My Authors
Read all threads
FILAMU MAARUFU ZENYE AJALI NA VIFO
SEHEMU YA PILI( TRAGIC ACCIDENTS ON THE SETS OF FAMOUS MOVIES AND SERIES)
Jana niliweza kuwaletea sehemu ya kwanza ya Ajali na Vifo kwenye filamu chache sana na nikagusa kidogo miaka ya 1910 na kidogo nikagusa 1989, 2019 na kumalizia na ajali
chache za mwaka 2020. Jana niliogopa kuumiza mioyo ya watu na kutonesha vidonda vilivyopona kwenye zile ajali zilizotugusa kwenye hii tasnia ya filamu, lakini baada ya wengi kuridhia kuwa tuendelee, basi leo nakuletea sehemu ya pili ya Uzi huu na Mungu akijalia tutaenda hadi
sehemu ya 3
Uzi huu wa leo utaangazia zile filamu maarufu pasipo kujali mwaka maadamu ni picha iliyotikisa kwa kipindi hicho. Wanasema miaka ya nyuma kutokana na kutokuwepo sheria kali ilipelekea kutokea kwa ajali nyingi sana kwenye MOVIE SET (Movie set inaweza kikawa chumba,
mtaa, mji, meli kama TITANIC, white house kama kwenye Olympus has fallen, mfano mwingine kama kingslanding ya Game of throne ambazo huwa zinatengenezwa maalumu kwa ajili ya upigaji wa picha za filamu zinaweza kutengenezwa kwa mabox, mbao au chuma na kuonekana kabisa kama kitu
halisi ambacho kipo au cha kufikilika) Ajali ambazo tunaziangazia leo ni zile zilizotokea kwenye Scene za movie Sets na sio nje ya movie sets kama ile Ajali ya Paul walker wa Fast and Furious iliyotokea mtaani akiwa haigizi movie yoyote.

1. 1928 NOAH'S ARK....Filamu hii
ilionyesha mafuriko makubwa yaliyotokea enzi ya nabii Nuhu katika kuonyesha uhalisia mapipa maelfu kwa maelfu yalimwagwa kupata scene ya mafuriko na wale watu wetu wanaoitwa extras wakamwagwa kwenye eneo hilo la mafuriko, maji yalikuwa mengi yakiienda kwa kasi na yalisababisha
vifo vya extras watatu na magari ya wagonjwa zaidi 12 yalikuwa yanatibu watu walikuwa taabani kutoka na ajali hii. sheria nyingi za usalama ziliingizwa kwenye sheria mpya kutoka na ajali hii.

2. THE MAZE RUNNER....Dylan O'Brien wakati wakipiga picha ya movie hii ambapo Mwenyewe
alicheza kama stunt katika mojawajo ya scene ngumu alitakiwa kutembea kutoka juu ya gari moja na kwenda juu ya gari nyingine yakiwa yapo kwenye speed kali, kitu kisichotegemewa kikatokea na Dylan aliumia vibaya sana, picha ilitakiwa kutoka mwezi february mwaka 2017 ila ikaja
kutoka mwaka mmoja baadae januari 2018 kumpa jamaa nafasi ya kupata matibabu.

3. XXX (2002) ... Inasemekana hii picha ilikuwa na mianguko mingi na action nyingi zilizohitaji sana stunts, basi bwana double wa Vin Diesel kama stunt nikimaanisha mtu aliyechukua uhusika wa Vin
kwenye scene hiyo hatarishi aliitwa Harry O'Connor ambaye alianguka bahati mbaya na kuangukia kichwa kwenye daraja la meli na kufa kabla ya mwili wake kutumbukia majini ..baadhi ya sehemu ya tukio hili limeachwa kwenye filamu kama kumbukumbu ya kumuenzi Harry.
4. GONE IN 60 SECOND 2 (1974) hii sio ile iliyotengenezwa upya ya Nicolous cage na Angelina Jolie ila ni Original ya mwaka 1974.
Halicki aliyekuwa ameoa muda si mrefu na baada ya kugongana magari mengi sana kwenye scene mbalimbali za movie alikuwa tayari tena kufanya vitu vyake,
wakati wakiandaa anguko la maji kutoka juu ya mnara (tower) kuja ardhini mojawapo ya kamba iliyoshikilia tower ilikatika na mnara ukaenda kugonga nguzo ya nyaya za simu iliyokuwa karibu na kumwangukia muongozaji wa picha (Director) na kumua hapo hapo, kutoka na msiba huu picha
ikafutwa(cancelled) na vipande vilivyoisha vikawekwa kwenye DVD kama vistori vifupi vifupi nahisi akina cage ndo wakaanzia hapo nimesema nahisi.

