My Authors
Read all threads
Mysteries of Missing
Kwa muda mrefu tumekuwa tunaangazia Tamthilia nyingi labda za Actions, mapenzi na za kufikilika na nyingi nyinginezo lakini leo naona tuangazie Tamthilia inayazozungumzia mambo ya ukweli yaliopata kutokea na kuwaacha watu midomo wazi kwa maana Tamthilia hii
inaongelea kupotea kwa watu pasipo kujulikana walikoenda, kupotea kwa miji na isionakane tena, meli kubwa kutoweka kabisa katika uso wa dunia na kutoonekana hata kipande chake, ndege kupotea na abiria kutoonekana hata mwili mmoja wala kipande cha ndege
hata kimoja, uzi huu utakuacha ukishangaa muda wote na mdomo ukiwa wazi

Tamthilia ya Mysteries of missing imetengenezwa na vipande vipande vya mambo ya ukweli yaliyotokea na hayajapata majibu hadi leo. huku kwetu tungeweza kusema
ni uchawi au miujiza na pengine majini kabisa.
Tamthilia hii imetoka mwaka 2017 ikiwa na mahadhi ya Makala (Documentary) na kupata kiwango cha 7/10 katika viwango vya IMDb
Mwelezeaji mkuu katika Tamthilia hii ni Terry O' Quinn na wataalamu mbalimbali wakielezea kiutaalumu nini
kiliweza kutokea hadi kusababisha kupotea kwa vitu tajwa hapo juu. hapa panakuwa na nadhalia (theories) mbalimbali za ukinzani kutokea kwa wataalamu hawa wakidadavua matukio haya ya kustaajabisha. Ngoja sasa tuangazie visa hivi vya kupotea kwa maana viko vingi na tutakuwa tunatoa
kisa kimoja kwenye uzi mmoja kwa siku.

