupoteza kazi kwa ujinga wake mwenyewe.
Tupendane na tusaidiane Kama ndugu.
***Asante Sana***
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Philipo Bethuel👨🏽‍💻

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!