5. THE DARK KNIGHT (2008) . Hii ni picha maarufu kutokana na kifo cha muigizaji aitwaye Heath Ledger (Joker) huyu hakufa kwenye movie
set ya picha hii, yeye alichanganya madawa aliyopewa kwa matibabu na kupelekea kifo chake, lakini sisi kwenye movie set ya picha hii tunamwangazia Stuntman aliyeitwa Conway Wickliffe ambaye alishafanya stunts za kumwaga kwenye picha za , Batman Begins, Casino Royale, na Die
Another Day. wakati wakiwa kwenye movies set na wakifanya zoezi ya jinsi watakavyofanya kwenye scene yenyewe, Scene ilitakiwa iwe hivi gari la Batman lilitakiwa kulipuliwa kutumia rocket launcher ambayo Joker angeipiga hivyo basi Conway ambaye angecheza uhusika wa Joker alitoa
mwili nje ya dirisha katika ile hali ya kuweza kufyatua rocket launcher wakati akiwa kwenya hali hiyo na wakiwa speed dereva alishindwa kupiga kona ya nyuzi 90 wakiwa kwenye speed ya km 20 kwa saa waligonga mti, ingawa dereva hakufa lakini Conway alipasuka kichwa na kufa hapo
hapo. Picha hii imetolewa kama kumbukumbu kwa Health Ledger na Conway Wickliffe.

6. SYRIANA(2005)..Madhara ya Ajali nyingine hayajitokezi papo kwa papo yanachukua muda na kuwa madhara makubwa baadae baada ya muda kupita.
Katika picha hii ambapo uhusika wa Clooney ulikuwa
umefungwa( hapa inamaanisha muigizajia aliyekuwa anaigiza uhusika huo alifungwa) kwenye kiti akiwa anateswa mwishowe kiti kilisukumwa kwa nyuma na kuanguka kwenye sakafu na Clooney aligonga kichwa chini na kuumia nyuma ya kichwa kwa muda huo haikuonekana kuwa ajali kubwa lakini
baadae muigizaji huyu alikuwa anapata maumivu makali sana yasioelezeka hadi akafikia kutaka kujiua ili aachane na maumivu aliyokuwa anataabika nayo lakini baadae sana wakati jamaa kishakuwa mlevi wa kutupwa madaktari wakagundua tatizo na kumfanyia operesheni na kuweza kupona.
7. TOP GUN (1986) ... Watu wengi sana huogopa kupaa hewani wangine huogopa urefu akiwa ghorofani juu kabisa hawezi kuangalia chini anapata woga au kizunguzungu, lakini wanasema usafiri wa anga ndo njia salama ya kusafiri kuliko njia zingine maana ajali hutokea mara chache sana,
Hapa tunamuongelea Stuntman maarufu sana wa vitendo vya ndege (stunt pilot) alijulikana kama Art Scholl, ambaye alishawahi kufanya vitu vyake kwenye movies kama, Right Stuff, Iron Eagle, na Indian Jones and the Temple of Doom. Mradi wake wa mwisho ulikuwa kwenye picha ya Top Gun
Ilikuwa hivi akiwa kwenye ndege aina ya Pitts S-2 Camera plane, wakati akifanya vitu vyake angani (kumbuka na hili anga linakuwa sehemu ya movie set pia) na baada kuivingilisha ndege na kurudi sawa ndege iligoma kukaa kwenye altitude iliyotakiwa ikaanza kuporomoka... Haya
yalikuwa maneno yake ya mwisho "I have a problem. I have a real problem" akimaanisha " Nina tatizo, Nina Tatizo Kubwa'" baada ya maneno hayo ndege yake akaangukia baharini na kuanzia hapo hadi leo hakuonekana mwili wake wala ndege yake na hivyo hata chanzo cha ajali hakikuweza
kufahamika.