1. TUKIO LA NJIA YA DYTALOV (Dytalov Pass Incident)
Tukio hili linaelezea vifo vya Warusi tisa waselelekaji kwenye barafu (hikers) waliokufa kaskazini mwa mlima wa "Ural Mountains kati ya tarehe 1 na 2 february 1959 katika mazingira
yasioweza kuelezeka na kutatanisha, timu ilitengenezwa kwa dhumuni la kwenda kuseleleka kwenye barafu (skiing) likiongozwa na Igor Dyatlov aliyekuwa na umri wa miaka 23 aliyekuwa akisomea uinjinia wa radio na masters ya skiing katka chuo cha Ural polytechnical na ambaye
aliwakusanya vijana wenzake hao tisa ambao wengi walikuwa wanafunzi, hawa wote walikuwa na uzoefu mkubwa wakiwa na vyeti grade II na walitegemewa waje wapate vyeti grade ya III kwenye skiing, timu hii ilikuwa na wavulana 8 na wasichana 2 kwa kipindi hicho hivi vyeti
daraja la 3 ambavyo wangevipata ndivyo vingekuwa vyeti vya juu na daraja la juu kwa nchi nzima ya urusi walitakiwa kusafiri km 300 walitakiwa wafike kwenye mlima wa Gora Otorten km 10 kutokea kwenye eneo la tukio na kwa mwezi wa february eneo hilo linakuwa gumu sana kufikika na
kupewa daraja la 3 kwa ugumu, Wanafunzi hawa walianza zoezi lao 23 january kwenda gora km 300, kufikia tarehe 28 january mmoja wao hakujisikia vizuri hivyo alilazimika kurudi, nyendo za safari yao zilikuwa zinaandikwa kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu ambavyo vilisaidia kujua
mwenendo mzima wa safari yao. Tarehe 1 walianza safari kwenye njia waliyotakiwa kupita lakini kwa bahati mbaya kutoka na hali mbaya ya hewa iliyowafanya wasiweze kuona vizuri waendako wakajikuta wamepotea na kuamua kuwa wapige kambi kwa siku hiyo ili asubuhi washuke
bondeni kuifuata njia sahihi kosa walilofanya ni kupiga kambi hapo kwa sababu eneo lilikuwa wazi lenye miti michache walijenga kambi yao ktk mitelemko ya Kholat Syakhl katika eneo lilipewa jina la Igor Dyatlov kwa heshima ya kiongozi wa timu hiyo iliyokufa. mauzauza yanaanza
usiku kwa kitu kilichowafanya wachane turubai la hema lao na kutoroka kupitia tundu walilochana kwenda nje na wengi wao wakiwa nusu uchi kwenye barafu iliyoganda pasipo mavazi rasmi ya kuzuia baridi kali iliyokuwepo nje kitu ambacho sio cha kawaida kwa watu wenye uzoefu kama
wa kwao, haijulikani hadi leo ni kitu gani kilichowakurupua ndani na kufanya maamuzi ya kutoka nje ya hema yao. Kufikia tarehe 12 february baada ya ndugu kuona muda mrefu umepita pasipo timu kurejea wakaona inawezeka ukawa uchelewaji wa kawaida lkn ilipofika tarehe 20
february ndugu wakaomba uokozi (rescue), mwanzo walianza watu wa kujitolea wanafunzi na walimu lakini baadae jeshi lilihusishwa kwa kutumia ndege na helicopter, kufikia tarehe 27 feb watafutaji waliweza kufika kwenye kambi ya akina Igor hali ya hema walivoikuta iliwaduwaza
sana walikuta hema nusu iko chini ikiwa imefunikwa na barafu juu na hakuwemo mtu cha kushangaza ilichanwa kwa kisu kutokea ndani vitu vyao vyote hasa viatu vilikuwepo hemani lakini wao wenyewe hawakuwepo. Wachunguzi walisema walikuta nyayo (footprints) za watu
tisa waliokuwa wamevaa soksi au kiatu mguu mmoja au ambao walikuwa pekupeku, nyayo hizo ziliweza kuonekana kuelekea kwenye kingo ya msitu uliokuwa karibu, kufikia mita 500 hivi nyanyo zilianza kufukiwa na barafu, kwenye ukingo kabisa wa msitu kulionekana dalili ya moto
uliwashwa, na Kwenye eneo ilo walifanikiwa kukuta maiti 2 zote zikiwa hazina viatu na wakiwa wamevaa chupi tu,na matawi ya miti ya hapo walipo yalivunjwa kama mita 5 kwenda juu dalili labda mmoja wapo alipanda juu ili aweza kuona hema lao lipo wapi ama ni katika harakati za
kujiokoa na kitu hatarishi? Walipoenda mbele kidogo katikati ya msitu na hema wakakuta maiti zingine 3 zimekufa zikiwa kwenye mwelekeo kama walikuwa wanataka kurudi hemani kwa maana walikutwa wamekufa mmoja mita 300 wa pili mita 480 na mwingine mita 630
kutoka kwenye ukingo wa msitu, kuwapata maiti wengine wa nne ilichukua miezi zaidi ya miwili na kuonekana tarehe 4 May, wakiwa chini ya barafu mita 4 mita kama 75 kutoka kwenye ukingo wa msitu baada ya miili mitano ua kwanza kuoneka uchunguzi mara moja ukaanza kutafuta chanzo
cha kifo chao hapa ndipo tukio hili linaoneka kuwa si la kawaida. Maiti tano za kwanza baada ya uchunguzi wa hospitali (postmortem) zilionekana kutokuwa na majeraha yanayoweza kupelekea vifo vyao ingawa mmoja alipasuka kichwa kidogo na kwa wakati huo haikuoneka kuwa tatizo
na wakasema inawezekana Kilicho waua ni HYPOTHERMIA

Hypothermia ni hali inayomtokea mtu akiwa kwenye hali ya hewa chini ya hasi nyuzi 35 (-35°C) hali kwenye kiwango hiki cha baridi inajulikana kama mild hypothermia mtu hutetemeka na kuchanganyikiwa akili, hali inavozidi na
kufikia moderate kutetemeka kunaacha na kuchanganyikiwa kunazidi inapofikia hatua ya juu kabisa (severe hypothermia) mtu hupatwa na hali ya kusikia kama joto Kali na kukerwa na nguo zake alizovaa na huanza kuvua na kuzitupa na kupelekea kupata baridi zaidi na na
kuufanya moyo kusimama. Hii ndo mwanzo walisema kuwa chanzo cha vifo vyao...lakini swali likabaki ni nini kiliwaondoa ndani ya mahema yao kwa haraka hivyo hata kushindwa kuvaa vizuri??
Baada ya uchunguzi huu miezi miwili baadae baada ya
kuonekana maiti zingine nne mtizamo wa kwanza wa chanzo cha vifo ulibadilika kabisa baada ya uchanguzi wa maiti 4 zilizopatika mwisho kwa maana maiti hizi zilikuwa na majereha makubwa sana kwa ndani, mmoja kichwa kilibondeka na wawili sehemu ya kifua ilivunjikavunjika kwa
ndani wataalamu wanasema nguvu ya kuweza kufanya hivyo ni sawa nguvu ya mgongano wa magari. Cha kushangaza hakukuwa na majereha nje kama vile waliwekwa kwenye kitu chenye pressure kali kilichovunja vunja vitu ndani na kuacha mwili nje bila majereha na maiti
moja ilikutwa imekatwa ulimi, kutolewa macho, na midomo mwingine kope ziliondolewa.
Nadharia ya vifo:
1. Nadharia (theory) ya kwanza ni kuwa hawa watu waliuawa na kabila la Mansi linalokaa sehemu hiyo lakini watu wa kabila hilo walihojiwa lakini uchunguzi wa jinsi
hawa watu walivyokufa ulikinzana na nadharia hii na pia ilikataliwa kwa maana hakuna binadamu ambaye angeweza kutoa pressure ya kuharibu viuongo vya ndani na kuacha ngozi juu ikiwa nzima

