My Authors
Read all threads
Kulingana na level ya teknolojia ilivyo kwa sasa kumekuwa na maswali hasa kwa wanasayansi juu ya uwezekano wa mtu kusafiri kurudi nyuma ya muda ama kwenda mbele wakati ujao (time travelling) na mpaka sasa jibu lililopo Ni kwamba haiwezekani. Lakini tukija kwenye filamu zetu
ambazo mostly huwa ni zenye matukio ya kufikirika zaidi. Jambo ili linaonekana kuwezekana, filamu na Tamthilia nyingi tu zimeonyesha uwezekano wa Jambo ili ata kwa kujaribu kutumia theory mbalimbali kuipa idea hii uhalisia flani uku nadharia zao zikiwa zimeegemea zaidi kwenye
nadharia ya "Quantum Physics. Anyways tuwaachie wanasayansi nadhalia zao si Tuangalie zetu movie, UZI wa Tamthilia kadhaa ambazo zinazungumzia zaidi time travelling ambazo unaweza kuziangalia na ukazipenda pia zikiwa na mapigano ya apa na pale pamoja na science bila kusahau drama
TIMELESS: Garcia Flynn mwarifu alie bobea na mwanajeshi mstaafu ye na kundi lake wanaiba mashine ya kusafiria kurudi nyuma ya muda, akiwa na lengo ya kuibadilisha Marekani kama tuijuavyo kwa kubadilisha matukio kadhaa ya nyuma (Change History), inabidi team maalumu ya Watu watatu
mwanasayansi, mwalimu wa historia na mwanajeshi kupewa jukumu la kuhakikisha wanamzuia Flynn hasitimize dhamira take.

LEGENDS OF TOMMOROW: Rip Hunter mtu ambaye amebahatika kuona muda ujao (Future) anarudi nyuma ya muda na kukusanya team ya watu Wenye uwezo tofauti tofauti lengo
ikiwa Ni kuhakikisha matukio flan hayatokei kwa kurudi nyuma ya muda wakipambana na hatari ambazo zinatishia usalama wa dunia pamoja na muda wenyewe (time line) , wapenzi wa DCU na movie za Supergirl na flash wataipenda Hii zaidi.
TRAVELERS: miaka 100 ijayo kizazi pekee Cha binadamu kilichobakia wanagundua njia ya kuweza kurudi nyuma ya muda, kikundi Cha Watu sita wenye uwezo tofauti tofauti wanarudi kwa ajili ya zoezi la kuhakikisha wanaokoa kizazi Cha binadamu cha karne ya 21 kwa hatari watakayo kutana
nayo Kwenye wakati ujao. Hii Ina action zilizo simama safi sana
12 MONKEYS: Mwaka 2043 sehemu Kubwa ya binadamu itakuwa imekufa kutoka na kulipuka kwa ugonjwa uliouua karibu 90% ya binadamu wote. James Cole kupitia Doctor Jones anarudi nyuma ya muda mwaka 2015 na kuungana na mwanadada Dr Cassandra Railly kuhakikisha wanazuia
kulipuka kwa ugonjwa huo hatari ambao kwa taarifa walizo nazo mtu haitwae Lelandal Frost ambaye ndo aliaminika kuhusika na kuachia virusi hatari vya ugonjwa huo.
FREQUENCY: Mwaka 2016 Askari mpelelezi Remy Sullivan anagundua uwezo wa kuongea na baba yake ambae hawakuwa na maelewano mazuri kupitia redio ya hewa (Ham radio) ambapo baba yake alifariki mwaka 1996, wawili Hawa wanaunga ushirikiano wa kuhakikisha matukio
kadhaa hayatokei Tena ikiwemo la kumtafuta mtu Alie muua mama yake Remy.
TERMINATOR; THE SARAH CONNOR CHRONICLES: Idea ya Terminator sio ngeni kwa wengi. Hii matukio yake yameegemea Sana baada ya Terminator 2 Judgement day(1991). Baada ya kujitoa muhanga kwa Dr. Miles na T-800 model 101. Familia ya Connor inajikuta bado
ikiwindwa na mawakala wa Skynet kutoka wakati ujao (future), familia ya Connor inaamua kuacha kukimbia Tena na badala yake wanapambana kuzuia kuanzishwa kwa Skynet kabsa.
TERRA NOVA: Mwaka 2149 dunia ikiwa iko karibu kuharibika kabsa kutokana na machafuzi ya mazingira (pollution), Askari mpelelezi Jim Shannon aliefungwa kwa kosa la kulea mtoto wa ziada kinyume Cha Sheria, anaachiwa ndani ya muda Mfupi na kuungana na familia
yake ambapo walikuwa wanaenda sehemu maalumu ijulikanayo kama time-space-continuum rip, ambapo ni Kama wanarudi zama za uwepo wa dinosaurs lakini kukiwa na uwepo wa teknolojia ya sasa pia
THE CROSSING: Miaka 180 dunia ilikuwa ikitawila na watu wenye uwezo zaidi ya binadamu wakawaida (super enhanced) wakijulikana Kama Apex, binadamu kadhaa waliobaki wanafanikiwa kupata njia ya kurudi nyuma ya muda kabla ya kuzaliwa kwa Apex lakini miongoni mwao
akiwemo Apex mmoja Reece ambaye aliamua kusaliti jamii yake ili kumlea mtoto Leah ambaye ni alikuwa binadamu wa kawaida na ilikuwa ni kinyume Cha Sheria kwa Apex kufanya hivyo.
MANIFEST: Baada ya ndege ya Montego Air Flight 828 kutua salama kutoka kwenye safari ya masaa 5 abiria pamoja na wahudumu wakashangaa pale wanapokuta masaa yao 5 angani ni sawa na miaka 5, huku umri wao
ukiwa pale pale lakini Watu walio waacha wakiwa miaka yao imekwenda mbele. Pamoja na kurudi kwao salama lakini wanagundua na Mambo mengine ya kustaajabisha zaidi.
FLASHFORWARD: Baada ya Watu wote kuanguka nakupoteza fahamu kwa muda wa Kama dakika 2 na sekunde 17. Kwa muda huo watu wote waliweza kuona maisha yao miezi 6 ijayo kinaundwa kikundi maalumu Cha
FBI kuchunguza tukio ilo na kubaini ni nani hasa aliweza kuhusika na tukio zima na Kama walicho kiona ni mapicha picha tu ama Kweli ni matukio yatakayo tokea mbeleni Kweli na kama tukio ilo litatokea tena..
Hizi ni kadhaa tu kati ya nyingi zinazo onyesha mambo ya time travelling, kitu ambacho wengi tunatamani kingekuwa kinawezekana ili tuweze kurudi nyuma ya muda na kubadilisha vitu kadhaa ama maamuzi ambayo hayakuwa sahihi.

@CipherdotM @CipherdotSV
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!