8. TRANSFORMERS: DARK OF THE MOON
pamoja na ukali wote, umakini na matumizi ya Computer katika kutengeneza picha hizi bwana Michael Bay bado naye alifikwa na ajali katika utengenezaji wa filamu hii, hii ilikuwaje: wakati wakipiga picha kwenye movie set, kamba ya
chuma (steel Cable) iliyokuwa imeishikilia gari juu ilikatika na kamba hiyo ilienda kumpiga extra aliyeitwa Gabriela Vesillo aliyekuwa amekaa kwenye boneti ya gari na kumuacha akiwa uso umeharibika kabisa, ubongo kuharibika kabisa, hakujitambua tena akawa zezeta baada ya kesi
mahakamani familia yake ililipwa kiasi cha dola Milioni 18 ($18 milioni) kama fidia kwa mdada ambaye maisha yake yote hataweza kupona tena.

9. MIDNIGHT RIDER (2001)
Gregg Allman Maisha yake yalikuwa yageuke na kuwa mtu mwingine pale walipoamua kutengeneza picha katika mazingira
tofauti. Lakini mbaya zaidi siku ya kwanza ya kutengeza picha hii Director alifanya kosa moja ambalo liligharimu na kumuharibia kabisa maisha yake. Ilikuwaje twende pamoja
Wakati movie set yake ilipohamia katikati ya reli inayofanya kazi katika mji wa Georgia Crew member Sarah
Jones aligongwa na train na kufa baada ya kupewa tahadhari (warning) muda wa dakika moja tu kuwa alihitajika kuondoka mwenye reli yeye na vifaa vingine vyote lakini muda huo ukawa ni mchache, hakuweza kufanikiwa na kupelekea kifo chake. Hapa sasa mtiti ukaanza ikaonekana Director
hakuwa na kibali cha kufanya eneo hilo kuwa kama sehemu ya movie set, pamoja na yote wazalishaji pamoja na director Randall Miller walifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashitaka ambapo director huyu alifungwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kuua pasipo kukusudia na kuingia eneo
pasipo kibali (manslaughter and traspassing).

10. RAMBO: FIRST BLOOD PART II
Kwenye picha hii ambako milipuko ilikuwa kama kitu cha kawaida.. Wanasema hakuna picha zenye hatari kama zile zinazohusisha milipuko, basi bwana hii picha nayo iliua mtu tena si mtu wa kawaida bali
mtaalamu wa utegaji wa mbomu alitambulika kama Cliff Wenger Jr alikufa akiwa anatega mabovu kwenye movie set hadi leo haijafahamika alikufakufaje. Wengine wanasema aliporomoka na kuangukia majini kwenye mto wangine wanasema labda alikufa wakati bomu alilokuwa akilitega kumlipukia
11. SYLVESTER STALLONE IS WALKING DISASTER ZONE.. samahani ndugu zanguni hii sio filamu bali ni mapitio ya Ajali mbali mbali za STALLONE katika filamu zake Wanasema kwa mtu aliyecheza Rocky na Rambo na bado kuwa mzima hadi leo ni miujiza
• tukianzia na ile ya first Blood wakati
wakati yeye mwenyewe akicheza kama muigizaji na stunt akicheza uhusika wa John Rambo alianguka kutoka mlimani kwenda bondeni ambako kulikuwa na miti mingi aliangukia kwenye matawi ya mti yaliyomvunja mbavu za kutosha na kilio cha kugumia unachokisia au ulichokisika ndani ya
filamu hiyo ni kilio cha KWELI kilichomtoka kutoka na maumivu aliyoyapata ya kuvunjika mbavu.
• Kwenye movie set ya Rocky wakati Rocky akipigana na drago (Dolf Lundgren) STALLONE alipigwa ngumi nzito sana yenye kilo 300 iliyosafiri kwa speed kali kwenye kifua na kuufanya moyo
kuyumba na kupelekea kuvimba (ikumbukwe Dolf ni mcheza Karate mwenye Black Belt) na hivyo kulazwa akiwa mahutuhuti kwa wiki 2 na huku maisha yake yakiwa kwenye hali ya hatari.
•Kwenye movie set nyingine ya The Expendables Stallone ailipata hatihati nyingine ya kidogo kufa wakiwa
wakiwa wanapigana na Steeve "Stone Cold" Austin, Stallone alianguka vibaya katika purukushani hiyo na kuvunja uti wa mgongo na kupelekea kuwekewa vyuma kwenye uti wa mgongo