2. Nadhalia ya pili kuwepo kwa majaribio ya silaha za kijeshi
za serikali ya Urusi ambapo maiti zilipimwa kuona kama zilikuwa na mionzi, ni maiti moja tu iliyonekana kuwa na mionzi kwa kiwango kidogo na hivyo kuondoa nadharia hii kama chanzo cha vifo

3. Nadhalia ya 3 kuwepo kwa maporomoko ya Barafu (Avalanche) na kwamba wakati barafu
inaporomoka hawa watu waliamka na hofu kubwa ya kuona kuwa uhai wao upo hatarini kwa kuhofia kuzikwa wakiwa hai na barafu na hivyo kutoka haraka ndani na kwa kuwa mlango ulikuwa umezibwa na barafu ikawalazimu wachane hema na
kutokea sehemu hiyo, na kukimbilia sehemu zenye miti ambazo zingepunguza nguvu ya maporomoko na hawakuvaa vizuri kwa sababu walikuwa wamelala na walivua baadhi ya nguo zao. Wale walikufa wakiwa na mwelekeo wa liliko hema walikuwa wanarudi hemani baada
ya hali ya hatari kupita lakini baridi ilikuwa kali wakaganda na kufa kabla ya kufikia hema na wale wa nne walikufa kwa kufukiwa na Avalanche

Ushaidi unaopingana na nadhalia hii.
. Hapakuwepo na dalili yoyote ya kutokea Avalanche katika
eneo hilo kwa maana kama lingetokea basi wangekuta uchafu mwingi uliobebwa toka sehemu nyingine, pia maiti 5 za mwanzo zilionekana juujuu kabisa ingekuwa Avalanche zingefukiwa mita nyingi chini, na zingesombwa na maporomoko, pia nyanyo zilizowaongoza watafutaji
zingefukiwa kama Avalanche ingetokea,

pia miti yote ya eneo hilo ingevunjikavunjika lakini hakuna mti hata mmoja uliovunjika. Na kama ingekuwa Avalanche basi hizi maiti zingeachwa na majereha makubwa sana kwenye miili yao maeneo ya nje na ndani ya miili yao kitu
ambacho maiti hazikukutwa nazo.
. Zaidi ya makundi yapatayo 100 yalifanya matembezi ya kiuchunguzi kwenye eneo hili baada ya ajali na wote hawakuweza kuona dalili ya aina yoyote ya maporomoko yaliyotokea au yanayotarajiwa kutokea.
.kama Avalanche ingetokea basi ingeifanya hema kuanguka kwenye mwelekeo wa bondeni lakini hema halikuanguka kwa mwelekeo huo na pia lingetakiwa lifukiwe na maporomoko lakini hema walilikuta likiwa nusu limebomoka nusu bado zima.
Dyatlov (kiongozi) na mkubwa wake kwa umri bwana Zolotaryov walikuwa wanasoma degree ya pili (masters) katika ukufunzi wa kuseleleka barafuni( ski instructor) kwa elimu hii waliyokuwa nayo haiwezekani kabisa wangepiga kambi kwenye eneo lenye dalili ya uwezekano wa kuwepo kwa
Avalanche
. M fumo wa nyayo zao kutoka kwenye hema kwenda chini ulikuwa unaonekana kama watu waliokuwa wanatembea kwa hiari yao, kama watu 9 wangekuwa wanakimbia Avalanche, mfumo wa nyayo zao ungekuwa tofauti kabisa, hii inaonyesha sio sababu ya kifo
Kutoka na ushahidi hapo juu ni wazi kabisa timu hii haikufa kwa Avalanche.

Kuna nadharia kama 10 hivi na mabishano makubwa ya wataalamu mbalimbali ambayo nakuachia wewe ukazione na kuzisikiliza na wewe mwenyewe kwenye tamthilia hii ya
Mystries of missing na ujue nini kiliwaua hawa jamaa.

RT na follow us @CipherdotM backup acc @CipherdotSV
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!