12. THE CROW
Hii ni Historia kubwa na iliyochukua nafasi kubwa katika Ajali za huko Hollywood inayomuhusu
mtoto wa Bruce Lee mfalme wa martial arts aliyekuwa anajulika kama BRANDON LEE
Ajali ilitokeaje?? Wakati wakiwa kwenye movie set uhusika wa brandon Lee ulitakiwa kupigwa risasi lakini prop gun iliyotumika haikusafishwa vizuri ili kuondoa uchafu wa risasi baridi (blanks) brandon
Lee alitakiwa apigwe risasi na muigizaji Michael Messe alipomlenga brandon Lee na kufyatua vipande vya blanks vilivyobaki kwenye bunduki vilitoka na kuruka kwa speed ya risasi na kumpiga brandon Lee kifuani na kuanza kutokwa damu nyingi pamoja na juhudi zote kuokoa maisha yake
lakini brandon Lee alitokwa na damu nyingi iliyopelekea mauti yake. kifo hiki kilimuumiza sana Messe na kumfanya kuacha kuigiza kwa kipindi cha mwaka mzima.

13 THE TWILIGHT ZONE (1983) hii ni mojawapo ya tamthilia bora na inayopendwa sana na watu mwaka 1983 picha hii iliongozwa
na madirector 4 lakini ajali ilitokea wakati muongozaji aitwaye John Landis akiwa kazini na mbaya zaidi kisheria hairuhusiwi kuajili watoto wa umri mdogo kuigiza makubaliano yalifanyika kinyemela
Scene ilikuwa hivi muigizaji Vic Morrow na watoto wawili Myca Dinh Le na Renee
Shij-Yi waliokuwa wanafukuzwa na helikopta Vic akiwa amewabeba watoto hao wawili wakiwa kwenye movie set kwa bahati mbaya kwa hali isiyotegemewa mlipuko ulitokea kwenye eneo la stunts na ulilipuka karibu kabisa na mkia wa helikopta na kuhaiharibu kabisa Roter ya helikopta na
kuifanya helikopta hiyo kupoteza muelekeo na kuanguka na kuwaua Vic na watoto wote wawili hapo hapo na kufanya vifo vitatu kwa mara moja.

Hii inakamilisha sehemu yetu ya pili ya uzi huu kama mtakuwa hamjachoka tutawaletea sehemu ya 3 kwa maana ajali ni nyingi sana na kwa jinsi
mambo yalivyo unaweza sema ata sehemu za movie set kuwa ni hatarishi zaidi kuliko tunavyo dhani, wahaya wanasema "Ofcourse Anything Can Happen"..

KAMA UZI HUU UMEKUGUSA NA IMEUPENDA BASI TUNAOMBA UTUZAWADIE RT ZA KUTOSHA NA WENGINE WAELIMIKE ZAIDI.
Kama hizi ajali zimekugusa basi fanya RT za kutosha nasi tutajisikia kuwa supported
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!